Waziri Selina Kombani (Katiba na Sheria) na Hatima ya Katiba Mpya

Katiba ina garama gani ambayo sirikali imeshndwa?? Ajipange atafute la kuzungumza na Watz, sio hewa tena, hata sisi tuna uwezo wa kuchanganua mambo. Hatukubali kuburuzwa tena. Katiba mpya ni muhimu. Watanzania waitake ninyi muikate!
 
Waziri Kombani ametukana wananchi | Gazeti la MwanaHalisi

CELINA Kombani – Waziri wa Sheria na Katiba, ametukana Watanzania. Hata akiomba radhi hatakubaliwa.
Watanzania wenye nia nzuri wanasema tuwe na Katiba mpya inayoondoa uwezekano wa wananchi kuchinjana pale watakapokuwa wameshindwa kuelewana.

Lakini Kombani anawajibu kuwa Katiba mpya haina maslahi kwa serikali wala taifa. Kwamba serikali haina fedha za kuanzisha mchakato wa kuandika katiba. Kwamba wanaodai katiba hawajampelekea madai yao.
Wenye nia njema kwa taifa lao wanasema kuwepo mkataba mpya (katiba), kati ya watawala na wataliwa; ule unaolingana na matakwa ya sasa; wenye kwenda na wakati tuliomo na siyo wakati wa ukoloni na utawala wa kikiritimba wa chama kimoja.

Lakini waziri Kombani anawajibu kuwa wale wanaodai kuwepo katiba mpya ni watu wa barabarani na wasiokuwa na uelewa juu ya masuala ya katiba na utawala. Wenye uchungu na nchi hii wanasema kuwepo katiba inayoruhusu kila mmoja kushiriki siasa za nchi yake – kuchagua na kuchaguliwa – na siyo ubaguzi uliowekwa ndani ya andiko kuwa ili uchaguliwe sharti uwe mwanachama wa chama chochote.

Lakini Kombani anasema serikali yake inaridhika na katiba iliyopo na kwamba itaendeleza utaratibu wake kuiwekea viraka kila itakapoona inafaa. Watanzania wenye shauku ya kuona ustawi wa nchi yao wanasema kuwepo katiba mpya, itakayokuwa mwongozo katika kila kitu ili kuepusha migogoro kwa kujenga misingi ya haki.

Wanasema ukasuku wa "umoja, amani na utulivu" si lolote si chochote, mahali ambapo hakuna katiba inayounganisha fikra za watu wote na kusimamia haki ya kila mmoja. Lakini Kombani anasema serikali anayotumikia hailazimiki kuwa na katiba mpya kwa vile kuwa na katiba mpya siyo sera ya Chama Cha Mapinduzi.

Ni bahati mbaya kwamba tunatukanwa na mtu mdogo sana aliyeibuliwa mvunguni na kuitwa waziri. Lakini ni bahati mbaya zaidi, kwamba Kombani amemtukana na kumtukanisha Rais Jakaya Kikwete ambaye amempa kazi.

Celina Kombani, kwa kauli zake, andhalilisha umma wa Tanzania; anajenga ghadhabu mioyoni mwa wengi; anaelekeza watu watupe chini matumaini yao; wakate tamaa na kuamua kuishi utumwani milele.

Wenye nia nje na nchi hii wanasema kuwepo tume huru ya uchaguzi. Tume isiyo ya rais. Tume isiyo na madaraka ya kuteua rais, bali yenye majukumu ya kusimamia uchaguzi ili wananchi wapate matokeo ya uchaguzi wao. Celina anasema, tena kwa jeuri, kuwa hayo hayamo katika ilani ya uchaguzi wa chama chake.

Kipofu huyu; kipofu na siyo asiyeona; hawezi kutambua haki ya wananchi kumrudi mbunge au rais wao. Hawezi kuheshimu uhuru wa wananchi kuchagua watu safi na siyo wezi wakuu na majambazi yaliyokubuhu kwa kuliibia taifa.

Celina Kombani hawezi kuona umuhimu wa fursa kadha wa kadhaa za wananchi kukataa kutawaliwa na wezi ambao wamethibitika kwa ushahidi wa mahakama. Huyu ni waziri wa sheria anayekataa kuwa na katiba mpya inayotoa fursa zote hizo ambazo zinakuza uhuru wa mtu binafsi; kunawirisha fikra za jamii na kuwapa wananchi madaraka ya kujitawala kwa kusimamia uongozi safi uliochaguliwa.

Kwa jeuri au kutojua, Celina Kombani anasema wanaodai katiba hawajampelekea madai yao. Kwa akili yake, anaona kuwa ana uwezo wa kushika utumwani taifa hili kama anavyopenda; na hadi atakapoamua kulifungulia.

Waziri huyu anafikiri kuwa mabadiliko ya katiba huanza kama madai ya wastaafu wa iliyokuwa jumuia ya Afrika Mashariki. Anataka orodha. Anadhani ni jambo la binafsi.

Hii ina maana yake. Kwamba akiwa mtawala, Celina hawezi kuona mambo yanayoweza kuleta hatari ya baadaye hadi atakapoandikiwa kwenye karatasi na kukabidhiwa mkononi. Kipofu.

Celina Kombani ametukosea, lakini kuna aliyetukosea zaidi kama taifa. Ni Rais Kikwete. Amemtoa wapi mtu wa aina hii ambaye anajenga mazingira ya mifarakano katika jamii?

Orodha ya watakaoitwa mbele ya mahakama ya kimataifa kueleza kushiriki kwao katika kuleta machafuko nchini Tanzania, sasa inaendelea kukua.
Tulianza na John Chiligati. Wasomaji wa makala zangu wakaleta majina mengine: Yusuf Makamba na John Tendwa.

Mmoja wa wasomaji aliandika kwa ukali. Soma aliyoandika: "Kwa nini humtaji rais? Unamwogopa?" Sasa Kombani amejiunga na orodha ya wasiopenda nchi yao. Watu wenye shari. Wasiopenda amani. Waliotayari kuona taifa linaagamia alimradi wao wako madarakani.

Hakuna Mkenya awezaye kujivuna sana kwamba ana katiba. Ipi? Iliyokuja baada ya kukatana mapanga; kuuana na kuwa wakimbizi?

Katiba iliyochelewa, inayokuja kuzika, kukausha majeraha na kuandika kumbukumbu za maafa? Tanzania inahitaji katiba mpya leo. Benjamin Mkapa, rais mstaafu amesikika, ingawa kwa kupitia sauti ya mwingine na katika nchi ya jirani ya Burundi. Amefumbuka.

Ni maneno yake kuwa Katiba ndiyo "moyo wa nchi; moyo wa binadamu unaofanya mwili mzima ufanye kazi."
Rais Kikwete, Celina Kombani atafanya nini pale kama siyo kukuumbua na kukuletea uadui zaidi na Watanzania wenye nia njema kwa taifa lao?

Tusifike anakotaka Kombani. Waziri binafsi aweza kukimbia; lakini kuna sisi ambao tuliapa hatutatoka hapa, ije mvua lije jua. Kuna umma usiong'oka kwao.
 
Kweli ametukosea sana!!! Ni vema akatuomba radhi!! Yeye ni mtu gani asiyetaka mabadiliko???????????????????
 
Kwake mabadiliko ni kubalishana ofisi za uwaziri huku akiwaambia ndg zake pale msimbazi centre kuwa mungu ndie aliyewawezesha yeye na mshikaji wake haj mponda kuwa mawaziri kupitia mja wake jakaya.... Which is true.

Tumpe muda atarejea ktk utimamu wake punde
 
Haya ndiyo matunda ya kumpa kusimamia sheria mtu mwenye background ya ualimu wa UPE
 
Nchi za watu viongozi kama hawa huwa ni siku hiyo hiyo anawajibishwa!

Huyo waziri inaonekana hata mhajui nini majukumu yake kama waziri wa Sheria na Katiba.
Huo ni Ununda wa kupindukia:whoo:
 
Hivi ana mume huyu au ndiyo wale wale akina alikwina? Ndiyo wanakuwa na kawaida ya kuleta dharau kwa wapiga kura, si mnakumbuka ya SS alivyokuwa anamsifia EL alivyo mwanaume wa shoka?
 
