Jamani hebu Wanasheria humu JF tusaidieni kwa hili" Naibu Meya kuficha kura kwenye chupi" je ni kosa gani katika sheria za nchi ambalo mtuhumiwa anaweza kushitakiwa nalo. Maana mimi kwa mawazo yangu tendo hilo ni sawa na kukanyaga katiba ya nchi kwa makusudi. Huyu tayari keshajidhalilisha mwenyewe.Nilikuwa ukumbini na kushuhudia sakata hili,baada ya kupigwa kura,kura za Hapana zilipatikana 14 na kura za Ndio zilikuwa 12,baada ya Nchimbi kuona meya aliyekuwa akimtaka yeye apita amekataliwa akaamua kutumia umafya wa kuforce matokeo na kwa kushirikiana na naibu meya wakatangaza matokeo kinyume,ndipo moto ulipoanza kuwaka,wakaitwa madiwan wawil pale mbele wahesabu kura zile na baada ya kuhesabu tena kura zile,matokeo yalionesha Hapana ni 14 na NDIO ni 12,hapo ndipo naibu Meya Marium Dizumba alipoiba kura na kuzificha kwenye Chupi na sio kwenye pochi waandish wanapotosha,hali ilikuwa tete na kusababisha Diwan wa kata ya misufin(chadema)salumu mfamaji kugongwa na gar na kada wa chama cha mapinduz,bwana Nchimbi wazir aliamua kukimbia na sanduku la kura baada ya kuona wameshikwa pabaya.wanachokifanya ccm ni kulazimisha kumpitisha meya jambaz ambaye sio wananch tu hata madiwan wenzake wa ccm hawamtaki.Wanaharakat wote tuungane kote tz kusimamia hak na kupinga wale wote naotaka kutupeleka watanzania kubaya kwa maslah yao binafsi.
Naibu meya wa songea mjini Marium Dizumba jana alisababisha uchaguzi wa umeya wa manispaa ya songea kuvurugika baada ya kuiba kura na kuzificha kwenye chupi,ili kumuwezesha ndugu Charles Mhagama kushinda nafas hiyo.
Wananchi na madiwan wengi wakiwemo na wa ccm hawamtaki bwana Mhagama awe meya wa manispaa yetu ya songea kwa kuwa hana sifa za uhadilifu hata kidogo na alipitishwa ili akasimamie maslahi ya wachache akiwemo mbunge Emanuel Nchimbi, kilichofanyika ni madiwani wa chadema kuungana na baadhi ya madiwan wa ccm na kupiga kura ya hapana,zoez hil liliwezekana na kura za hapana zilipatikana 14 na za Ndio 12. Hapa ndipo walipotaka kufanya njama za kubadil matokeo ili yawe kinyume, hali iliyosababisha naibu meya Marium Dizumba bila aibu kuiba kura na kuzificha kwenye chupi, huku wazir Nchimbi akikimbia na sanduku la kura nje ya ukumbi.
Wakati hali hii ikiendelea madiwan wa ccm na chadema wakazipiga kavu kavu ndan ya ukumbi huo wa manspaa huku kada mmoja wa chama cha mapinduzi Hamisi abdalar Ally akimgonga na gari nje ya ukumbi, diwani wa kata ya misufin chadema bwana Salumu Mfamaji na kumsababishia maumivu makali.
nani sasa aache? nchimbi au mwandishi wa thread hii??acheni siasa za maji taka
Hii thread imejaa umajitaka sana kwahiyo siwezi kupoteza muda wangu kuichangia hata neno moja. Upuuzi mtupu tena haina mashiko kabisa.