Waziri wa Miundombinu (Zanzibar) ajiuzulu

norbit

JF-Expert Member
Jul 30, 2007
835
699
Waziri wa miundombinu na mawasiliano (Zanzibar) Hamad Masoud Hamad (CUF) amejiuzulu kufuatia ajali ya boti ya Mv Skagit.

Nafasi yake imerithiwa Mhe. Rashid Seif Suleiman (Ziwani, CUF)


Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Zanzibar, Hamad Masoud Hamad amejiuzulu wadhifa wake leo jioni imeelezwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee ilisema tayari Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein amekubali ombi la Waziri Hamad Masoud kujiuzulu.

"Tarehe 20 Julai, 2012 Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mheshimiwa Hamad Masoud Hamad alimuandikia barua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk Ali Mohammed Shein ya kumuomba ajiuzulu kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Skagit iliyotokea Julai 18,2012" Ilisema taarifa ya Dk. Mzee.

Kufuatia kujiuzulu kwa waziri huyo, Rais Dk Shein amemteua Mwakilishi wa
Jimbo la Ziwani(CUF) Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano.

"Kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano,Rais amemteua Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano" Taarifa ya Ikulu ilisema.

Uteuzi wa Waziri mpya wa Miundombinu na Mawasiliano umeanza Julai 23 mwaka huu.

Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein ameunda Tume ya kuchunguza ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Skagit.

Mwenyekiti wa Tume hiyo ni Jaji Abdulhakim Ameir Issa, wajumbe ni Meja Jenerali S.S. Omar, COMDR. Hassan Mussa Mzee, Kapteni Abdulla Yussuf Jumbe, Kaptein Abdulla Juma Abdulla, Salum Taoufiq,Kaptein Hatibu Katandula, Bi. Mkali Fauster Ngowo, Ali Omar Chengo na Shaaban Ramadhan Abdalla Katibu wa Tume.
 

Attachments

  • hamad-masoud.jpg
    hamad-masoud.jpg
    33.5 KB · Views: 75
That was obvious kwa mtu aliyemuelewa vema Prof. Lipumba alichosema siku alipokutana na waandishi wa habari. Kudoz kwa CUF...mmeonyesha uwajibikaji
 
Inaonekana kweli ameumia sana kwa kuwajibika labda yeye siyo gamba hebu fuatilieni zaidi
 
Mh ......mie hapa sitii neno manake hawa bana !.....mbona hakujiuzulu kwenye ile ajali ya mwanzo?
 
Hussein Mwinyi una masikio? Roho za Wanambagala na WanagongolaMboto zinakulilia.
Nampongeza sana huyu Waziri. Wazanzibari sometimes ni waungwana!
 
Bi kiroboto anasubiri nini? Maana meli yake ishazama siku nyingi.
 
kufuatia ajal ya meli,mv skagt
waziri mwenye dhamana ya uchukuzi na miundombinu mh Hamad masoud ajiuzulu wadhifa wake wa uwaziri
 
Back
Top Bottom