Waziri wa ujenzi Dr.P.Magufuli apiga marufuku matuta kwenye highway

matuta mengine ni Upuuzi mtupu kama pale mwananyamala mita 20 tuta hiyo sio haki ni kuongeza foleni na na kuaribu magari , badal ya hizo hela kutengezeza mifreji wao wanongeze matuta Mkurugenzi wa jiji kwa matuta ya mwananyamala anaonekana shule hakuna hata saizi ya magari hajui gari dogo mpaka upinde mara tano ndio unapanda, njoo pale Bunju a magari yanapita 180,000 pamoja na pale boko, badala yake wanapita pembeni kunaanza kubomoka
 
mimi binafsi nampongeza waziri magufuli, ni mchapakazi hodari. keep it up minister.kweli matuta mengi kupita kiasi kwenye barabara kuu yanaudhi sana, actually mengi yanasababisha ajali kwani ni marefu sana na pia hayana warning signs zozote. unatakiwa uwe mzoefu wa barabara husika kujua tuta liko wapi lakini kwa dreva mgeni unashtukia tuta liko mbele yako ghafla na katika kufunga breki u end up kusababisha ajali.
 
Futa matuta yoote inawezekana, waweke alama za barabarani za kutosha, kuwe na faini nzito kwa wavunjaji wa sheria za baranbara. Wananchi wanatakiwa kujua kuwa ile ni highway, mabalozi na watendaji wafanye kazi ya kuwaelimisha.

Pia ujenzi wa highway uwe mbali na kijiji na watu wakatazwe kutembea au hata kupita na baskeli.
 
Hapa na mimi namuunga mkono 100% matuta ni kero kubwa sana

Hivi kwa waliotumia hii bara bara ya chalinze segera, Km 125 za kwanza from chalinze zina matuta ya kufa mtu, hadi kero.....na ndo wamefanya upanuzi wa barabara! waanze nayo hayo
 
Back
Top Bottom