Waziri wa Mkapa amshukia Kikwete ataka CCM imtose 2010

Mateo qaresi is lost, past and frustated politician...his views are biased...analalamika tu kwasababu yeye yuko nje ya system..alikuwa mzigo na useless figure wakati wote wa utumishi wake..keep quite you losser..

Enjoy your freedom of expression..lakini huna lolote jipya..kwenye maelezo yako JK is better than you and your past comrades by far..get your record right dude...
 
losser

bwa ha ha ha ha
 
Date::12/3/2009Makamba awatukana wanaoshauri Kikwete asigombee 2010
kikweteha.jpg

Rais Kikwete kongamano la Nyerere limemweka katika lawama za kutokuwa na maamuzi na kuwa asipendekezwe kugombea awamu ya pili.

Na Leon Bahati
Mwananchi

KATIBU mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, ambaye katika miezi ya karibuni amekuwa akihaha kutoa ufafanuzi, kukanusha au kujibu tuhuma mbalimbali dhidi ya chama hicho tawala, jana alikuwa na kazi nyingine ya kumtetea Jakaya Kikwete baada ya waziri katika serikali ya awamu ya tatu kushauri asiteuliwe kugombea urais 2010 iwapo atashindwa kufanya maamuzi magumu dhidi ya mafisadi.

Safari hii, Makamba alitumia maneno makali kumjibu waziri huyo, Matheo Qares akisema watu wenye fikra kwamba CCM inaweza kumtosa mwenyekiti wake kwenye mbio za urais wakati wa uchaguzi mkuu wa mwakani, "ni wehu".

Qares, ambaye aliwahi kushika wadhifa nyeti wa Waziri wa Menejimenti ya Utumishi wa Umma, alitoa rai hiyo juzi kwenye kongamano la kumuenzi muasisi wa taifa la Tanzania aliposema kuwa CCM haina budi kutafuta mwanachama mwingine wa kugombea nafasi ya urais mwaka 2010 iwapo Kikwete atashindwa kufanya maamuzi magumu dhidi ya mafisadi, ambao alisema hawakijui chama na wengine uraia wao una utata.

Lakini jana, Makamba alisema watu wenye fikra hizo ni wehu kwa kuwa uteuzi wa wagombea ndani ya CCM ni mchakato usiotoa ruhusa kwa mawazo binafsi ya watu.
"Mtu mwenye akili nzuri hawezi kusema kwamba Rais Kikwete ameshindwa kutekeleza wajibu wake. Anayefikiria hivyo, ni mwehu," alisema Makamba alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu kauli hizo.

Alisema ni vyema watu hao wakafahamu kuwa mgombea urais wa CCM anateuliwa kwa mujibu wa taratibu za chama kupitia vikao mbalimbali hivyo, wazo binafsi halina nafasi.

Alipoulizwa kuhusu shutuma zinazoelekezwa kwa Rais Kikwete, Makamba alisema asingependa kujibu hoja zilizotolewa na mjumbe mmoja mmoja kwenye kongamano hilo.

Lakini akaeleza kwamba yupo tayari kutoa maoni yake binafsi baada ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuwasilisha kwake mapendekezo waliyofikia kwenye kongamano hilo.

"Mimi mwenyewe sikuwepo kwenye kongamano hilo. Wala sijui mapendekezo yao. Siwezi nikatolea maoni hoja za mtu mmoja mmoja alizotoa kwenye Kongamano hilo. Nitakapopata mapendekezo ya jumla ya taasisi hiyo, nitakawa katika nafasi nzuri ya kutoa maoni yangu."

Katika kongamano hilo, Rais Kikwete amekuwa akilaumiwa kwa kutochukua hatua dhidi ya watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi, wengi wao wakielezwa kuwa ni wafanyabiashara ambao wanatuhumiwa kukiteka chama kwa kutumia nguvu zao za pesa.

Wakati fulani Joseph Butiku, mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere ambayo iliandaa kongamano hilo, alisema Rais Kikwete amezungukwa na mafisadi ambao wanaitafuna nchi.

Akizungumza kwenye kongamano hilo juzi, Qares alisema rais hana budi kufumba macho na kuwashughulikia hao watuhumiwa ambao wanadai Kikwete hakujuana nao barabarani na kama atashindwa basi ashauriwe kuwa miaka yake mitano inamtosha.

Kabla ya Qares, Musa Nkangaa, ambaye aliwahi kuwa waziri kwenye serikali ya awamu ya pili, aliituhumu CCM kuwa imepoteza hadhi na kujikuta ikikumbatia matajiri wachafu.

Kwa mujibu wa Nkangaa, CCM imekuwa si chama cha wakulima na wafanyakazi tena, bali kimebaki kuwa chama cha matajiri. "Ndiyo maana imekuwa ikiweweseka kuwashughulikia watuhumiwa wa Richmond na Kagoda," alisema akimaanisha kashfa ya utoaji zabuni ya ufuaji umeme wa dharura kwa Richmond Development Company LLC na tuhuma za wizi wa mabilioni ya fedha kutoka BoT.
 
Mzee wa pombe za bure upo...utakufa na pombe za mbowe mpaka 2015 utakuwa na obesity ya kufa mtu..you dumb!

mimate inakutoka mwenyewe maana maboko haramu hata pombe mnajifanya kuwa hamnywi.

BTW - ule mpango wenu wa kupiga marufuku baa zote za pombe Tanzania kwa vile ni haramu umeishia wapi? Ushauri wa bure tu - kasome shule kwa wakatoliki ili ujue lugha ambayo unajaribu sana kuitumia hapa jamvini (huku ukichapia kaa umechanganyikiwa vile).
 
Hatutapiga tena marufuku baa zote usiwa na hofu utapata vya deso kutoka kwa sponsor wako mpaka 2015 atakapogombea na wewe utakuwa mgombea mwenza ok..

Ushauri wako mpe mbowe maana ame-disco mara mbili shule, wanaweza kumsaidia huko vyeti wanatoa burebure..ok

In between we dumb..kati ya vilaza hapa JF...
 
hizi lugha za madrassa tabu tupu
 
Wengine sisi tulishasema bila woga, toka siku nyingi kwamba Muungwana JK ni kilaza.

Angalia signature yangu hapa chini.
 
Pombe pombe eh next..

Pombe pombe eh next.......... Somalia.
__________________
Ni aibu kwa JF kujadili mambo ya kitaifa..ki-waraka waraka lol.

Kweli ni aibu sana na hasa waraka unapokuwa wa KUIGA original waraka.
BTW. Nasikia ndugu zako Somalia wamelipuana wenyewe kwa wenyewe. Kesho watafanya hivyo Pakistan. Imekaa safi sana hii. Kuna haja ya kuvunja Muungano na wale wote wa siasa kali tunawapeleka Zanzibar na milele wasikanyage bara.
 
qaes kajitahidi,

wangapi wanweza kutamka hayo nani ya ccm. japo alifulia siku nyingi lakini angalau anaonyesha anaweza kubweka akiamua. nimemsoma na nkhangaa yule aliyepata kuwa waziri wa kwanza wa mkapa wa tamisemi.

lakini tujiulize. wote hawa wanajua bahati haiji mara mbili, walipopata madaraka hatukuona wakifanya hayo wanayoita maamuzi magumu (wasitake kutuaminisha kuwa maamuzi magumu hufanywa na rais tu), leo hawana madarak ndio wanaona haja ya hayo maamuzi magumu. tupokee mawazo na changamoto zao, tusikatae kwa kuwa wametoa wao lakini kwa wale walio madarakaniau watakaopatta madaraka, kumbukeni mtatutendea wannchi haki zaidi "mkikumbuka shuka kabla usiku haujaisha"

nawasilisha
Na wewe bana..sasa ulitegemea kwa level yake Nkangaa angefanya maamuzi gani?hapa anazungumziwa rais sio mawaziri...
 
Waziri wa Mkapa amshukia Kikwete ataka CCM imtose 2010

ATAKA CCM IMTOSE 2010 KAMA HAWEZI KUFANYA MAAMUZI MAZITO
"Matajiri hao hawana wala hawajui hata historia ya CCM, wengine kwanza uraia wao una utata ni wageni."

Baada ya kumaliza kutoa mchango wake ulioufanya ukumbi kuzizima, Dk Salim, ambaye alionekana kumudu vema mkutano huo, alisema: "Ndiyo maana ya mkutano huu. Hapa tunapokea maoni ya watu mbalimbali, lakini si lazima yakubalike na wote, wengine wanaweza kupinga au kukubali."

Kama asingekuwa anajulikana kuwa mropokaji hovyo mashuhuri ningejua amesema kwa manufaa ya nchi au chama. Anajulikana Qares kutokuwa makini na kauli zake na ni mchapiaji anayekatisha wengine tamaa. Tutajuaje labda anashauri achaguliwe mtu mwingine kuwa raisi ambaye atampa cheo kikubwa serikalini huku yeye akichapa usingizi bila kufanya kazi? Na wazembe anaowasema ni pamoja na yeye mwenyewe. Amefanya nini alipokuwa mkuu wa mkoa Mbeya ila matusi kwa watu waliokuwa wanaathirika na majanga asilia.

Sijasahau aliposema kwamba wanyakyusa wanajenga nyumba mbovu, eti hata kuku akipiga teke anaweza kuangusha nyumba hizo. Maneno ya punguani hayo. Hakuna Mnyakyusa wa sifa za aina hiyo popote uendapo. Nakubali zipo nyumba ambazo sio bora, lakini not such a generalized statement as such!

Bungeni alikuwa full time anauchapa usingizi wakati wenzake wanakukuruka. Bahati mbaya alikujaumbuliwa na ujio wa TV live show za shughuli za wabunge bungeni ambapo tulimwona kila siku akilala usingizi, pale anapopata nafasi ya kuongea ni pumba tu. Kwa hiyo mafisadi wameanza kuondoloewa, ni pamoja na yeye kunyang'anywa cheo alichoshindwa kukifanyia kazi.

Kikwete atamalizia miaka mitano mingine kama jadi ya CCM, Qares na wenzake wapende ama wasipende. Si mnajua Bongo? Qares alipong'olewa kila cheo ilikuwa ni faraja kwa wengi.

Leka
 
hawa wote walikuwa serikalini na mambo bado yalikuwa mabaya na rushwa ilikuwa kubwa,ni kwa sababu wamenyang'anywa tonge mdomoni sasa wanatapatapa,pia hawa walikuwa against kikwete na hata salim mwenyewe yuko against kikwete kwa namna moja au nyingine ni lazima watamponda kikwete,mbona wao walipokuwa madarakani walikuwa hawataki kukosolewa na wamefanya nini cha maana kwa watanzania?
Mkuu, tatizo sio walikuwa upande upi au wakishika nafasi zipi au mambo yalikuwaje walipokuwa madarakani. Bali tatizo ni hali ilivyo sasa ambayo inafanya watu wengi zaidi kuilaumu serikali na viongozi wake kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao (itashangaza kama wewe huoni kuna tatizo). Hasa majukumu ambayo viongozi wote walikula kiapo kuyatekeleza.

Sheria za nchi haziwezi kuwahukumu watu wachache na wengine kuwa immune nazo. Kama sheria ni msumeno, basi zikate pande zote.

Kila mtu anayo haki ya kukosoa pale anapoona panafaa. Hakuna watu wengi wanaoweza kufurahia kukosolewa au kukashifiwa (hasa wanasiasa). Hivyo, kama wao waliweza kutunyamazisha na kutakubali, labda wao hawakubali kunyamazishwa wanapotaka kusema. Ni uamuzi na haki ya kila mtu kutoa maoni yake, ili mradi maoni/mawazo hayo hayatolewi kwa kuvunja sheria.

Mkuu wao hawana sababu ya kuhofia kumkosoa Mkuu wa nchi kwasababu wanajua hawatapoteza lolote hata kama Mkuu huyo atakasirika/atahuzunika sana. Kwa hiyo hii ndiyo nafasi waliyonayo ambayo si ajabu huko nyuma hawakuwa nayo kwa kuwa walikuwa upande wa wakosolewaji.
 
Mateo qaresi is lost, past and frustated politician...his views are biased...analalamika tu kwasababu yeye yuko nje ya system..alikuwa mzigo na useless figure wakati wote wa utumishi wake..keep quite you losser..

Enjoy your freedom of expression..lakini huna lolote jipya..kwenye maelezo yako JK is better than you and your past comrades by far..get your record right dude...

Mkuu hakuna mtu ambae hayuko biased kwenye jambo/mambo mbalimbali yanayomhusu. Kuwa biased huku ndiko kunakosababisha mtu kufanya uchaguzi wa jinsi ya kutoa kauli, aina ya kauli anazotoa na wapi anapojisikia kuzitoa kauli hizo, kabla ya kuhakikisha kuwa kauli zake zinafanyiwa kazi.

Nimejaribu kuelewa unachomaanisha ukisema analalamika kwa kuwa yuko nje ya system. Uelewa wangu unanifanya nifikirie yafuatayo:
1. Kwamba hakuna tatizo katika uongozi wa nchi, isipokuwa tu akina Quares wanazusha kwa kukosa kupewa madaraka
2. Angekuwa madarakani asingesema aliyoyasema au angetetea uongozi uliopo
3. Alitakiwa kusifia uongozi uliopo na kuutetea kwakuwa nae aliwahi kuwa kiongozi
4. Si ruhusa kwake kusema lolote analoliona kuwa baya kwa kuwa nae alikuwa kiongozi kwenye serikali kama hiyo, na mambo hayakuwa mazuri sana
5. Anatakiwa kuwa mvumilivu kwa serikali na viongozi wake ili kuepusha chama chake na serikali kukosa uaminifu kwa wananchi.
6. Kwakuwa wananchi wanadanganyika kwa urahisi, kwa viongozi wa zamani kusema maovu hadharani kunaharibu heshima ya chama na serikali

Kwa vyovyote vile kama unamaanisha lolote katika hayo hapo juu, ni sawa na kumtaka Mateo Quares kuwa mnafiki na kutetea uzembe, uhalifu na uharamia ambao unafanywa na baadhi ya viongozi katika chama chake na serikali. Ni imani yangu kuwa, kama Quares au mtu mwingine yyote atafuata ushauri kama huo, si tu kwamba hata heshima kidogo aliyokuwa nayo itatoweka, bali pia hatakuwa ametendea wema wale wanaomuamini.
 
Kama asingekuwa anajulikana kuwa mropokaji hovyo mashuhuri ningejua amesema kwa manufaa ya nchi au chama. Anajulikana Qares kutokuwa makini na kauli zake na ni mchapiaji anayekatisha wengine tamaa. Tutajuaje labda anashauri achaguliwe mtu mwingine kuwa raisi ambaye atampa cheo kikubwa serikalini huku yeye akichapa usingizi bila kufanya kazi? Na wazembe anaowasema ni pamoja na yeye mwenyewe. Amefanya nini alipokuwa mkuu wa mkoa Mbeya ila matusi kwa watu waliokuwa wanaathirika na majanga asilia.

Sijasahau aliposema kwamba wanyakyusa wanajenga nyumba mbovu, eti hata kuku akipiga teke anaweza kuangusha nyumba hizo. Maneno ya punguani hayo. Hakuna Mnyakyusa wa sifa za aina hiyo popote uendapo. Nakubali zipo nyumba ambazo sio bora, lakini not such a generalized statement as such!

Bungeni alikuwa full time anauchapa usingizi wakati wenzake wanakukuruka. Bahati mbaya alikujaumbuliwa na ujio wa TV live show za shughuli za wabunge bungeni ambapo tulimwona kila siku akilala usingizi, pale anapopata nafasi ya kuongea ni pumba tu. Kwa hiyo mafisadi wameanza kuondoloewa, ni pamoja na yeye kunyang'anywa cheo alichoshindwa kukifanyia kazi.

Kikwete atamalizia miaka mitano mingine kama jadi ya CCM, Qares na wenzake wapende ama wasipende. Si mnajua Bongo? Qares alipong'olewa kila cheo ilikuwa ni faraja kwa wengi.

Leka

Kwani uongo!!! nenda Mwanjelwa,Sai na Soko Matola..zile sio nyumba ni mazizi ya mbuzi ..so Quares alisema ukweli na kushangilia kwenu kutolewa kwake U kuu wa mkoa ni kutokuwa na maarifa ya kuchambua alichokisema..yes nyumba zenu hata zikipigwa teke na kuku zinaanguka...

It is true that JK na serikali yake wameshindwa kuongoza...huhitaji kufanya thesis ya Masters au PhD kubaini hilo
 
..........makamba na tamwe hiza wanasema wanaotaka jk asigombee wanalia wivu kwa kuwa mgombea wao[salim] alisindwa mwaka 2005...
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom