Waziri Nchimbi umetia aibu

leo asubuhi hii (morning magic-magicfm) waziri wa michezo nchimbi kapigiwa simu, kaulizwa inakuwaje
juzi uwanjani neti(nyavu) ilikatika ikabidi ifungwe katani(ilichukua zaidi ya dk 5 kufunga katani) na fainali yake jana
umeme umekatika, tunaomba maelezo yako!! Aaagh jamaa akakata simu!!
Hii aibu sijui nani atai-handle!!


tuliambiwa kuongozwa na ccm kwa kipindi kingine ni janga la kitaifa hii ni trailler picha yenyewe inakuja
 
kumbuka matukio haya..kadhia ya wimbo wa taifa, juzi makatani(sijui mchezaji angepiga shuti hadi yakakatika ingeamuliwaje) na jana funga kazi tanesco wakatia CD zao pale taifa..watanzania tumeona na dunia yote imeona..!!
 
waziri akikata simu unampigia aliyemteua.
Huyo atacheka tuu
tteeh teeh teh ndugu mwandishi hihihihihi unajua hahahahaha kwikwikwikwi haya mambo ndugu mwandishi ehehehehe ule uwanja nilifungua mimi bwahahahaha vipi mwandishi studio hapo hehehehehehehe AC zinaoperate? hehehehe kik kik kik kik kik nikupe uongee na Riziwani? kwakwakwakwakwa hahahaha asanteni kwa kunisikiliza hihihihihihiheee
 
we unafikiri akipokea hiyo simu ataongea nini, zaidi ya kumbwelambwela na kufikilia posho na urais.
 
Leo asubuhi hii (Morning Magic-MagicFM) waziri wa michezo Nchimbi kapigiwa simu, kaulizwa inakuwaje
juzi uwanjani neti(nyavu) ilikatika ikabidi ifungwe katani(ilichukua zaidi ya dk 5 kufunga katani) na fainali yake jana
umeme umekatika, tunaomba maelezo yako!! Aaagh Jamaa akakata simu!!
Hii aibu sijui nani atai-handle!!
Ndo ma-"DR" wetu wenye kasi mpya na ari ileile.
 
tuliambiwa kuongozwa na ccm kwa kipindi kingine ni janga la kitaifa hii ni trailler picha yenyewe inakuja

kwa mtindo huu majanga ya kitaifa yatakuwa mengi sana, ngoja

  1. Maradhi(Ukimwi, Malaria, Kisukari, Fistula, Presha, Stroke.....)
  2. Ujinga (Kudesa, Kukubali kugawiwa tishet kwenye uchaguzi, Mikataba mibovu, .....)
  3. Makazi bora( Tembe...)
  4. Rushwa
  5. Ajira
  6. Umeme
  7. Foleni (mabarabarani, kulipia bills, kupiga kura, ATM, Kurudisha fomu za mikopo HESLB,....)
  8. Umaskini
  9. Wizi (hii ndio balaa, tangu zianze bodaboda yani ni noma)
  10. Kuongozwa na J.....endeleza list!!
 
mimi nimemskia akiongea hadi alipokata simu nimeshangaa sana!!
ni kwamba hana majibu au ni dharau!!!!!????
 
Halafu kuna kiumbe kingine kwenye serikali ya Jk kinalalama eti watanzania tuwe wamoja katika kudai ufisadi wa rada urudi kwenye serikali ya tz ili kulinda heshima ya nchi (eti tusiaibike)... sasa utashangaa akili za hawa matwana wa serikali ya jk .... hawanaga vipaumbele.

Kipi kinacholiabisha taifa ile mbaya; kushindwa kuwafikisha mahakamani mafisadi ila ukapata ujasiri wa kudai pesa ya kifisadi au umeme kukatika kwenye mechi ya kimataifa kama ile mbele ya macho ya ulimwengu kupitia supersport (ukiachilia mbali ile kadhia ya umeme kukatika hospitalini?

Well, vyote ni aibu, lakini hawa watu wameshakufa dhamira ya mioyo; nje wamevaa masuti lakini ndani ni makopo tu. Watanzania wajihesabu hawana serikali sasa, mpaka 2015.
 
