Wazo langu: Hivi haiwezekani CHADEMA ikafanya mkutano wa hadhara kwa amani?

Fujo hutokea pale tu polisi wanapokuwepo kwenye mikutano ya CHADEMA.

Kwenye tukio la jana, haingii akilini kwa nini polisi wengi walikuwa wanamzunguka mwandishi mmoja tu wa habari?

Zaidi ya hapo mkuu, mtu aliyejisalimisha huwa analala chini au anapiga magoti..sasa iweje mtu huyo aendelee kupigwa au kusubiwa na taasisi ambayo imepewa jukumu la kulinda na kutetea haki za raia?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Ndiyo matatizo ya kula kabla hujapiga mswaki.

Pitia habari hizi na angalia kama kulikuwa na MKUTANO WA NJE au maandamano.

Safari hii POLISI wamedai lazima kuwe na mikutano ya NDANI TU na si ya nje.

Ila hapohapo, Mwanza wameruhusiwa kufanya FIESTA (TAMASHA).

Na hata hivyo, sababu ya KUPIGA waandishi wa habari ni nini?

Kumbuka aliyeuawa alikwenda kuuliza kwa nini wanampiga Mwandishi mwingine.

Anyway, sikujua kuwa Waandishi wa habari walikuwa wanaandamana jana huko Iringa.

He pumguza jazba mr perfect unayekula baada ya kupiga mswaki,
Sipo hapa kutetea polisi mkuu wala kuhalalisha mauaji yao

Pitia tena bandiko lako na nilichokijubu naamini utanielewa
 
Haki inaambatana na wajibu mkuu na hakuna uhuru usio na mipaka

Kazi ya polisi haiishii kupokea taarifa tu na kuleta ulinzi, ni lazima pia waangalie hali halisi ya kiusalama inaruhusu hicho kinachotakiwa kufanyika kifanyike
Sasa kama polisi wataona kunasababu za msingi hicho kilichotaarifiwa kufanyka kitasababisha kukosekana kwa usalama ambao wao kama chombo cha kazi hiyo wanaona iwapo kikitokea na wakijaribu kizima inaweza kuleta mdhara basi wanawajibu wa kusitisha au kubadili utaratibu

Ingawa maranyingi Polisi wanakuwa wanatoa maamuzi ya kionevu na kibabe dhidi ya CDM lakini pia CDM nao wakati mwingine wawe wanaangalia pia, maana kuwashawishi tu watu kufanya kitu ambacho kinapelekea vifo na pengine kupeleke kukipa umaarufu zaidi chama tu sio busara nzuri pia

Na most of time ni maandamano/matembezi ndio yanaleta tabu na si mikutano
Naamini wanaweza kabisa kufanya mikutano yao vizuri na wananchi wakawasikia na kuwaelewa bila kuanza kuandamana mabarabarani
Unapoongelea polisi nadhani uwe unafikiri na aina ya polisi na mazingira waliyomo. Kama polisi wa nchi zilizoendelea ni sawa, lakini kwa polisi hawa wa Mwema, wanaokamata madawa ya kulevya na kisha wanayauza!!!! Wanaouwa wafanyabiashara kwa kuwaita majambazi, la hasha ndugu yangu. Hawa polisi wana bei tena ndogo sana ili kulinda wahalifu na kutetea kundi la kihalifu. Yawezekana huwafahamu vizuri, lakini ukweli ni kwamba matukio yote ya kihalifu wanashiriki kwa 100%. Kuanzia ujambazi mpaka biashara ya ushafirishaji haramu wa watu, madawa ya kulevya (Mirungi ndio usiseme). Tunajenga crime country kwa sababu ya kuwa na jeshi la polisi lililooza. Na uozo huu unalindwa na watawala, sababu jeshi hilo ndiyo kinga kuu ya uwepo wao madarakani, hivyo watalitumia kwa kadiri ya matakwa yao. Mfano: Kwenda kuzuia CHADEMA kufungua tawi lao kijijini Mafinga (Hii nayo inahitaji kibali cha polisi), tena kwa risasi na mabomu (Wakaua kwa makusudi mwandishi wa habari aliyepiga picha matukio hayo). Hivyo ama CHADEMA waamue kutii jeshi la polisi kwa kuendesha siasa kwa mujibu wa matakwa ya CCM, au waamue kudai haki yao kwa nguvu. KUMBUKA WAJIBU BILA HAKI, NI SAWA NA UHURU BILA USAWA.
 
Ndugu zangu wan JF embu leo naomba tuongelee hii kitu kutoka moyoni. Mimi sio mnazi wala mwanachama wa chama chochote ila kila ninaposikia CHADEMA wanataka au wanafanya mkutano mkubwa wa hadhara basi watazuiliwa na polisi then wao watakaidi amri hiyo mwishowe watafukuzana kwa marungu na mabomu ya machozi mpk watu wasio na hatia kufa na wengine kujeruhiwa.

Maoni nionavyo mimi ni kama vile CHADEMA wanfanya makusudi ili watu walichukiie jeshi la polisi baada ya kujeruhiwa.Hivi CHADEMA wakiahirisha mkutano wao mpaka siku watakokubaliana na jeshi la polisi kosa linakuwepo wapi?

Hivi hatuoni kwamba uhai wa binadamu una thamani kuliko hizi siasa za bongo tafadhali jamanii tujirekebishe hata kama polisi wamekosea lakini kama CHADEMA wangefuata maagizo yao asingekufa mtu Iringa,Morogoro wala Arusha.

Nawasilisha wadau

Binafsi sina undungu na watu wenye upeo mdogo wa kufikiri; na wenye ushabiki wa kisiasa bila kujua kuzisoma nyakati .

Nyie hao ndio mlikuwa mnasema vyama vya upinzani ni vyama vya "mjini", mara oh, kwa nini CHADEMA haiendi vijijini, na blah blah nnyingine kibao. Leo CHADEMA kimeanza kwenda vijijini, mmefufua agenda yenu ya mwaka 1995 (ITV mtakumbuka) kuwatisha watu kuwa upinzani ndio utaleta vita. Ukweli ni kuwa, na watanzania walio wengi wanajua, CCM, na serikali yake, ndicho kinawaua watanzania wasio na hatia na wala si CHADEMA au chama kingine cha siasa.

Mungu hatakaa kimya, CCM kitashushiwa gharika na waliomo hawatapata nafasi ya kuingia katika safina. Mwenye macho, haambiwi tazama. Mnazi utakaopandwa leo, hata kama ni mbegu fupi, hautatoa dafu kabla ya sala yangu kutimia. Amina
 
jamani ytuulizane ingekuwa wewe ungeweza kuwahmasisha watu waende kwenye mkutano wakti unajua polisi wamezuiia na unajua kitakahotokea mbele tusiishabikie tu kisa chadema basi hawakosei la hashaa inabidi tuonee ukweli n kama ndugu yako akifa utamlaumu kwenye maandamano ya chadema utamlaumu nani polisi au chadema walioandaa mkutano kifo kinauma jamini ndio maana naongea hivi lakini kuna baadhi ya watu ukisema unchohisiwao wanafikiri ww ni gamba kisa unaiponda chadema sitaki kuamini kwamba muda wote chadema kipo sahihi people do learn from mistakes lakini chadema hawaonekani kubadilika labda sielewi ukweli jibu kuniconvince lakini sio unatikuna mimi gamba kwa kutegemea nitakueliewa naeleeshwa kwa hooja sio kwa matusi
 
wewe mwehu uliyetoroka matibabuni,wanaopigwa wala hawahusiki na cdm.ila polis wenu wanamakengeza.

Ndio maana ya kupigana, kunakuwa na collateral demages, walilengwa waliokaidi amri halali ya polisi.
 
Ndio maana ya kupigana, kunakuwa na collateral demages, walilengwa waliokaidi amri halali ya polisi.
wewe kuna amri ipi ilitolewa???washenzi kama wewe,mbona fiesta na chaguzi zenu zinaendelea???zenyewe hazihusiani na sensa.
lenye mwanzo mbaya mwisho wake huwa mbaya kama ccm ilivyo.
 
mi nadhani wote wana makosa, cdm na polisi.
Polisi wanatumia nguvu kupita kiasi tena hata isipo stahili lkn cdm nao wamekuwa wakaidi maranyingi kutii wanacho ambiwa na polisi.
Polisi wanapaswa kubadilika ktk hili na cdm nao
Wanatakiwa wawe mfano ktk kutii sheria.0ubabe na ushindani hauto tufikisha popote.
 
Acha kulala mika umejifunga kwa maandishi yako mwenyewe, sasa sisi tukusaidie nini wakati maandishi yako ymetaja wewe ni chama gani!

Wewe ni gamba kabisa.
Mbona umeshindwa kujiuliza kwanini watumie silaha kwa watu wasio na silaha!

haingi akilini kuamini kwamba mara zote polisi hawawatendei haki chadema na pia ni ngumu kwa mimi kuamini kwamba chadema wapo sahihi mara zote yaani hawakosei kuna kitu wankipandikiza jamnai tufunguke nilijua mtaniita mimi gamba lakinii huu ndio ukweliambao mimi naudhania
 
Haki inaambatana na wajibu mkuu na hakuna uhuru usio na mipaka

Kazi ya polisi haiishii kupokea taarifa tu na kuleta ulinzi, ni lazima pia waangalie hali halisi ya kiusalama inaruhusu hicho kinachotakiwa kufanyika kifanyike
Sasa kama polisi wataona kunasababu za msingi hicho kilichotaarifiwa kufanyka kitasababisha kukosekana kwa usalama ambao wao kama chombo cha kazi hiyo wanaona iwapo kikitokea na wakijaribu kizima inaweza kuleta mdhara basi wanawajibu wa kusitisha au kubadili utaratibu

Ingawa maranyingi Polisi wanakuwa wanatoa maamuzi ya kionevu na kibabe dhidi ya CDM lakini pia CDM nao wakati mwingine wawe wanaangalia pia, maana kuwashawishi tu watu kufanya kitu ambacho kinapelekea vifo na pengine kupeleke kukipa umaarufu zaidi chama tu sio busara nzuri pia

Na most of time ni maandamano/matembezi ndio yanaleta tabu na si mikutano
Naamini wanaweza kabisa kufanya mikutano yao vizuri na wananchi wakawasikia na kuwaelewa bila kuanza kuandamana mabarabarani

Umejaribu kutoa hoja lakini umekwama kuuangalia ukweli.
Unakumbuka matukio ya Arusha ??
Baada ya watu wawili kuuawa Arusha, mikutano na maandamano yote ya Chadema yaliofuata baada ya pale hayakuwa na ulinzi wala vibali vya polisi.
Sasa niambie, au angalia kumbukumbu za matukio ili uone kama kulitokea vifo na vurugu katika mikutano na maandamano hayo!!
Unafiki na woga na kujipendekeza kwa watawala dahalimu hakutatufikisha popote.
 
CCM wamewahi kuzuiliwa hata siku wakitaka kufanya mikutano yao??mwanzisha thread kajipange upya usitake kuleta ngebe bana....

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
wewe kuna amri ipi ilitolewa???washenzi kama wewe,mbona fiesta na chaguzi zenu zinaendelea???zenyewe hazihusiani na sensa.
lenye mwanzo mbaya mwisho wake huwa mbaya kama ccm ilivyo.

Uchaguzi ni mkutano wa ndani. Imezuiliwa ya hadhara.
 
Mndengeleko, Sensa haizuii kazi na shughuli nyingine za kimaendeleo kuendelea. Ndio maana chaguzi ndni ya CCm zinaendelea katika kipindi hiki cha sensa. Acha unazi
 
mi nadhani wote wana makosa, cdm na polisi.
Polisi wanatumia nguvu kupita kiasi tena hata isipo stahili lkn cdm nao wamekuwa wakaidi maranyingi kutii wanacho ambiwa na polisi.
Polisi wanapaswa kubadilika ktk hili na cdm nao
Wanatakiwa wawe mfano ktk kutii sheria.0ubabe na ushindani hauto tufikisha popote.
nakubaliana na wewe asimia mia kwamba policcm na cdm wana makosa,lakini natofautiana na wewe kwa aina ya makosa kwa asimia zote!
kwanza polisi wanatumia silaha walizo nazo kwa upole sana na wanawaogopa viongozi wakubwa wa cdm badala yake wanawalenga (shoot) wanananchi wa kawaida na ambao hawahusiki moja kwa moja na wengine wako katika kazi zao tu za kujipatia riziki kihali au wapita njia. Pili polisi hawavai magwanda ya ccm iliwajulikane wazi bali wanajidai polisi kumbe ni ccm in command.
cdm wao hawajui adui yao maskini! wanadhani jeshi la polisi,mahakama jwtz,tbc,usalama wa baadhi ya viongozi wa dini nk wanatumiwa kotekote na ccm kumbe hao wote ndio ccm yenyewe! fikiria unapigana na adui usie mjua, what a mistake!kutokana na kutojua aina ya adui wanaepigana nae ,matokeo yake wanatumia nguvu isiyolingana na uwezo wa adui matokeo yake yatakuwa kama ya watangulizi wake yaani akina nccr,cuf nk. mimi sio chadema ila nikiri nami kuna kipindi nilikuwa na mawazo kama yao,hivyo nikawa nawasapoti lakini nilipojua ukweli nikawaambia hawakunielewa nikaachana nao.mfano leo asubuhi nililipoti ofisi iliyo karibu kuripoti nikiwa full ngwamba tayari kwa kazi,jamaa wananiambia tusubiri viongozi wakuu watatoa tamko!nikaondoka kwa hasira,nikaenda ofisi za ccm ofisi ya kata tu nikakuta jamaa wanapanga mipango ya kazi wakati cdm ngazi ya mkoa wao wanahadithiana na kulaani yalitotokea!
 
Nafikiri ukisoma juu, jamaa wengi wamekujibu na vizuri tu. Sina haja ya kuongeza.

Usemi wako ungelikuwa sawa kwa POLISI wa kweli ila siyo hawa wa Tanzania.

Vinginevyo, naona tupo MTUMBWI mmoja. Kesho hawa POLISI wanaweza kukuuwa wewe au mie kwa BAHATI mbaya tu kwa sababu ulikuwa/nilikuwa kwenye WRONG PLACE at the right time. Hawahitaji sana sababu ya maana ya kukuuwa. Si lazima kama wewe unavyodai hadi uwe kwenye Mkutano au maandamano ya Chadema. Inaweza hata kuwa umeenda kumtembelea COUSIN wako wa kike na jamaa linadhani umelichukulia Girlfriend wake, linakuuwa.
He pumguza jazba mr perfect unayekula baada ya kupiga mswaki,
Sipo hapa kutetea polisi mkuu wala kuhalalisha mauaji yao

Pitia tena bandiko lako na nilichokijubu naamini utanielewa
 
kama kuwafanya watu wagomee amri yya polisi ndio kilaza basi nitaendelea kuwa kilaza maishani mwangu mwote sio mara zote polisi wankuwa wrong kwani chadema wangewapa polisi angalau siku 3 au 4 then waendelee na mikutano yao haya yote yangetokea tatizo tunacheza na maisha ya watu mbona hujawahi kusikia kiongozi mkubwa hata m1 amejeruhiwa ktk maandamano ukiacha mchumba wa dr slaa kule arusha cha kwanza cha kupima ni kuangalia kweli hawa viongozi wana nia na dhati na kuendeleza maisha yetu kama ndio basi tujisacrifice kwa ajili yao lakini kama la basi tujipime upya na kwa taariifa yenu mnaniita mimi gamba mimi hata sio gamba ingawa nilikuwa sitaki kusema sasa inanibidi niseme ingawaje kura ni siri ya mtu but 2010 kura nilimpigia mnyika ya ubbunge pamoja na diwani wakata ya temboni coz mimi nakaa mbezi temboni lakini pia matokeo ya mnyika yalivyokuwa yantaka kuchakkachuliwa nilikesha nae pale kwa angalau siku 1 sasa vipi unaniita mimi gamba.
 
Wakati Chadema wakipigwa na kuuliwa kwa kufanya kikao huko Iringa, CCM wamefanya ufunguzi wa kampeni huko Zenji na makamu wa Rais alikuwepo kumnadi Mgombea.

Sasa wewe mtani wangu Mdengereko, ukiitwa KILAZA huoni ni WAJIBU wa kila Mtanzania mtaka mabadiliko?

Jana Zanzibar....
03.jpg



Soma hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/317621-ccm-yaenda-kinyume-na-marufuku-ya-polisi.html
 
Back
Top Bottom