Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako afuta posho za kusahisha mitihani ya Mock na NECTA

LTN USU WA MADOSO

JF-Expert Member
Sep 14, 2016
1,193
859
Wizara ya elimu sayansi na teknolojia imefuta posho ambazo walikuwa wanalipwa walimu pindi wako kwenye kazi ya kusairisha mitihani kama pesa yao ya kujikimu badala yake serikali imedai kuwa zoezi hilo ni sehemu ya kazi yao wakati huo posho hizo zilikuwa zinawasaidia walimu kujikimu pindi walipokuwa kwenye zoezi hilo.

Pia Prof. Joyce Ndalichako amesema yupo mbioni kuisuka wizara ya Elimu Upya.

Chanzo: Magazeti ya leo
 
katika jambo ambalo kakurupuka ni pamoja na hili! bila posho walimu hawatakua na moyo wa kusahisha pia watajikimu vipi wanapokua mbali na mazingira yao ya kazi, pia suala la usafiri watasafirishwa vipi bila posho?

hapa Profesa ajiangalie upya na hili litamshinda nauhakika
 
Zamani ualimu ilikuwa ndio last resort ....mtu ukikosa uelekeo kwenye course zngine unakimbilia ualimu bt sasa hivi dah
 
Professor of what?
Kama ni hivyo basi kila shule iwe na mitihani yake na isahihishwe na walimu wahusika. Kusiwe na mtihani wa taifa.
Posho zote zifutwe kwa wafanyakazi wa idara zote, kuanzia wabunge na mawaziri, hata kama ni safari, kama ni ya kikazi wasilipwe.
 
Kazi ya kusahihisha mitihani ilivyokuwa ngumu hivyo halafu leo kwa tamko tu wafuta haki yao ya msingi, salary zao kwanza ndogo, hawana posho yoyote zaidi ya akipangiwa kusimamia au kusahihisha mitihani ndo angalau nao wanajiskia, tutegemee elimu yetu kushuka zaidi maana hakuna motivation wala morale ya kazi tena hapo, NAISHAURI SERIKALI YANGU YA WANYONGE KAMA SERA YA ELIMU BURE NI NGUMU KUTEKELEZEKA, RUDISHENI UTARATIBU WA KUCHANGIA ELIMU, KWA MTAZAMO WANGU MNAHARIBU ZAIDI KULIKO KUJENGA, PERIOD
 
katika jambo ambalo kakurupuka ni pamoja na hili! bila posho walimu hawatakua na moyo wa kusahisha pia watajikimu vipi wanapokua mbali na mazingira yao ya kazi, pia suala la usafiri watasafirishwa vipi bila posho?

hapa Profesa ajiangalie upya na hili litamshinda nauhakika
Nauli ya kwenda na kurudi utapatiwa mwalimu. Pia naomba ufahamu kuwa serikali imeamua kubana matumizi na kupeleka pesa itakayopatikana kwenye miradi yaa maendeleo. Naomba tuwe wavumilivu na tuunge mkono nia njema ya serikali yetu. Naomba ifahamike kuwa nia na malengo ya serikali mema kabisa. Inachofanya serikali si yo ukatili kama baadhi yenu mnavyofikiria. Serikali inataka kila mtanzania afaidike na matunda ya serikali yake. Wakati utaongea. Mtayaona hayo matunda kwa macho yenu. Asanteni.
 
Back
Top Bottom