Waziri Sitta: Dowans ni genge la ulaji wa vigogo watatu; tusiwalipe!

...Hii sasa inaonesha ni kweli, "Sitta alichakachuliwa kwenye nafasi ya Uspika". Ni dhahiri kwa vile inaonesha jinsi gani "Genge la Mafisadi" waliyomo kwenye "Mfumo-tata wa Ufisadi wa CCM" unavyoweza kutumia mbinu za kimkakati na au kisera katika kufanikisha ufisadi na ujambazi wa kiserikali. Kuna mambo matatu (3) muhimu ambayo Mh. Sitta anawajibu wa kuyatolea maelezo, nayo ni:
  1. Inaonesha yeye (Mh. Sitta) anawajua wamiliki wa Richmond (cum Dowans) na ndiyo maana anasema kwamba wanajiandaa kwa Urais 2015;
  2. Nini kilifichwa na Mh. Mwakyembe wakati hoja ya Richmond ilipokuwa inajadiliwa Bungeni; na
  3. Kwa nini Serikali (na Wabunge wa CCM) waliifunga hoja ya Richmond ilhali hatma yake ilikuwa inatokota na sasa tunaona matokeo yake?
Kama muungwana, Mh. Sitta anawajibu wa kuueleza umma wa Watanzania juu ya masuala hayo matatu. Na zaidi ataonekana shujaa (mfia nchi yake) kama ataamua kusema ukweli kisha asulubiwe kwa "collective responsibility" kama ilivyowahi kumkuta Mh. Agustino Lyatonga Mrema. Mh. Sitta anatakiwa aoneshe "uzalendo" na kusimama "kidete" ili aonekane kweli akitetea maslahi ya umma na si maslahi ya mafisadi wachache wa CCM.
 
Mzee Sitta umenena, ni watanzania wachache wenye kuelewa nini umemaanisha. Usikate tamaa endelea kutetea kodi zetu. wasilipwe kabisa hao, tunajua janja yao. Wamemaliza hela kwenye uchaguzi 2010, sasa wanasaka za 2015. :pray2:EEee Mungu tusaidie watanzania.
 
Tafadhalini someni mstari kwa mstari ni muhimu sana kuelewa kabla ya kufikia maneno ya mwisho yaliyoandikwa kwa italic style

(SOURCE:tanzania daima 8/12/2010)


NILITAMANI sana kukupigia simu siku ile ‘ulipochakachuliwa' kwenye nafasi ya uspika. Ni kwa bahati mbaya kwamba nilipoongoza majeshi kwenye ofisi za manispaa ya Arusha kudai matokeo ya kura za ubunge yatangazwe kama yalivyo simu yangu ilichukuliwa na namba zako nikazipoteza. Waliichukua vijana ambao wameteseka kwa muda mrefu ndani ya manispaa ya Arusha ambao maisha yao ya kesho hayajulikani.
Ni wale vijana ambao hutembea barabarani kutwa nzima wakiuza seti mbili za vikombe vya chai. Ni vijana hao ndio hawaoni mwanga wa kwenye maisha yao huko waendako. Ndio hao walioamua kufanya mabadiliko ya uongozi. Ndio waliosimama nje ya geti la jengo la manispaa ya Arusha wakidai matokeo.
Waliwasili hapo tokea saa 12 asubuhi na hawakutoka bali waliongezeka mpaka saa 11 jioni matokeo yalipotangazwa rasmi. Walipoamua kuchukua simu nilikubali na kuwaachia.


Mheshimiwa Sitta, nasikitika kushindwa kuwasiliana nawe kwa sababu nimekuwa rafiki yako wa karibu siku hizi na bila shaka kama ningewasiliana nawe ungenisikiliza na usingefanya maamuzi uliyoyafanya hivi sasa ambayo kimsingi ndiyo yanayonifanya nikusikitikie.
Tatizo kubwa ni kwamba ulipata nafasi ya kuwa shujaa zaidi ya mara mbili lakini hukuitumia. Sasa nakusikitikia kwa sababu njia uliyoiendea naona inakupeleka kusiko. Umenifanya nikumbuke maneno yangu niliyokuandikia kwenye makala ya Kalamu ya Mwigamba ya Agosti 26, mwaka jana iliyokuwa na kichwa kilichosema, "Mheshimiwa Sitta, Waweza kuwa Shujaa Ukiamua". Najua ulishasahau japo baada ya kusoma makala ile tuliongea kwenye simu. Naomba niweke hapa sehemu tu ya makala ile kwa ajili ya kukukumbusha nilishosema kabla sijafunga makala yangu ya leo:


"MHESHIMIWA naomba uniazime muda kidogo na uyapitie kwa makini sana yale yote kalamu hii iliyonuia kukueleza kwa kuwa kwa kiwango cha uelewa wa kalamu hii yatakuwa yanabainisha hatma ya maisha yako ya kisiasa. Hata hivyo, kalamu hii siku zote imeweka mbele uungwana na kutoa uhuru.

Kwa hiyo waweza kuchagua kuisikiliza ili uishi kisiasa na vile vile waweza kuchagua kutupilia mbali maneno yake kwa hatari ya kufa kisiasa ama kubaki kama ‘boya' katika siasa ambalo kama ujuavyo hufuata upepo. Lakini nakufahamu vizuri Mzee wa Viwango na Kasi a.k.a Standard and Speed (SS). Naamini hutatupilia mbali maneno ya kalamu hii bali utayatafakari vema si tu kwa faida yako ya kisiasa bali pia kwa manufaa ya taifa hili.

