Wazo langu: Hivi haiwezekani CHADEMA ikafanya mkutano wa hadhara kwa amani?

Hii ni dunia......hakuna binadamu wa kawaida anayeweza kushangilia mauaji hata kama ni ya adui yake......kumbuka leo ni kwa Daudi(R.I.P) .....kesho inaweza kuwa kwako au kwa ndugu yako wa karibu......hutakufa kwenye maandamano ya CDM manake wewe sio mwanachama wao ila utauliwa hata na majambazi.......narudia tena hii ni dunia!

Hii hata asiyekuwa na ubongo ataielewa
 
Hilo kwake halipo ndugu yangu na ndio maana anashabikia kifo cha Daudi (R.I.P)......yeye ni mkamilifu sana hivyo hawezi kukumbwa na chochote cha bahati mbaya......anajua atakufaje, wapi ? na lini? ndio mana haoni tatizo kufurahia kifo cha mwenzie!

Ndo tatizo la binadam kujisahau na kutoa maneno ambayo ni kufuru hata kwa Mungu
 
Ila pole uwezo wako wakufikiri ndo umefika mwisho,uwe unaingia humu kiwa fiti na sio kururopoka,au umetumwa"kajipange.
 
Ndugu zangu wan JF embu leo naomba tuongelee hii kitu kutoka moyoni. Mimi sio mnazi wala mwanachama wa chama chochote ila kila ninaposikia CHADEMA wanataka au wanafanya mkutano mkubwa wa hadhara basi watazuiliwa na polisi then wao watakaidi amri hiyo mwishowe watafukuzana kwa marungu na mabomu ya machozi mpk watu wasio na hatia kufa na wengine kujeruhiwa.

Maoni nionavyo mimi ni kama vile CHADEMA wanfanya makusudi ili watu walichukiie jeshi la polisi baada ya kujeruhiwa.Hivi CHADEMA wakiahirisha mkutano wao mpaka siku watakokubaliana na jeshi la polisi kosa linakuwepo wapi?

Hivi hatuoni kwamba uhai wa binadamu una thamani kuliko hizi siasa za bongo tafadhali jamanii tujirekebishe hata kama polisi wamekosea lakini kama CHADEMA wangefuata maagizo yao asingekufa mtu Iringa,Morogoro wala Arusha.

Nawasilisha wadau

Umekosa mabwana Facebook umekuja kuwatafuta huku JF?
 
Kwa mujibu wa Katiba Polisi hawana uwezo wa kuzuia watu kuandamana kwa amani wala kuzuia mikutano ya chama chochote cha siasa. Wajibu wa Polisi ni kuhakikisha amani na utulivu katika shughuli zote za kisiasa za vyama yaani kuwasindikiza kwenye maandamano na kuwatia nguvuni wale watakaokiuka amani na uhuru wa wengine. Jeshi la Polisi hapa bila ya hata tone la aibu limekuwa kama tawi la CCM kwa kutekeleza kila wanaloelekezwa na mavuvuzela wa CCM kwa mfano hakukuwa na uhalali wa Polisi kuzuia maandamano ya CHADEMA Morogoro ati kwa sababu 'bararara nyembamba' wakati CCM walikuwa na shamrashamra za maandamano hayo hayo mitaani wakiandamana kuwasindikiza wagombea waliokuwa wakirudisha fomu za kugombea nafasi katika jumuia ya wazazi wa CCM! Na kule Iringa vile vile sababu zilizotolewa ni za unyanyasaji na kuwahujumu CHADEMA ati 'Muda wa sensa umeongezwa' wakati mahali pengine nchi hii hii CCM walikuwa katika heka heka za kampeni mbalimbali ikiwemo ile ya Bububu Zanzibar ambako kunaendelea kampeni za kuziba nafasi iliyo wazi! Kwa kifupi Polisi wa Tanzania hawana adabu hata chembe kwa waajiri wao ambao ni wananchi wanaowanyanyasa,kuwateka nyara, kuwajeruhi, kuwatesa, kuwamwagia tindikali na kuwaua kwa visingizio visivyokuwa na uzito hata kidogo. Ingekuwa serikali yenye maadili Mkuu wa Jeshi la Polisi angejiuzulu kuanzia tukio la kule Arusha, lakini badala ya kuwajibika wamekuwa bize kutunga uongo mbalimbali kuhalalisha vitendo vyao vya kihuni, kibabe na kishenzi dhidi ya raia waliowaajiri. Ipo siku watajibu kila nukta ya uovu waombeleya jamii au watafute pa kukimbilia.
 
Ndugu zangu wan JF embu leo naomba tuongelee hii kitu kutoka moyoni. Mimi sio mnazi wala mwanachama wa chama chochote ila kila ninaposikia CHADEMA wanataka au wanafanya mkutano mkubwa wa hadhara basi watazuiliwa na polisi then wao watakaidi amri hiyo mwishowe watafukuzana kwa marungu na mabomu ya machozi mpk watu wasio na hatia kufa na wengine kujeruhiwa.

Maoni nionavyo mimi ni kama vile CHADEMA wanfanya makusudi ili watu walichukiie jeshi la polisi baada ya kujeruhiwa.Hivi CHADEMA wakiahirisha mkutano wao mpaka siku watakokubaliana na jeshi la polisi kosa linakuwepo wapi?

Hivi hatuoni kwamba uhai wa binadamu una thamani kuliko hizi siasa za bongo tafadhali jamanii tujirekebishe hata kama polisi wamekosea lakini kama CHADEMA wangefuata maagizo yao asingekufa mtu Iringa,Morogoro wala Arusha.

Nawasilisha wadau
MNAZI HAJIFICHI(utamjua kwa LUGHA na mitazamo yake),We unafikiri POLICCM wataridhika lini CDM wafanye mkutano?,Kama CDM wanafanya Makusudi POLICCM wanafanya kwa BAHATI mbaya?, Acha U-Mabwepande wako
USHAURI:ACHA UVIVU WA KUFIKIRI au ndomwisho wako kabisa? RUDI SHULE BASI.
 
ulianza vizuri ila mwisho umejionesha kuwa umetumwa na magamba ili ulete chuki kwa CHADEMA....wasema wewe sio mnazi wala mshabiki ila nadhani umetumwa na hao wanazi na washabiki wa magamba
 
kwa arusha ninajua kwamba kabisa polisi walichemka lakini vipi seemu nyingine ambapo chadema waliambiwa kuna sensa na wenyewe wakanagania kufanya mkutano

Mjomba ficha upumbavu wako...
Usione kama vile umefanikiwa labda kupandisha jaza za watu...
Hili swala si la kuja kutafutia umaarufu hapa JF.

Swala la Sensa unalolisema wewe liko Iringa tu au nchi nzima?
Je mbona CCM wanafanya mikutano huko Zanzibar?
Au je mbona Clouds wamefanya Fiesta Mwanza?
Huko Sensa hakuna?
Au Sensa iko kwenye mikutano ya Chadema tu?

huna hoja ya kuzungumzia hapa, futa hii thread au laa kachukue kopo ukachambe.
 
Tusiende mbali mkuu...angalia walivyovaa jeshi la polisi kenya kuzuia vurugu mombasa ambako kuna kundi la alshabaab pia...the compare na hawa polisi wetu huko nyololo iringa..
Walizuia mikutano ya chadema kwa siku tano na chadema walitii agizo hilo....baada ya kuzuia nyololo waliamua kufanya mikutano ya ndani kama walivyoruhusiwa na ndio maana viongozi wake walikamatiwa ofisini.
Ni mpuuzi tu ndio anaweza kujustify mauaji ya polisi hawa...kazi ya polisi si kuua ni kusimamia na kulinda raia na mali zao.....polisi hutumia silaha kumsalimisha anaedaiwa kufanya vurugu ili waweze kupata taarifa ili kukamilisha investigation.
SOMETIMES HAINA HAJA YA KUPAMBANA NA WANANCHI,NDUGU ZAKO,RAIA ZAKO AMBAO UNAJUA HAWATALETA MADHARA.
MBONA MECHI ZA KIRAFIKI ZINAENDELEA NA TUNAKUSANYIKA TENA MECHI YA YANGA TUMETOKA TUNAKIMBIA MABARABARANI.....
KWA TAARIFA TU:pOLISI WALISHAZOEA KUUA GIZANI SASA WANAUA NURUNI..TUMEPOTEZA NDUGU ZETU KWA KISINGIZIO CHA JAMBAZI SUGU KUMBE NI KUPISHANA KIDOGO NA KADA MAARUFU AU WATU WANAOABUDIWA!
 
dada sweetlady why unasema jamaa [Mndengereko] katumwa. ameandika ishu ambayo ameiona. sio kila mtu akiandika kitu ambacho hakisifii chadema basi ni katumwa. jamaa amesema hatoki chama chochote thats it. kama angesema ametoka ccm ungemfanya nini au unadhani anaogopa mtu humu jf.
 
Ndugu zangu wan JF embu leo naomba tuongelee hii kitu kutoka moyoni. Mimi sio mnazi wala mwanachama wa chama chochote ila kila ninaposikia CHADEMA wanataka au wanafanya mkutano mkubwa wa hadhara basi watazuiliwa na polisi then wao watakaidi amri hiyo mwishowe watafukuzana kwa marungu na mabomu ya machozi mpk watu wasio na hatia kufa na wengine kujeruhiwa.

Maoni nionavyo mimi ni kama vile CHADEMA wanfanya makusudi ili watu walichukiie jeshi la polisi baada ya kujeruhiwa.Hivi CHADEMA wakiahirisha mkutano wao mpaka siku watakokubaliana na jeshi la polisi kosa linakuwepo wapi?

Hivi hatuoni kwamba uhai wa binadamu una thamani kuliko hizi siasa za bongo tafadhali jamanii tujirekebishe hata kama polisi wamekosea lakini kama CHADEMA wangefuata maagizo yao asingekufa mtu Iringa,Morogoro wala Arusha.

Nawasilisha wadau

SWALI lako fanani umeuliza wrong audience, wakuulizwa ni polisi, kwa sababu hata siku moja haijawahi kutokea CDM wakapiga mtu wakaua, wao ndio wananokung'utwa na kuuwawa na polisi: waulize polisi, hivi kwa nini mnawauwa CDM katika mikutano yao?

MIMI ninaishauri CDM isije hata siku moja ikakubali kutii amri ZISIZO HALALI za polisi waliotumwa na CCM kufanya kazi ya CCM (kwani wakitii tu, ndo watakuwa wamekwisha, watakuwa wamenasa kwenye mtego wa CCM wa kuwazuia kufanya siasa. TAMBUA ndg sasa hivi CDM wamebakiwa na political platform moja tu yaani mikutano ya hadhara, na wao sio kwamba wanapenda kutumia njia hii ghali bali wamelazimishwa kufanya hivyo na CCM baada ya kuzuia mijadala BUNGENI wakimtumia MAKINDA na wenzake, na kuminya vyombo vya habari. NJIA PEKEE KWA CDM ni kurudi kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara; wakikubali hiyo nayo ikafungwa basi watakuwa wamekubali kufa kisiasa): ni wazi inafahamika, wala haihitaji uwe mwanasheria kutambua kuwa kuna (1) amri halali, lawful order, na (2) amri isiyo halali - amri za polisi kuzuia mikutano ya vyama si halali, hazipaswi kuzingatiwa, hii kwa mujibu wa maamuzi ya kesi nyingi tu za mahakama KUU na ya RUFANI kama vile REV MTIKILA V AG & OTHERS, AMAN KABOUROU V AG & OTHERS nk. POLISI ndio wanaovunja sheria, hawatii maamuzi ya mahakama, tena mahakama ya RUFANI, the highest court in the land - it is dangerous, kwamba kazi ya polisi ni kulinda mikutano wala siyo kukubali kama au la mkutano uitishwe, hili la kuitishwa mikutano lilikwisha amriwa na sheria na polisi wanapaswa kutii kwamba kazi yao ni kutoa ulinzi tu; wananchi tuendelee kupiga kelele na kulaani matendo yao ya ukaidi wa sheria huku wao wakiwataka wengine wazitii 'bila shuruti'.

NAPENDA niwaambie ukweli ulio wazi kabisa ambao ndio unaotawala PSYCHOLOGY ya polisi, nao ni kwamba polisi sasa hivi hawataki kabisa kufanya kazi walioajiriwa kuifanya kisheria: KULINDA WATU NA MALI ZAO, hii ni kwa sababu wakija mkutanoni kuilinda CDM wanakosa muda wa kuingia mtaani kudhulumu wananchi na kujipatia pesa. POLISI sasa hivi wameshazoea kabisa na kufanya kuwa hii ndiyo kazi yao halali, UNYANG'ANYI, na wala siyo ulinzi wa watu na mali. KWA hiyo wanapokuja kwenye mkutano wanakuja huku wakiwa wamechukia kwamba, 'aaaaaaaa sasa CDM nao nini tena wanatukatili dili zetu, basi twende kuwavurumisha alafu tunarudi kwenye dili'. WAKUBWA huu ndo ukweli, na tatizo ni kubwa kwani hawapendi hata kutoa ulinzi kwa viongozi wa kitaifa kama WAZIRI MKUU PM na hata RAIS PRES, na askari anayepangwa kutoa ulinzi kwake huwa ni adhabu...
 
Ndugu zangu wan JF embu leo naomba tuongelee hii kitu kutoka moyoni. Mimi sio mnazi wala mwanachama wa chama chochote ila kila ninaposikia CHADEMA wanataka au wanafanya mkutano mkubwa wa hadhara basi watazuiliwa na polisi then wao watakaidi amri hiyo mwishowe watafukuzana kwa marungu na mabomu ya machozi mpk watu wasio na hatia kufa na wengine kujeruhiwa.

Maoni nionavyo mimi ni kama vile CHADEMA wanfanya makusudi ili watu walichukiie jeshi la polisi baada ya kujeruhiwa.Hivi CHADEMA wakiahirisha mkutano wao mpaka siku watakokubaliana na jeshi la polisi kosa linakuwepo wapi?

Hivi hatuoni kwamba uhai wa binadamu una thamani kuliko hizi siasa za bongo tafadhali jamanii tujirekebishe hata kama polisi wamekosea lakini kama CHADEMA wangefuata maagizo yao asingekufa mtu Iringa,Morogoro wala Arusha.

Nawasilisha wadau

Ndugu zangu Watanzania tuache uvivu wa fikra na tufuatilie ishu kwa umakini mkubwa kama huna taarifa na uwezo wa kuchmambua mambo kaa kimya. Huyu jamaa hawezi fanya tathmini??!!! CHADEMA hwazunguki tuu, iko taratibu kupitiia kwa Tendwa na program nzima ya ziara inaeleweka, licha ya hivyo hii sio CCM ambapo gharamza za ziara zinatokea EPA, sie tunachangia chama tunaumia sana na hiki ndicho kinachouma kwamba tunaingizwa gharama zisizo za lazima na Mafisadi hawa. Hivi wewe huuoni uonevu huu? are you myopic? Mbona hujiulizi wao ccm hawazuiwi?
 
GT
Mimi naona mleta mada na wachangiaji wameanza kuzusha tafrani jukwaani, naomba taratibu tufuatane-
1. Mleta mada, kwa mtizamo wangu, inaonekana hana taarifa na ushahidi kuhusu jinsi CDM walivyo watiifu kwa Sheria za nchi bila shurti. Lkn pili namuona kama vile ni mwana-ccm aliyeingia jukwaani kuamsha hisia na hasira za wananchi wanaofuatilia habari za kisiasa. kwanini nasema hivi-
(a)CDM mara zote wamekuwa wakitoa taarifa polisi kabla ya mikutano na maandamano kufanyika.
(b)polisi hukaa pamoja na viongozi wa CDM na kukubaliana jinsi ya kuendesha kazi hiyo ya siasa iwe katika mkutano/maandamano
(c) makubaliano hayo hutolewa na polisi kimaandishi,
(d)Lakini kinachotokea siku ya mwisho yaani kwa mfano leo JUMANNE mkutano/maandamano ni kesho, leo jioni ndipo polisi wanadai eti intellijensia yao inawaambia kutakuwa na fujo, hivyo kusitisha shughuli za siasa za CDM wakati tayari viongozi wote wako kwenye eno la tukio na gharama nyingi zimeshatumika. hivi ktk mazingira haya nani mgomvi, si police-ccm na chama chao cha ufisadi cha ccm. hiki ndicho kilichotokea Arusha, matokeo yake polisi wakaua raia wasio na hatia. Ushahidi upo , kama anabisha amuulize Spika wa Bunge, ushahidi aliouwasilisha Mhe. G. Lema, spika akakimbia nao hadi leo haujajadiliwa

2. Pili CDM walipokuwa Morogoro, walikuwa wamekubaliana na Polisi kufanya maandamano na mikutano na njia watakazopita. Lakini wakazuia kuwa kuna Sikuu kuu ya Nane Nane, polisi wengi wanalinda huko hivo waende wakaanzie Mikumi na Kilosa baada ya Nanenane warudi Morogoro kuendelea na kazi zao. CDM walifanya hivo, lkn Dr. Slaa akiwa Mikume katika hosteli za VETA alifukuzwa usiku na mkuu wa VETA na hakuna kauli yoyote ya Serikali ilitolewa. CDM Walipomaliza ziara ya Mikumi na Kilosa, wakarudi Morogoro mjini kama walivyokubaliana na Polisi, cha ajabu, asubuhi/jioni kama nakumbuka vizuri, wanaambiwa wanaruhusiwa kufanya mkutano bila maandamano, raia wakakataa na kuandamana, polisi wakamwua muuza magazeti, TV zingine zilichakachua habari, ITV ikawaumbua polisi kwa kutoa tukio zima kama lilivyo, polisi wakawa wanauma maneno.

3. Maandamano na Mikutano ya Iringa ilikubalika Polisi, lakn walidai CDM isubiri zoezi la sensa lipite, CDM WAKAKUBALi na kuwaambia watafanya kazi ya ufunguzi wa matawi. kazi ya kufungua matawi ilifanyika vizuri sehmu nyingi lkn CCM na police-ccm walipoona mwitikio wa wananchi ni mkubwa kuwa wnataka mabadiliko ndipo wakaibuka na kuwapiga mabomu. Mwandishi wa habari amepigwa bomu na polisi mchana kweupe, picha na video zipo wala hazina chenga, unaweza kuwaona police wote na kama unawajua utawatambua wote,

nimeona nieleze kiufupi ili magamba , chama cha mafisadi/mabwepande/mafia na mafisadi wao wajue tunaujua ukweli kuliko wanavyodani wao. hata watanzania hawadanganyi tena, wana taarifa za kina na za wazi zisizoacha hata tone la shaka katika mioyo yao.

aluta continua
 
UMEANZA vizuri ila mwisho UKAJIFUNUA GAMBA LAKO.

Nani kakuambia POLISI wanaruhusiwa KUZUIA au KURUHUSU Mikutano/Maandamano?

Wao wana taarifiwa tu ili watowe ulinzi na hayo mengine hayawahusu.

Hiyo ndiyo KATIBA YA NCHI kwa sasa. Kama mambo huyajui KAA KIMYA.

HAKI HAIOMWBI ILA INAPIGANIWA.

Ni wachache wanaolijua hilo !
 
CHADEMA hawana vurugu, hawana silaha, wenye shida ni Polisi ambao kazi yao ni kusimamia amani ya Wananchi. Wananchi wapokuwa na mkutano wanaomba kibali, na kupewa Polisi wa kusimamia kuona kuwa hakuna uvunjifu wa amani. Inapotokea kuwa Polisi ndio wanaoleta fujo kwenye hiyo mikutano basi sisi tujiulize ni kwa nini? Wanatumwa na nani kufanya fujo hizo? Mbona CCM wanaendelea na mikutano yao na hawafanywi chochote? C.C.M wao anashikiana mpaka silaha, huko CHADEMA ushaona mtu anaenda kwenye mkutano na silaha? Tusipende kufuata mkumbo, tujaribu kufikiria mbali zaidi.

Mwandishi wa habari katika hali ya kawaida huwa hauwawi, internationaly hawa watu huwa wanalindwa sana kwani wanakusanya habari ambazo wanakuja kuzileta kwa public ili wajue ni kitu gani kinachoendelea, unapomuua mtu ambaye yupo anakusanya habari inatia shaka kidogo.

On the other hand, nashawishika kusema kuwa jeshi la Polisi limeoza, halina professionalism maana askari wengi ni failures wa la 7 ambao wanafundishwa kutumia nguvu na sio akili. Kuua raia ni crime against humanity, ni kweli kuwa hawafundishwi kutokuua raia ovyo?wanafundishwa, lakini hawatumii akili. Nadhani ni wakati muafaka kwa jeshi la polisi kuundwa upya, ifike mahali mtu anapotaka kuwa Polisi awe hata angalau na elimu ya kidato cha 6 na kuendelea, na wafundishwe sheria kwa ujumla. As for IGP Said Mwema, anatakiwa awajibike kwa makosa ambayo vijana wake wamekuwa wakiyafanya dhidi ya raia wema na hata siku moja sijasikia wamepew adhabu,angekuwa amejenga tabia ya kuwaadhibu wahalifu wake ndani ya Jeshi hayo yote yasingetokea. As for RPC wa Iringa, inatakiwa naye ang'atuke ndani ya masaa 24 maana ameprove failure, raia hawawezi kuuwawa mbele ya presence yako wewe kama kiongozi, achilia mbali kuwa aliyeuwawa ni mwandishi wa habari. Kitendo cha Polisi wale kumpiga mtu na hata kumuua ilihali wakijua kuwa RPC yuko eneo hilo inatosha kabisa kuonyesha kuwa kulikua na ushirikiano baina ya pande hizo mbili, hainiingii akilini mtoto wangu mimi amtukane mtoto wa jirani mbele ya macho yangu, kwa mwenye akili timamu lazima atajua kuwa ni mambo tumekua tukijadili ndani na leo mtoto kayatoa nje, vivyo hivyo, RPC wa Iringa aisee is in for this, there is no way out anaweza kulikwepa zigo hili. How i wish angewajibishwa, ila only in Tanzania utasikia kuwa ni bahati mbaya.
 
Back
Top Bottom