Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako afuta posho za kusahisha mitihani ya Mock na NECTA

Kazi ya kusahihisha ni ngumu kwa sababu inahitaji kufikiri.
Haiwezi kufanyika bila posho na ikawa na ufanisi mzuri, walimu wataifanya Kwa kulipua bila umakini (bora liende) na hapo ndiyo utakuwa mwanzo wa kudorora kwa ubora wa elimu.
 
Kwani huwa mitihani ya Necta inasahihishiwa mashuleni? Au nakosea kufikiri kwamba washihishaji huwa wanakusanywa katika baadhi ya vituo ilikufanya kazi hiyo? Kwa maana nyingine posho wanayopewa ni ile ya kuwa nje ya vituo vyao.
Hawazi kufuta hiyo posho, hizo ni Habari za magazeti tu.
Mimi kama Mwl. Nafahamu ugumu wa kazi hiyo.
 
Mbona hio habari haina chanzo cha kuaminika? anaejua source ya taarifa hio aweke apo ili tumaini, lkn pia ni necta ipi form iv au form II?
 
Nvhi hii ya ajabu sana tena inaleta mchezo na Elimu. Hivi mtu aende kusahihisha mtihani wa taifa bila kulipwa posho kweli tutakuwa na uhakika na anachokisahisha? Kama ni sehemu ya kazi yao, je wako tayari waalimu wasahishe kutoka saa 2 asubuhi mpaka saa 10 jioni tu maana huo ndo muda wa kazi rasmi? Mwalimu akiamua kudaka mshiko ili aweze kupiga tiki kuzipendelea baadhi ya shule au watahiniwa tutamlaumu nani? Kwani hata hivi viposho vya msimu navyo mwataka kuvibana ili mwalimu asionje posho maisha yake yote?

Serikali haiokoi chochote kwa kuwafanya waalimu wasahishe bure. Naamini kabisa kiasi kinachookolewa kwa kuwafanya waalimu wasahishe bure hakizidi marupurupu ya waziri. Waziri akitaka kubana matumizi afute posho zake-maana ana posho za uwaziri na ubunge. Afute maandazi na vinywaji ofisini kwake maana ofisin sio sehemu ya kula.

Kama kweli tuna nia ya dhati ya kubana posho basi serikali iingie kwenye majeshi yetu. Huko wanakula posho ya laki tatu kila mwezi wakati mshahara wanapata. Huyo askari polisi, askari magereza na mwanajeshi wa JWTZ ana matatizo gani kumzidi mwalimu kiasi kwamba apewe posho ndefu namna hiyo? Tena waalimu wana mazingira magumu zaid ya kufanyia kazi. Vituo vya polisi, Magereza na kambi za jeshi zote ziko mjini, lakin kuna shule ziko katikati ya milima ambako kila huduma ni ghali. Kwanin tusimpe posho huyu mwalimu anayekaa katikati ya milima kama mjusi? Kosa kubwa la waalimu ni kushika chaki badala ya bunduki.

Wabunge kazi yao ni kujadili rasimu za sheria, kutunga, kushauri na kuisimamia serikali. Mbona wao wanalipwa posho kubwa sana za vikao wakati kimsingi wanakuwa kwenye kazi zao? Mbunge anayekuwa Dodoma analipwa hela ya kujikimu(laki) na posho ya vikao kila siku. Kwanini mwalimu asipewe posho ya kusahisha mtihani wa taifa wakati mtihani wenyewe unafanyika mara moja kwa mwaka?

Wananchi wa TZ wana mkosi sana na mawaziri wa elimu ambao tunapata. Actually ni nuksi, sio mkosi.
 
Huyu mama anachanganyikiwa akidhan ndo anamfurahisha magufuli...unafuta posho sasa inamaana tofaut ya mwalim.alieenda kumark papers na yule ambae hakwenda inakuwa wapi? Asijifanye yy ndo anauchungu pekeake wa hii nchi
 
........Kuna Watu watazimia Jamanii maana daah ! hali inazidi kuwa mbaya kila kukicha ....ila itasaidia maana kuna walimu wana zaid ya miaka 10 kazini hawajawahi kusimamia mitihani kwa sababu ya upendeleo wa maafisa.wajigawie posho sasa tuone
 
Walimu walimu walimu walimu walimu walimu walimu....ngoja ninyamaze tuu
 
walimu wengi wanatoka familia za kimasikini, ivi kama home pako vizur utahangaika na Huo ualimu Kwa nini usisimamie miradi ya home au kuchukua mtaji ukafungua biashara zako
 
na ajiandae pia at the same tyme mitihani kuleake coz teachers hv no money even allowance? mbona yy hakusema anafuta posho ya vikao vya bunge wakati pale napo anatekeleza majukumu yake? majanga wallah
 
Nauli ya kwenda na kurudi utapatiwa mwalimu. Pia naomba ufahamu kuwa serikali imeamua kubana matumizi na kupeleka pesa itakayopatikana kwenye miradi yaa maendeleo. Naomba tuwe wavumilivu na tuunge mkono nia njema ya serikali yetu. Naomba ifahamike kuwa nia na malengo ya serikali mema kabisa. Inachofanya serikali si yo ukatili kama baadhi yenu mnavyofikiria. Serikali inataka kila mtanzania afaidike na matunda ya serikali yake. Wakati utaongea. Mtayaona hayo matunda kwa macho yenu. Asanteni.
Eti matunda!!!! fild zingine mbona hamzigusagi ovyo ovyo,.....

Futeni basi na hizi posho kwani ni moja ya sehemu ya majukumu ya kazi ya wapokea posho hizo.........

a) posho za wabunge
b) posho za madiwani
c)posho za vikao vya halmashauri na wilaya
d) posho za maaskari pale wanapo safirisha wafungwa
e)posho za madaktari na wauguzi
d) posho za majaji, mahakimu na TRA

Field ya ualimu ndio fild pekeee ambayo mwalimu anakatwa mshahara wake kuchangia darasa, dawati, na meza yake ya kukalia ofisini!!!

haijawai tokea askari kukatwa mshahara akachangia kununua pingu, kupanua gereza ama godoro la kulalia mfungwa!!!

haijawai tokea daktari akakatwa mshahara kununua kitanda, godoro ama shuka la mgonjwa

mwaka jana waalimu hawa hawa walisimamia mitihani ya kidato cha nne, bila aibu serikali hii imewadhulumu na mpaka leo hijawai walipa!!! nabungeni walikiri kuwa hawaja walipa lakini wiki mbili zilizo pita waziri uyo uyo kaja na takwimu kuwa kesha walipa wooote !!!!


namshukuru mungu aliye nipa nguvu kuachana na kazi na nawapa pole mlio baki humo jamani!!! nina miaka miwili sasa nipo uraiani natafuta kwa jasho langu!!!


kazi kama imelaaniwa vile!!!! kila kiongozi ameshawaona waalimu kama maboya!!!! ni vitisho, dharau na kejeli kila kukicha!!!

waalim nao kutokana na umaskini walio nao wanshindwa kupaza sauti kuyakemea haya, wanagugumia myoyoni na mgomo wao wanauamishia kwa watoto!!!!

sijawai kuona kazi ya ajabu ajabu kama ya ualimu nchin TANZANIA!!! hawa watu sio lazima muwape mishahara mikubwa!!! hata mkiwaheshimu tu na kuwa aknoweldge ni mshahara tosha!!!!

mnawafanya kama watoto!!! madaraja kuwapandisha mpka mtake nyinyi, mwenge ukipita mnawakata kimyakimya,!!! hamna aibu....????

skuizi wengi wamekua wajasiliamali na kufanya ualimu kama sorce yakupata mikopo kufanya biashara zao binafsi na sio kufundisha!!! tafuta mwalimu yeyote asiye jishughulisha, yaani awe yeye na mshahara mshahara na yeye hana tofauti na mtu asiyenakazi!!! wengine msio kwenye fild mtasemahana malengo!!!


huu ni upuuzi !!!!!!!!!!

shame on you AFRIKA kwa kupuuza elimu!!!!!! aibu kwako waziri kwa kuwa mwalimu unae waumiza waalim wenzako!!!! hemu waeshimu kidogo icho unacho waondolea ndio una wa demolorize totaly!!!
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom