Waziri vs katibu mkuu. Huu mfumo ni sawa

Zing

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
1,767
470
Kuna hivyo vyeo viwili kwenye wizara . Binafsi naona vinaweza kuwa ni chanzo ha baadhi ya matatizo kwenye serikali.

Kwanza nahisi kunaweza kuwa kuna mngongano wa kimadarakaau majukumu katika vyeo hivi viwili. Naelewa kuwa waiziri yuko juu ya hierarchy ya uongozi kwenye wizara. Lakini naelewa pia kuwa mtendaji mkuu wa wizara si waziri bali ni katibu mkuu. Hapa nahisi kuna tatizoukizingatia post hizi zote ni presdential appointment.


Pili kwa kufuata hoja ya kwanza hapo juu naona hivyo vyote vinaongeza mzigo wa viongozi. nadhani kwa uwajibikaji zaidi tunaweza kubaki na cheo kimoja.Kuwa na Top two figures kwenye taasisi amabzo zote ni za kuteuliwa sioni kuwa ni sahihi. Inatakiwa abaki Mmoja au

Tatu kama ni muhimu vyote viwepo basi hiki cheo cha katibu mkuu kisiwe cha kuteuliwa kiwe cha kusailiwa. Na kama ni muhimu kwa katibu mkuu kuteuliwa basi uwe ni uteuzi baada ya mtu kufanya application na kueleza mkakati wake akichukua cheo hicho. Na rais akiona unaendana na mikakati yake basi anamteua . Hii nadhanani itaongeza uwajibikaji. Hata kwenye nafasi za kurugenzi nyingi bado mpaka leo ni za kuteuliwa . Kwa kuteuana teuana tunaendekeza uvivu na kuleana leana. Style ni hii kwenye taasisi nyingi kama BOT,nk


Changamoto hii pia mikoani kuna RC( Regional COmmisioner) na RAS( Regional administrative secretary) Wilayani wapo ma DC na ma DAS. Hawa RAS na DAS nadhani ni veyo vinatkiwa mtu afanye application na afanyiwe usaili. Hii nadhani ni njia ya maendeleo na uwajibikaji kwa viongozi

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom