Waziri sitta amedanganya

Zao la Kata

New Member
Apr 8, 2011
3
0
Leo Waziri Sita amepata kibano cha kutosha kutoka kwa Waziri wa Sheria wa Zanzibar. Mzanzibar huyo amemwambia Mh.Sitta kwamba ni mungo kutokana na kauli ya kusema kwamba Zanzibar imeshirikishwa vya kutosha katika kuandaa Mswada wa Katiba mpya. Swali linakuwa ni je, Sitta alikuwa hajui ukweli huo au aliamua tu?. Au ndiyo CCM wanambebesha zigo hilo ambalo lina chembe chafu za uongo ambazo Mh. Sitta kama asipokuwa makini zitamchafua Kisiasa?. Ndugu yangu Sitta, usiwaamini hao CCM, siyo wenzako. Wamekupeleka Zanzibar ili ukachafuke. Ila nachokusifu ni kwamba wewe ni mkweli. Umetufafanulia ni kwa nini HATI YA DHARURA imetumika. Hiyo nafasi ulivyoitumia kama angepewa TAMBWE HIZA, nakuhakikishia Wazanzibar wangemfanya UROJO.
 
huyu Sitta naye bana...yaani linakuwa kama tambala la deki ...linasemwa weee huku sisiemu lakini bado tu ..utadhani mtoto asiye kuwa na kwao..hata mlichape mlifukuze linarudi tu
 
Mtoto wa nyoka ni nyoka; Sitta siyo kusema yeye ni msafi, bali katika msafara wa vipofu yeye ana kengeza.
 
Kigogo, wanaotafuta maoni ya wananchi ni wabunge kupitia kamati ya katiba,sheria na utawala. Kwa hiyo Sitta hakuwa Zanzibar kama CCM wala waziri, bali kama mbunge na mjumbe wa kamati hiyo.
 
Mtoto wa nyoka ni nyoka; Sitta siyo kusema yeye ni msafi, bali katika msafara wa vipofu yeye ana kengeza.

Hapo umenena kweli katika msafara wa mamba na kenge kweli huwamo!! Sitta ni mnafiki tu hana lolote na wenzie wanamjua hivyo!!!
 
Back
Top Bottom