Waziri Nchimbi umetia aibu

Sizinga

Platinum Member
Oct 30, 2007
9,100
6,022
Leo asubuhi hii (Morning Magic-MagicFM) waziri wa michezo Nchimbi kapigiwa simu, kaulizwa inakuwaje
juzi uwanjani neti(nyavu) ilikatika ikabidi ifungwe katani(ilichukua zaidi ya dk 5 kufunga katani) na fainali yake jana
umeme umekatika, tunaomba maelezo yako!! Aaagh Jamaa akakata simu!!
Hii aibu sijui nani atai-handle!!
 
Hana majibu je?? Hongera Yanga waliosema tumebebwa nadhani ngebe zimewaisha jana!!
 
Cha kuchekesha..kawau(mtangazaji) mwishoni kasema jamani nisije kufa na kijiba cha roho...huyu Waziri kanikatia simu na sio tatizo la mtandao!! dah noma!!
 
yaliyotokea jana uwanja wa Taifa umeme kukatika ni jambo la aibu kwa nchi yetu Tanzania. Nilikuwa naangalia mpira kupitia Super Sport
walichofanya ili kufinya aibu ni kuweka matangazo ya biashara.
nilijaribu kufuatilia kupitia Star Tv, nilichokiona ni aibu sana. Ambulance ya kubebea wagonjwa ndio ilitumika kumulika eneo la
kukabidhiwa zawadi na kombe.
Waziri wa michezo alionekana akipiga simu nahisi zilikuwa za kuomba umeme urudishwe bila mafanikio.

Hii ni aibu kwa nchi yetu Tanzania.
 
anakula pesa ya walipa kodi....hajui kuwajibika....tutabakia amani na mshikamano ndio ngao yetu!!! taifa linateketea hili
 
Dah! ..sikujua kwamba ni moja wapo ya majukumu ya waziri katika serikali ya Tanzania mwenye dhamana ya michezo kuhakikisha kwamba nyavu za magoli zimefungwa sawasawa au kama standby generator ya uwanja wa taifa iko operational, sikulijua hili.
 
Nchi hii watu wakitoana ngeu heshima ndio itarudi kila mtu atakuwa anajua wajibu wake ni nini Ngeleja naona anauza sura tu
 
Dah! ..sikujua kwamba ni moja wapo ya majukumu ya waziri katika serikali ya Tanzania mwenye dhamana ya michezo kuhakikisha kwamba nyavu za magoli zimefungwa sawasawa au kama standby generator ya uwanja wa taifa iko operational, sikulijua hili.

Mkuu ilipokuwa inasisitizwa waziri wa ulinzi ajiuzulu baada ya mabomu ya mbagala ni jukumu lake kutunza mabomu au kujua yanaeksipaya lini?
 
aibu hii katika uwanja wa taifa itaisha lini? mara cd ya nyimbo za taifa zigome kuimba na jana tena umeme umekatika wakati yanga wanajiandaa kukabidhiwa kombe. ina maana uwanja huu wa kisasa hauna stand by genereta?..........
 
Hivi mtu kweli unategemea Nchimbi ajibu simu juu ya hili ? Jamaa anawaza Urais mwaka 2015 .
 
Kila Wizara haiko makini na yanayofanyika chini yake, wanaona kama hayawahusu! Tulikuwa tunatia aibu ndani ya nchi lakini sasa tunaionyesha dunia ni jinsi gani serikali yetu ilivyo ya hovyo.

Kama ingekuwa kombe limechukuliwa na nchi nyingine tungesema ilikuwa ni njama!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom