Waziri wa Ulinzi Cyprus ajiuzuru - mlipuko wa mabomu kama Go/mboto, Mbagala

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,886
6,883
Waziri wa ulinzi wa Cyprus amejiuzuru kutokana na scandoo ya mabomu kulipuga kutoka ghala la silaha la jeshi na kusababisha hasara kubwa. Taarifa ya habari za kimataifa kutoka CNN, zinasema ni kitu kisichovumilika katika utendaji na uwajibikaji wa kiongozi ha hivyo kulazimika kujiuzuru.

Serikali ya Tanzania licha ya kutokea zaidi ya mara moja lakini hakuna kujiuzuru na wala kuonywa na viongozi wa juu hasa waziri mhusika Husein Mwingi akitangaza kwamba hana kosa na hajiuzuru. Hii ni aibu sana kwa utendaji wa serikali nchini mwetu. Je serikali inajifunza nini kutoka kwa hawa wenzetu wanavyowajibika>
 
wa hapa ni mwana wa mfalme aliyepita labda huyo wa "bold" ni mtoto wa mkulima wa mpunga
ali

Ndo maana yake.

Lakini tukio la awali aliuambia umma wa watanzania kwamba kosa lile halitatokea tena, na lilipotokea tena kilikuwa na kielelezo dhahiri cha uzembe wa hali ya juu na kutowajibika kwake.
 
na wahapa atajiuzuru 20115 usihofu kwani bado uchunguzi unaendelea, au wewe umesha sikia report ya tume iliyoundwa? kama hujasikia jua kuwa bado tume inaendelea na kazi yake ikikamilika na yeye atajiuzuru
 
Waziri wa ulinzi wa Cyprus amejiuzuru kutokana na scandoo ya mabomu kulipuga kutoka ghala la silaha la jeshi na kusababisha hasara kubwa. Taarifa ya habari za kimataifa kutoka CNN, zinasema ni kitu kisichovumilika katika utendaji na uwajibikaji wa kiongozi ha hivyo kulazimika kujiuzuru.Serikali ya Tanzania licha ya kutokea zaidi ya mara moja lakini hakuna kujiuzuru na wala kuonywa na viongozi wa juu hasa waziri mhusika Husein Mwingi akitangaza kwamba hana kosa na hajiuzuru. Hii ni aibu sana kwa utendaji wa serikali nchini mwetu. Je serikali inajifunza nini kutoka kwa hawa wenzetu wanavyowajibika>
Kujiuzulu ni ukomavu wa kiongozi, huyu wakwetu hapa hajakomaa na hata hiyo nafasi aliyonayo sio saizi yake kwahiyo asitarajie kuipata ya ukuu wa kaya
 
Waziri wa ulinzi wa Cyprus amejiuzuru kutokana na scandoo ya mabomu kulipuga kutoka ghala la silaha la jeshi na kusababisha hasara kubwa. Taarifa ya habari za kimataifa kutoka CNN, zinasema ni kitu kisichovumilika katika utendaji na uwajibikaji wa kiongozi ha hivyo kulazimika kujiuzuru.

Serikali ya Tanzania licha ya kutokea zaidi ya mara moja lakini hakuna kujiuzuru na wala kuonywa na viongozi wa juu hasa waziri mhusika Husein Mwingi akitangaza kwamba hana kosa na hajiuzuru. Hii ni aibu sana kwa utendaji wa serikali nchini mwetu. Je serikali inajifunza nini kutoka kwa hawa wenzetu wanavyowajibika>

Mkuu unategemea Serikali ya magamba ijifunze chochote kutoka nchi nyingine? Angalia hii issue ya umeme, nchi nyingine Ngeleja angeshatimuliwa miaka mingi sana lakini bado anapeta. Huyo Hussein Mwinyi naye hali kadhalika. Mkullo mwaka jana katengeneza bajeti ya Serikali kwa miezi 12 kumbe ilikuwa ya miezi 6 tu!! January mwaka huu wakaanza kupitisha kibakuli chao cha kuomba omba kwa Wafadhili. Kwa Serikali ambayo sio taahira hawa wote wangefukuzwa kazi muda mrefu lakini si kwa Serikali ya magamba.
 
Kujiuzulu ni ukomavu wa kiongozi, huyu wakwetu hapa hajakomaa na hata hiyo nafasi aliyonayo sio saizi yake kwahiyo asitarajie kuipata ya ukuu wa kaya

Mwajiri wake mkuu aliyempa cheo hicho kwa malipo ya kukirimiwa atakwambia ajipime mwenyewe na aamue kujiuzuru kwa hiari yake
 
Da aisee wee unauliza makubwa sana....waziri ajiuzulu kutokana na vile vijibomu, vilivyoua dazeni kadhaa ya watu? Si unakumbuka mkuu wa kambi alisema lakini hakuna mwanajeshi aliyepoteza maisha; hiyo imewatosha kabisa. Lini uliona mwananchi wa kawaida akathaminiwa hapa kwetu?
Unathubutu kuulizia uwajibikaji wa waziri wa nishati? Muheshimiwa yule yule aliyesinzia pembeni mwa mkuu wa nchi wakati wa mkutano nje nchi? Si mwenyewe alishamuona anasinzia kazini na akaridhika naye? sasa wewe unahoji nini hapo? Tumempa nchi iwe kama banda lake la uani, afanye atakavyo. Kwa hiyo sisi tunyamaze tu, muda wake utakwisha, ataondoka, atakuja mwengine, atafanya yaleyale, hadi hapo tutakapoamka na kuanza kuwawajibisha viongozi. Mpaka hapo kukikucha, ila sasa hivi tuwaache tu wajilie nchi yao hii.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom