WAZIRI TIBAIJUKA: VIPI MIGOGORO YA VIWANJA WAZO HILLna KISANGA?

zaleo

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
1,902
764
Professa Tibaijuka alisemea habari za migogoro ya viwanja Kigamboni, lakini alianza vizuri uwaziri wake, nadhani naye wamemdhibiti wenye hela. Aliwahi kwenda mwenyewe kujionea uzandiki wa matapeli wa viwanja kule Kisanga WAzo Hill na akaahidi kushughulikia, mwaka unakatika na matapeli yanaendelea kupeta kwa kuwatumia wafanya kazi wa kulekule wizarani!

Watu wamenyang'anywa viwanja mchana kweupeeeee. Wanyonge wametishiwa, wengine kupelekwa mahakamani ili waachie, kila kukicha watu wanalia kule kwa sababu wenye hela wanaenda na hati feki kutoka wizarani wakati mwenye kumiliki kwa halali anaendelea kulipia kila mwaka kulekule wizarani. Kuna jamaa aliporwa hekari 5 akaachiwa kipande chenye kibanda, lakini alikuwa amejenga kisima. Watu wa ardhi wakachora upya ramani na kumchomekea Kamishna wao asaini ramani mpya ili kuhalalisha undava wao kwa kumgawia mtu mmoja dalali kwa kukikata kisima kile katikati (Mwizi ni rahisi kumtambua). Haieleweki wachora ramani mpya waliwezaje kugawa shimo lililojengwa (Kisima) katikati tena pasipo mwenye mali kushirikishwa. Kuna malalamiko mengi mengi mengi kila mahali DSM.

Kule WAzo Hill hata Halima Mdee (Mbunge) na hata Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni walishaenda kule. Watu walikwishapigana mapanga sababu za kuvamiwa viwanja vyao na wenye hela. Jamani Tibaijuka, unangojea wafe zaidi? Walalahoi hawatakubali kunyanyaswa sababu ya kutokuwa na hela tu, Bora kuwanusuru. Watu wanashindwa kuendeleza mambo yao sababu ya migogoro inayotengenezwa na watumishi wako wizarani hapo kwa kuwatumia madalali!
 
katika wizara ambazo waziri wake kachemka yaani kashindwa kazi ni wizara ya tibaijuka. Huku kinyerezi viwanja vya wazi ambavyo vilitengwa na serikali kwa ajili ya hospital,shule,viwanja vya michezo na maeneo ya taasis,na eneo la bible collage watu wako wanajenga na taarifa zilishafika ofisi husika lakini hakuna isue. Watu wameidharau serikali ndio maana wanajenga bila hata chembe ya kuogopa dola.
 
Unajua mawaziri hawa wanajua sana kuchonga lakini hawawezi kufanya kazi. Kila asimamapo ni majisifu tu ....oh nimefanya kazi umoja wa mataifa, ni profesa chuo kikuu, nimekuja kusaidia wananchi....lelelellelelelelelele .... hamna kitu. Damu inayomfaa mgonjwa wa anemia sio ile unayoiona kwenye chupa, bali ni lile tone linaloingia kwenye mshipa. Siasa za nini wakati wenye hela ndio waendesha nchi??
 
Back
Top Bottom