Waziri Mwandosya: Kikwete Angeniacha Nipumzike

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Waziri mpya wa Ofisi ya Rais(Asiye na Wizara Maalum),Prof.Mark Mwandosya amekaririwa akisema kuwa kama Mhe.Rais angezingatia hali yake ya kiafya na ushauri aliopewa na Madaktari juu ya kupata mapumziko,angemuacha apumzike.Akizungumza na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda,jana nyumbani kwake Kunduchi-Dar es Salaam,Prof Mwandosya alionyesha kutoridhishwa kwake na uteuzi wa Rais juu yake.

'Nahitaji mapumziko makubwa Mkuu' alisema Prof.Mwandosya akimueleza Pinda aliyeonekana kukubaliana naye. 'Niheri nirudi UDSM nikafundishe Wahandisi wangu' aliongeza Prof Mwandosya.Mimi tu kuwaletea habari...

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
  • Thanks
Reactions: SMU
mchango wa mtu mwenye busara na hekima au mchapakazi mara nyingi huwa unahitajika siku zote, nadhani kikwete kwa kuzingatia uzoefu wa Profesa mwandosya uchapakazi wake na hata hekima zake ameona bado anamuhitaji sana katika baraza lake la mawaziri. kumpa uwaziri usio na wizara ni kumpunguzia majukumu pia kwani hatokuwa bounded na kazi flani flani na nadhani kazi yake kubwa ni kuangalia mahala palipo na mapungufu katika wizara mbali mbali na kutoa mchango wake.

hebu tuangalie enzi zile MREMA akipewa unaibu waziri mkuu chao ambacho hakipo kwenye katiba yatu but kutokana na uchapakazi wake na umuhimu wake Mwinyi aliona mtu huyu anahitajika kupewa nafasi ambayo itamfanya aweze kuingia katika wizara zingine na kutoa mchango wake pia

pia sitaki kuamini kuwa Mwandosya hakupewa taarifa awali, maana nachokifahamu kabla ya kutangazwa lazima muhusika (hasa wale katika nafasi muhimu na nzito), aelezwe kisha atoe maoni na akubali. So nahisi ili nalo limekuzwa tuu.
 
Waziri mpya wa Ofisi ya Rais(Asiye na Wizara Maalum),Prof.Mark Mwandosya amekaririwa akisema kuwa kama Mhe.Rais angezingatia hali yake ya kiafya na ushauri aliopewa na Madaktari juu ya kupata mapumziko,angemuacha apumzike.Akizungumza na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda,jana nyumbani kwake Kunduchi-Dar es Salaam,Prof Mwandosya alionyesha kutoridhishwa kwake na uteuzi wa Rais juu yake.

'Nahitaji mapumziko makubwa Mkuu' alisema Prof.Mwandosya akimueleza Pinda aliyeonekana kukubaliana naye. 'Niheri nirudi UDSM nikafundishe Wahandisi wangu' aliongeza Prof Mwandosya.Mimi tu kuwaletea habari...
Kwani kufundisha wahandisi ndio kupumzika?
 
Yaani wanasiasa bana hawaaminiki kabisa. Ni unafiki kwa kwenda mbele!

Kama kweli anataka apumzike kulikuwa na ugumu gani kwa yeye kuomba kujiuzuru hata kabla ya mabadiliko yaliyofanywa karibuni? Na hata baada ya kujua kuwa Rais anafanya mabadiliko angeweza pia kumpigia simu Rais na kuomba apumzishwe! Nakumbuka vema tu kina Kingunge waliwahi kuomba kupumzika kipindi kile baada ya baraza la EL kuanguka.

Hata hivyo nampa pole Mh Mwandosya na namuombea apone kwa haraka.
 
ndo amejua leo kuwa anatakiwa kurudi kufundisha wahandisi....akaae humo humo kudadadeki hakuna kutoka

hahahahahahahaha. . .
Captain j.K kashtuka meli imegonga mwamba. .. Sasa kilichobaki ni kuwakomalia wafuasi wa meli yake kuto kuruka majini. .
 
Kwa hiyo mbio zake za kuwania urais zimeishia ukingoni?!!

kiongozi makini uwezi kuililia kuiongoza t.Z after vasco da gama kuondoka. . . Uozo aliouacha yahitaj mtu kama benny kuja kusafisha. .Mark atavuta kabla hata ya awamu ya kwanza!Bora arudi akashike marker pen
 
hivi kumbe kufundisha wahandisi ni kupmzika na sio sio kazieeee?!!!
 
Ina maana hakushirikishwa juu ya uteuzi wake? Kama ndivyo basi ana haki kusema hayo lakini kama alijua basi ni unafiki tu.
 
Hizi habari siziamini sana ila hapakuwa na mawasiliano kati ya jk na mwandosya kabla ya uteuzi? Jk anamshitukiza nani sasa
 
Mleta thread inabidi aweke source. Otherwise ni majungu tu. Haiingii akilini kwamba Prof Mwandosya hakujua uteuzi wake. Lazima alifahamishwa kabla. Kama alikubali na wakati hawezi kufanya kazi, hiyo ndo tamaa ya fedha na madaraka sasa. Kwenye uwaziri kuna Chenji ya kumwaga ndo maana hakukataa.
 
Kwani kufundisha wahandisi ndio kupumzika?

Hapo sasa? Angesema apumzike siasa sawa. Kama ni kweli basi inaonekana Mwandosya amechoshwa na siasa na anataka kurudi kwenye taaluma. Nasikia kuna miaka ya nyuma huko wakati yuko Katibu Mkuu nishati aliwahi kutaka kurudi tena kufundisha wahandisi.

Kazi ya kufundisha ni nzito kuliko Waziri asiye na Wizara maalumu hivyo kama ni kupumzika ni kwenye uwaziri usio na wizara maalum kuliko kurudi CoET na kupangiwa vipindi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom