Waziri ngeleja akata viuno akiomba kura jukwaani mwanza

Zurii

Member
Mar 6, 2012
64
24
WaziriNgelejaakikatamauno.JPG WaziriNgelejaakikatamauno.JPG WaziriNgelejaakikatamauno.JPG


Waziri Ngeleja akisakata rhumba kwa kukata kiuno.


Mbunge wa Afrika Mashariki, Dk. Amani Walid Kabouru (kushoto) na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Joyce Masunga wakisakata muziki.


…Akihutubia wananchi kwenye kampeni hiyo.
WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja, mwishoni mwa wiki iliyopita alijikuta akitoa shoo ya bure baada ya kupanda jukwaani, kisha kusakata muziki.
Waliompa sapoti ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Dk. Amani Walid Kabouru na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Joyce Masunga ambao nao waliserebuka stejini.

Ngeleja alifanya hivyo katika eneo la Mwembe Sangara, Kirumba,wakati wa kuhitimisha kampeni za kumnadi aliyekuwa mgombea udiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Kirumba Jijini Mwanza, Jackson Robert ‘Masamaki’ – mgombea ambaye alibwangwa na Bahati Kahungu aliyekuwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita.

Kana kwamba yupo kwenye steji ya bendi ya Twanga Pepeta, Ngeleja aliendelea kunogesha kampeni hizo kwa takribani dakika 10 akisakata rhumba na kuwaacha hoi wananchi, kabla ya kuhutubia kuomba kura kisha akamaliza kwa staili ile ile aliyopandia jukwaani kwa kucheza muziki.

HABARI/PICHA: MASHAKA BALTAZAR, MWANZA
 
duh, mbaba ana uno huyu, lol, utadhani kalikonekti gridi ya taifa.
 
nilijua nitakuta video anasakata. Kumbe mi still picture, sijaona kiuno hapo....
 
wajukuu wa cameron viuno vinawapa tabu sana mkiona tu mnatoa tafasiri za uingereza hapo ni mwanza jamani
 
Labda akiendele kukizungusha kiuno sana ataweza ku produce megawati 1...... Atakua ametusaidia sana.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom