Waziri wa Nishati amuumbua Mkono; Asema anamiliki kampuni ya madini Dubai

Hata ukimfuta mkono huna la kumfanya yeye ni tycoon Kama Yule mwamba wa kaskazini lowassa tu

Wewe hujui maana ya Forum hapa tunajadili hoja.

Halafu Mkono sio Tycoon kama unavyojidanganya Tycoon anachukuwa posho bungeni.

Tycoon ni Kazuo Okada, Carlos Slim Helu, Alisher Usmanov, Mikhail Prokhorov...Tanzania hakuna Tycoon.
 
Huyu Mkono toka alivyokuwa analipwa na Balali, BOT mamilioni ya dola nilimfuta kabisa, lakini siku hizi amekuwa kipenzi cha Pro-Chadema JF.

mkuu Ritz, waziri wa nishati alishindwa kujibu hoja ya msingi, je kuna mushkeli katika uuzwaji wa mgodi wa Kiwira?...waziri angejibu kwanza hilo kisha ndio angeendelea na hizo porojo nyingine
 
JUMAMOSI, JUNI 23, 2012 10:50

NA BAKARI KIMWANGA, DODOMA


*Asema anamiliki kampuni ya madini Dubai
*Adai anaishambulia Serikali kwa kunyimwa ‘tenda'
*Mwenyewe, ajibu mapigo, amtaka Waziri afute kauli


WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amejibu mapigo dhidi ya Mbunge wa Musoma Vijijini Nimrod Mkono (CCM).

Amesema kuwa, Mkono aliishambulia Serikali bungeni juzi kuhusu Mgodi wa Makaa wa Kiwira, kwa sababu mbunge huyo ni mmoja wa wamiliki wa kampuni moja ya madini iliyopo Dubai, ambayo iliomba kununua mgodi huo na kunyimwa.

Profesa huyo aliyasema hayo bungeni jana baada ya juzi, Mkono kulitaka Bunge liunde Kamati Teule, ili kuchunguza ufisadi katika mgodi huo.

"Pamoja na hatua zote, jana (juzi), kuna mbunge alizungumzia Mgodi wa Kiwira, siwezi kulizungumzia hilo kwani uchunguzi umebaini kwamba, naye ni mmoja wa wamiliki wa kampuni mojawapo ambayo ina makao yake Dubai, ambayo ilikuwa imeomba kununua mgodi huo.

"Na kwa kuwa mbunge huyo naye ni mwekezaji, siwezi kulizungumzia hili na huenda kuna maslahi na mgongano wa kibiashara katika hili," alisema Profesa Muhongo.

Kauli hiyo ya Profesa Muhongo ilionekana kutomfurahisha Mkono, kwani baada ya waziri huyo kumaliza kuzungumza, aliomba Mwongozo wa Spika na kukiri kuwa anamiliki kampuni ya madini.

"Mheshimiwa Spika ninaomba muongozo wako, hili suala la mimi kuwa mmiliki wa kampuni mbona ‘nili declare Interest' mapema!.

"Kati ya watu ninaowaheshimu sana ni pamoja na mheshimiwa waziri, kwa hiyo naomba afute kauli yake humu humu ndani bungeni," alisema Mkono.

Alipomaliza kusema hayo, Spika wa Bunge Anne Makinda hakumruhusu waziri kuzungumzia alichosema Mkono, kwa kile alichosema kuwa, Profesa Muhongo hakutaja jina la mtu alipokuwa akichangia.

"Hapa Waziri sikumsikia akitaja jina la mtu na hata kama unasema ulilisema jambo hilo, nahisi hukusema wakati wa kuchangia jana (juzi), sasa naomba tuendelee na shughuli za michango ya bajeti," alisema Spika Makinda.

Awali Profesa Muhongo akizungumzia mikakati ya Serikali katika kukamilisha miradi mbalimbali ya umeme nchini, waziri huyo wa Nishati na Madini alisema, hivi sasa wako mbioni kuhakikisha wanatekeleza mradi wa megawati 3000 hadi 5000.

"Nichukue fursa hii kuwataka wananchi wote ambao wamefanya malipo yao kwa jili ya kuunganishiwa umeme, kwamba tayari nimeshatoa agizo kwa TANESCO hadi kufikia Juni 30 mwaka huu, wananchi wote waliofanya malipo wawe wameunganishiwa umeme.

"Endapo TANESCO hawatafanya hivyo, basi nitapambana nao kwa mujibu wa sheria na nawaomba wateja wote wawasiliane nami kwa hatua zaidi pindi watakaposhindwa kuunganishiwa umeme," alisema Profesa Muhongo.

Waziri huyo, alisema pamoja na matatizo yanayozikabili nchi za Afrika, nchi hizo lazima zijipange na kuhakikisha zinaandaa bajeti kulingana na mahitaji yao.

Akizungumza nje ya Bunge jana, Mkono alisema suala hilo si kweli na atahakikisha analiweka sawa, ili kuondoa utata.

"Si kweli kwamba mimi ni mmoja wa wamiliki wa kampuni iliyoomba mgodi huu na hakuna ukweli wowote katika hili na haijatokea mimi kuomba kumiliki mgodi huu," alisema Mkono.

Akichangia mjadala wa bajeti juzi, mbunge huyo wa Musoma Vijijini alisema, mgodi huo wenye thamani ya matrilioni ya shilingi, umeuzwa kwa Dola za Marekani 700,000 (Shbilioni 1.1), kwa kampuni ya Intra Energy ya Australia.

Mgodi huo uliwahi kuzua malalamiko baada ya kumilikishwa kwa Kampuni ya ANBEN Limited, inayomilikiwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa na Waziri wa zamani wa Fedha, Daniel Yona
.
Alichosema Mh. Msigwa kinaonekana dhahiri. Badala ya waziri kujibu hoja kuhusu mgodi wa Kiwira, anazungumzia mtu kunyimwa tenda.
 
Mwandishi hakutoshi? Unaweza kumgoogle ukapata anafanya kazi gazeti gani; kwanini niweke Mwandishi iwe habari

Ya kuchonga?

Sikufikiria hata chembe kama habari niya kuchonga bali nilitoa ushauri katika uboreshaji wake. Anyway, thanks
 
Back
Top Bottom