"Mheshimiwa Sitta, Spika wa Bunge la viwango Afrika Mashariki na Kati, kwanza kabisa niruhusu nikupe pole kwa yaliyokukuta ndani ya mji mkongwe wa Idodomya. Lakini napenda nikupongeze kwa stahili yako ya kuruka vihunzi.

Najua wengi wameponda habari za kwamba uliomba radhi na umeandikwa sana. Rafiki yangu mmoja alikuita ‘jemedari aliyesalimu amri'. Lakini mimi nina sababu mbili za kukupongeza kwa yaliyotokea ndani ya NEC. Kwanza kabisa kwa sasa wengi tumekosa uhakika ikiwa ni kweli uliomba radhi au hukuomba. Gazeti moja ninalolipenda sana na kuliamini wiki iliyopita liliandika kwamba wewe hukuomba radhi ila ulitamka kwamba "kutenda kosa si kosa, bali kurudia kosa". Maneno haya kama ni kweli ndiyo uliyoyatamka ndani ya kikao cha NEC basi sisi hatuwezi kujua ulichomaanisha mpaka wewe mwenyewe utakaposema.

"Sababu yangu ya pili ni kwamba kuna wakati ambapo jeshi hulazimika kunyanyua mikono ili kujipa muda wa kutafuta namna ya kujinasua. Huko nyuma niliwahi kueleza kwamba hata chama chako cha CCM imekuwa ni mbinu yake kwa muda mrefu. Si unakumbuka wakati wana CCM wengi mmekubali kwamba Waziri Mkuu ajiuzulu na kufanya Bunge lisiendelee kwa siku mbili kwa kuwa hakukuwa na serikali?
Ile ilikuwa ni mbinu ya kunyanyua mikono halafu umwangalie adui kakaaje halafu umshambulie. Kwa ujumla kile ambacho Watanzania wengi wamekuwa wakikiita kutoana kafara ndani ya serikali ya CCM ni kunyanyua mikono ili kutafuta njia ya kutoka na wewe unalijua zaidi hilo maana uko jikoni kwa CCM.

"Yaani wanafika mahali kwa sababu wamebananishwa wanakubali kwamba wamekosa na kufanya mambo machache ya kuudanganya umma kwamba wamekiri na wameamua kubadilika kumbe wanageuka ghafla na kurejea kule kule. Nachukulia mfano mwingine wa kukubali kwamba kumekuwa na ufisadi wa kutisha ndani ya serikali na Benki Kuu na kumfukuza kazi gavana wa Benki Kuu na kuagiza kwamba waliohusika warudishe pesa ama wapelekwe mahakamani na hatimaye ‘vifisadi' vichache vidogo vidogo vinafikishwa mahakamani kwa kesi za kizushi halafu serikali inatangaza kwamba inapiga vita ufisadi ili kuwafumba macho wadanganyika na wao waendeleze ufisadi tena kwa Ari mpya, Nguvu mpya na Kasi mpya.

"Kwa hiyo sitashangaa kama kauli yako iliyotafsiriwa na baadhi ya watu kwamba ni kuomba radhi, itakuwa ni kurudisha majeshi nyuma ili ujipange upya. Kama ndivyo nakuunga mkono kwa sababu moja. Kwamba kama ungeamua kuwa ngangari pale pale na kukataa kutoa kauli yenye ‘radha' ya kuomba radhi, wangekuvua uanachama pale pale na ungetoka ukiwa si mwana CCM na hivyo si mbunge na si Spika wa Bunge la Jamhuri. Najua kuna watakaosema kwamba kuna protokali kwamba ni lazima waiandikie ofisi ya bunge barua ya kuonyesha kwamba huna uanachama wa chama chao tena, na hivyo nafasi zako za ubunge na uspika ziko wazi. Lakini bado katika muda huo wa kufanya hivyo wewe usingekuwa na la kufanya tena. Usingekuwa tena na nguvu ya kuwaita majemadari wako na kupanga nao mikakati ya namna ya kutoka na yumkini wengi wangekataa hata kukusapoti wakihofia mustakabali wao. Ni muhimu kukumbuka kwamba wakati huo ungewaita ukiwa raia wa kawaida kwa hiyo wangeweza hata kutotilia maanani ushauri ambao ungekuwa unawapatia.


"Baada ya kusema hayo sasa nikueleze yajayo na kukupatia ushauri wangu. Mheshimiwa, kwa sasa unasimama njia panda. Mbele yako kuna njia mbili za kufuata, nazo ni kufyata mkia mbele ya mafisadi na ‘ukafa' kisiasa au kutunisha misuri mbele ya mafisadi ‘ukafa' kimaslahi ya muda lakini ukainuka juu ya ardhi ya Tanzania na kuwa shujaa wa aina yake ambaye kwa hakika tuzo yako itakuwa inakaribia ile ya Nyerere katika nchi hii na duniani. Ukichagua njia ya kwanza yafuatayo yanakusubiri: Kwanza unajua vizuri kwamba wakubwa wengi wa CCM wameshakuweka alama kwamba wewe ni mpinzani wao.

Kalamu hii inapenda ikuhakikishie kwamba hata kama utaamua kufyata mkia bado hutakuwa mwenzao. Wataendelea kukupiga vita maana hawatakuwa na uhakika kwamba hutawageuka tena. Ubunge wa Urambo Magharibi utaupata kwa shida kwa kuwa utakuwa na wapinzani watatu ambao wote utalazimika kuruka vihunzi vyao.
"Mpinzani wako namba moja watakuwa ni mafisadi ambao walitaka kukuvua uanachama. Watafanya kila liwalo usirudi bungeni na unajua maana ulishasema kwamba tayari wako jimboni wakitaka kukung'oa. …Wataendelea na juhudi zao za kukung'oa kwa sababu niliyoieleza hapo juu kwamba hawatakuwa na imani kwamba umefyata mkia kweli na kwamba hutawasulubu tena bungeni. Mpinzani wako wa pili watakuwa ni wananchi wenyewe wa Urambo ambao hata juzi umewahakikishia kwamba uko ‘ngangari' na kwamba utaendelea na kasi ile ile ya utendaji na baadaye ukawaambia waandishi wa habari kwamba utapigana na mafisadi mpaka kufa. Wana Urambo kwa kusaidiwa na watanzania kwa ujumla wataona kwamba umewasaliti wataazimia kukunyima kura zao.

Na mwisho utakuwa unapambana na kijana mmoja machachari kutoka CHADEMA ambaye tayari umesikia habari zake kwamba ametangaza kukuvaa. Utaponea wapi rafiki yangu. Na bado hata ukipenya kwenye tundu la sindano watahakikisha unabaki mbunge wa kawaida hata uenyekiti wa bunge usipate.

"Mheshimiwa Sitta, njia ya kwanza ni hatari kwako. Ni sumu itakayokuua pole pole lakini kwa uhakika. Utaendelea kutesa na uspika kwa mwaka mmoja uliobaki kabla rais hajalivunja Bunge hapo Agosti mwakani, lakini kwa taabu kubwa. Sisi Watanzania kwa ujumla tutakuzomea na hatutasita kukuweka kundi moja na mafisadi.

Maneno ya wachangiaji wengi waliochangia hoja ya kukuvua uanachama ndani ya NEC walisema unaichachafya serikali kwa maslahi binafsi ukitumia mgongo wa vita dhidi ya ufisadi. Napenda nikuhakikishie kwamba ukifyata mkia utakuwa umewawezesha Watanzania kupigia mstari kwamba madai hayo yalikuwa ya kweli. Hebu fikiria! Fikiria jinsi utakavyoporomoka na kushusha hadhi yako mbele ya jamii.
Fikiria watakavyokuona kumbe na wewe fisadi na kwamba vita yako ilikuwa kwa sababu ya kunyimwa fursa za ufisadi na uamue kukataa njia hii ambayo kila mwana CCM aliye upande wa pili anatamani uichukue halafu wakumalize.

"Njia ya pili ni hii. Kwamba utaamua kusimama imara. Na kwamba utaonyesha uimara wako hapo Novemba utakapoongoza bunge kuikataa taarifa ya serikali juu ya utekelezaji wa maazimio ya bunge kuhusu mkataba tata wa Richmond. Na utaongoza bunge kuwa kali kabisa na kwa kuanzia, Bunge litamlamzimisha waziri mkuu kujiuzulu na asipofanya hivyo utaliongoza Bunge kupokea na kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.

Akina Slaa wako tayari kuleta hoja ndani ya bunge na unao wabunge wengi ndani ya CCM ambao watakuunga mkono kukubali hoja hiyo. Na hata hivyo, sheria itakuwa ikikulinda kwamba serikali imelidharau bunge.
"Mheshimiwa, maamuzi haya hayatapita hivi hivi. Watakaa kwenye kikao chao na kukuita ujieleze kwa nini umekaidi maelekezo yao. Natoa ushauri kwamba usihudhurie kikao hicho maana dhamiri inanituma kuamini kwamba ‘wataku-kolimba' kwa kukuwekea vile ‘vitu' vyao kwenye microphone. Usiende kabisa pale utakapoambiwa kwamba unaenda kuhojiwa.

Na kama hutajua agenda za kikao halafu ghafla kufika huko ukasikia unaambiwa ujieleze, basi utasimama kana kwamba unataka kujieleza halafu unatoka nje ya kikao na kupanda shangingi lako na kutokomea nyumbani Urambo. Utawaacha wakujadili wenyewe, waulize maswali wenyewe, wajibu wenyewe na kuamua kukuvua uanachama wenyewe.
"Wakati huo, utakuwa umeshaweka mikakati na makamanda wako. Na nakushauri mikakati hiyo uiweke sasa, usisubiri wakati huo. Waulize kwanza mmoja mmoja upate wale wanaokuhakikishia kwamba watapigana mpaka mauti itakapowakuta. Hao ni lazima ukubaliane nao kwamba mbele yenu kuna kuvuliwa uanachama na ubunge wenu kwa pamoja. Hao mkubali na muwe tayari kwa hilo. Na kwa sababu hiyo mtakuwa tayari kuhamia chama cha upinzani chenye sera na mikakati inayofanana na hiyo ya kwenu. Kalamu hii inakupa uhakika mmoja tu, kwamba wewe mheshimiwa Sitta ukipata wabunge wenzako watano tu ambao watakuwa tayari kuvuliwa uanachama na wakajiunga na upinzani.

Halafu tukakodi helikopta mkazunguka nchi nzima mkawaeleza wananchi kile kinachoendelea ndani ya lile dude kubwa liitwalo CCM, ndiyo utakuwa mwisho wa CCM, mwanzo mpya, mwanzo wa fikra mpya, mabadiliko halisi, uhuru wa pili wa mtanzania na maendeleo yenye ‘viwango na kasi'. Kama vile Nyerere anavyotukuzwa kwa kujitoa mhanga kuwafukuza wakoloni, ndivyo na wewe na wenzako mtakavyotuzwa pamoja na mashujaa wenzenu akina Mbowe, Slaa na wengineo kwa kuwafukuza wakoloni weusi.

Mwisho wa siku utamshuhudia yule rafiki yako mnayepambana naye akiwa kwenye viti vya upinzani bungeni …. na wewe ukiwa umekalia kiti cha Waziri Mkuu ndani ya ukumbi huo huo.
"Huenda haya ninayoyazungumza yakaonekana kama hadithi za Alinacha lakini ukitafakari kidogo na kuirejea historia ya dunia ukitilia maanani historia za watu kama Nelson Mandela, utanielewa na utachukua hatua ninazokueleza leo na mwisho wa siku utaishukuru kalamu hii kwa kukusaidia kuwa Shujaa wa Mwaka na shujaa wa mwongo".


Tafakari maneno yangu ya Agosti, mwaka jana uone ni uamuzi upi uliouchukua. Kwanza kuhusu Richmond na Dowans dada yake, ulifyata mkia ukafunga hiyo hoja bila hitimisho na leo taifa linakabiliwa na kulipa bilioni 185 kama faini kwa Dowans. Na kama nilivyokueleza kwamba kuufyata mkia kusingekusaidia, ni kweli umepenya ubunge wa Urambo kwa taabu na hatimaye uspika wakakuchinjia baharini.

Sasa umefanya kosa lingine la kukubali kuwa kwenye baraza la mawaziri tena uwaziri wenyewe wa Afrika Mashariki ! Halafu bado unatamba kwamba utaendeleza vita dhidi ya ufisadi !? Mheshimiwa umekosea sana. Hujui kinachokusubiri mbeleni na nataka nikutahadharishe kwamba mwanzo wa mwisho wako kisiasa umeshaanza. Muda si mrefu tutakusahau. Endelea kufuatilia vyombo vya habari.

Watanzania hawakuamini kwamba ni wewe uliyejinasibu kwa kupigana vita dhidi ya ufisadi leo unakubali kuwa kwenye baraza la mawaziri la rais yule yule, waziri mkuu yule yule, na mbaya zaidi la chama kile kile ambacho juzi tu kilikutosa kwenye uspika kwa sababu kwamba kwa kupigana kwako na ufisadi ulihatarisha maslahi ya chama.

Leo kwa kukubali kuwa kwenye baraza lile lile ambalo kama unavyojua leo likiamua kuingiza Richmond namba mbili utakuwa umehusika kwa kanuni ile ya uwajibikaji wa pamoja, unawezaje kuuzuia umma kukubaliana na maelezo ya wajumbe wa NEC ya chama chako waliosema : unaichachafya serikali kwa maslahi binafsi ukitumia mgongo wa vita dhidi ya ufisadi ?
Sasa ngoja jamaa walete hoja binafsi bungeni kwamba wewe na kundi lako mmeliingizia hasara taifa kwa kusababisha taifa lilipe bilioni 185 kumbe mlikuwa na ajenda binafsi ya kutaka kumng'oa waziri mkuu na hatimaye na nyinyi muingie serikalini kwenye uwaziri. Sijui mtaponea wapi ?

Na kuna kauli ile ya Kardinali Polycarp Pengo kwamba waliokuwa wakipiga kelele wakati ule ndani ya CCM za vita dhidi ya ufisadi ni kwa sababu walikuwa wamekosa nafasi za ‘kufisidi'.
Mara baada ya kukamilisha ‘mission' mliyokuwa nayo mkafunga mjadala na kutulia.

Na sasa mmeingizwa serikalini ndo mtatulia kabisa. Maneno ya Kardinali hayatakuwa yametimia ?

Tafakari na uchukue hatua ! vinginevyo mimi rafiki yako nasubiri kuona.
 

Dowans ndiyo ilirithi mkataba wa Richmond na kwa mujibu wa Sitta, njama za kuileta kampuni hiyo zilisukwa na vigogo watatu ambao ni wabunge wa muda mrefu na wamekuwa wanahusishwa na matukio mbalimbali ya ufisadi, na mmojawao ni mwanasheria maarufu aliyebobea katika masuala ya mikataba ya kimataifa. Kwa sababu za kitaaluma, gazeti hili litahifadhi majina yao kwa sasa.


Doh! Huna hata haja ya kuuliza ni nani????

Get your bucket of salted POPCORN 2015 Movie has just started!!!
 
atakuwa Fabregas au Van Pierse Au Alhaji-Mtaalamu wa Bariadi? lakini mind you Bariadi ni kubwa ipo Magharibi/Mashariki nk
 
WAMETAJWA SANA, NIMEWACHOKA! Andrew Chenge, Rostam Aziz [huy c mtanzania, msomali haramia], na Edward Lowasa!
Mtu mwenye documents za serikali wekeni. TUIFANYE JF KAMA WIKILEAKS YA WATANZANIA. Hapo tutafanikiwa kuijenga nchi ye2.

Hapo Bwn umefika, nasikia kabla ya hukumu hiyo kutolewa EL alikuwa Parie sijui ndo alikwanda kusuka na hou majaji?

