Waziri Nundu aipa Sumatra siku 7 kuitema Majembe

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173

Waziri Nundu aipa Sumatra siku 7 kuitema Majembe

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 24th December 2010 @ 23:30


KILIO cha Wamiliki wa mabasi yanayofanya safari zake jijini Dar es Salaam na yale yaendayo mikoani, kimesikika na sasa serikali imeiamuru Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kusitisha haraka mkataba wake na kampuni ya udalali ya Majembe.

Amri hiyo ya serikali ilitolewa jana na Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu aliyeagiza amri hiyo kutekelezwa ndani ya siku saba, akitaja kuwa ni njia mojawapo ya kutekeleza mpango wa kuondoa matatizo ya usafirishaji wa abiria.

Nundu alitoa agizo hilo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa anatoa taarifa ya majibu na mapendekezo ya utekelezaji wa hoja 14 zilizowasilishwa na Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) na Chama cha Wamiliki wa Daladala (DARCOBOA).

Alisema Kampuni ya Majembe Auction Mart imekuwa ikifanya kazi za askari wa usalama wa barabarani kinyume cha sheria kwa kukagua matairi, kuangalia leseni ya barabara, bima, taa za magari na vioo wakati hawana ujuzi wala mamlaka ya kufanya hivyo kisheria.

“Ili kuondokana na kero hiyo Sumatra wameagizwa kusitisha mkataba wake na Majembe ifikapo Desemba 31 mwaka huu,” alisema Nundu.

Nundu alisema wizara yake imepitia kwa makini hoja zote 14 ambapo hoja nne zitaendelea kufanyiwa kazi kwa kina, hoja tatu zimekataliwa na hoja saba zimeanza kutekelezwa kwa kuzingatia maagizo yanayotolewa na Wizara.

Katika maagizo hayo, Majembe imezuiwa kusimamia ukaguzi wa madaraja ya mabasi na kwamba kuanzia Desemba 9, mwaka huu kazi hiyo imekuwa ikifanywa na Sumatra.

Agizo lingine lililotolewa na wizara na kutakiwa kutekelezwa mara moja ni Sumatra kuacha kutoa lugha chafu kwa Taboa na mamlaka zinazohusika kuwaondoa wapiga debe katika vituo vyote vya mabasi nchini.

Nundu ameagiza wafanyakazi na wakala wa mabasi kupewa vitambulisho maalumu na ifikapo Januari 15 mwaka kesho, mamlaka zinazohusika ziwe zimeandaa utaratibu wa kuwatambua wafanyakazi na wakala wa makampuni ya mabasi ili kudhibiti wapiga debe.

Pia Sumatra imetakiwa kukutana na wamiliki wa mabasi kujadili ongezeko la nauli kisha hoja hiyo ipelekwe kwenye kikao cha wadau na ikiwezekana jambo hilo liwe limefanyika ifikapo Januari 31, 2011.

Waziri Nundu alisema hoja zinazoendelea kufanyiwa utafiti kabla ya kutolewa maamuzi ni kuhusu vibali vya kukokota mabasi yanayoharibika, maombi ya kutaka mabasi kuwa bidhaa za mtaji na kulegeza masharti ya leseni na ratiba za mabasi ili gari linaloharibika iwe rahisi kutuma basi jingine kuchukua abiria badala ya kusubiri basi lililoharibika litengenezwe.

Maombi mengine yatakayopitiwa kwa makini kabla ya Serikali kutoa maamuzi ni pamoja na mabasi kuruhusiwa kufanya safari kwa saa 24, yaani na usiku na mchana, kufuta utaratibu wa mabasi kupitia kwenye stendi za mabasi hata kama hakuna abiria anayeshuka wala kupanda ili mabasi hayo yalipe ushuru, na suala la wageni kujihusisha na usafirishaji abiria nchini, ni jambo ambalo linaonekana tishio la kibiashara kwa Taboa.

Nundu alisema maombi ya Taboa kutaka mabasi ya abiria kutopimwa kwenye mizani hayakubaliki kwa kuwa upo uthibitisho kwamba baadhi ya mabasi yamekuwa yakizidisha uzito.

Akijibu hoja ya kuondoa matuta barabarani, Nundu alisema pamoja na kero zinazosababishwa na matuta hayo yataendelea kuwepo ili kuhakikisha madereva wanapunguza mwendo wanapopaswa kufanya hivyo.

Hata hivyo, Wizara ya Uchukuzi kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi zitachukua hatua mwafaka za kuhakikisha kuwa ujenzi wa matuta barabarani unafuata viwango pamoja na kuweka alama zinazoonesha kuwepo kwa matuta hayo.

Pia Serikali imetupilia mbali malalamiko ya Taboa dhidi ya Sumatra ya kushirikisha katika vikao wajumbe ambao sio wasafirishaji na kueleza kuwa upo umuhimu wa kuendelea na mikutano inayoshirikisha watoa huduma ya usafiri na walaji.

Ndulu alisema anaishukuru Taboa kwa kusitisha mgomo wao na kukubaliana na majibu pia mpango wa utekeleza ji wa kuondoa matatizo ya usafirishaji na kuahidi kuwa Wizara yake itaendelea kufuatilia kwa kina utekelezaji huo ili kuboresha huduma ya usafirishaji.
 
Waziri Nundu aipiga ‘stop' Majembe Friday, 24 December 2010 20:40

Fidelis Butahe na Zulfa Msuya
WAZIRI wa Uchukuzi, Omari Nundu ameitaka Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), kusitisha mkataba wake na Kampuni ya udalali ya Majembe ifikapo Desemba 31 mwaka huu. Taarifa hiyo itakuwa ya furaha kwa madereva wa mabasi yafanyayo safari zake ndani ya miji na yale yaendayo mikoani baada ya kupambana na maofisa wa Majembe kwa muda mrefu, wakilipishwa faini kubwa, kuwekwa mahabusu na kuzuiwa kufanya shughuli zao kwa muda mrefu na hivyo kupunguza "hesabu".

Wamiliki na madereva wa mabasi walipinga mara kadhaa uamuzi wa Sumatra kuitumia kampuni hiyo na wakati mwingine kuendesha migomo ya kutoa huduma za usafiri, wakidai kuwa maofisa wa kampuni hiyo ya udalali hawaelewi vizuri masharti ya leseni za usafirishaji. Walidai kuwa maofisa hao wa Majembe waliwalipisha hadi faini ya Sh250,000 kwa madai ya kufanya makosa ya kukiuka masharti ya leseni, na kushauri polisi ndio waendelee na jukumu lao la kawaida la kusimamia sheria hizo.

Kilio chao kilimfikia waziri ambaye pia ameagiza kuwa wapigadebe waondoke katika vituo vyote vya mabasi nchini, huku akizitaka mamlaka husika kabla ya Januari 15 ziwe zimeandaa utaratibu wa kuwatambua wafanyakazi na wakala wa makampuni ya mabasi. Kutokana na tamko hilo kuanzia Januari Mosi mwakani Majembe, ambayo imekuwa ikitumiwa na taasisi nyingi za serikali, haitajihusisha tena na kazi hiyo na badala yake Sumatra imetakiwa kuandaa wafanyakazi kwa ajili ya kufanya kazi hiyo. Waziri Nundu aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuwa "haiwezekani kila kazi ifanywe na Majembe tu... tulikaa na Chama cha Wamiliki wa Mabasi (Taboa), pamoja na Chama cha Wamiliki wa Daladala (Darcoboa) na walitoa mapendekezo yao na haya ndiyo majibu yake".

Alisema: "Kutokana na utata uliojitokeza katika ukaguzi wa madaraja ya mabasi kwa kutumia Majembe, niliagiza Sumatra kusimamia wenyewe zoezi hilo na walishaanza tangu Desemba 9 mwaka huu. Kwa hiyo kuanzia Desemba 9 Majembe hawasimamii tena ukaguzi wa madaraja ya mabasi." Akionekana kukerwa na jinsi Majembe inavyopewa zabuni na taasisi tofauti, Waziri Nundu alisema: "Kuhamisha watu katika nyumba, Majembe; udalali wa magari, Majembe; kila kitu Majembe. Kampuni hii ina kazi zake bwana, sasa katika hili Sumatra na Jeshi la Polisi ndio watakaohusika na utekelezaji," alisema Nundu.

Kuhusu wapiga debe ambao wanalamikiwa kuwa wanapewa vitambulisho na baadhi ya mawakala na kushirikishwa kwenye vikao vya maamuzi huku wenye mabasi wakitengwa, Nundu alisema serikali imeagiza kwamba waondoke katika vituo vyote vya mabasi nchini mara moja. Alisema kuwa mamlaka zinazohusika ziandae utaratibu wa kuwatambua wafanyakazi na wakala wa makampuni ya mabasi ikiwa ni pamoja na kuwatafutia vitambulisho maalum. "Najua kwamba hili suala la wapigadebe limekuwa kero ya muda mrefu, kuanzia sasa waanze kutafuta njia mbadala ya kujipatia kipato, wakiamua kuchakalika watakuwa matajiri wakubwa, lakini kwa sasa hamna ruhusa tena.

