TANZIA Waziri Salome Mbatia afariki dunia, maswali yaibuka!

Nadhani mzee mwanakijiji nikupe wazo,HAPA JF TUMUOMBELEZE MAMA KWA 7 DAYS(1 WEEK)NA KATIKA KUMUOMBOLEZA TUIWEKE,ILA BADA YA MAOMBOLEZO KUISHA TUITOE ,AU UNAONAJE MKUBWA
 
mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi.
pole kwa wafiwa wote.
 
jamboonormal_pichayaajali.jpg

Picha ya Ajali ya Bi. Salome Mbatia jioni ya leo...

Mungu azilaze roho za marehemu wote pema peponi, Amina

Mwenyezi mungu amlaze mahali pema peponi. (RIP)

Ajali hii jinsi gari lilivyoharibika inaonyesha kabisa kuna uzembe wa aidha speed na kutokuwa mwangalifu unapokuwa barabarani. Hizi gari zina safety bags mbele na pembeni pamoja sizioni kama zilijifyatua maana magari haya ya bei mbaya lazima yawe na vitu kama hivyo. Tungoje report ya askari wa usalama barabarani.(Vile vile inakuwaje mawaziri wanakaa mbele?)
 
Twendeni mbele turudini nyuma,na huyu zitto nae alikuwa anatoka wapi?,mana kwa ripoti,mama salome alikuwa kwenye kampeni za ccm za uchaguzi huu ujao,dr matayo alikuwa anatoka songea kukagua kilimo cha umwagiliaji,je zitto nae alikuwa anatoka wapi?
 
kwani wee hujui ?? mimi sijui ningekuwa najua ningekwambia mkuu !
 
Nadhani mzee mwanakijiji nikupe wazo,HAPA JF TUMUOMBELEZE MAMA KWA 7 DAYS(1 WEEK)NA KATIKA KUMUOMBOLEZA TUIWEKE,ILA BADA YA MAOMBOLEZO KUISHA TUITOE ,AU UNAONAJE MKUBWA

miye kwa kweli sijali how long itakaa hapa, kama watu wengi washaona nitaitoa kwani situkuzi kifo. Nilitaka tu watu waone na kupata ukaribu wa wale waliokuwa eneo la ajali. Walioko nyumbani wataiona kwenye magazeti huko...
 
Zitto hakuwa anatoka, alikuwa anelekea Songea kwenye kampeni za Udiwani... ukisoma kurasa chache huko nyuma utaona imeelezwa.
 
Huu ndio uswahili, nimewaambia ni picha ya ajali, mlidhania ni picha ya harusi? Nilitoa muda mrefu wa watu kuamua na hakuna aliyepinga sasa mmeiona ati "inatisha"... mlidhania watu wako mezani wanakula?

Sasa hapo unakejeli, Hiyo picha kwa ufupi inatisha na sio vema kuiweka hapa. Kwa namna moja utazidi kuiumiza familia ya Mbatia. Iwapo una picha ambayo haionyeshi jinsi marehemu alivyokuwa akiteseka katika dakika zake za mwisho, itakuwa ni bora zaidi kuliko hiyo. Hili ni suala la UTU jamani...
 
Inakuwaje haya mafuso hayana break yanaruhusiwa kutembea barabarani? Nani abebe lawama? Saa ingine tunamsingiziaMungu bure kwa uzembe wetu sisi wanadamu!
 
Sasa hapo unakejeli, Hiyo picha kwa ufupi inatisha na sio vema kuiweka hapa. Kwa namna moja utazidi kuiumiza familia ya Mbatia. Iwapo una picha ambayo haionyeshi jinsi marehemu alivyokuwa akiteseka katika dakika zake za mwisho, itakuwa ni bora zaidi kuliko hiyo. Hili ni suala la UTU jamani...

soma posti yangu ya kwanza kuhusu kubandika hiyo picha sikuficha na niliwaambia watu kuwa inaonesha sehemu ya Marehemu, ulipinga?
 
Bwana alitoa, bwana ametwaa. Jina lake na lihimidiwe. Poleni sana wafiwa wote, Mungu awajalie moyo mkuu katika kipindi hiki kigumu! Wametangulia wenzetu nasi njia ni hiyo hiyo, Cha msingi tujiandae muda wowote kwani hatujui saa wala dakika ya zamu yetu itakapo timu.
 
Nimepata picha ya eneo la tukio, kwa kweli inasikitisha sana. Sijui kama kuiweka hapa itakuwa sawasawa kwani sehemu ya mwili wa Marehemu inaonekana.

Ok sikusoma hapa.. Hata hivyo picha umeshaiweka natumai ni kutokana na idadi kubwa ya waliomba kuona picha hiyo.

Zaidi msimamo wangu upo pale pale kuwa picha hiyo haifai kubandikwa.
 
Back
Top Bottom