Waziri Mwakyembe ashushuliwa.

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
11,556
7,085
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Harison Mwakyembe amejikuta katika wakati mgumu katika ziara yake ya kushtukiza alyoifanya katika kituo cha mabasi Mwenge.

Waziri huyo alifika maeneo hayo na kuanza kuamrisha madereva wa mabasi yanayofanya safari za Makumbusho-Bagamoyo waondoe mabus hayo kwa sababu sio mahali stahili.

Aliwaamrisha wayapeleke mcus hayo katika kituo cha Makumbusho kama ambavyo imeandkwa kwenye magari yao.

Ndipo madereva, makondakta pamoja na wapga debe walipomjia juu na kumwambia kuwa serikali imefanya ufisadi wa kuuza eneo la makumbusho ambako hvi sasa panajengwa Ghorofa.

Madereva hao waliskika wakisema kuwa wamechoshwa na ubabaishaji unaofanywa na serikali ya CCM.

Madereva hao walisema kuwa hawaondoki eneo hlo hadi hapo watakapopatiwa eneo jngne ambalo linatakiwa.

"Haiwezekani kila siku tunalipia ushuru hapa halafu leo unakuja kusema kuwa si sahii. Hakikisheni kuwa kituo cha makumbusho kinarekebishwa ndipo sisi tuende huko" Aliskika mmojawapo wa madereva hao.

Palitokea mzozo mkali wa maneno baina ya Waziri Mwakyembe na vijana hao wanaofanya kazi katika daladala hzo.

Mwishoni kabisa waziri Mwakyembe alisikika akisema "Suala la eneo la Makumbusho nimelisikia na nitalifanyia kazi"
mwishoni ikabidi awpe number za simu ili awasiliane nao ndpo akaamua kuondoka kwa aibu bila kuacha maagzo yoyote

My Take: Napenda viongozi wasipende kufanya ziara ya kushtukiza bila kufanya uchunguzi kwanza kupitia wawakilishi.

Chanzo Cha Habari ni Mimi mwenyewe nilikuwepo eneo la tukio..
 
Mbona sijaona sehemu aliyoshushuliwa hapa. Zaidi wamempatia ukweli kwa ajili ya kuufanyia kazi. Ili kama kuna mtu aliuziwa kituo chao pale Makumbusho then Mwakyembe anatakiwa afuatilie na kuwapatia ufumbuzi...tuache ushabiki wa kijinga.
 
Uchunguzi huo ataufanya nani? Ikiwa Polisi wanashindwa kufanya uchunguzi wa Ulimboka wataweza uchunguzi wa kujua wapi serikali inafanya ufisadi.

Kwa kifupi Serikali ya Magamba za viongozi wake imefikia mwisho wa kifikiria.
 
Waziri kuzungumza na wapiga debe wapi na wapi? Hana watendaji wa chini, je vijana walioranduka na mibangi wanayovuta wangeamua kumpa kisago si angewasumbua FFU na kuongeza overhead cost kwa jeshi la polisisiem? Hizo ni sifa za kijinga, asome budget then aende kwenye utekelezaji tumechoka na maneno matupu ya magamba, mwenzie Magufuli kila mwaka anasoma kilomita lukuki lakini tunapigwa vumbi tu huku kitaa. Heri nchi ipate janga la Tsumani kuliko hili janga la CCM
 
Watanzania tunasiktsha,hv angekaa ofisin tu ndo ungemwna mtendaji bora,tusichnganye siasa kwa kila k2.
 
Kila anapokwenda Mwakyembe anaacha number yake ya simu, hata kwa wasafiri wa Treni kawapa number ya simu!
 
Mbona sijaona sehemu aliyoshushuliwa hapa. Zaidi wamempatia ukweli kwa ajili ya kuufanyia kazi. Ili kama kuna mtu aliuziwa kituo chao pale Makumbusho then Mwakyembe anatakiwa afuatilie na kuwapatia ufumbuzi...tuache ushabiki wa kijinga.

Wewe ndo mnafki. Hivi ukweli huo alpashwa kuupata moja kwa moja toka kwa watu wa chn yake au wapga debe?
 
Watanzania tunasiktsha,hv angekaa ofisin tu ndo ungemwna mtendaji bora,tusichnganye siasa kwa kila k2.

Je alienda kituo cha makumbusho kwanza aone ni kwa nini daladala hzo hazpaki mle?
 
Habari umeweka kinafiki,wewe lazima utakua gwandaz.

Majebere, usijali sana ndugu yangu. Viongozi wote wa ccm ni safi, chama kiko imara na 2015 mambo yote yatakuwa swaaafi kabisa. Haya maneno kwamba kuna hali ngumu ya maisha ni maneno tu na yatapita, mbona maisha bora Watanzania wanayo? Na ukisikia mtu analalamikia ugumu wa maisha jua huyo ni mvivu wa kutupwa anaetegemea serikali impe vya bure! Tupo pamoja.
 
tusiwakatishe tamaa watendaji wa selikari wanapotimiza majukumu yao,akikaa ofisini mnasema waziri hafanyi kazi.
 
If this thing is true hii sasa ni Lipua Lipua Show if not Orchestra...

Hilo la watu wa Bagamoyo kupaki hapo mbona dogo. Hivi hajanona makubwa hapo Mwege. Ukiwa kituo cha Mabasi Mwenge unashindwa kutofautisha kati ya kituo cha basi na siku ya gulio Katerero.

Ni aibu kubwa mno. Hakuna njia, hakuna mahali pa magari kupaki. Vibaka kibao. Mwenge Bus stop is more than a disaster na a serious show down of uzembe na ufisadi katika masuala ya mipango miji.

Kuna ufisadi mkubwa sana pale hasa katika collections. Ikifanyika stori ya uchunguzi hapo kutaibuliwa masuala ya ajabu. Naona Richard Makore wa Nipashe amekuwa akijaribu kugusa gusa. Asonge mbele. Watu wanafanya collection kubwa pale bila kulipa kodi hata thumuni...

Ok huko Makumbusho nako mbona kulishaharibika siku nyingi. Mtanzania waliandika stori hiyo zaidi ya miaka miwili iliyopita. Londa, aliyekuwa Meya wa Kinondoni (kumbuka kesi ya Londa na Makamba Vs Halima Mdee, Kamati ya Kanuni, Kinga na Madaraka ya Bunge) alihusishwa katima hilo deal. Hakuna hatua iliyochukuliwa.

Back to Mwakyembe, if this report is true kuwa ulikuwa pale na kilichoandikwa ndicho kweli kimejiri, can't u plz do a little research. Usisahau kuwa serikali yako imeoza kama mti wa mbuyu, ambao unakuwa umeoza ndani kote, lakini kwa nje unaonekana mkuuuuuuuuuuuubwa, ni suala la time to ya wawindaji kuugusa hata kwa bahati mbaya tu unaanguka.

Hilo la Mwenge mbona ni show ndogo tu kati ya shows nyingi na kubwa zinazodhihirisha kuwa u have failed this nation almost in every walks sphere of life, elimu, afya, maji, miundombinu, n.k, halafu eti muendelee kuaminiwa kuongoza! What.

Poleni Watanzania.
 
Lkn ni hatua nzuri kwa waziri kufika eneo la tukio na kuongea wahusika wenyewe yaani ma dereva na makonda na si uongozi wa kituo
 
Bila kushtukiza ataupataje ukweli?

Mijitu mingine kama si kangara basi ni bangi.
 
Dr Mwakyembe ameanza kuwa kama wale Drs wa kufoji wakati yeye aliusotea kuupata. Waziri kwenda kuongea na madereva wa daladala kituoni nadhani hapo itifaki haikuzingatiwa. The best he could have done ilikuwa kwenda kwa uongozi wa stand na kuwapa hayo maagizo na awape siku za kutekeleza na wamletee ripoti.
Utawala bora ni ule wa ku delegate powers then unasimamia utekelezaji.

Najua watumishi wengi wa wizara ni michwa but akiweka strategy ambayo inaweza kuwa implemented na yeye vizuri naamin atafanikiwa. nchi ni kubwa sana aache mambo ya kutafuta umaarufu wa shs 50.

Kama waziri anatakiwa atengeneze strategies na plans on how to implement them ili kuondoa msongamano wa usafiri Dar na kuhakikisha uchukuzi wa nchi nzima. Sasa kwa mtindo huu ataenda stand ngapi nchi nzima?

Pale posta mpya na ferry ukitaka kwenda mbagala lazima upitie kwenye dirisha la DCM.

Ikifika mwisho wa mwaka, mabasi kwenda mikoani nauli inakuwa mara 3 mpaka 4.

Dr.Mwakyembe please change ur management style. Tanzania sio kama Burundi ambayo unaikagua kwa siku mja na kuimaliza.
 
My Take: Napenda viongozi wasipende kufanya ziara ya kushtukiza bila kufanya uchunguzi kwanza kupitia wawakilishi.

Mimi naona ni bora anavyoshtukiza ili ajionee hali halisi .. 2nd hand info za wawakilishi zitachakachuliwa tu!
 
Habari umeweka kinafiki,wewe lazima utakua gwandaz.
kwa sababu haijakufurahisha unasema unafiki sijui gwandaz
Ndani tu ya magamba kuna layers zaidi ya NNE za Gamba, kila layer kivyake.
Uko wapi?
 
Back
Top Bottom