Mpiga debe anafikia hatua ya kumpiga ‘kabari' dereva wa basi, hii ni sawa kweli," alihoji Nundu. Akizungumzia suala la nauli za mabasi Nundu aliagiza zoezi la kupitia nauli ambalo linasimamiwa na Sumatra, lifanyike haraka iwezekanavyo na likamilike ifikapo Januari 31 mwakani na kuiagiza Sumatra ikutane na wamiliki wa mabasi kujadili maombi yao kabla ya kufanya kikao cha wadau wote wa usafiri nchini. "Kuna suala la vikao vya wadau wa Sumatra kuwa na wajumbe ambao si wasafirishaji na wasioelewa usafirishaji; mpango wa sasa wa kuwahusisha watoa huduma za usafiri na walaji uendelee. Hata hivyo Sumatra wakutane na wamiliki kwanza kujadili kero zao kabla ya kukutana na wadau wote," alisema Nundu.

Alisema kwamba licha ya baadhi ya mabasi kugundulika kuzidisha uzito ni muhimu zoezi la upimaji mabasi liendelee ili kukidhi matakwa ya sheria ya usalama barabarani pamoja na kulinda miundombinu ya usafiri. Kuhusu matuta, Waziri Nundu alisema: "Matuta barabarani yamekuwa kero na ni chanzo kingine cha ajali, lakini bado kuna umuhimu kuwa na matuta ya barabarani kama njia ya kuhakikisha kuwa madereva wanapunguza mwendo kasi. "Wizara ya Uchukuzi kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi tutachukua hatua muafaka ili kuhakikisha ujenzi wa matuta haya unafuata viwango," alisema Nundu. Kuhusu mapendekezo ya Taboa kwamba bidhaa za mabasi ya abiria zinazoingizwa nchini zisamehewe kodi, Nundu alisema kuwa pamoja na kuwa misamaha ya kodi ni kivutio cha uwekezaji, lakini inaathiri mapato ya serikali hivyo serikali italiangalia suala hilo ili kuhakikisha haliathiri mapato yake.

Pia alizungumzia mapendekezo ya Darcoboa kuhusu nauli ndogo ikilinganzishwa na gharama kubwa za uendeshaji na akasema wameagiza kuitishwa kwa mkutano wa wadau na marekebisho ya bei yawe yamekamilika nchi nzima ifikapo Januari 31 mwakani. "Walilalamikia pia suala la kutozwa faini kubwa kuliko makosa wanayofanya, hivyo Wizara kwa kushirikiana na Sumatra, wadau na mwanasheria mkuu kupitia upya adhabu hizo kabla ya Juni 2011," alisema Nundu.

 
hii imetulia tunangoja utekelezaji

Na ingependeza zaidi kama kwenye Halmashauri na Manispaa kote nchini wakaamrishwa kurudia majukumu yao ambayo wamaeyabinaifsisha kwa makampuni ambayo miliki yake ina uhusiano na watendaji hao waandamizi wa serikali za mitaa.......................shughuli kama ukusanyaji wa kodi mbalimbali na mapato mengine ya taasisi hizo.......................Vinginevyo huduma hafifu zitaendelea kutukabili na huko kero zikiendelea kuchanua bila ya udhibiti wowote ule na Halmashauri na Manispaa zikiendelea kulia na mapato duni.............We really need a transformation...............
 
Kuna ka uwezekano ka Majembe kwenda mahakamani kwa kufutiwa mkataba? Kama kako, itakuwa "tunaruka mkojo tunakanyaga mavi"
 
Hili suala la kwamba serikari itashitakiwa siyo kweli in this case. Kwani Majembe walikuwa ni contractor wa Sumatra hivyo Sumatra ndiyo iliyomuajili Majembe kufanya kazi on their behalf. Kwa hiyo ni ngumu kidogo kwa contractor kumshitaki Serikali kwani inaonekana Majembe akiwa in wawakilishi wa Sumatra walikuwa wakifanya kazi chini ya Kiwango na pia nje ya anga zao.
 
..waangalie tu, Sumatra, au serikali, wasije wakaburuzwa mahakamani na kulazimishwa kulipa mabilioni ya fedha.
 
siyo waziri kufikia hatua ya kuvunja mikataba lazima awe amfuatilia mkataba
 
aaagr hata sioni majembe wana fanaya kitu cham maana. Zaidi ni unyanyasaji tuu wa madereva wa dala dala na Rushwa tuu.
 
Back
Top Bottom