Waziri Muhongo ni muongo?

mi nahisi hiyo ni jama za mafisadi kumng'oa pale sababu kawabana hawapati mijihela waliyozoea kupata kabla proff hajaja.
 
Prof Muhongo na Maswi wameharibu mipango mingi ya mafisadi na wanatafuta jinsi ya kuwachafua waonekane hawafai.

Mkuu wangu ktk Tanzania usimwamini yeyote na hasa waliopo sehemu nyeti kama hii ya Nishati na Madini. Kuna habari kwamba vita hii ilikuwa na mambo mengi binafsi ikiwemo mahusiano ya kifuska kati ya Maswi na wabunge wawili wa viti maalumu CCM, Sarah Msafiri na Vicky Kamata!
 
Naomba niwe PILATO.
 
hivi hamna njia ya kufanya kutokua na imani na spika ili atolewe uspika au sheria zinasemaje?
 
Nitanzania tu nchi ambayo inaweza kukaa na Waziri Muongo, tena kwa kuthibitishwa na mtu mzito kama Spika na bado mtu huyu akaendelea kuwa na uwaziri wake.
 
Naamini kwamba waziri wetu wa nishati na Madini ni aina ya Mtu ambaye Tanzania inakaribia kuwapoteza. Ana tumia akili alizonazo,hashawishiwi kwa pesa na anafuata maadili yake. Tusiwe wajinga hongo iliyopo nishati na madini ni zaidi ya ndoto za wachangiaji kwenye Uzi huu. Tumpe support ndugu yetu HUYU na tuache kulaumu kwa sababu za udhaifu binafsi
Kwa wanaoifahamu vyema wizara ya madini na nishati na mfumo mzima wa hujuma ndani ya TANESCO wanaelewa Prof. anachosema. Ukweli ni kwamba wizara hiyo haijawahi kumpata mtu wa aina ya Prof. Muhongo ambaye kwa sasa anashambuliwa toka kila upande ili aachie ngazi, awaachie mafisadi mwanya wa kupumua. Alichojaribu kukifunuaa Prof. ni "Tip of an iceberg" pole pole ukweli utajifungua na mkweli kuthibitika, kama si kaatika awamu hii ya serikali angalau ijayo.
Prof. Muhongo anahitaji kutiwa moyo na kupata "support" ya watanzania wotekwani si mnafiki kama baadhi tunaoamini ni "wachapakazi" kumbe ndani yao ni ufisadi mtupu!
 
Taifa lolote Duniani ili liendelee lazima kuwepo na watalaam makini, wasemao ukweli daima na sikukumbatia uongo!!! Namfahamu sana Prof, hapendi kabisa kukumbatia uovu hata kidogo naweza nikasema anaamini sana katika ukweli, na alichokisema bungeni ni ukweli daima, kama sio kweli basi angepewa dakika 5 za kujitetea ama kuomba musamaha bungeni, hili halikufanyika nami bado naamini katika ukweli aliousema, Mnyika aliomba muongozo akapotezewa wenye akili tukajua maovu yamefunikwa, jamani yatufaa sana kumuombea na kumtia moyo maana mapambano aliyonayo ni makali sana tena yanaweza kuanzia juu, wengine wanaonekana kuchapakazi ni kuibua mambo, naamini ndani yake ni kamali tu.
 
Mimi naamini kamati ya ngwilizi,makinda na wabunge wamesema uongo,namwamini prof. muhongo kwakuwa hata kama atadanganya sio kiasi kikubwa,bunge limeogopa kudhalilika lakini ukweli upo na wabunge wanaujua ukweli huo.

Ni kweli mkuu hapo imepikwa siasa tu ndo maana wameishia kusema tuwasamehe. Kuna ukweli umefichwa hapo. Waziri alisema alikuwa na ushahidi usiokuwa na chembe ya shaka. Sasa wamemtwist tu aseme zilikuwa allegations ili wabunge wasafishike na hili lilijulikana mapema tu.
 
Ndugu wana jamvi kama mlivyoona kauli ya spika kuwa waziri ni mwongo na asirudie tena kuwatuhumu watu wakat hana ukweli.
je Ana faa kuendelea kuwa waziri wakati ni mwongo?
kwa wasio na kumbu kumbu ya nyuma waziri alisema wabunge wamehongwa na makampun ya uuzaji mafuta ili kuyapendelea! Kamat imesema si kweli!!
Au kwa vile Tanzania kujiuzuru ni neno geni! Na haritumiki kwa serikali hii?

Prof. Muhongo ni malaika ukimlinganisha na mawaziri wote waliomtangulia katika wizara hiyo. Mwacheni achapekazi. Hii ripoti ya Ngwilizi imepikwa tu ili wabunge wasafishwe basi. Kuna mambo makubwa na mazuri sana tu anaendelea kuyafanya katika wizara hiyo. Tutarajie mabadiliko makubwa tu wasipomhujumu. Tumeona mradi wa ujenzi wa bomba la gesi umeenza baada ya kuhujumiwa na wazee wa majenerata kwa muda mrefu.
 
Ndugu wana jamvi kama mlivyoona kauli ya spika kuwa waziri ni mwongo na asirudie tena kuwatuhumu watu wakat hana ukweli.
je Ana faa kuendelea kuwa waziri wakati ni mwongo?
kwa wasio na kumbu kumbu ya nyuma waziri alisema wabunge wamehongwa na makampun ya uuzaji mafuta ili kuyapendelea! Kamat imesema si kweli!!
Au kwa vile Tanzania kujiuzuru ni neno geni! Na haritumiki kwa serikali hii?

UMEONA watuhumiwa wa EPA JELA??? na WANAJULIKANA??? NDIO TANZANIA kusafishana... Ili kuendelea kuiba... WOTE WEZI...
 
Ni bahati mbaya Prof. Muhongo hakupewa fursa ya kueleza alichosema. Nadhani angefanya hivyo, pangechimbika mjengoni.
 
Mkuu wa CIA Marekani ajiuzulu kwa kashfa ya uzinzi. Uzinzi na uongo kipi ni hatar kwa taifa kinapofanywa na kiongozi.
 
katika siasa za dunia ya tatu uongo ni sehemu muhimu ya siasa ila tu uongo huo uwe unakaribiana na ukweli. Ni mwanasiasa gani ambaye huwa hasemi uongo. Je ni kweli ahadi zilizoahidiwa 2010 na chama tawala zitaweza kutekelezwa kabla ya 2015? Je ile ndege tuliyoambiwa imeanza kupaa na fl 2006 ya kwenda kwenye maisha bora imefikia wapi? Je tunaweza sasa kutengeneza mvua kama alivyokuwa ameahidi EL kipindi kile? nk, nk, nk.
 
Muhongo huon wiz huu? Nimepa umeme 10,000 halafu cheki wezi walivyochanganua then change hakuna.....
Summary
units :18.20 kwh
total unt cost:tsh4027.85
tax(VAT18%EWURA1%REA3%):tsh886.13
fixed amount:tsh 3841.00tena
tax(VAT18%EWURA1%REA3%tsh845.02
total cost :9860.00 je hiyo 140/=inakwenda wapi? Na wangapi wanakatwa? Na waziri yupo
 
Prof Muhongo ni Muongo saana. Kwanza keshatudanganya hakuna mgawo wa umeme wakati tunashinda na wakati mwingine tunalala giza. Sasa kama sio uongo ni nini???

Yaa, muongo kama lilivyo jinale. Mgao upo though kimya kimya
 
Yaa, muongo kama lilivyo jinale. Mgao upo though kimya kimya

No research no right to speak je Prof Muhongo si anajua hilo je ni kweli huwa anasema bila kuwa na uhakika? Kama ni hivyo BASI AJIULIZE SANA AU NI MBINU ZA WEZI!
 
Watanzania siyo wajinga;Anne Makinda aliwekwa pale kitini na mafisadi ili kulinda mafisadi.Hicho ndicho akifanyacho.Wabena ni wakweli daima-imekuwaje huyu bibi kuwa Mwongo aliyekubuhu.

Hoja ya Zitto ilikuwa nzito na muhimu, Werema akaifutilia mbali,werema kama Makinda wapo kuwalinda mafisadi.
Zitto mkweo nini. Mwanasheria Mkuu wa Serikali alieleza baadhi ya hoja za Mhe. Zitto kuwa zinashughulikiwa na taasisi zingine tayari. Baadhi akakubaliana na kusema zinahitaji kufanyiwa Kazi kwanza. Naona wewe hukusikiliza ila ulikuja kusimuliwa tu. pole.
 
Prof Muhongo ni Muongo saana. Kwanza keshatudanganya hakuna mgawo wa umeme wakati tunashinda na wakati mwingine tunalala giza. Sasa kama sio uongo ni nini???

Wewe ndo mwongo. Umeona wapi mgao wa Umeme. Jifunze, na nadhani itakusaidia maishani Mwako, kutofautisha Kati ya mgao wa umeme kwa upande Mmoja na kukatika kwa Umeme kwa hitilafu zinazotokea bila hodi na pia kwa matengenezo yaliyopangwa. Kukatika kwa ghafla tumeona baada ya matengenezo Wananchi wakiombwa radhi na kuzima Umeme kwa matengenezo taarifa hutolewa mapema. Sasa Kama wewe hisikilizi wala husomi vyombo vya habari ndo matokeo hayo. Pole tena
 
Hata hili nalo unataka tubishane????? Tatizo ambalo naliona kwa watanzania tulio wengi ni kuishi kwa mazoea. Tumeshazoea kuwapa heshima hata watu wasiostahili na ndio maana hata viongozi Wazinzi, Waongo, Wtukanaji, Wezi, wahujumu uchumi wa nchi badala ya kuwaambia ukweli huwa tunaishia kuwasifia. Ni vizuri NYEUSI tukaiita nyeusi na NYEKUNDU tukaiita nyekundu. Kiongozi wa umma lazima uwe tofauti na kiongozi wa kijifamilia cha watu wa3 au wa4 ambao unaweza ukawaambia lolote kwa sababu tu wewe ndio unawatafutia chakula. Come on Watanzania, it's now high time we start facing the facts in order to save our nation for us and the generation to come. ukweli kwanza jamani.

Back
Top Bottom