Waziri wa Nishati na Madini ajiwekea kitanzi shingoni...

agapetc

Member
Jul 21, 2012
29
4
kutokana na kauli yake bungeni kuwa kukatika kwa umeme itakuwa ni historia katika nchi hii wale mafisadi walioshika mpini wanajipanga kuhakikisha mgao unakuwepo ili kauli yake imfunge.
 
leo umeme umekatika saa kumi usiku sabasana na mpaka sasa saa tisa na dakika 11 badu kurudi' hongera mafisadi!

macinkus
 
Angalau huyu Waziri anaonekana ni mtendaji na sio mwanasiasa kama mawaziri wengine.
 
mleta mada, hakuna fisadi bila anayefisadiwa. Ushindi wa fisadi utategemea unyonge/ujinga wa wanaofisadiwa.
 
huyu bwana ametupa matumaini

tumuombee, tunawahitaji viongozi wa design hii katika nchi yetu. Mungu ampe nguvu na ujasiri na ulinzi na hekima aendelee kutenda yale yanayotarajiwa na watanzania
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nilipenda pale alipomjibu JJ Mnyika kuwa yeye prof sio mwanasiasa kama JJM kwa hiyo anapofanya maamuzi lazima ajiridhishe kwanza ili kutoa haki sawa. Lilikuwa ni swali kwamba baada ya kumshughulikia Exe Dir. Tanesco vipi sasa kuhusu watendaji wake Wizarani?
 
kutokana na kauli yake bungeni kuwa kukatika kwa umeme itakuwa ni historia katika nchi hii wale mafisadi walioshika mpini wanajipanga kuhakikisha mgao unakuwepo ili kauli yake imfunge.

Nadhani hata wewe na wananchi wengine watajua kuwa dhamira ya Prof. ni nzuri ingawa katika kutekeleza kuna vikwazo kama hao unaotaka kuwapa nafasi
 
huyu bwana ametupa matumaini

tumuombee, tunawahitaji viongozi wa design hii katika nchi yetu. Mungu ampe nguvu na ujasiri na ulinzi na hekima aendelee kutenda yale yanayotarajiwa na watanzania

Umeongea kweli mkuu,maana soon na yeye utasikia yupo India kwa matibabu...akirudi huko anakua kavaa kofia na gloves kama mwakiembe
 
huyu bwana ametupa matumaini

tumuombee, tunawahitaji viongozi wa design hii katika nchi yetu. Mungu ampe nguvu na ujasiri na ulinzi na hekima aendelee kutenda yale yanayotarajiwa na watanzania
unadhani kwa system ya nchi yetu anaweza akafurukuta?isije ikawa ni kama kijiko cha sukari baharini
 
Ni kweli Mh.. Muhongo ametoa matumaini, hofu niliyonayo ni kukosa ushirikiano maana huu mtandao wa kuifisadi TANESCO ni mpana na unawahusu wakubwa wengi!
Itafika wakati jamaa atachoka na kubwaga manyanga na ukombozi ndio utakwamia hapo.
 
Unachosema ni kweli kabisa lakini jinsi mafisadi walivyokuwa na nguvu ndani ya Serikali wanaweza kumkolimba au kumbambikia baya lolote lile ili atoswe, pamoja na hayo ni mapema sana kuona huyu ni tumaini katika Wizara ya Madini na Nishati ambayo imejaa madudu ya kutisha ambayo yanaimaliza nchi yetu. Kipindi cha miezi sita ijayo nadhani tutakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kutathmini utendaji wake kama hawajamlambisha vya kumlambisha

huyu bwana ametupa matumaini

tumuombee, tunawahitaji viongozi wa design hii katika nchi yetu. Mungu ampe nguvu na ujasiri na ulinzi na hekima aendelee kutenda yale yanayotarajiwa na watanzania
 
Kuwataja mafisadi na kuwasimamisha kazi bila kuwachukulia hatua za kisheria hakutoshi.ninaimani kuwa ndani ya serekali ya ccm hakuna mwenye ubavu wa kumchukulia mwenzake hatua za kisheria.sana sana watakao chukuliwa hatua za kisheria ni vidagaa tu.na mapapa wataendelea kutesa km kawaida.
 
Ni bora ajiweke kitanzi kwa ajili ya walalahoi ambao tumechoka kuibiwa, hakika Mungu atamuongoza!
 
Back
Top Bottom