Waziri Mwandosya: Kikwete Angeniacha Nipumzike

Hata wewe utaumwa na kufa na kufunikwa udongoni,kauli kama hii ingetolewa na mtu ambaye yeye hawezi kukutwa na Ugonjwa wala Mauti...hizi ni chuki Binafsi tuu weweeee.

Prof Mwandosya ni Msomi aliyebobea katika Sayansi na Teknolojia na mwenye weledi wa kutosha unaoaminika ndani na nje ya Nchi na amelitumikia taifa letu kwa muda mrefu na kwa weledi wa hali ya juu,tuambie wewe ni nani na umeifanyia nini Tanzania?Wewe Pia utaumwa na Utakufa siku Moja,potea hapaa.
 
Unajua mara nyingine watu tunapima uwezo wa mtu kufikiri kutokana na nini unaamini. Sio kila kitu cha humu JF unapaswa kuamini na kulipuka kutoa comment zako. Nyerere aliwahi kumuuliza mwandishi wa habari wa Kenya kwamba, leo hii ukisikia watu wanasema mie ndiye baba yako utaamini kwa kuwa tu watu wamesema hivyo?

Inaonyesha watu wengi wa JF wakisikia Nyerere alikuwa baba yao mzazi wataamini.

Jiulize, mtu kama Mwandosya ataenda kwa PM Pinda kulalamikia kitu ambacho hakitaki wakati ana nafasi lukuki za eidha kujiuzulu mwenywe, au kumkatalia raisi uteuzi wake? Pia, hakuna mtu anateuliwa kuwa waziri au nafasi nyingine na kutangazwa kabla hajaambiwa na kuulizwa kama anakubaliana na uteuzi, ili Raisi asije umbuliwa. Nadhani mmesikia watu wanasema Lipumba alikataa uteuzi wa kuwa mbunge.

Nyerere kabla hajakuteua hata alikuwa akisema, nataka uwe waziri wa Wizara fulani, je utaweza?
 
Waziri mpya wa Ofisi ya Rais(Asiye na Wizara Maalum),Prof.Mark Mwandosya amekaririwa akisema kuwa kama Mhe.Rais angezingatia hali yake ya kiafya na ushauri aliopewa na Madaktari juu ya kupata mapumziko,angemuacha apumzike.Akizungumza na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda,jana nyumbani kwake Kunduchi-Dar es Salaam,Prof Mwandosya alionyesha kutoridhishwa kwake na uteuzi wa Rais juu yake.

'Nahitaji mapumziko makubwa Mkuu' alisema Prof.Mwandosya akimueleza Pinda aliyeonekana kukubaliana naye. 'Niheri nirudi UDSM nikafundishe Wahandisi wangu' aliongeza Prof Mwandosya.Mimi tu kuwaletea habari...

Source please...., other wise crappppp.........
 
Hata wewe utaumwa na kufa na kufunikwa udongoni,kauli kama hii ingetolewa na mtu ambaye yeye hawezi kukutwa na Ugonjwa wala Mauti...hizi ni chuki Binafsi tuu weweeee.

Prof Mwandosya ni Msomi aliyebobea katika Sayansi na Teknolojia na mwenye weledi wa kutosha unaoaminika ndani na nje ya Nchi na amelitumikia taifa letu kwa muda mrefu na kwa weledi wa hali ya juu,tuambie wewe ni nani na umeifanyia nini Tanzania?Wewe Pia utaumwa na Utakufa siku Moja,potea hapaa.
hilo la kutumia utaalamu wake kwa mimi naona kashindwa, licha ya kuwa msomi aliye bobea au weledi wa kutosha sababu alikuwa katibu mkuu wizara ya madini na nishati lakini alishindwa kutumia elimu yake kutuletea umeme wa kutosha, amekuwa waziri wa maji bado ameshindwa kuleta ufanisi katika sekta ya maji, amekuwa waziri wa mawasiliano na uchukuzi pia napo hakuleta ufanisi wowote zaidi ya kuia ttcl? kuna siku Mengi aliwahi kusema kuhusu wasomi wa tz badala ya kutumia utaalamu wao kuanzisha vitu vikubwa kama viwanda hata vidogo vidogo kama vikubwa vina washinda wao wana fuga ngombe wa zero grazing au kuku, wanyama au wa mayai nyuma ya nyumba zao zilizo katika maeneo ya makazi, badala yakuwa wanakuwa wao wanavubaa katika kila angle.
 
Yawezekana. Kama ndivyo, hajafurahishwa na ile kuwa "waziri asiye na wizara maalumu." Hii ni sawa na kuwa tembo mweupe!Hata hivyo, Rais ametumia busara kumteua. Mteuliwa pia ametumia hekima kutaka apumzike.Lakini:Nikweli ameyasema hayo?
 
Waziri mpya wa Ofisi ya Rais(Asiye na Wizara Maalum),Prof.Mark Mwandosya amekaririwa akisema kuwa kama Mhe.Rais angezingatia hali yake ya kiafya na ushauri aliopewa na Madaktari juu ya kupata mapumziko,angemuacha apumzike.Akizungumza na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda,jana nyumbani kwake Kunduchi-Dar es Salaam,Prof Mwandosya alionyesha kutoridhishwa kwake na uteuzi wa Rais juu yake.

'Nahitaji mapumziko makubwa Mkuu' alisema Prof.Mwandosya akimueleza Pinda aliyeonekana kukubaliana naye. 'Niheri nirudi UDSM nikafundishe Wahandisi wangu' aliongeza Prof Mwandosya.Mimi tu kuwaletea habari...

hapo kwenye red unamaanisha nini??
 
kweli hata mimi sijafurahishwa nauteuzi wake. ila hii naona limekaa kisiasa zaidi. kwa upeo wangu nilionao naona mikoa yenye msukosuko wa kisiasa amejitahidi sana kuweka mawaziri angalau ainusuru lakini naona kwa mbeya elewa majimbo ya mbeya mengi hayako salaama hata haya ya Dr. mwakyembe,Prof. Mwandosya hata Mwakyusa sio salaama sana kunawapizani wanayataka sana na vuvungu lakisiasa kwa mikoa ya iringa na Mbeya ni kubwa mno. jk alitakiwa kujua amefanya makosa ikiwezekana ampumzishe sio mbaya.
 
Tuache kejeli na dhihaka, kwanza alianzisha hii thread hajatoa source. Tulichokiona ni picha tu kwenye gazeti la mwananchi na hakuna habari yoyote kuhusu hoja hoja inayozungumziwa. Prof. anaumwa tuwe wa ungwana na tutakuwa hatujamtendea haki tukianza kuzungumzia suala kutotaka kuteuliwa kwake wakati hatujamsikia akiongea hivyo.
 
Usiniambie aisee! Kumbe mkulu huwa anawateua bila kukubaliana na wahusika
 
Waziri mpya wa Ofisi ya Rais(Asiye na Wizara Maalum),Prof.Mark Mwandosya amekaririwa akisema kuwa kama Mhe.Rais angezingatia hali yake ya kiafya na ushauri aliopewa na Madaktari juu ya kupata mapumziko,angemuacha apumzike.Akizungumza na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda,jana nyumbani kwake Kunduchi-Dar es Salaam,Prof Mwandosya alionyesha kutoridhishwa kwake na uteuzi wa Rais juu yake.

'Nahitaji mapumziko makubwa Mkuu' alisema Prof.Mwandosya akimueleza Pinda aliyeonekana kukubaliana naye. 'Niheri nirudi UDSM nikafundishe Wahandisi wangu' aliongeza Prof Mwandosya.Mimi tu kuwaletea habari...

