Waziri wa Mambo ya Ndani aagiza Rage achunguzwe; DPP anafanya nini?

Ni ajabu sana OCD wa Igunga hakuwa amechukua hatua hizi zinazoelekezwa na Waziri mpaka sasa, kielelezo kingine cha Polisi kupoteza uweledi wao. Anapaswa kuwajibishwa kwa hili
 
Nkumbuka babu yangu miaka ya themanini alipanda kwa basi na pamba za jadi zakinyakyusa na akawa amebeba engwego ie kama mkuki fulani polisi walimweka kando na kumwambia mzee hauko vitani nunua kitu ivilingishe ndo uende nayo.
Ebu imagine mimi nina ruhusa ya kumiliki Riffle so nitinge nayo jukwaani
Hawa wanaomtetea Rage wamenifanya nianze kuamini kuwa common sense is sometimes not common
Kwa mtu anayejua maana ya silaha kuionyesha ni hatari zaidi kwa maadui zako kuliko kuificha isionekane
 
Kama anaimiliki hio bunduki kihalali kuna kosa gani?tusichanganye siasa na sheria

duh! kwa hiyo kila anayemiliki silaha atembee nayo nje nje? uko kwenye nyumba ya ibada pembeni ya amekaa mtu na rifle, kwenye dala dala mtu ana shortgun sokoni watu wana silaha kibao je nchi hii itakalika hebu tuwe wastaraabu. sio kila mahali mtu anabeba silaha zina maadili yake
 
Mimi siitwi masaburi..Masaburi ni Meya wa Jiji la DSM! Mimi naitwa rejao!
Hivi mbona wewe mtoto unalazimishia sana kuingia kwenye siasa? Kule MMU ndio kunakufaa zaidi.

Ebu peaneni no.za sm mjibizane,jambo hili la rage c dogo jaman ni hatar sana kutaka kubadili Tz iwe kama Somalia.
 
Unafahama maana ya neno asilimia kubwa?
Una data gani kuhusu haya maneno yako?
Siyo kila kitu lazima uchangie..jifunze kukaa kimya kwenye issue ambazo huzifahamu

nawewe jufunze umakini..twambie unachokijua tofauti na asilimia kubwa aliyoisema,
 
Nimejiuliza hibohivo kwenye akili yangu,na nikauliza hivo kwenye mtandao wa Mwananch,,,,ina maana bila maagizo wasinge-mhoji
Leo gazeti la Mwananchi leo limeandika kuwa Waziri wa Ndani Shamsi vuai Nahodha kawaagiza polisi kumhoji Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage kuhusiana na tuikio lake la kubeba bastola kiunoni Igunga wakati akihutubia mkutano wa CCM wa kampeni.

Jee hili si thibitisho tosha la kile kinachodaiwa kila mara, hasa na Chadema, kwamba Polisi hupata maagizi kuhusiana na kazi zao kutoka kwa wanasiasa, hasa katika shughuli za kisiasa kama vile kampeni?

Jamani, kuna ushahidi mwingine zaidi ya agizo hili la waziri kwa polisi? Kwani polisi si wako kibao Igunga, hawakuliona hili tukio. Jee ingekuwa ni Tundu Lissu ndiye alibeba silaha katika mkutano wa Chadema, saa hizi si angekuwa tayari lupango?
 
Kama anaimiliki hio bunduki kihalali kuna kosa gani?tusichanganye siasa na sheria
Unafahamu vema maana ya sheria??Je sheria za uchaguzi unazijua vizuri au ni valuer za mapema??Uruhusiwi kwenda kwenye mkutano wowote wakisiasa ukiwa na Silaha,wanao ruhusiwa ni vyombo vya usalama vilivyopewa jukumu hilo tu!
 
Unafahama maana ya neno asilimia kubwa?
Una data gani kuhusu haya maneno yako?
Siyo kila kitu lazima uchangie..jifunze kukaa kimya kwenye issue ambazo huzifahamu
Hivi Rejao unafahamu kwamba Bastola ni kitu kidogo sana? kama unadhani bastola ni ishu anza kufuatilia bei zake na mchakato wa kununua, Ukiwa na M1 unaipata ndani ya wiki mbili tuu, laki saba buying price, laki nne chai ya mamlaka husika.
 
Kuna kifungu cha sheria nimeiona hapo juu,2.2(c)jamani ni ya mwaka 62 haina marekebisho imetimia,adhabu ya mtu wa kuvunja sheria hiyo ni kitanzi au jela miaka 200 na viboko 20 kila hasubuh.NATUMAHI MAHAKAMA ITATUTENDEA HAKI WATZ NA ITAKUWA FUNDISHO KWA WENGINE.
 
Leo gazeti la Mwananchi leo limeandika kuwa Waziri wa Ndani Shamsi vuai Nahodha kawaagiza polisi kumhoji Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage kuhusiana na tuikio lake la kubeba bastola kiunoni Igunga wakati akihutubia mkutano wa CCM wa kampeni.

Jee hili si thibitisho tosha la kile kinachodaiwa kila mara, hasa na Chadema, kwamba Polisi hupata maagizi kuhusiana na kazi zao kutoka kwa wanasiasa, hasa katika shughuli za kisiasa kama vile kampeni?

Jamani, kuna ushahidi mwingine zaidi ya agizo hili la waziri kwa polisi? Kwani polisi si wako kibao Igunga, hawakuliona hili tukio. Jee ingekuwa ni Tundu Lissu ndiye alibeba silaha katika mkutano wa Chadema, saa hizi si angekuwa tayari lupango?
Mbona hajatoa agizo Mukama ahojiwe kuhusiana na makomandoo kutoka libya na afganstan aliowataja kwa mbwembwe tena kwa majina na sehemu walipo??
 
Leo gazeti la Mwananchi leo limeandika kuwa Waziri wa Ndani Shamsi vuai Nahodha kawaagiza polisi kumhoji Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage kuhusiana na tuikio lake la kubeba bastola kiunoni Igunga wakati akihutubia mkutano wa CCM wa kampeni.

Jee hili si thibitisho tosha la kile kinachodaiwa kila mara, hasa na Chadema, kwamba Polisi hupata maagizi kuhusiana na kazi zao kutoka kwa wanasiasa, hasa katika shughuli za kisiasa kama vile kampeni?

Jamani, kuna ushahidi mwingine zaidi ya agizo hili la waziri kwa polisi? Kwani polisi si wako kibao Igunga, hawakuliona hili tukio. Jee ingekuwa ni Tundu Lissu ndiye alibeba silaha katika mkutano wa Chadema, saa hizi si angekuwa tayari lupango?

sheria zinafuatwa kama chadema wakifanya makosa ila magamba yakifanya makosa aaaaah, sheria hakuna. yatakwisha hayo tu.
 
Unajua watu wengi huwa tunasoma sheria moja tu na kujiridhisha kuwa haitutii hatiani hivyo tunafanya vitu tukijiamini kuwa si kosa. Rage kwa kutumia sheria ya kumiliki silaha ni kweli iko silent kuhusu kuonyesha silaha hadharani. Lakini akasahau kuwa yuko kwenye kampeni za uchaguzi ambazo pia zinalindwa na sheria zake.

Hapa ndipo CCM wamechemka maana sheria ya maadili ya uchaguzi inamtia hatiani Rage maana haruhusiwi kubeba silaha ya aina yoyote anapokuwa kwenye mikutano ya kampeni. Sasa hili sijui litakuwa ni koasa kwa mahakama zetu au si kosa kwa sababu limetendwa na bosi wao?

Ngoja tusubiri tuone japo pia sijui adhabu yake ni ipi maana haya ni maadili tu. Sidhani kama hili la kubeba silaha linapashwa kuwa ni issue ya maadili tu maana najua kama wananchi wakiamua kuja na sime na mapanga yao kiunoni sijui kama itachukuliwa kuwa ni issue ya maadili au ndo tutawasahau huko Jera?
 
Angekuwa sasa hivi ananyea debe Tabora mjini na kupelekwa na chopa kabisa full ulinzi

Kwa kweli hapa lazima tuelewe kulikuwa nini mpaka anatunishia wananchi msuli kwa bastola. Tunajivunia tanzania yetu ina wasomi, ina wanaharakati ina wanasheria ambao wanatulinda watusaidie kumfikisha huyu jamaa mahakamani. Huyu waziri hii mechi haiwezi na hapo amesha maliza kesha ondoka zake.

Tunaomba kama tanzania kuna chama cha wanasheriria waungane wampeleke huyu mtu mahakamani na sisi wananchi tupo tutaungana nao. Tumechoka kukandamizwa, kunyanyaswa, kutishiwa, wakati tunatafuta haki yetu. Sheria za tanzania zinatumika kuwaumiza masikini na wanyonge ni kwa nini ndugu zangu tujiulize? Acheni kumtetea huyu jamaa amejitakia mwenyewe.

Hili suala RAGE tunalichukulia ni ndogo lakini ni suala kubwa sana. OCAMPO ndio anawatafuta watu kama hawa lakini hawapelekwi. Huwezi kuwaita watu majumbani mwao unakwenda kuwahutubia ukiwa na chombo cha moto kiunoni wakitofautiana ni kitu gani kingetokea.
 
Leo gazeti la Mwananchi leo limeandika kuwa Waziri wa Ndani Shamsi vuai Nahodha kawaagiza polisi kumhoji Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage kuhusiana na tuikio lake la kubeba bastola kiunoni Igunga wakati akihutubia mkutano wa CCM wa kampeni.

Jee hili si thibitisho tosha la kile kinachodaiwa kila mara, hasa na Chadema, kwamba Polisi hupata maagizi kuhusiana na kazi zao kutoka kwa wanasiasa, hasa katika shughuli za kisiasa kama vile kampeni?

Jamani, kuna ushahidi mwingine zaidi ya agizo hili la waziri kwa polisi? Kwani polisi si wako kibao Igunga, hawakuliona hili tukio. Jee ingekuwa ni Tundu Lissu ndiye alibeba silaha katika mkutano wa Chadema, saa hizi si angekuwa tayari lupango?

Ccm hamna uongozi makini,ni Kama pango la kambale kila mmoja ana ndevu.Vp kama kitendo hiki cha Rage kingefanywa na kiongozi wa upinzani!!!?
 
Naangalia haya ya rage yatakwenda vipi baada ya hapo nitajua mstakabari wangu wa ama nitembee na siraha au la
 
Rage anasema alipanda nayo kwa kuwa mwenyekiti wa chadema igunga alimtishia maisha.
So Rage alipanda nayo ili kuitumia, na kwa nini asitoe taarifa polisi kama alitishiwa maisha. CCM karibu wataingia msituni.
Kama alikuwa ametishiwa maisha kwa namna yeyote ile, je, aliwataarifu polisi ili waweze kulifanyia kazi hilo? Ama nani aliyeandikiwa kuwataarifu jeshi la polisi kwa aina yeyote ya kitisho na yupi yeye kapewa mamlaka ya kumkabili aliyemtisha pasipo kuitaarifu dola? Shame on him!
 
Back
Top Bottom