Lakini waziri Kombani anawajibu kuwa wale wanaodai kuwepo katiba mpya ni watu wa barabarani na wasiokuwa na uelewa juu ya masuala ya katiba na utawala.

Kwa hiyo anasema Mkapa na majaji wa Mahakama za juu Tanzania walionukuliwa kutaka katiba mpya nao ni "watu wa barabarani wasiokuwa na uelewa juu ya masuala ya katiba na utawala" ?
 
"He who pays the piper calls the tune" this is what minister Celina Kombani implies when she says:
"the country's donors and other development partners have often raised concern over such obsolete and bad laws, where some have threatened to stop aid. ''Tanzania has so many outdated laws. We need to amend them as soon as possible. My office is ready to provide all necessary support," Source: Daily News :Minister calls for review of obsolete laws

This is sheer absurd because when the Tanzanians called for New Constitution, she claimed it is too expensive and unnecessary. But what the donors demand that is urgent! Now I get it... whose government do we have... donors'! We should ask the donors to force the government to facilitate us to write a new constitution? I hate to think this way but it seems this is the way!
 
Sheria nyingi zilizopitishwa na Bunge mwaka huu ni zile ambazo wafadhili walishazidai. Zile ambazo wananchi wanadai serikali haitaki kuzitunga. Siku wafadhili wakisema katiba irekebishwe utaona itatokea mara moja. Jiulize sheria ya NGOs na ile ya Terrorism.

Pengine kuna sababu. Wafadhili wakisema sheria itungwe au iliyopo irekebishwe, wanatoa pesa kufanya hivyo. Kwanza wanachukuliwa maafisa wa serikali, ikiwa ni pamoja na waziri, kutembelea nchi fulani eti kujifunza namna sheria yao ilivyotungwa na inavyofanya kazi. Pili wanatoa pesa za kuendesha seminar mbali mbali hivyo wahusika wanapata ulaji. Tatu wanaleta consultants ambao huja na copy paste ya sheria husika hivyo watendaji wetu wanakuwa hawahitaji kuumiza vichwa vyao. Nne kama sheria hiyo ikishapita, kunakuwepo na msururu wa semina nyingi za kuisambaza.

Katika hali kama hii, ngekuwa wewe ni serikali, ungetekeleza ya wananchi au ya mfadhili?
 
me nadhani celina kombani kapewa wizara iliyomzidi upeo na ujuzi.ni sawa na mtu aliyenunuliwa kiatu over-size.its been only a month or two lakini tayari its obvious hana uelewa na anayoyatamka
 
Celine Kombani, Another slip of the tongue?????? Watch out, why dont you think before you talk??

Wananchi wanataka Katiba Mpya hutaki,
Wafadhili wanataka sheria mpya haraka saana,oh sheria nyingi outdated tutatoa support.

Kumbuka umechaguliwa na wananchi ili uwatumikie, hukuchaguliwa na wafadhili ili uwanyeyekee.

Wake up Celina
 
me nadhani celina kombani kapewa wizara iliyomzidi upeo na ujuzi.ni sawa na mtu aliyenunuliwa kiatu over-size.its been only a month or two lakini tayari its obvious hana uelewa na anayoyatamka

Pia nina wasi wasi na uwezo wa katibu mkuu wa wizara hiyo katika ku-handle mambo ya sheria kwani Bwana Oliver Mhaiki profession background yake ni education na librarianship na sio law.
 
me nadhani celina kombani kapewa wizara iliyomzidi upeo na ujuzi.ni sawa na mtu aliyenunuliwa kiatu over-size.its been only a month or two lakini tayari its obvious hana uelewa na anayoyatamka

Au hausgal unampa u office manager
 
Kwa Tanzania cheo anaweza kupewa mtu yeyote. Sishangai Celina kuwa waziri wa Sheria. Zile enzi za kumweka waziri kwa kufuata taaluma yake ziliondoka na Nyerere. This is Animal Farm my friends. we are the Benjamins and they are Pigs." Ignorance is Strength" - Robert Owen, the Author of Nineteen Eighty Four:
 
Back
Top Bottom