Kwani Rais huwa hawa-consult hawa wateule wake kabla hajawatangaza?? Na kwa kuwa Prof alikuwa kwenye Baraza la Mawaziri lililobadilishwa (sijui neno sahihi ni lipi hapa; kubadili; kuongeza mawazir; nk) na alipotoka India kwenye matibabu naamini Serikali walipewa ripoti ya matibabu yake. In maana RAIS hajui maana ya sentensi hii "APATE MAPUMZIKO MAKUBWA"???

Kazi kweli kweli.......
 
hilo la kutumia utaalamu wake kwa mimi naona kashindwa, licha ya kuwa msomi aliye bobea au weledi wa kutosha sababu alikuwa katibu mkuu wizara ya madini na nishati lakini alishindwa kutumia elimu yake kutuletea umeme wa kutosha, amekuwa waziri wa maji bado ameshindwa kuleta ufanisi katika sekta ya maji, amekuwa waziri wa mawasiliano na uchukuzi pia napo hakuleta ufanisi wowote zaidi ya kuia ttcl? kuna siku Mengi aliwahi kusema kuhusu wasomi wa tz badala ya kutumia utaalamu wao kuanzisha vitu vikubwa kama viwanda hata vidogo vidogo kama vikubwa vina washinda wao wana fuga ngombe wa zero grazing au kuku, wanyama au wa mayai nyuma ya nyumba zao zilizo katika maeneo ya makazi, badala yakuwa wanakuwa wao wanavubaa katika kila angle.

Jaribu kuwa unafikiria kutumia kichwa chako usiongee kama kama Mtu mjinga usielewa tatizo la Tanzania, tatizo hapa CCM na mfumo zee ambao umeoza na haufai,unategemea hao wasomi wao watafanya nini? ulishaambiwa CCM inawenyewe mbona watu wengine mnakuwa wagumu kufikili! hata umweke nani ndani ya serikali ya CCM utaishia kutukana na maneno ya Kejeli,angalia sasa mnataka kufanya JF kama Genge la majungu na maneno ya hovyo! mmekalia kumshambulia Mwandosya na mtu mwenyewe mgonjwa haya sasa yeye ndiyo amifikisha Tanzania hapa ilipo katika miaka hamsini? yeye ndiyo angeleta Maji? hebu shirikisha Ubongo wako kufikiri vizuri. CCM ndiyo tatizo kama hujui akina Nundu wasomi wazuri na ozoefu wa kimataifa wenyekushimika wameishia kufedheheka na Mfumo wa hovyo ambao mnaupigia kura kila uchaguzi na kuishia kulalama kwenye keyboard huku hamchukui maamuzi yeyote ya maana.

Watanzania tukiendelea na maneno bila vitendo tutaona cha mtema kuni,mtapiga kelele wenzenu wataendela kuiba na sisi tutabaki kutukana tu kwenye keyboard! UFINYU WA MAWAZO
 
kwa nn alikubali kuapishwa? aache usanii, wapiganaji cheo kina raha yake, Hamuone wengine wanalalamika na kulia wameonewa kumwagwa.
 
Waziri mpya wa Ofisi ya Rais(Asiye na Wizara Maalum),Prof.Mark Mwandosya amekaririwa akisema kuwa kama Mhe.Rais angezingatia hali yake ya kiafya na ushauri aliopewa na Madaktari juu ya kupata mapumziko,angemuacha apumzike.Akizungumza na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda,jana nyumbani kwake Kunduchi-Dar es Salaam,Prof Mwandosya alionyesha kutoridhishwa kwake na uteuzi wa Rais juu yake.

'Nahitaji mapumziko makubwa Mkuu' alisema Prof.Mwandosya akimueleza Pinda aliyeonekana kukubaliana naye. 'Niheri nirudi UDSM nikafundishe Wahandisi wangu' aliongeza Prof Mwandosya.Mimi tu kuwaletea habari...

Non sense!
 
Uteuzi haukufanyika kwa kushtukiza, maana kabla ya jina kutajwa mteuliwa anaelezwa mapema kuwa ni miongoni mwa wateuliwa, sa iweje leo mtu ajutie uteuzi ? si angemwambia mkuu aondoe jina kwenye list mapema ?
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom