Waziri Mwijage: Kwa sasa Tanzania ina zaidi ya viwanda 52, 000

Kuna tofauti kubwa sana ya ilani (agenda) na formal policy inayolenga kufikia malengo.

Kusudio liwe viwanda vinajengwa na serikari au watu binafsi. Policy inatoa maelezo halisi na mbinu ambazo zitatumika kufikia malengo watu wanaweza pima pamoja na mkakati unaoeleweka, unaweza fanyiwa assessment etc with policy appraisal.

Wengine tuliliona hili mapema sana na kusema kwa mtazamo wa serikari viwanda itakuwa hadithi tu; kilichobaki ni figusu figusu tu ambazo ni unrealistic.
 
Mungu naapa hata wakihesabu mashine za kukoboa na incubator nchi nzima kwa mwaka hazifikii 52,000. mtu anaetoa kauli kama hii anatakiwa akamatwe aonyeshe hivyo viwanda vilipo
Umenena kweli mkuu. Viwanda 52000? Hawapo serious
 
Tunapoongelea suala la nchi ya viwanda hatutegemei takwimu kama hizi. Huwezi kujisifia kwamba umewezesha uwekezaji kwa uwekezaji huo usipokuwa na tija. Kama katika takwimu hizo hata hatuna viwanda 2000 vikubwa na vya maana ni bure. Viwanda vidogo (kama wengi wanavyoviongelea) vingi ni juhudi za watu binafsi pasipo mchango wa serikali hata kwa asilimia moja. Vyenyewe vinazalisha bidhaa kwa matumizi ya kawaida tuu ni vichache sana vinavyouza bidhaanzake hata kwa nchi jirani tuu
 
duuh after 5 years tutakuwa navyo 800,000 HAPA KAZI TU.
MUNGU atupe nini watanzania wenzangu.
 
Tatizo hapa watu wanashindwa kuelewa nini maana ya viwanda ,mh waziri alitakiwa afafanue ni viwanda vya aina gani hasa jee ni viwanda vikubwa,viwanda saizi ya kati na viwanda vidogo au viwanda vya kuzalisha vipuri vya mashine,kimsingi vyote hivyo ni viwanda.
 
View attachment 424435

Kuelekea uchumi wa viwanda nchini, serikali imefanikiwa kufufua na kuanzisha viwanda ambapo kwa sasa vinavyofanya kazi vipo zaidi ya 52,000. Sekta hiyo pia imetajwa kuwa inatarajia kukuza uchumi wa watanzania asilimia 40.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonesho ya viwanda Tanzania yanayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam kuanzia Disemba 7 hadi 1, 2016.

“Kuelekea ujenzi wa uchumi wa viwanda, nilipewa maelekezo kufanya mambo matatu, ikiwemo uhakikisha vilivyopo ambavyo vingi vilikuwa vinazalisha chini ya kiwango vinaongeza uzalishaji, pili vilivyobinafsishwa ambavyo havifanyi kazi vinafanya kazi na la mwisho nilipewa agizo la kuhakikisha wekezaji wa ndani na nje ya wanakuja kuwekeza,” amesema na kuongeza.

“Katika kipindi cha mwaka mmoja tangu serikali hii iingie madarakani, kuna viwanda 52,000 vinafanya kazi na kwamba asilimia 40 ya watanzania uchumi wao utatokana na viwanda.”

Aidha, Mwijage amesema Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia taasisi yake ya Mamlaka na Maendeleo ya Biashara Tanzania, imeandaa maonesho yatakayokutanisha wadau wa sekta ya viwanda kwa lengo la kutangaza pamoja na kujadili fursa za masoko ya ndani na nje ya nchi.

Amesema maonesho hayo pia yatatoa taswira ya juhudi za ujenzi wa viwanda katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.


Chanzo: Dewji Blog


Hahahahahaaa usikute wamehesabu na ile mashine yetu ya familia ya kusaga mahindi kule Manyara!
 
Nauliza kuhusu Mwanza Textile, Musoma Textile, Urafiki, Sungura Textile, Tanganyika packers vimefufuliwa au vimefufuliwa viwanda vya mawese tu ndiyo vitakavyotufikisha kwenye Tanzania ya viwanda. Mwijage kuweni serious. Hongera kwa kufufua viwanda vya SIDO.
 
Back
Top Bottom