Wazo kwa waTanzania wote

mstahiki

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
308
5
Imedhihirika kwamba Viongozi waTanzania nchi imewashinda...Mnaonaje tukaingia mkataba na nchi moja ya Magharibi iliofanikiwa kiuchumi kuendesha nchi yetu kwa miaka 100 ili kuboresha Maisha ya Mtanzania..Miaka 100 ya kujenga mabarabara,shule,hospitali na mengine muhimu...na wao wawe na full control ya kila kitu..vipi wadau mnaonaje hio?
 
Sikubali: Kwanini usiende huko ili mimi nibaki na TZ yangu? Kwanini usisema tuwafukuze wote? Ishi yaani wanibinafisishe? Wewe vipi?
 
Mimi naona bora tuiuze tu kila mtu apate chake na sio kila siku RA, RA, EL
 
Bora Mkoloni??

Reunion wamekataa uhuru na wapo china ya Wafaransa hadi leo! Na kwao ni poa masha yao poa kuliko Comoro ambao walidai uhuru!
 
Na unadhani hao utakaoingia nao mkataba watafanya hivyo ambavyo sisi vinatushinda?
 
Wanaingia mikataba ya hovyo ya kufua umeme na kuchimba madini ambayo baada ya kuisaini tunakuwa hatuna tena uwezo wa kuifuta au kuisitisha. Je, wakiingia mkataba wa kuibinafsisha nchi una uhakika gani kuwa baada ya miaka 100, hata kama hayo maendeleo yatakuwa yamepatikana, tutakuwa na uwezo wa kuirudisha nchi mikononi mwetu? Upunguani unaotufanya tushindwe kuendesha nchi ndiyo huo huo utakaotufanya tushindwe hata kuidai tena nchi yetu. Wewe kama unataka kurudi nyuma ya mwaka 1961 rudi mwenyewe sisi tutapambana na mafisadi wetu. Swali? hivi wewe binafsi umefanya nini kukabiliana na changamoto za matatizo?
 
Imedhihirika kwamba Viongozi waTanzania nchi imewashinda...Mnaonaje tukaingia mkataba na nchi moja ya Magharibi iliofanikiwa kiuchumi kuendesha nchi yetu kwa miaka 100 ili kuboresha Maisha ya Mtanzania..Miaka 100 ya kujenga mabarabara,shule,hospitali na mengine muhimu...na wao wawe na full control ya kila kitu..vipi wadau mnaonaje hio?
hebu chukulia kuwa umeoa halafu mkeo mkahitilafiana, je suluhisho ni kumtafuta mume bora umkabidhi mkeo mpaka atakapotengemaa kitabia? fikiri kabla ndugu yangu.... (kwa ufupi hautapata kura yangu ng'o)
Sikubali: Kwanini usiende huko ili mimi nibaki na TZ yangu? Kwanini usisema tuwafukuze wote? Ishi yaani wanibinafisishe? Wewe vipi?
well said nakuunga mkono mkuu
Mimi naona bora tuiuze tu kila mtu apate chake na sio kila siku RA, RA, EL
unaichukulia serius ile kauli ya kwamba mali zilizomo humu nchini ni urithi wa taifa? na warithi ndo sisi? well ni kwamba ukishauza nyumba yako uliyojenga na kuishi bila maandalizi ya uendako basi hiyo ndo akili tata, au mwenzetu umejiandaa kutimkia bara lipi? au utaenda kuishi kenya?
Wanaingia mikataba ya hovyo ya kufua umeme na kuchimba madini ambayo baada ya kuisaini tunakuwa hatuna tena uwezo wa kuifuta au kuisitisha. Je, wakiingia mkataba wa kuibinafsisha nchi una uhakika gani kuwa baada ya miaka 100, hata kama hayo maendeleo yatakuwa yamepatikana, tutakuwa na uwezo wa kuirudisha nchi mikononi mwetu? Upunguani unaotufanya tushindwe kuendesha nchi ndiyo huo huo utakaotufanya tushindwe hata kuidai tena nchi yetu. Wewe kama unataka kurudi nyuma ya mwaka 1961 rudi mwenyewe sisi tutapambana na mafisadi wetu. Swali? hivi wewe binafsi umefanya nini kukabiliana na changamoto za matatizo?

...the question is Mr. Ruge umefanya nini binafsi kukabiliana na changamoto za matatizo?
 
Wanajamii wote nawasalimu, hii ni mara yangu ya kwanza kuchangia mada.

Sijawahi kuona wazo lilizosahihi kama hili, kwa kweli batanzanie ni vyema tukaingia contract hii muhimu maana hakuna hata kiongozi mmoja wa juu au grassroot asiekua corrupt basi, ni kwamba haruna silika ya uongozi hivyo tuingie contract na wenye uwezo.

Au waangaliwe wali walioweza kuendesha makampuni yao kwa ufasaha yakafanikiwa na yasiona hao vigogo ndani yake ndio wawe wasaidizi wa hao tutakaoingianao mkataba.

Kwakweli ni wazo la juu sana sana sana
 
Imedhihirika kwamba Viongozi waTanzania nchi imewashinda...Mnaonaje tukaingia mkataba na nchi moja ya Magharibi iliofanikiwa kiuchumi kuendesha nchi yetu kwa miaka 100 ili kuboresha Maisha ya Mtanzania..Miaka 100 ya kujenga mabarabara,shule,hospitali na mengine muhimu...na wao wawe na full control ya kila kitu..vipi wadau mnaonaje hio?

Mstahiki salam ,
JE umeshawahi kuishi angalau miaka MIWILI katika moja ya nchi ya magharibi unayodhani imefanikiwa kiuchumi???? nitachangia zaidi baada ya jibu lako.
 
Miaka mia ni mingi sana..watatupekecha..tuwape vipindi vifupi vifupi ili tuweze kuwafanyia assesment/performace appraisal...
 
Back
Top Bottom