Waziri Nundu ndani ya DAKIKA 45 ITV,sasa hivi.

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,377
1,952
wana JF,waziri wa uchukuzi, Mh omar nundu anaongea sasa hivi ndani ya independent television (ITV) wadau mnaweza angalia na kumsikiliza,ili mwisho tuweke maoni yetu kutokana na mahojiano hayo.

Mimi naendelea kuanalia na kumsikiliza.....baadae tuchangie kama great thinkers!
 
Sie wa satelit Dish tushawasahau hao ndugu wa IPP. Hawapatikani hewani
 
waziri wa uchukuzi mheshimiwa Omar nundu.anahjiwa na selemani semunyu,ndani ya dakika 45 itv sasa hivi,ebu angalieni kipindi na kisha great thinkers mtoe maoni yenu kulingana na majibu yake
 
Dr Omar Nundu yuko vizuri! Yuko focused sana Mzenj huyu
Binafsi ninamuona kama mfano halisi wa waziri anayekifahamu kile anachokifanya na laiti kama Jk angekuwa na mawaziri walau sitya watendaji kama huyu,basi tungekuwa tofauti na tulipojikuta leo
 
Hana jipya huyu!
Mshaurini asibariki ujenzi wa Eapoti za kisiasa kama Bagamoyo!
 
Binafsi ninamuona kama mfano halisi wa waziri anayekifahamu kile anachokifanya na laiti kama Jk angekuwa na mawaziri walau sitya watendaji kama huyu,basi tungekuwa tofauti na tulipojikuta leo

Nundu ni Waziri bora kabisa kwenye serikali! Hana mbwe mbwe anazijua idara zote za wizara yake!! Anazungumzia reli ya Kati hasa gode gode
 
Anapania kuifufua ATC,na mpaka sasa serikali imetoa bilioni Tano kati ya bilioni 16 zilizopangwa ili kulifufua shirika,anasema ile issue ya airbus ni nzito na hawezi kuiongelea sasa hivi na anasubiri serikali ichukue hatua zaidi kwa wahusika,anasema serikali haiwezi kulipa zile gharama za ukodishaji ndege hiyo kwani si halali.
Kuhusu reli anashukuru uzalendo umewarudia wafanyakazi na wamewaachia wao kulisimamia na jukumu la serikali litakuwa kuwawezesha tu
 
Ameteleza tayari anasema kuna vijigazeti uchwara (raia mwema)amelitaja mwenyewe kwamba lilimsema vibaya linamuandama mno kwa kumfuatilia zaidi yeye.
Anasema linataka kumgombanisha na rafiki yake kawambwa. Kimsingi naye anatetea safari zake za nje kama rais wake Jk.na ametufungua macho kuhusu mmiliki wa Exim bank kwamba yuko china na alimfuata wakaongea
 
wana JF,waziri wa uchukuzi, Mh omar nundu anaongea sasa hivi ndani ya independent television (ITV) wadau mnaweza angalia na kumsikiliza,ili mwisho tuweke maoni yetu kutokana na mahojiano hayo.

Mimi naendelea kuanalia na kumsikiliza.....baadae tuchangie kama great thinkers!

Huyu waziri anatumia muda mwingi kufuatilia wajenzi wa bandari wenye gharama Shs 250mill na Shs500mill. Shs500mill ni kitu gani kwa serikali. Pesa kibao zitumika kwenye shughuli za hovyo, sasa serikali inakosa shs250mill?
 
wana JF,waziri wa uchukuzi, Mh omar nundu anaongea sasa hivi ndani ya independent television (ITV) wadau mnaweza angalia na kumsikiliza,ili mwisho tuweke maoni yetu kutokana na mahojiano hayo.

Mimi naendelea kuanalia na kumsikiliza.....baadae tuchangie kama great thinkers!

Namuona ni kama hajui kujibu hoja badala yake anatoa toa maneno ya kuudhi au kukera mfano "wametumwa" "kigazeti uchwara" yaani yeye akitofautiana na mtu ni uchwara, nina imani kama angeandikwa vema na Raia Mwema asingeliita ni gazeti uchwara!
 
Sjiui kwa nini huyu waziri kila akiongea anasema 'wametumwa'? Kila mwenye kungelea kero za idara ya hii wizara yake katumwa! Ni nani anatuma watu? Haya si madharau kwa watanzania? kwamba hawajui mbele wala nyuma mpaka 'watumwe' la kusema?
 
Amemaliza mahojiano na binafsi nimetafakari na nimemuona kama ni mtu mwenye kuyajua mazingira yake ya kazi na ni msimamizi mzuri,
Tatizo ni hasira alizonazo zinamuondolea sifa ya uongozi, bali anapaswa kuwa mtendaji,akiwa chini ya kiongozi.na ni aina fulani ya viongozi wenye kuendekeza uhasama na visasi kwa wale ambao ni wakosoaji kwake..kwani yeye huwaona kama maadui na "WAMETUMWA"

Kiongozi mzuri ni yule ambaye anakubali kukosolewa pale anapokosea au hata kusikiliza upande wa pili bila jazba.kwani unakuwa kiongozi wa watu wengi wenye elimu,uelewa na maoni tofauti kwa wakati mmoja. Na wote mkiwa wananchi wa nchi moja kwa maslahi yenu na ya vizazi vyenu vilivyopo na vya baadae. Kama anadiriki kuwafokea waheshimiwa wabunge live,tena ndani ya bunge,akiwa na cheo Cha uwaziri wa miundombinu,Itakuwaje akiwa na madaraka zaidi ya hayo? kwa mfano, ukuu wa majeshi,uwaziri mkuu na au urais, na ikatokea wananchi au viongozi wenzie wakatofautiana naye kimtazamo. katika utekelezaji wa majukumu kiutendaji au kimtazamo? Nini kitawapata? tutafakari

Kuna uwezekano mkubwa humu ndani ya JF, kuna wengi ambao mnamfahamu kwa undani bila shaka mtaendelea kutujuza, na kwa vile katika mahojiano yake leo ameanzisha mjadala mwingine kitaifa kwa kuyaita baadhi ya magazeti ambayo yanaheshimika kwa wasomaji wengi nchini na yenye waandishi na wahariri makini nchini. kuwa ni "magazeti uchwara"(kauli ambayo si stahiki kutolewa na kiongozi mwandamizi kama yeye)
Ni imani yangu kuwa tutarajie kusikia mengi kutoka kwa watanzania wa kada mbalimbali kuhusiana na kauli hiyo tata.
 
Back
Top Bottom