Waziri Sophia Simba aumbuka Channel 10!

carelessness.jpg
Mungu wangu JK hawezi hata kutofautisha kati ya $ 300,000 na two hundred thousand as it appears kwenye cheque
 
HUYU MAMA SI NDIYE ALIYEIMBWA NA MPOKI kwenye wimbo wa shangazi. kama ni yeye hakuna kitu.

kwanza anaonekana hata akiwa anaongea hayuko serious kama wamama wengine ambao ni strong, ie migoro, tibaijuka, mongera.

mimi namfananishaga na Khadijaaa KOPPPA
 
Yule mama ni sawa na gauni lililotundikwa juu kwenye sanamu katika maduka ya kuuza nguo kwa ajili ya kulionyesha gauni lilivyo ili mteja avutiwe.hamna zaidi ya kuwa ka sanamu.
 
Hiyo ni mikakati yake ya maendeleo ya jamii kwa jinsia moja. Hongera kina mama kuwakilishwa na Waziri anayependa maendeleo ya Kina mama , lakini mbona clinic za Wajawazito vijijini na hata sehemu zingine za mjini ni mbovu?.......Jinsia na Maendeleo?...Haya yangu macho.
 
Katika wanawake wa CCM wenye viherehere, Sofia anaongoza. Huwa hana ajualo zaidi ya kuwaza atamfurahishaje bosi wake?
 
Kwanza mimi binafsi simuelewi kabisa huyo mama Sophia Simba! Na nina mashaka makubwa juu ya uwezo wake kiutendaji. Hii inatokana na namna anavyoongea wakati wote-hajali anaongea nini na wakati gani!Ni kama anabwabwaja tu muda wote. Inaelekea anafaa sana kuwa mwimbaji wa taarab.
 

Jamaa aliangalia figure tu akasahau kuoanisha na maandishi! Huyu ndo Dr. JK msomi wa uchumi! Mzungu alitaka ku-prove kama ni kweli ukitaka kumficha Mswahili kitu, weka kwenye maandishi.

Mzungu proved postive! Nadhani na kwenye mikataba ya madini na uwekezaji kuna vitu kama hivi!
 
Sasa anagawa familia, akiwa Waziri Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto, anelekeza wanawake tu wasiende kwenye maandamano ya CDM inaama kwa maana ya jinsi watoto+vijana+wazee (yaani wote waliobaki isipokuwa wanawake) wataenda.
 
Unajua kwa nini mawaziri wengi wa JK ni vituko? Hawateuliwi kwa uwezo wao wa kazi isipokuwa wanajipendekeza vipi kwa RA, wanachangia vipi fenda ktk kampeni za JK, ni maswahiba kiasi gani na wakuu wa Mtandao nk. Unakumbuka lile baraza la mawaziri sitini? Wizara ya Usalama wa Raia v. Mambo ya ndani? Basi inasemekana JK alipofika madarakani alidhani RA na EL watamwachia ajitawale akiwapa nafasi lakini haikuwa hivyo. Kwanza RA akasema hataki uwaziri ila akaleta majina ya watu wake kama kumi hivi, Mzee wa Monduli kama umjuavyo akaleta wake kama 33 hivi, bila kusahau wazee wa siasa kama kina King Gunge wa Ngombare asingeweza kuwatupa. Yeye mwenyewe JK akawa na watu wake. Pia usisahau mtazamo wa CC emu kuhusu uwakilishi kimikoa katika Baraza la Mawaziri. Hivyo kufikia mwisho unaajikuta una watu kama mia hivi? Huwezi kuamini kirahisi lakini hao sitini (60) walikuwa ndo kiwango cha chini zaidi kilichowezekana kwa wakati huo maana bado kuna wapambe wengi ambao bado hawakupata nafasi

Kwa hiyo usishangae kumkuta Mama yangu Simba siku zote kuwa mropokaji. Inawezekana yupo hapo kwa sababu alienda kwa RA kuomba uwaziri na RA akampa kimemo ampelekee JK "Apewe nafasi anayopenda. Ni mtu wetu wa karibu!" Kisha JK akainua simu kuripoti kwa bosi wake RA "Tayari Mkuu"

Hujaipata hiyo? Inasemekana tangu wanamtandao waanze kutafuta madaraka (miaka kama 18 hivi imepita) hakuna siku waliwahi kujadili watatatua vipi tatizo lolote kubwa (umeme, maji, barabara, kilimo duni nk.) hapa nchini. Mazungumzo yao mengi ilikuwa wapi watapata fedha na vipi watamwondoa nani katika mlinganyo nk. Inasemekana hata zile kashfa za Sumayi kuwa fisadi na pesa nyingi (Inawezekana ni kweli. Sipingani na hilo maana CCM sijui utamwamini nani wote hayohayo) ziliwekwa wazi ili Mkapa (fisadi mwingine lakini aliyemudu makashkashi) asipate nafasi ya kumwachia urais.

Mkuu!
Ulichoandika kinaweza kisiwe kweli 100% lakini to be sincere kina-reflect hali halisi kwa kiasi kikubwa sana..Ni kweli kabisa inagoma akilini kuamini mtu kama SS kuwa alichaguliwa uwaziri kwa uwezo wake...tunayaona toka kwake ndiyo ukomo wa uwezo wake kifikra,inasikitisha sana,wapi tutafika kama watu wa type yake wanaweza kupata nafasi kubwa kama uwaziri?mchango gani constructive watakaoutoa?

Nakubaliana na wewe pia kama kweli kwa dhati kabisa hawa watu wana nia ya kutatua matatizo makubwa uliyoyabainisha;chochote wanachofanya unapokuja kusikia behind unachoka kabisa,unaambiwa fulani ana hisa hii au kamisheni ile na kweli mwisho wa siku ndiyo hayo yanayoibuka mpaka inafikia mahali tunachezewa sinema (DOWANS) ambayo hata mtoto mdogo anajua ni usanii...nini tutegemee hapo?
 
Sio kosa lake, ni kosa la yule aliyempa hicho cheo kama kweli anafahamu uwezo wake. Sasa hapa ana maana kuwa hakuna wanawake ambao ni wanachama wa CDM, ila wanaume tu.
 
Inabidi tufanye utafiti iwapo Kuna uhusiano wa Vyeo ndani CCM na uwezo wa Kufikiri.Nahisi kila mtu anapopata cheo ndani ya ccm uwezo wake wa kufiri unapungua? kuna watu wengi walipokuwa na vyeo vidogo walionekana watu wa watu, wachapa kazi wazuri la mara walipo pata ukubwa wanachefua mno. Sample zetu zianzie na mkuu mwenyewe, huyo dada SS, Makamba mkumbwa, Wasira, Pinda na Na Tambwe. haiwezekani mtu akiona mumewe hafanyikazi an conclude wanaume hawafanyi kazi. Lakini pia watu hao hao wakipigwa chini wananza ongea mambo ya msingi mfano mh. Sumaye na Ngoyai( si wasafishi jamani na justify hypothesis yangu) na hata mangura baada ya kupigwa buti na Jah people tumsikia akisema uongozi ndani ya CCM ni kama mnada, kabla ya hapo aliimba wa namba one CCM.
 
sishangai Sophia kusema hili kwani alishawai kuwataka wanawake wawanyime unyumba waume zao kama watawaunga mkono wapinzani so sofia amaamin kwa nguvu ya ngono anaweza kumwendesha na kupata chochote kutoka kwa mwanaume.
Akili yake inawaza ngono tu na labda JK kampa hiyo WIZARA kama offa au aweke draft ya ngono kuzima harakati za ukombozi.
Ni wanawake wajinga tu kama yeye watakaomuelewa.

My take:WANAWAKE TUNATESEKA ZAIDI YA WANAUME NA HUU UGUMU WA MAISHA sasa sexy slave sofia anamaanisha nini?

Afadhali wamama wenyewe ndo mmesema sisi tusingeeleweka!! Nashangaa hivi anafikiri haya maisha magumu yanawaathri wanaume tu? Akina mama ndo zaidi na ninashukuru kwamba hata kwenye hivyo viwanja na akinamama wako msitari wa mbele.

Ila mama kwa ngono huyuuuuu! Hajambo. Ndo maana akina KK walimpitia asubuhi na mapema. Nina mashaka huko mjengoni kama siyo mama gawa gawa huyu!!
 
Mwacheni mama wa watu wala msimuandame mlitaka aseme nini wkt uwezo wake kiakili na kufikiri umeishia hapo?
 
Nadhani wametuma serikali nzima kuipiga vita CDM maana hata jana nilimwona Wassira nae anajiumauma TBC kuhusu CDM. Ukweli wanapigana na ukuta hawataweza.

Kama kweli CCM wamefanya hivi basi CHADEMA inachukua nchi 2015. Kwa watu wanaojua political strategies hii ni distraction tosha ya kuwafanya CCM waache kutekeleza mambo yatakayowafanya 2015 wapige kampeni kifua mbele. Mtu ukiwa kwenye madaraka hutakiwi kujibu hoja kwa propaganda bali kwa kufanya mambo ya maendeleo, maana ukisema hali ya maisha si ngumu wakati wapiga kura wanaumia na maisha unaonekana upo out of touch. Na kitendo chochote cha kuiongelea CHADEMA ni kuipa umaarufu. Mtu kwenda au kutokwenda kwenye maandamano si kazi ya serikali hiyo ni kazi mwandamanaji mwenyewe kulingana na nafasi yake, Kusema maandamano haya ni kama ya Misri au Libya ni kuhamasisha watu waone kuwa huenda kweli kuwa kuna ukombozi unaweza patikana kwa kuandamana na hivyo kuhamasisha watu wengi zaidi.

CCM walitakiwa kukaa kimya kabisa na wasiongelee CHADEMA hata kidogo, wao wahamasishe maendeleo kwa kuanzisha miradi isiyo ya kifisadi ya kusaidia maeneo mbali mbali na siyo kuonesha hamaki ya kinachoanywa na CHADEMA. Hii inaonesha wazi kwa wananchi kuwa CCM na serikali yake wanaangalia masilahi yao zaidi ya yale ya nchi. Waache demokrasia ifanye kazi, kama wanaogopa watangaze kufuta vyama vingi na kuendesha nchi kidikteta
 
Kusema ukweli hakuna hata siku moja ambayo nilimuona huyu mama kasimama sehemu na kutoa jambo la maana katika nchi hii,hivi ana nguvu gani mpaka kupewa wizara na hata kuongoza taasisi ya wakinamama?
 
Waziri wa Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto Mh.Sophia Simba amejikuta kwny wakati mgumu pale alipowalaumu vikali CHADEMA kwa kuendesha maandamano kanda ya ziwa na kusema kua huko ni kuiga Misri na Libya!! Mama huyo badala ya kuzungumzia kilichompeleka studio kuzungumzia Siku ya wanawake duniani yeye akaanza na kusema wanawake wasiende kwny maandamano ya CDM maana wao wana kazi nyingi za kufanya kuliko wanaume ambao hawana kazi ndio maana wanaenda kwny maandamano hayo!!! Ulipofika muda wa watazamaji kuchangia ndipo huyo mama alipoanza kushambuliwa na kila mchangiaji kwamba afute kauli zake za kwamba "wanaume hawana kazi ndio maana wengi wanaenda kwny maandamano hayo" na "kufananisha maandamano ya CHADEMA na yale ya nchini Misri au Libya" Ninachojiuliza hapa wana JF wenzangu hivi hawa viongozi wetu kwann wanakua mambumbumbu kiasi hiki na ufinyu wa uelewa? Kuhusisha maandamano ya CDM na yale ya Misri au Libya huu si ndio uchochezi wenyewe!!! Halafu napenda kuuliza wana JF wenzangu nini maana ya JINSIA?! Nawakilishaa.
Hata sijui huwa tunatumia Criteria zipi kuwapa watu nafasi za juu. Huwa najiuliza wanazungumza nini kwenye mikutano ya kimataifa maana kwengine hizi nafasi hazishikwi na wapuuzi kama huyu mama kabisa, yaani hata kazi ya ushauri katika wizara yake aliyopo hapati.

Kaazi kweli kweli
 
Waziri wa Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto Mh.Sophia Simba amejikuta kwny wakati mgumu pale alipowalaumu vikali CHADEMA kwa kuendesha maandamano kanda ya ziwa na kusema kua huko ni kuiga Misri na Libya!! Mama huyo badala ya kuzungumzia kilichompeleka studio kuzungumzia Siku ya wanawake duniani yeye akaanza na kusema wanawake wasiende kwny maandamano ya CDM maana wao wana kazi nyingi za kufanya kuliko wanaume ambao hawana kazi ndio maana wanaenda kwny maandamano hayo!!! Ulipofika muda wa watazamaji kuchangia ndipo huyo mama alipoanza kushambuliwa na kila mchangiaji kwamba afute kauli zake za kwamba "wanaume hawana kazi ndio maana wengi wanaenda kwny maandamano hayo" na "kufananisha maandamano ya CHADEMA na yale ya nchini Misri au Libya" Ninachojiuliza hapa wana JF wenzangu hivi hawa viongozi wetu kwann wanakua mambumbumbu kiasi hiki na ufinyu wa uelewa? Kuhusisha maandamano ya CDM na yale ya Misri au Libya huu si ndio uchochezi wenyewe!!! Halafu napenda kuuliza wana JF wenzangu nini maana ya JINSIA?! Nawakilishaa.


Ndugu yangu kama hujagundua kwa sasa viongozi wetu wanaishi kwa wasiwasi kama jambazi anayetafutwa na polisi kwani kila akiona mtu aliyenyoa hukimbia akifikiri ni askari kanzu anamfuatilia.
Pia viongozi wengi ambao wamepata madaraka kwa favour ya JK hizi ndizo tabia zao kuu za kujikomba na kuwa washabiki wa JK badala ya kubuni mbinu za kuboresha uendeshaji wa shughuli za serikali kwa manufaa ya mtanzania. Mimi nawasifu CHADEMA kwa kutumia mbinu ambayo imetudhihirishia kwamba CCM hawana kazi bali kukaa kwenye vijiwe na kusikilizia mikutano na maandamano ya CHADEMA. Wanatoa wapi muda wa kuongea mambo ya CDM wakati wao CCM wana mengi ya kuongea ikiwa ni pamoja na kufufua chama ambacho kwa hakika kipo ICU?.

Kufananisha maandamano ya misri na Tunisia na ya Chadema ni sawa na kufananisha Meli na Mtumbwi na ni kiashirio kwamba viongozi wetu wana upeo mdogo wa kutofautisha vitu viwili vyenye sifa tofauti.

Msameheni Sofia tunamjua pale tumeliwa hapo ndipo uwezo wake wa kufikiri unpoishia.
 
Back
Top Bottom