Waziri tamisemi na katibu mkuu wawajibike kwa kuchelewesha huduma za fedha katika halmashauri

Jun 30, 2012
6
0
Kuanzia tarehe 1 July 2012 (mwaka mpya wa fedha) malipo ya fedha katika Halmashauri yamesimama. Hii imetokana na TAMISEMI kutaka kuanzisha mfumo mpya wa malipo ambao unakuwa centralized. Ina maana mapato na matumizi ya kila siku ya halmashauri yatakuwa yanaangaliwa na TAMISEMI mojamoja kwa kutumia mtandao na jambo hilia ni zuri kwani litawezesha TAMISEMI kuwa na uwezo wa kuzuia malipo yasiyo kwenye mpango na hivyo kudhibiti fedha za serikali na pia litasaidia kujua kinachoendelea halmashauri kuhusu fedha. Kwa kweli naipongeza serikali kwa hilo.

Tatizo linakuja ni kuwa mpaka leo mtandao huo haujaanza kufanya kazi na malipo yamesimamishwa na hivyo huduma za fedha katika halmashauri zimesimama na hivyo kufanya maisha kuwa magumu sana kwa wananchi wanaotegemewa kuhudumiwa na halmashuri. Halmashauri zimeshindwa kutoa huduma kwa mwezi mmoja. Je ni hasara kiasi nchi na wananchi wameingia? Je, kiasi cha fedha halmashauri inachotumia kujiendesha imekitoa wapi?

Je, sheria hazivunjwi na taratibu kupata fedha hiyo ya kujiendesha isiyo na maelezo? Na kama zikivunjwa ni halali kuwashtaki watumishi wenye nia nzuri ya kuokoa jahazi. Halafu mwisho wa mwaka serikali itazioji halmashauri kwa kutofikia malengo wakati inashindwa kuanza kutekekleza mpango mpaka leo? Ni kwani waziri na katibu mkuu TAMISEMI wasiwajibike kwa hilo?

Kwanini wasingefanya tafiti mwaka mzima kuhusu mfumo huo na kufanya maandalizi mwaka mzima ya mfumo huo kuliko kuanzisha mpango na kuanza kufanya majaribio humohumo na kusababisha ucheleweshaji mkubwa wa huduma na hasara kubwa kutokana na shughuli za halmashauri kusimama nchi nzima. Je, watendaji wa TAMISEMI wakiwa wamesomea masuala ya planning hawakuliona hilo?

Waajibishwe kwa poor planning amabyo iathiri wananchi wengi wa Tanzania kwani wanaishi kwenye halmashauri na mpaka sasa hakuna huduma ya kueleweka kukana na mfumo huo wa EPICOR kutokufanya kazi. Bunge ilivalie njuga hili kwani madhara yake ni makubwa, Watanzania sio watu wa kufanyiwa majaribio.
 
Ndio tatizo la kukurupuka. Hivi huo mfumo haukufanyiwa majaribio kabla ya kuamua kuwa utumike?
 
We have big issues in setting our priorities, executing and sustaining them. We work in small pockets...anayeamua hawasiliani na anayetekeleza na kusimamia. Basi ni matatizo matupu
 
Tamisemi ni poor kabisa.mfumo wenyewe tangu mwaka jana ni ngojera tu .na mbaya sana hata facilitation ya it specialist katika halmashauri haikufanyika. Ni uozo mtupu.ni ujinga kung'angania systems zilizonunuliwa kwa rushwa na akina blandina nyoni wakati huo akiwa chief accountant wa serikali ndio inatesa hivi , wakati kuna softwares nzuri na user friendely kama oracle yenye options na customization ya kutosha.poor pinda,poor ghasia ,poor mwanrie
 
Back
Top Bottom