Tusiogope kufungiwa JF ifanye kazi kama Wikileak kila kitu kiwekwe hadharani ili kama serikali sijui takukuru hawataki kufanya kazi umma wa Watanzania utawaukumu.
Je Ndg yangu Dr Mwakyembe anasemaje kuhusu hili maana yeye alikuwa M/kiti wa tume iliyofichua huu uozo. Sasa tena ni wakati wake kama mwanasheria kupambana ili nchi yetu tuipendayo Tanzania isikamuliwe hadi DAMU TUKIONA.
WOTE MLIOKO SERIKALINI PAMBANA KUINUSURU TANZANIA NA WIMBI LA MAJAMBAZI.
TENA KILA WAKIONEKANA MITAANI AU MAHALI POPOTE TUANZE KUWAZOMEA MAANA NI WEZI NA MAJAMBAZI!!!!!!!!!!!
 
Wako wengine zaidi!!!!! Ni hawa hapa_;
4: Jakaya Mrisho Kikwete- kiranja mkuu wao wa kuwalinda na kuwapa hifadhi ndani ya CCM na serikali; Huyu ndiye aliyewasifu wakati wa kampeni na kuwapa sifa ya kuendelea kupeta!!!
5: Benjamin William Mkapa; ndiye aliyefungua milango ya kuangamiza taifa hili kiuchumi-EPA ndiye aliyetajwa kuwa authority; na mengine yakazaliwa baadaye!!!!!!!!!!!!!!!!
Hawa ni miongoni mwa waliotajwa na CDM Mwembeyanga, na Jangwani!!!!; Tangu wakati huo hawajajitokeza na kukana,ingawa waziri 6 amewaaficha kwa kutowataja magazetini!!!!!!!!!!
Kwa vile tangu watajwe hawajakana, na mimi najificha ndani ya tajo hizo mbili kama kinga!!!!!!!!!!!!!!!!!

Cha ajabu-wote ni vigogo ndani ya sisiemu chama tawala, na serikali yake, na kuwapa wakati wote kinga za kichama na kiserikali!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!Bungeni wanategemea sana wingi wa kura za sisiemu kuwa kinga yao-bila shaka spika Anna na Naibu wake Ndugae nao watawalinda, hasa dhidi ya makombora ya Chief Whip Tundu Lissu na makamanda wake; maana ndiyo waliowafadhili kupata viti hivyo!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Sidhani kama umewasaidia wasomaji hapa! Kama huna ushahidi si ungekaa kimya badala ya kuanzisha kitu halafu unataka mpaka upigiwe makofi ndo utaje kama vile wew ni mwanamuziki aliye jukwaani na ambaye nasubiri ashangiliwe ndo anengue.
 
Naona Sitta kaamua kujitoa Muhanga, he have got nothing loose. kama wale wa palestine na kama uwaziri wenu unautaka haya chukua.
Bado mwakyembe na wengi neo.
 
Wanajulikana ..ni ROSTAM AZIZ-raia wa IRAN anayemiliki passport ya kiTanzania na ambaye amaeanza kuhamishia biashara zake na mitaji yake Uganda,Kenya na south africa,Mzee wa Banki M a.k.a kikofia chekundu,Mamvi na wapambe wao Karamagi na Chenge
Expose them !!!
 
Wednesday, 08 December 2010 08:13

ASEMA HIZO NI NJAMA ZA GENGE LINALOTAFUTA FEDHA ZA UCHAGUZI MKUU 2015

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI mpya wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri, amesema hatua yoyote ya kulipa fidia ya Sh 185 bilioni kwa kampuni ya Dowans, ni kuhujumu uchumi wa nchi.

Sitta, ambaye aliongoza Bunge la Tisa lililotikisa nchi kwa kuibua kashfa za ufisadi, pia amesema kuna kila dalili za genge linalohujumu nchi kuandaa mpango wa kutafuta fedha kwa ajili ya uchaguzi wa 2015.

Sitta alikuwa akitoa maoni yake baada ya kuulizwa na Mwananchi kuhusu hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuhishi wa Kibiashara (ICC) iliyolitaka Shirika la Umeme (Tanesco) kuilipa Dowans Sh185 bilioni kutokana na kuvunja mkataba bila ya kufuata taratibu.

Tanesco ilivunja mkataba huo wa kuzalisha umeme mwaka 2008, ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya kuisha, ikieleza kuwa mkataba huo ulikiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma. Tanesco imesema itazungumzia suala hilo baada ya hukumu hiyo kusajiliwa nchini.

Hukumu hiyo imeamsha mjadala mkubwa uliokuwa umepoa kuhusu kampuni ya Dowans ambayo ilirithi mkataba uliobainika kuwa wa kifisadi wa Richmond Development LLC ambayo ilitakiwa izalishe umeme wa dharura wakati kulipotokea tatizo kubwa la umeme mwaka 2006.
Jana Sitta alizidi kuukoleza mjadala huo aliposema: "Kuna kila dalili ya genge la watu wenye fedha chafu kujaribu kuandaa mpango wa kuihujumu nchi."
"Hakuna uhalali wowote wa kuilipa Dowans kiasi hicho cha fedha, si haki hata kidogo.
"Kuilipa Dowans Sh185 bilioni ni kuhujumu uchumi wa nchi, na kuna kila dalili ni genge lilelile ambalo sasa linatafuta fedha kwa ajili ya uchaguzi wa 2015."
Sitta, ambaye aliweka bayana dhamira yake ya kuendelea kupambana na ufisadi mara baada ya kuapishwa kuwa waziri, aliendelea kusema: "Ni genge ambalo halina huruma na nchi na umasikini wa Watanzania... na kama likiachwa lijiimarishe, Watanzania wasubiri matatizo makubwa zaidi huko mbele.
"Genge hili limekuwa likiwafanya Watanzania kuwa ni wajinga wasioweza kufikiri. Ni kwa sababu limeshika nchi, linafikiri siku zote litafanya mambo ya hovyo na kuangaliwa... sijui linawatafuta nini Watanzania wazalendo?"
Mbunge huyo wa Urambo Mashariki ambaye wakati akiwa spika Bunge lilijadili kwa kina kashfa ya Richmond iliyokuwa na matokeo ya kihistoria baada ya Edward Lowassa kulazimika kuachia uwaziri mkuu na kufuatiwa na mawaziri wengine wawili, alisema kinachofanyika sasa ni genge hilo kujiandalia mazingira ya kujikusanyia mabilioni ya fedha chafu za uchaguzi wa 2015.
Pamoja na Tanesco kuvunja mkataba na Dowans mwaka 2008, shirika hilo la umma liliibuka na mapendekezo ya kununua genereta za kampuni hiyo zinazoendeshwa kwa gesi, mapendekezo ambayo Bunge la Sitta liliyakataa kwa maelezo kuwa yanakiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma.
Msimamo huo wa Bunge ulimfanya mkurugenzi wa zamani wa Tanesco, Dk Idris Rashid kukubali kwa shingo upande akilaumu wanasiasa kwa kukwamisha masuala ya kitaalamu na kunawa mikono kwamba asilaumiwe kwa matatizo ya baadaye ya umeme.


Wakati nchi ikiwa imeingia kwenye tatizo jingine kubwa la umeme linalokaribiana na la mwaka 2006, ICC ilitoa hukumu ambayo imeamsha mjadala huo na Sitta alisema jana kuwa Tanesco isilaumiwe kwa uamuzi huo akielekeza lawama zake kwa genge hilo ambalo hakutaja walio ndani.
"Nitashiriki kikamilifu kuhakikisha maslahi ya taifa yanalindwa na hakuna mianya yoyote ambayo genge hili inaweza kuitumia kuhujumu nchi," alisema Sitta, ambaye ni mmoja wa wanasiasa wazoefu walio kwenye baraza jipya la mawaziri.


"Hili nataka uninukuu vizuri, kwamba sasa ni dhahiri kuna mkono wa ambao kila dalili unaonyesha ni genge linalotaka kufanya hujuma. Linachotaka kufanya ni mchezo mchafu ambao sisi serikalini tutajitahidi kuuzuia."
Alifafanua kwamba watu hawapaswi kuitwisha mzigo Tanesco kwani uamuzi uliangal;ia kwa kina maslahi ya taifa kuliko baadhi wanavyojaribu kupotosha.


Sitta alisema huu ni wakati wa kuhakikisha genge hilo halifanyi hujuma zake kwa nchi.
Sitta pia alidai kuwa baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi nchini wamekuwa wakikwepa kufungua kesi zao kwenye mahakama za ndani kwa hofu ya kuumbuka.
Dowans ilifungua kesi hiyo kwenye mahakama hiyo ya ICC ambayo makao yake makuu yako Paris, Ufaransa.
:angry:

Sitta: Kuilipa Downs ni kuhujumu uchumi
 

Dowans ndiyo ilirithi mkataba wa Richmond na kwa mujibu wa Sitta, njama za kuileta kampuni hiyo zilisukwa na vigogo watatu ambao ni wabunge wa muda mrefu na wamekuwa wanahusishwa na matukio mbalimbali ya ufisadi, na mmojawao ni mwanasheria maarufu aliyebobea katika masuala ya mikataba ya kimataifa. Kwa sababu za kitaaluma, gazeti hili litahifadhi majina yao kwa sasa.


Doh! Huna hata haja ya kuuliza ni nani????

Get your bucket of salted POPCORN 2015 Movie has just started!!!

Mambo haya yanauma sana.Yaani wananchi wetu wanaogelea kwenye dimbwi la umaskini, lakini wengine wanjichotea mihela tu.Lakini hata lini Mungu ataendelea kunyamazia mambo haya?
 
Sitta afyatuka
• Adai Dowans ni genge la ulaji wa vigogo watatu

na Mwandishi wetu


amka2.gif
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema ametishwa na hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC), iliyoipa ushindi Kampuni ya Dowans dhidi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), lakini akasema haya ni matokeo ya genge la watu wachache wanaofahamika ambao wameamua kutafuna rasilimali za taifa bila huruma. Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano katika miaka mitano iliyopita na ambaye aliruhusu Bunge kujadili masuala kashaa ya kifisadi, alisema hayo jana katika mazungumzo maalumu na Tanzania Daima kwa simu kutoka Kampala Uganda.
Alisema vigogo hao waliileta Dowans makusudi baada ya kampuni ya awali iliyopewa zabuni ya kufua umeme wa dharura, Richmond Development LLC, kushindwa kutimiza malengo.
Dowans ndiyo ilirithi mkataba wa Richmond na kwa mujibu wa Sitta, njama za kuileta kampuni hiyo zilisukwa na vigogo watatu ambao ni wabunge wa muda mrefu na wamekuwa wanahusishwa na matukio mbalimbali ya ufisadi, na mmojawao ni mwanasheria maarufu aliyebobea katika masuala ya mikataba ya kimataifa. Kwa sababu za kitaaluma, gazeti hili litahifadhi majina yao kwa sasa.
Kwa mujibu wa Waziri Sitta, hili ni genge ambalo limeamua kutafuna rasilimali za taifa bila huruma, na bila kujali maslahi ya vizazi vijavyo.
“Nakwambia hakuna jambo ambalo linakera kama kuona genge la watu wachache limeamua kutafuna rasilimali za taifa hili bila huruma. Wameshindwa kufikiria kizazi kijacho kitanufaika vipi.
“Hii inaletea hisia kuwa kundi hili linaendesha hujuma nzito dhidi ya mali za taifa hili… haiwezekani hata kidogo kununua jenereta halafu unasema huu ni uwekezaji… huu si uwekezaji,” alisema Sitta.
Alisema hukumu iliyotolewa dhidi ya TANESCO ni mwendelezo wa hujuma kubwa dhidi ya taifa kwa vile inaonekana wazi kwamba kuna kundi la watu maarufu ambalo ndilo chanzo cha suala hilo, na ambalo kwa namna moja au nyingine lilishiriki kuhujumu mwenendo wa kesi ili serikali ishindwe, wao walipwe pesa.
Alisema Dowans ni mali ya wachache hao ambao wameamua kufumba macho ili kufanikisha malengo yao kibiashara, na kwamba umefika wakati serikali iamue kwa nguvu zote kuwashughulikia bila huruma kwa vile ni sawa na wahujumu uchumi.
“Sisi tulioko serikalini lazima tukomeshe hali hii… kwani mchezo huu umekuwa ukijirudiarudia mara kwa mara. Lazima tujipange vizuri ili kuhakikisha nchi haichezewi tena.
“Serikali iko kwa ajili ya watu. Sasa iweje tushindwe kujipanga vizuri, tunataka kuona wananchi wetu wananufaika na rasilimali zilizopo, na hiyo ndiyo sifa (yetu) kwa taifa,” alisema Sitta.
Alisema hata hukumu hiyo ni matokeo ya watu fulani ambao walitaka kesi hiyo isikilizwe nje ya nchi kisha wagawane fungu la fedha zitakazopatikana.
“Inashangaza mno kuona kuna watu fulani wamekuwa wakipendekeza kesi hizi zisikilizwe nje ya nchi… lazima tujiulize, wanavuna nini? Hata hii inawezekana wazi ulikuwa mpango wao wa kuhakikisha wanapokamilisha mambo yao wanagawana wanachovuna.
“Wamesababisha mahakama zetu zinyang’anywe uwezo wa kusikiliza kesi hizi... wanawapelekea Wazungu… hii haijakaa sawa hata kidogo,” alisititiza.
Kauli ya Sitta ni ushahidi mwingine wa vita ya makundi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali ambayo imeibuliwa upya na sakata la Dowans.
Sitta anatoa kauli kali hii siku moja baada ya mwanasheria mkongwe anayeheshimika nchini, Jaji Mark Bomani, kuzungumza na gazeti hili juzi akisema ushindi kampuni ya Dowans dhidi ya TANESCO ni matokeo ya namna taifa lilivyoshindwa kushughulikia vema mikataba mikubwa ya kimataifa katika uwekezaji na nishati.
Alisema: “Sakata la TANESCO na Dowans linasikitisha. Nafikiri liliendeshwa kwa namna ambayo ingewafikisha wahusika pabaya kama ilivyotokea.
“Fundisho ni kwamba unaposhughulikia masuala yanayogusa mikataba ya kimataifa kama haya yanayohusu nishati, madini na mengineyo, umakini mkubwa unatakiwa,” alisema Bomani.
Mjadala wa mitambo ya Dowans, uliwahi kuligawa taifa kwa kipindi kirefu mwaka 2008 baada ya Kamati Teule ya Bunge chini ya Uenyekiti wa Dk. Harrison Mwakyembe baada ya kutoa taarifa ya kuchunguza uhalali wa kampuni ya Richmond na mtakaba kati yake na serikali.
Kutokana na taarifa iliyowasilishwa bungeni Februari mwaka 2008 aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alijiuzulu ikiwa ni ishara ya kuwajibika kama kiongozi mkuu wa ofisi yake iliyodaiwa kushiriki katika kuiwezesha Richmond kushinda zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura.
Hali ilipokuwa tete, aliyekuwa Mkurugenzi wa TANESCO, Dk. Idris Rashid, aliishauri serikali kuinunua mitambo hiyo, lakini baadhi ya wanasiasa walilisukuma Bunge kukataa kununua mitambo hiyo kwa maelezo kuwa Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004 inakataza serikali au taasisi zake kununua mitumba.
Wengine walikwenda mbali zaidi wakisema ununuzi wa mitambo hiyo utaifaidisha Dowans ambaye ni dada yake Richmond.
Katika uamuzi wa ICC uliotolewa na jopo la majaji watatu chini ya uenyekiti Gerald Aksen na wasuluhihi Swithin Munyantwali na Jonathan Parker, TANESCO imeamriwa kuilipa Dowans fidia ya zaidi ya sh bilioni 36 na riba ya asilimia 7.5 kwa mwaka inayofikia kiasi cha zaidi ya sh bilioni 26 tangu Juni 15 mwaka huu, hadi fidia hiyo itakapolipwa.
Kadhalika, jopo hilo liliamuru malipo ya sh bilioni 60 na riba ya asilimia 7.5 ambayo ni sawa na sh bilioni 55 kuanzia Juni 15, 2010 hadi wakati wa malipo.
Jopo hilo lilisisitiza kuwa ada na gharama za wasuluhishi wa ICC na utawala ni sh bilioni moja zinazotakiwa kulipwa na pande zote.
Source Tanzania Daima

Tanzania Daima hawawezi kutaja majina kwa sababu mmoja katika hao watatu ni kiranja wa gazeti lao.
 
...Hii sasa inaonesha ni kweli, "Sitta alichakachuliwa kwenye nafasi ya Uspika". Ni dhahiri kwa vile inaonesha jinsi gani "Genge la Mafisadi" waliyomo kwenye "Mfumo-tata wa Ufisadi wa CCM" unavyoweza kutumia mbinu za kimkakati na au kisera katika kufanikisha ufisadi na ujambazi wa kiserikali. Kuna mambo matatu (3) muhimu ambayo Mh. Sitta anawajibu wa kuyatolea maelezo, nayo ni:
  1. Inaonesha yeye (Mh. Sitta) anawajua wamiliki wa Richmond (cum Dowans) na ndiyo maana anasema kwamba wanajiandaa kwa Urais 2015;
  2. Nini kilifichwa na Mh. Mwakyembe wakati hoja ya Richmond ilipokuwa inajadiliwa Bungeni; na
  3. Kwa nini Serikali (na Wabunge wa CCM) waliifunga hoja ya Richmond ilhali hatma yake ilikuwa inatokota na sasa tunaona matokeo yake?
Kama muungwana, Mh. Sitta anawajibu wa kuueleza umma wa Watanzania juu ya masuala hayo matatu. Na zaidi ataonekana shujaa (mfia nchi yake) kama ataamua kusema ukweli kisha asulubiwe kwa "collective responsibility" kama ilivyowahi kumkuta Mh. Agustino Lyatonga Mrema. Mh. Sitta anatakiwa aoneshe "uzalendo" na kusimama "kidete" ili aonekane kweli akitetea maslahi ya umma na si maslahi ya mafisadi wachache wa CCM.

Sio Sitta huyu tunayemfahamu. Hawezi kuyafanya haya. Alishindwa kuyafanya haya akiwa na nafasi kubwa zaidi ya Uspika sasa hawezi tena.
 
Wana JF tukaze buti, mwendo unazidi kunoga!!!!!! Tuendeleze aliyotoboa waziri 6!!!!!!!! Hivi CCM ya Kikwete ni tofauti na ile ya waasisi?????? Mbona haina tofauti na Taliban dhidi ya watanzania?????????
 
Kuyamaliza haya yote ni kudai katiba mpya!!!!!!!!! Katiba mpya ndio itawamaliza mafisadi!!!!!!!! Mnaona kenya hivi sasa mambo ni mazuri kabisa......katiba mpya inawalinda!!!!!!!
 
Tafadhali someni mstari kwa mstari ili kujenga taswira ya mada.

Source:Tanzania Daima 8/12/2010

Tafakari maneno yangu ya Agosti, mwaka jana uone ni uamuzi upi uliouchukua. Kwanza kuhusu Richmond na Dowans dada yake, ulifyata mkia ukafunga hiyo hoja bila hitimisho na leo taifa linakabiliwa na kulipa bilioni 185 kama faini kwa Dowans. Na kama nilivyokueleza kwamba kuufyata mkia kusingekusaidia, ni kweli umepenya ubunge wa Urambo kwa taabu na hatimaye uspika wakakuchinjia baharini.


Sasa umefanya kosa lingine la kukubali kuwa kwenye baraza la mawaziri tena uwaziri wenyewe wa Afrika Mashariki ! Halafu bado unatamba kwamba utaendeleza vita dhidi ya ufisadi !? Mheshimiwa umekosea sana. Hujui kinachokusubiri mbeleni na nataka nikutahadharishe kwamba mwanzo wa mwisho wako kisiasa umeshaanza. Muda si mrefu tutakusahau. Endelea kufuatilia vyombo vya habari.

Watanzania hawakuamini kwamba ni wewe uliyejinasibu kwa kupigana vita dhidi ya ufisadi leo unakubali kuwa kwenye baraza la mawaziri la rais yule yule, waziri mkuu yule yule, na mbaya zaidi la chama kile kile ambacho juzi tu kilikutosa kwenye uspika kwa sababu kwamba kwa kupigana kwako na ufisadi ulihatarisha maslahi ya chama.

Leo kwa kukubali kuwa kwenye baraza lile lile ambalo kama unavyojua leo likiamua kuingiza Richmond namba mbili utakuwa umehusika kwa kanuni ile ya uwajibikaji wa pamoja, unawezaje kuuzuia umma kukubaliana na maelezo ya wajumbe wa NEC ya chama chako waliosema : unaichachafya serikali kwa maslahi binafsi ukitumia mgongo wa vita dhidi ya ufisadi ?
Sasa ngoja jamaa walete hoja binafsi bungeni kwamba wewe na kundi lako mmeliingizia hasara taifa kwa kusababisha taifa lilipe bilioni 185 kumbe mlikuwa na ajenda binafsi ya kutaka kumng'oa waziri mkuu na hatimaye na nyinyi muingie serikalini kwenye uwaziri. Sijui mtaponea wapi ?


Na kuna kauli ile ya Kardinali Polycarp Pengo kwamba waliokuwa wakipiga kelele wakati ule ndani ya CCM za vita dhidi ya ufisadi ni kwa sababu walikuwa wamekosa nafasi za ‘kufisidi'.
Mara baada ya kukamilisha ‘mission' mliyokuwa nayo mkafunga mjadala na kutulia.

Na sasa mmeingizwa serikalini ndo mtatulia kabisa. Maneno ya Kardinali hayatakuwa yametimia ?

Tafakari na uchukue hatua ! vinginevyo mimi rafiki yako nasubiri kuona.
 
Back
Top Bottom