Umenena vyema ndugu. Siasa za TZ zina mambo ya ajabu kabisa....mimi naona hata wabunge kuikataa bajeti ya wizara ya nishati na madini na kuitaka serikali ijipange vyema ni mchezo wa kuigiza tu.
Kama sikosie (ruhusa kusahihishwa) bajeti ya kila wizara uwa inajadiliwa kwanza katika level ya kamati husika! Kwa case hii, ni kamati ya nishati na madini; sasa kamati hiyo ilipaswa iikatie bajeti hiyo mara moja kwa vigezo ambavyo waziri mkuu alivisema wakati ikitoa hoja ya kuhahirishwa kwa majadiliano ya bajeti hiyo.
Kama kamati iliipitisha bajeti hiyo na kisha wabunge (ambao wengine wamo kwenye iyo kamati) wakaikataa bajeti hiyo, basi hapa kuna mushkeri!! Au ndio uwezeshaji wa ndugu Jairo ulifanya kazi?!
Kamati inapaswa kuwachunguzwa pia na kuwajibishwa kwa mujibu wa kanuni kama ikibainika kuna foul plays!!
Asilimia ngapi ya wanakamati wakikubali ndo bajeti inapita katika kamati?? Yawezekana sio wote wanakamati wamekubali bajeti ipite? Hawa kenge ndo walio kwenye msafara wa mamba ndo wa kuvua ubunge na kenge wengine wizarani wafungwe gerezani....