Waziri Wa Polisi Aibiwa Gari

SASA huyu ustaadh aliyeibiwa hakuna simu poa wenye makao makuu yao pale CCM BAR ..zenj asiyemfahamu..akifika huwa wanamshangilia kwa kuwa wanakuwa wana uhakika...lakini hata hivyo jamaa ni mtu asiyekuwa na makuu wala majivuno..ni jk style!!..ila kama wazanzibar wana jidanganya hawaongozwi au hawataongozwa na mlevi wanajidanganya [except for mzee mwinyi,jumbe and wakil..]

Kamanda hapo chumvi umezidisha, Mkuu huyo CCM Maisara sio baraza
yake...
 
GARI la Naibu Waziri wa Usalama wa Raia MOHAMED ABOUD Mohamed, lenye alama, NW-UR,aina ya GX, limeibiwa na dereva wake aitwaye Tumaini Mbaga, ametoweka tokea Jumamosi iliyopita.

Hii imekaa kama tangazo vile? Kwa mwenye information kitita bei gani? Ihope there is that best part....zawadi NONO
 
Gari la waziri wa mapolisi laibwa

.Dereva naye kapotea
.Msako mkali waanza


MWANDISHI WETU
Dar es Salaam


GARI la serikali aina ya Land Cruiser GX analotumia Naibu Waziri wa Usalama wa Raia, Mohamed Aboud Mohamed, limeibwa na dereva wake, Tumaini Mbaga amepotea.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na polisi zinaeleza kwamba, kwa mara ya mwisho dereva wa gari hilo lenye rangi ya bluu alikuwa kazini Jumamosi iliyopita na hajaonekana tena hadi jana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jamal Rwambow, alithibitisha kutokea kwa gari hilo ambalo limesajiliwa kwa namba STK 2523 na kwamba polisi wanaendelea kulitafuta.

Rwambow alisema dereva wa gari hilo aliachana na Naibu Waziri Jumamosi iliyopita saa sita mchana hadi alipotafutwa tena kikazi juzi Jumatatu.

Kwa mujibu wa habari hizo, naibu waziri huyo alielekea Zanzibar mwishoni mwa wiki na kwamba hapakuwa na mahitaji yoyote ya gari hilo hadi juzi aliporejea Dar es Salaam na kukosa mawasiliano na dereva wake.

Tayari polisi wameanza upelelezi kujua liliko gari hilo linalotumia namba za NW-UR na kuna hofu ya kuwapo uwezekano wa dereva wake kutekwa ama kuuawa.

Rwambow alisema mke wa dereva huyo alipokea ujumbe wa simu ya mkononi kutoka katika simu ya mume wake (Tumaini) ikieleza kwamba amepata safari ya dharura kwenda Dodoma kikazi alikoitwa na bosi wake na kwamba angerejea siku inayofuata lakini hadi jana hakuwa amerejea nyumbani kwake Kimara.

Dereva huyo anaelezwa kuwa na kawaida ya kuegesha gari lake katika maegesho ya CCM Kimara, Dar es Salaam ambako hajaonekana tangu Jumamosi alipoondoka.

Jeshi la Polisi Tanzania liko chini ya Wizara ya Usalama wa Raia na tukio hilo limeelezwa kuwatikisa maofisa wa Polisi ambao wamekuwa wakihaha kutafuta wahusika.

Aboud aliithibitishia KULIKONI kuhusu kutokea kwa tukio hilo, lakini hakupenda kuingia undani kwa maelezo kwamba taarifa rasmi zitatolewa na Polisi ambao wako katika harakati za kuwatafuta wahusika na kuandaa taarifa.

"Polisi wamo katika upelelezi na kuwatafuta na RPC atatoa taarifa rasmi kwa sababu sio vyema kila mtu akatoa taarifa kwa sasa," alisema Aboud.

Hata hivyo, Aboud alisema pamoja na kuwa binadamu wanaweza kubadilika, dereva wake alikuwa mwenye maadili mema na hajawahi kuwa na mashaka naye hata mara moja.

"Tumaini sio mlevi na hana tabia za ajabu ajabu kwani mara kwa mara hata funguo za nyumbani kwangu huwa namwachia anakwenda kuwasimamia wanaofanya usafi tunaposafiri na hajawahi kufanya jambo baya hata mara moja. Lakini kwa kuwa hatujui tusubiri polisi," alisema Aboud.

Hili ni tukio la kwanza la aina yake kutokea mwaka huu ndani ya wizara ambayo husimamia polisi katika kipindi ambacho serikali imepata mafanikio makubwa katika kupambana na majambazi na uhalifu mwingine.

Source: Kulikoni Na.234, JANUARI 23, 2008
 
Kamanda hapo chumvi umezidisha, Mkuu huyo CCM Maisara sio baraza
yake...


kaka inaeleweka kuwa ccm maisara si kijiwe cha mshkaji..ILA NIMESEMA KUWA NDIO KIJIWE CHA SIMU POA UNGUJA....UKIKOSA KOOTE NENDA PALE ..HATA ULE MWEZI...,NA HATA KAMA SI MASKANI YAKE ..HAKUNA AL WATTAN UNGUJA ASIYEFIKA PALE JAPO KUSABAHI....ILA KUNA WENYE KIJIWE HIKI ...SIMU POA NA "NDUGU ZETU WALE" WAKIWA MOJA YA WAGENI MAARUFU BARZA LILE....

YULE SERENGETI YAKE YA MOTOOO ..HUPENDELEA ..
 
ila kama wazanzibar wana jidanganya hawaongozwi au hawataongozwa na mlevi wanajidanganya [except for mzee mwinyi,jumbe and wakil..]

Hivi PhM unataka kuniambia Mhd Aboud atakua Rais wa SMZ? Maana niliwahi kusikia mahali kwamba anaandaliwa kwa kuwa yeye ni Mpemba na pia ana asili ya Kiarabu kwa hiyo rangi rangi yake atawamudu CUF katika uchaguzi mkuu ujao
 
hadi dereva apatikane ndio itajulikana kama katoweka nalo au katekwa, hawa polisi wababaishaji hawako competancy kwenye statement zao ndio maana wakikamata watu na bangi au madawa wanajua bei yake kivipiiiiiii!!!!
 
Hivi PhM unataka kuniambia Mhd Aboud atakua Rais wa SMZ? Maana niliwahi kusikia mahali kwamba anaandaliwa kwa kuwa yeye ni Mpemba na pia ana asili ya Kiarabu kwa hiyo rangi rangi yake atawamudu CUF katika uchaguzi mkuu ujao

kumekuwa na hisia ya jk kuwa na lengo la kumjenga SEIF SHARIFF mpya visiwani....anajaribu,...hii itasaidia kuondoa tension iwapo seif mpya atatoka ccm..na hii itawezekana pale tu ccm itakapokubali kumsimamisha mgombea urais zanzibar kutoka pemba[lazima atashinda]...hapo tention ya wapemba itapungua ...na upinzani utapungua ..demokrasia itastawi visiwani...

maana you know hata seif alitofautiana na wenzake baada ya kunyimwa fursa ya kugombea urais..pamoja na kujikomba kwa mwalimu na kumfunulia siri za wachafuzi wa hali ya hewa....

kinachofanyika zanzibar ni kama kenya ambako wakikuyu wanaamini rais bora lazima awe mkikuyu...
 
Duh!!! Hii ngoma bado nzito sasa . Inahama kwenye wizi wa gari inaenda kwenda kwenye kugombea? Aboud hana akili ya Urais nimemsikia akitoa speech zake pale Arusha ni mtupu sana .
 
hadi dereva apatikane ndio itajulikana kama katoweka nalo au katekwa, hawa polisi wababaishaji hawako competancy kwenye statement zao ndio maana wakikamata watu na bangi au madawa wanajua bei yake kivipiiiiiii!!!!

Ngomanzito karibu jamvini
 
Guys Check new development of this story tunaweza kuchangia. Hawa jamaa hawako serious na maisha ya watu !!!

Polisi wahusishwa mauaji ya dereva wa Naibu Waziri




na Happiness Katabazi



JESHI la Polisi nchini linawashikilia watu wanne wakiwemo askari polisi wawili kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa dereva wa Naibu Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Usalama wa Raia, Tumaini Mbaga.
Vyanzo vya habari vya uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi viliiambia Tanzania Daima kwa nyakati tofauti kuwa, wengine wanaoshikiliwa kuhusiana na tuhuma hizo ni raia wawili ambao hawakuweza kuthibitisha iwapo ni watumishi wa serikali ama la.

Habari hizo zinaeleza kuwa, watu hao walikamatwa mapema wiki hii na wanaendelea kushikiliwa na jeshi hilo kwa siri.

"Jeshi limewakamata watu hao mapema wiki hii na linaendelea kuwashikilia kwa mahojiano zaidi, lakini hata hivyo baadhi ya maofisa waandamizi wa jeshi letu wanajitahidi kuendesha jambo hili kwa siri," kilisema chanzo chetu cha habari.

Habari hizo zilieleza kuwa chanzo cha mauaji ya dereva huyo ni wivu wa baadhi ya polisi ambao inadaiwa walikuwa wakichukizwa na aliyekuwa Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mohamed Aboud, kuendeshwa na dereva ambaye si polisi.

"Inasemekana baadhi ya madereva wa polisi walikuwa wakikerwa na dereva raia kumwendesha naibu waziri wakati madereva wa Jeshi la Polisi wapo," kilieleza chanzo hicho.

Taarifa za kukamatwa kwa watu hao zililifikia gazeti hili mwanzoni mwa wiki hii na tayari habari zimeanza kuenea mitaani.

Chanzo hicho cha habari kilieleza watuhumiwa hao ambao awali walikuwa wakihifadhiwa katika mahabusu ya jeshi hilo iliyopo eneo la Stakishali - Ukonga, lakini sasa wamehamishwa na haijafahamika wako mahabusu gani.

"Mpaka jana watuhumiwa hao walikwishahamishwa kutoka mahabusu hiyo, lakini hatujui ni wapi wamehamishiwa. Wamekuwa wakihojiwa na kikosi maalumu kilicho chini ya Ofisi ya Rais (Task Force), kikosi hiki kinaundwa na vyombo vya ulinzi na usalama kutoka JWTZ, Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa," kilieleza chanzo hicho.

Habari zaidi zinaeleza kuwa askari wanaotuhumiwa katika tukio hilo ni watatu, lakini mmoja alifanikiwa kutoroka baada ya kupata taarifa ya kufichuka kwa siri hiyo.

Miongoni mwa askari waliokamatwa, mmoja anatoka Kituo cha Polisi Msimbazi na mwingine anatoka kitengo cha Upelelezi, Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Mbali na askari hao, pia wapo raia wawili, mmoja wao ni mwanamke ambaye ni raia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), anayeishi Yombo, jijini Dar es Salaam.

Jana gazeti hili lilifanya juhudi za kuzungumza na Mkuu wa Jeshi hilo, IGP Said Mwema, ili kupata ufafanuzi, lakini halikuweza kuzungumza naye, baada ya simu yake ya kiganjani kupokewa na msaidizi wake, ambaye alieleza kuwa IGP alikuwa kwenye majukumu mengine ya kitaifa nje ya Dar es Salaam.

Aidha, gazeti hili lilifanya jitihada za kuzungumza na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, ambaye baada ya kupatikana hakuwa tayari kuthibitisha au kukataa, zaidi ya kulitaka gazeti hili kuwasiliana na Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana kwa ajili ya kupata taarifa za tukio hilo.

Hata hivyo, Kamanda Tibaigana hakuweza kupatikana baada ya simu yake ya mkononi kupokewa na mlinzi wake ambaye aliieleza Tanzania Daima kuwa kamanda huyo alikuwa kwenye kikao ambacho hakufahamu kitamalizika muda gani.

Mwishoni mwa Januari mwaka huu, polisi waliokota mwili wa dereva huyo ukiwa umetenganishwa na kichwa, eneo la Kwembe, ukiwa umeharibika vibaya, ikiwa ni takriban wiki mbili tangu alipotoweka.
 
Our security departments have clearly become sourec of our insecurity. Kweli hii ni hatari, i wonder kama watu watakuwa wanawaamini polisi! Kama kweli hii ilikuwa hivi inakumbusha jinsi askari wa Nduli wa Uganda walivyokuwa wakifanya.
 
Our security departments have clearly become sourec of our insecurity. Kweli hii ni hatari, i wonder kama watu watakuwa wanawaamini polisi! Kama kweli hii ilikuwa hivi inakumbusha jinsi askari wa Nduli wa Uganda walivyokuwa wakifanya.

Jeshi la polisi linapaswa kujisafisha au kusafishwa, matukio ya hivi karibuni yanaonyesha wazi uozo wa polisi tulionao. Angalia kisa cha kuuawa kwa wafanya biashara kutoka Mahenge (ambapo mkuu wa Zombe alihusika), kupigwa hadi kuchomwa visu viongozi wa CHADEMA huko Karatu, kuua dereva wa bossi wao nk. Ni dhahiri kwamba polisi wamepoteza dira, endapo hawawezi kujisafisha (IGP kuchukua hatua za makusudi) basi wasafishwe (Rais achukue hatua stahili, ikiwezekana kupangua ma RPC, ofisi ya DCI, wapelelezi, kitengo cha madawa ya kulevia nk.
 
Back
Top Bottom