BONGOLALA
JF-Expert Member
- Sep 14, 2009
- 16,507
- 11,883
Inasikitisha sana watanzania kutudanganya kila Siku na hawa watawala wetu.Yaani Leo waziri anaongea Kwa hasira kabisa,eti anatetea viwanda vingine.Anaturudisha kule pa cement kuuzwa sh 20,000 tabora mwanzaMbona hii serikali inekuwa na ndimi nyingi?
Jana 30/11/2016 taarifa ya habari ya ITV saa 2.00 usiku, huyu Mwijage nilimuona ITV, tena kwa kutuaminisha Watanzania alishika barua ambayo alidai kwamba imetoka kwa CEO wa Dangote. Eti barua hiyo ikieleza kwamba kiwanda cha Dangote, hakijasimamisha uzalisha wa cement. Ila kwasasa wanafanya matengenezo ya mitambo yao na kwamba hili ni jambo la kawaida kwa viwanda vinayoanza uzalishaji.
Sasa iweje leo 1/12/2016 hata kabla ya masaa 24 kupita, huyu huyu Mwijage anakuja tena na SOUND nyingine kwamba kiwanda cha Dangote kimesimamisha uzalishaji?
Ni waji.nga tu ndiyo wataamini kwamba Dangote akisimamisha uzalishaji, haitaathiri soko ya cement. Wakati huko Mtwara Dangote alipokuwa anazalisha cement, mfuko mmoja wa cement ulishafikia Tsh 11,500/-. Kusimamisha uzalishaji tu kwa week 1 tayari mfuko wa cement huko Mtwara umeshafikia Tsh 15,000/-.
Huyu huyu Mwijage ndiye anayesema kwamba ukiwa na cherehani 1 tayari ni kiwanda, ukiwa na mashine 1 ya kufyatua matofali tayari ni kiwanda. Kweli Tanzania tumempata Waziri wa Viwanda!