Waziri Mwakyembe: Mahakama ya mafisadi na wala rushwa unakaribia

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,251
mwakyembe-px.jpg

Waziri wa sheria na katiba Dr.Harrison mwakyembe amesema Mchakato wa Uundwaji wa mahakama ya mafisadi na wala rushwa unakaribia kukamilika huku mfumo wa mahakama hizo ukiundwa ndani ya mahakama zilizopo ili kuhakikisha unatekeleza majukumu yake bila kuingiliwa.

Akizungumza na waandshi wa habari baada ya kukutana na m/kiti wa tume ya Uchaguzi Jaji mstaafu Damian Lubuva alipotembelea wizara hiyo na kutoa Ushauri jinsi ya Uundwaji wa chombo hicho pamoja na maadili dhidi ya watumishi wa mahakama amesema bado wanannchi wengi wana imani na mahakama hivyo ni jukumu la mahakama katika kusimamia haki katika utoaji wa hukumu dhidi ya watuhumiwa.

Kwa Upande wake jaji Mstaafu Lubuva amesema Mahakama ni chombo kinachotakiwa kuamiwa na wananchi wote lakini chombo hicho kinaweza kisiaminike pindi kinapopindisha au kutoa hukumu batili.

Aidha Waziri mwakyembe amesema mkakati maalum umendaliwa dhidi ya Ubambikizaji kesi wananchi ambapo baada ya kutembelea mahabusu na jela amegundua wananchi wengi wamefungwa au kuwekwa mahabusu kwa kubambikiziwa kesi huku watumishi wa mahakama wakiandaliwa mpango maalum wa kuwadhibiti kimaadili dhidi ya Vitendo vya ukiukwaji wa maadili na Rushwa.

Chanzo:Channel Ten
 
mwakyembe mwenyewe na raisi wake magu wote watuhumiwa hiyo mahakama si itakuwa white elephant
 
Hivi hawa kama kweli wapo siriaz na hiyo mahakama waanze kwanza wao kujiudhuru nafasi zao maana nao ni majipu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom