Waziri Tibaijuka ameleta matumaini, tumsaidie

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
proftibaijuka.jpg
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka​

TUMEGUSWA sana na tamko la Serikali lililotolewa juzi kwamba haitakuwa na simile na watu waliojenga katika maeneo ya wazi na waliouza viwanja hivyo kinyume na taratibu. Tamko hilo linakuja baada ya kuwapo vilio na malalamiko ya wananchi kuhusu uuzwaji wa maeneo ya wazi uliofanywa na watendaji wasiokuwa waaminifu, jambo ambalo limechangia kuwapo kwa migogoro ya ardhi katika maeneo yote nchini.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa sekta ya ardhi uliohusisha watendaji mbalimbali, wakiwamo watathmini wa ardhi, maofisa wa ardhi, wapima ardhi, maofisa mipango miji na wasajili wa hati, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka alisema ubomoaji wa nyumba zilizojengwa kwenye maeneo hayo ya wazi utaanza wakati wowote kuanzia sasa na wala Serikali haitalipa fidia kwa wamiliki wa majengo hayo.

Tunasema tumeguswa sana na tamko hilo la Serikali kutokana na dhana potofu ambayo imekuwapo kwa muda mrefu miongoni mwa wananchi kwamba, wamiliki wa majengo hayo yaliyojengwa katika viwanja vya wazi ni watu wenye uwezo mkubwa kifedha, hivyo Serikali haiwezi kuwagusa. Dhana hiyo potofu ilijengeka kutokana na watendaji wa Serikali, manispaa na miji kuonekana wamekula njama na matajiri, hivyo kupindisha sheria na kanuni za ardhi na kuwauzia matajiri hao viwanja kwa njia za rushwa.

Tamko hilo la Serikali linaleta matumaini yaliyokuwa yamefifia kutokana na ukweli kwamba, huko nyuma hapakuwapo utashi wa kusimamia sheria na kanuni zinazosimamia ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi. Mara zote Serikali ilikuwa inaishia tu kutoa onyo kwa wavamizi wa viwanja na waliojenga nyumba pasipo kufuata mipango miji, lakini ilikuwa inashindwa kuchukua hatua dhidi ya watu hao.

Ni vigumu kufahamu kwa nini watendaji na viongozi katika wizara husika walikuwa wanashindwa kuchukua hatua, ingawa sheria zilikuwa wazi kuhusu nini la kufanya katika hali kama hiyo. Inasemeka kwamba nguvu ya fedha na ukwasi mkubwa waliokuwa nao wavamizi hao wa viwanja uliwafanya watendaji na viongozi wengi serikalini kushikwa na kigugumizi, hivyo kukosa ujasiri wa kuthubutu.

Hilo ndilo lilikuwa chimbuko la migogoro ya ardhi tunayoishuhudia hivi sasa katika kila pembe ya nchi yetu. Tunamuunga mkono Waziri Tibaijuka anaposema kwamba wakati wa watu kuishi kiujanjaujanja kwa kuuza viwanja na ardhi kinyume cha sheria umekwisha na tunakubaliana naye asilimia mia moja anaposema atahakikisha hati miliki zote za nyumba na majengo zilizotolewa kinyume na sheria zinafutwa.

Ni kweli kama alivyosema Waziri Tibaijuka, siyo watendaji wote serikalini ambao siyo waaminifu na ndiyo maana tunakubaliana naye pia anaposema kwamba, watumishi na watendaji wengine wameponzwa na tabia ya ukondoo ya kukubali maagizo yaliyo kinyume na sheria yanayotolewa kwao na baadhi ya viongozi na wanasiasa.

Hakika baadhi ya watumishi waadilifu wamekuwa wanatishwa na baadhi ya viongozi. Ndiyo maana tunadhani waziri huyo amefanya vyema kwa kuwaelekeza watumishi na watendaji hao wasikubali tena kupokea maagizo yanayokiuka sheria na kanuni za ardhi na kuwahakikishia kwamba atawalinda wale watakaozisimamia.

Tunamshauri Waziri Tibaijuka atambue kuwa, vita aliyoitangaza ni kubwa, hivyo atahitaji kuwa na ngozi ngumu kwa sababu wizara hiyo anayoiongoza imevurugwa na nguvu ya fedha kwa muda mrefu sasa. Hivyo, uwezekano wa kukwamishwa, kusalitiwa au kuingizwa mkenge na mafisadi kupitia kwa baadhi ya watumishi wa wizara yake ambao pia watakwazwa na msimamo wake usiotetereka wa kusimamia sheria na kanuni za ardhi, ni mkubwa.

Hatutazamii kwamba kasi ya waziri huyo baadaye itabadilika na kuwa nguvu ya soda. Tunamshauri asiogope kujitoa muhanga iwapo atalazimika kufanya hivyo, kwani huo ndiyo utakuwa mchango wake katika kuleta ukombozi katika sekta ya ardhi na makazi kwa kuwarithisha ardhi wananchi wengi maskini katika nchi yetu. Sisi tunasema tutamuunga mkono na ni matumaini yetu kwamba, wananchi wote watafanya hivyo.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Anaweza akawa na dhamira iliyo imara. Lakini katika corrupt system kuanzia ngazi ya juu kabisa, sijui kama atafika popote. Simkatishi tamaa, lakini kama utawala wa juu unawalinda mafisadi wa rada, dowans, etc, sijui kama atafanikiwa maana itabidi awaguse hao wanaojiita wakubwa. Mungu amtangulie nasi tupo naye.
 
Back
Top Bottom