Wazo la CDM kuanzisha TV na Radio mapema kabla ya Mwishoni mwa 2013!!

Not_Yet_Uhuru

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,304
431
Wadau na wapenda mabadiliko ya kifikra, kisiasa na kijamii!

Ni Wazo muafaka sana kwa sasa CHADEMA kuanzisha vyombo vyake rasmi vya Habari ikiwa ni pamoja na TV, Radio na Magazeti. Wazo hili limekuwa hamasa sana na linaungwa mkono na kila watu 8 kati ya 10 unaokutana nao na kuwauliza umuhimu wa CDM kuwa na chombo chake rasmi cha habari kinachoweza kuwafikia wananchi kwa asilimia kubwa popote Tanzania. Wengi wanasema CDM inasubiri nini? Au hadi Mafisadi wapeleke muswada kuondoa uhuru wa Vyama vya Siasa kumiliki vyombo vyao vya habari? Chama cha Mafisadi kimejiwekea mbinu zao za propaganda ikiwapo Radio-feki, magazeti-ya kufungia vitumbua nk....lakini wameishia kuchakachua haki za umma na kufisadi hata kujichakachua kwa siasa na kura za wao kwa wao! Sasa wanaelekea kule Baba wa Taifa alipokwishawatabiria!

Wadau, katika kulikomboa taifa, lazima tukubaliane kuwa gharama, kutoka jasho na kujitolea ni sehemu ya ukombozi, hasa kwa nchi ambayo imedhoofishwa na mafisadi kama taifa la Tanzania. CDM inayo nguvu ya umma na hakuna woga hata chembe ktk kuijengea umma ukurasa na jukwaa jipya la habari sahihi na siasa sahihi kwa ukombozi wa umma!!

Ili ukombozi uwafikie wananchi wote na waelewe kwa nini wao ni masikini kwa Miaka zaidi ya 50 toka wapate uhuru, na kwanini wamebaki dhaifu na kwa nini wanahitaji haraka kujenga fikra sahihi, na ni kwanini wachague siasa sahihi (waachane na maji-taka) na wapate maendeleo ya kijamii, suala la HABARI NI NGUVU KAMILIFU. "Information is Power" na hakuna wa kuibadili kauli na ukweli huo.

Maisha ya taifa hili kwa jinsi yaliyotokomea mifukoni mwa wajanja na mafisadi wachache, ni muhimu sana wapate habari, kwa haraka, mapema na zisizokuwa na ukandamizaji, na kujengewa woga. Tukumbuke kuwa, Mifumo ya mitandao kama Internet, e-mails nk kwa sasa inawafikia wachache sana na hasa waliojikusanya mijini. Ni wananchi wachache mno wanaoweza kupata habari za kweli kupitia Radio, TV na magazeti ya binafsi yasio na mlengo wowote wa kiitikadi, na hasa masikini waliojaa vijijini, ambao ndio wamebaki kuwa chambo na kuvikwa minyororo ya mateso na kitanzi na Chama cha Mafisadi ili kujichukulia na kujinufaisha kwa hali zao na kuwaangamiza watanzania kwa kuwaibia kura na kuwajengea woga wasiweze kujitetea, wazidi kutokujiamini ili kuwaibia rasilimali zao. Mwisho ndio sasa!!

HAKIKA, Sasa ni wakati muafaka kwa CDM kutangaza mkakati rasmi wa kuanzisha Vyombo vyake rasmi vya mawasiliano ikiwapo TV, Radio na Magazeti ili kukamilisha harakati za ukombozi wa Taifa ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya uraia, Katiba, na siasa safi kwa ajili ya kulinusuru taifa hili linaloangamia kwa kasi. CDM itakapotoa Tamko Rasmi kuhusu Mkakati huu, nchi itatikisika kwa jinsi Wananchi kwa mamilioni toka katika Mikoa yote, Wilaya, Majimbo, Kata, Tarafa, Vijiji hadi vitongoji watakavyojitolea kwa hali na mali tayari kwa Michango, kuchangia ufanisi wa ukombozi huu kwa njia zozote zile kama wafanyavyo bila kuchoka ktk masuala ya dini, sherehe nk. Tunaomba CDM itangaze rasmi mkakati huu mapema iwezekanavyo! Wananchi wamejaa HAMASA sana, ili ndani ya 2012 hadi mwishoni mwa 2013, tuwe katika ramani halisi ya kuwapa watanzania walichokikosa miaka yote. Muda ni sasa! MUDA ULIOBAKI KUFIKA 2015 NI MFUPI SANA NA UNAENDA KWA KASI SANA!. Watanzania wanahitaji kwa haraka Habari sahihi na Siasa sahihi na uongozi sahihi kuelekea 2014, MUDA NI MFUPI SANA! Mara ifikapo 2015 kuelekea kupiga kura, Taifa linatakiwa liwe limekomaa hasa! Taifa jipya linaundwa kutokana na Wapiga Kura waliojaa elimu, fikra na Hamasa za ukombozi na maendeleo ya jamii na nchi yao!

NAOMBA KUWASILISHA, tuchanganue na tujadili, TUTOE DIRA...TUSONGE MBELE! Wakati ni sasa!
TUPO PAMOJA....Mungu ibariki Tanzania....!
 
digital tv system inaanza mwisho wa mwaka huu itakuwa very cheap kuanzisha tv ...mfano tv kama sibuka ipo kwenye star times tu...so, its possible, wazo zuri sana
 
Nina wasiwasi FFU watakuwa wanakaa nje ya jengo kusubiri TV inatangaza nini?
 
vipi kuhusu leseni?? watapewa?

hili ni wazo zuri,lakini mbele ya hawa ma.ga.mba tutafanikiwa kweli,kwa kifupi habari ni silaha mhimu sana to the oppressed,sasa ma.ga.mba watapenda kweli kuona wanyonge wakipata silaha mhimu ya namna hii,by the way tusonge mbele ni hatua mhimu sana kwa cdm.
 
CDM? What does this stand for?

It (CDM) stand for CHAMA, DEMOCRASIA, MAENDELEO. Uiulize hiyo bangi yako kama kuna swali lingine la ziada kama hakuna, mpigie mkeo simu ujue alipo asije akawa yuko na Mwigulu za hizi. Nashukuru kwa swali zuri ajabu.
 
It (CDM) stand for CHAMA, DEMOCRASIA, MAENDELEO. Uiulize hiyo bangi yako kama kuna swali lingine la ziada kama hakuna, mpigie mkeo simu ujue alipo asije akawa yuko na Mwigulu za hizi. Nashukuru kwa swali zuri ajabu.

Mtu ameuliza vizuri tu kirefu cha CDM, umemjibu lakini wewe ndiye umetoa jibu ambalo si la mtu mwenye akili timamu bali aliyekula bangi.... si wote wanaojua CDM inasimama badala ya maneno gani bhana!
 
Mtu ameuliza vizuri tu kirefu cha CDM, umemjibu lakini wewe ndiye umetoa jibu ambalo si la mtu mwenye akili timamu bali aliyekula bangi.... si wote wanaojua CDM inasimama badala ya maneno gani bhana!

ni kichaa tu kama wewe ndo hajui CDM inasimama badala ya nini..na hata kama alikua hajui thread yenyewe inaonesha kua anaposema CDM anamaansha nin..
 
kweli kabisa hii itasaidia sn kutoa elimu kwa jamii na kudidimiza upotoshaji wa magamba
 
Big up mkuu, ni wazo zuri kwa chachu ya maendeleo ya nchi yetu. Naamini Dr. atalifanyia kazi haraka iwezekanavyo. Nashauri hivyo vyombo vya habari viwe na uwezo mkubwa wa kutufikia sisi wa vijijini, na wale walio nje ya nchi waweze pia kupata habari. Naamini nguvu ipo na uwezo upo hata kama kutakuwepo na ugumu kutoka kwa washawasha hawa.....ila mwishowe itafanikiwa....

Penye nia pana njia na hizi ni dalili njema za washawasha kupotea......
 
Back
Top Bottom