Kwanza siamini kama walikabidhiwa uwanja bila generator!Au Walikuwa hawana Dizel Nihaibu sana hii!!Lakini hata kiongozi wa nchi hana lakusema anaona sawa hii nisawa nakuwa na gari zuuri lakini hauna spare tyre!!
Mimi sishangai ila Soma Sinature yangu!!Chini ya haya maneno!

 
Mimi nimeshajiamulia kuwa Watanzania tunasumbuliwa na uswahili. Utanashati kwetu ni mwiko, ubabaishaji daima.Kwenye hili la Kagame cup, dalili za uswahili zilianza kujionesha mapema kabisa pale kombe lilipopokelewa airport. Kwa kawaida, ile ni shughuli rasmi ambayo ingetakiwa iwe na staha. Nchi zingine wangepamba rasmi na kutumia watoto waliovalia nguo safi za mchezo wa mpira kulipokea lile kombe. Maofisa wa TFF wangetakiwa wawepo na suti zao, glovu nyeupe za sufi, kuwepo carpet lekundu, mabaunsa watanashati na coverage nzuri ya TV. Kungekuwa na msafara mpaka mjini, na bendera za TFF, FIFA na Kagame Cup zingepamba barabara yote mpaka litapohifadhiwa kombe. Badala yake?....Picha kwenye gazeti zilimunoesha jibaba limoja limevaa ndala, kitambi hicho, mkono mmoja kashika sijui takataka gani, na mkono mwingine eti kashika kikomba kama vile ni kopo la kutawazia.Na ubaya zaidi, Super Sport ilikuwepo kuturekodi tulivyo wababaishaji
mkuu umeua mbaya, then tunatafuta wadhamin wa ligi! Upuuzi mtupu,
 
Watangazaji wengine professionalism yao siielewi kabisa. Kwenye suala kama hilo huwezi kumpigia simu waziri na kutaka ufafanuzi kwenye simu. suala lenyewe ni la aibu halafu eti una mpigia simu akujibu. kwa mfano wewe ulitaka ajibu vipi ili ulidhike? siyo kila isue unakurupuka kumtwangia simu waziri, inamaana kabla ya kufika kwa waziri nani mtu wake wa chini kicheo mliyempigia? hili ndio tatizo la kuokota okota watangazaji.

Waziri alitakiwa atoe msimamo/maoni yake kwenye tukio lile, kwani yeye ndie waziri wa ile wizara. Na si kama yeye ndio alitakiwa kuwasha generator au kufunga nyavu, mwandishi alikuwa sahihi kabisa.

Sasa nakuhakikishia, kama kawaida ya wababaishaji, hakuna fundisho lolote litapatikana kutokana na yale. Na itakuja kujirudia tena.
 
Hawa watangazaji wetu wa hizi redio nafikri wanatakiwa wapatiwe elimu ya kutosha anayetakiwa kujibu maswala ya nishati ya umeme ni NGELEJA na siyo waziri NCHIMBI na hata hilo la nyavu kutoboka kila mtu anajua quality ya vitu vya KICHINA na kumbukeni ni msaada huo hapo nafikiri TBS wanahusika.
 
wenzetu (wala sio EU/USA au Japan) ikitokea aibu kama ya jana anaitisha mwenyewe press conference angalau hata kuelezea masikitiko ya serikari. Lakini yule jamaa (Nchimbi) nilivyoona amesimama kabla ya umeme kukatika ilikuwa wazi anatafuta ile wanaita 'cheap popularity'. Na Mungu ni mkubwa, 'he's now popular'!!! Na bado huu muda uliobaki watavuna mengi zaidi ya haya.
Leo asubuhi hii (Morning Magic-MagicFM) waziri wa michezo Nchimbi kapigiwa simu, kaulizwa inakuwaje
juzi uwanjani neti(nyavu) ilikatika ikabidi ifungwe katani(ilichukua zaidi ya dk 5 kufunga katani) na fainali yake jana
umeme umekatika, tunaomba maelezo yako!! Aaagh Jamaa akakata simu!!
Hii aibu sijui nani atai-handle!!
 
Leo asubuhi hii (Morning Magic-MagicFM) waziri wa michezo Nchimbi kapigiwa simu, kaulizwa inakuwaje
juzi uwanjani neti(nyavu) ilikatika ikabidi ifungwe katani(ilichukua zaidi ya dk 5 kufunga katani) na fainali yake jana
umeme umekatika, tunaomba maelezo yako!! Aaagh Jamaa akakata simu!!
Hii aibu sijui nani atai-handle!!
Kuhusu nyavu kukatika nashauri waziri afungiwe kama YANGA na akipatikana na kosa la kukatika kwa umeme afukuzwe kama FROLIAN KAIJAGE!
 
yaliyotokea jana uwanja wa Taifa umeme kukatika ni jambo la aibu kwa nchi yetu Tanzania. Nilikuwa naangalia mpira kupitia Super Sport
walichofanya ili kufinya aibu ni kuweka matangazo ya biashara.
nilijaribu kufuatilia kupitia Star Tv, nilichokiona ni aibu sana. Ambulance ya kubebea wagonjwa ndio ilitumika kumulika eneo la
kukabidhiwa zawadi na kombe.
Waziri wa michezo alionekana akipiga simu nahisi zilikuwa za kuomba umeme urudishwe bila mafanikio.

Hii ni aibu kwa nchi yetu Tanzania.
mkuu bado unadhania hii ni nchi yetu??ni nchi yao maana wanafanya wanavyotaka tena bila consent ya wananchi
 
Waandishi wengine bwana nao wanatia kichefuchefu, kila mtu anaweza kutafuta habari, lakini si kila mtu anaweza kuulizwa habari za tukio. Suala la umeme kukatika na wavu wa goli kufungwa kwa katani haikuwa lazima sana maelezo hayo yatoke kwa waziri, na kwa sababu hiyo haikuwa lazima kwa waziri kutoa majibu na maelezo ya suala ambalo si lake na hata kama linaangukia kwake CECAFA au TFA wangestahili kulizwa suali lile. Aliyemuuliza waziri ama hajui uandishi au haijui kazi yake arudi shuleni ajifunze mgawanyo wa majukumu. hilo ni suala la kiutendaji aulizwe katibu mkuu wizara ikishindikana waziri anaweza kutoa ufafanuzi. Napenda udadisi lakini sipendi udandiaji. siipendi serikali hii lakini lawama zitafutiwe appropriate people or appropriate government urgency. Kwa leo Magic FM imemkosea waziri wamwombe msamaha. JF tendeni haki katika hili
 
Mambo yamekuwa yakijirudia hayo kwa hayo,kama kujifunza tungejifunza pale CD zilipo goma mbele ya muheshimiwa rais lile lilikuwa ni somo la kujifunza.Haya mashindano toka yaanze na-amini kumekuwa na matukio mengi lakini kutokana na utamadunu wetu wa "kazi ya Mungu" tunachukulia ni kawaida na wala vyombo vya habari haiwashughulishi kutujuza.
Wakati wa mashindao haya tumepata kusoma au kusikia vyumba vilivyo paswa kutumika vilifungwa na wachina waliondoka na funguo,umeme umekatika wakati shughuli ikiendedlea,sasa tunasubiri litokee lipi ili tuona kuwa sasa inatosha,najiuliza na Mungu atukinge na hili.mfano janga la moto likitokea katika mchezo kaka huu Simba vs Yanga au jukwaa likianguka,au utokee mtafarukuu wowote utakao pelekea watu kukanyagana tumejiandaa vipi? au ndio waheshimiwa watajitokeza kutoa mkono wa pole kwa wahanga,wasanii watatunga nyimbo za maombelezo na sisi tutapiga kelele ingekuwa hivi ingekuwa vile.Kwa nini juhudi hazifanyiki mapema? na sisi kaka sisi wanajamii tunayo nafasi ingawa finyu ya kuepusha haya,lakini tukiendelea na huu utamaduni yatakuja tokea zaidi ya yale ya Mbagala.
 
Nchi hii haina viongozi makini, ila wako makini kutengeneza mitandao ya kupelekana ikulu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom