Waziri Muhongo ni muongo?

Ndugu wana jamvi kama mlivyoona kauli ya spika kuwa waziri ni mwongo na asirudie tena kuwatuhumu watu wakati hana ukweli.
Je Ana faa kuendelea kuwa waziri wakati ni mwongo?

Kwa wasio na kumbukumbu ya nyuma waziri alisema wabunge wamehongwa na makampuni ya uuzaji mafuta ili kuyapendelea! Kamati imesema si kweli!!
 
Prof Muhongo ni Muongo saana. Kwanza keshatudanganya hakuna mgawo wa umeme wakati tunashinda na wakati mwingine tunalala giza. Sasa kama sio uongo ni nini???
 
Hii ni vita ya MGAO WA UMEME.
Ndugu wana jamvi kama mlivyoona kauli ya spika kuwa waziri ni mwongo na asirudie tena kuwatuhumu watu wakat hana ukweli.
je Ana faa kuendelea kuwa waziri wakati ni mwongo?
kwa wasio na kumbu kumbu ya nyuma waziri alisema wabunge wamehongwa na makampun ya uuzaji mafuta ili kuyapendelea! Kamat imesema si kweli!!
Au kwa vile Tanzania kujiuzuru ni neno geni! Na haritumiki kwa serikali hii?
 
Mimi niliweka mada kama hii kwa kiingereza, Mods wameitrash probably
 
Tikatika acha kutikisa mtogwa ulio kichwani kwako. Unategemea nini kamati ya bunge la ccm kuwachunguza wabunge wa sisiem? Hao waliotuhumiwa au kusingiziwa waende mahakamani ndiko mbivu na mbichi zitajulikana
 
Prof Muhongo ni Muongo saana. Kwanza keshatudanganya hakuna mgawo wa umeme wakati tunashinda na wakati mwingine tunalala giza. Sasa kama sio uongo ni nini???

Watanzania siyo wajinga;Anne Makinda aliwekwa pale kitini na mafisadi ili kulinda mafisadi.Hicho ndicho akifanyacho.Wabena ni wakweli daima-imekuwaje huyu bibi kuwa Mwongo aliyekubuhu.

Hoja ya Zitto ilikuwa nzito na muhimu, Werema akaifutilia mbali,werema kama Makinda wapo kuwalinda mafisadi.
 
Tikatika acha kutikisa mtogwa ulio kichwani kwako. Unategemea nini kamati ya bunge la ccm kuwachunguza wabunge wa sisiem? Hao waliotuhumiwa au kusingiziwa waende mahakamani ndiko mbivu na mbichi zitajulikana

Kama kuna mtu wa kwenda mahakamani hapo ni Mhando tu. Wakina Sarah Msafiri waende mahakamani kufanya nini wakati wameshasafishwa? Na Prof. Muhongo kakiri kwamba ilikuwa allegations tu
 
Nilimsikia Makinda pia akimtuhumu katibu mkuu wa Nishati Maswi kuwa ndio alitaka kuwahonga wabunge milion mbili mbili ila akamaliza kwa kusema anampa karipio kali asirudie! maajabu haya! Yaaani mtu atake kutoa rushwa ili kupindisha ukweli halafu unamuambia asirudie tena! hii si ilikuwa ni jinai? pia aliwakemea wabunge wasiwe wanasema mambo wasiyokuwa na uhakika nayo ila sikumsikia akijikemea mwenyewe kwa kukurupuka kuvunja kamati ya bunge ya nishati na madini bila kujiridhisha kweli walihongwa! huyu anafanana na spika ya redio mbovu!
 
Siku Watz tutakapojua uongo wa "uongo wa Muhongo" hatutaendelea kuwa wapole hivyo. Kuna umri huwaambia wanetu kwamba watoto wachanga hununuliwa hosp au sokoni, huu unakuwa ukweli kwa watoto hadi siku akili zao zitakapopevuka. Wakati mwingine wala hawahitaji kuuliza tena bali wataona tu mama jirani tumbo kubwaaa, lkn alipoenda hosp karudi na mtoto. Tz yamefanyika maovu mengi makubwa lkn hakuna anaekubali kuwajibika, na hili wanaloita kudhalilisha Bunge limeisha kienyeji hivi hivi. Something hidden.
 
Mimi naamini kamati ya ngwilizi,makinda na wabunge wamesema uongo,namwamini prof. muhongo kwakuwa hata kama atadanganya sio kiasi kikubwa,bunge limeogopa kudhalilika lakini ukweli upo na wabunge wanaujua ukweli huo.
 
Ukweli hautaujua kamwe!jaribu kufikiria nje ya box kidogo tu mtaelewa!Prof alitaka apasue ukweli na ku-resign awaachie upuuzi wao na uongo wao waendelee nao,wakaitwa kwa majadiliano,huyo bi kiroboto akaambiwa wasimsumbue Prof maana ana akzi kubwa sana kwa manufaa ya taifa hasa kwenye madini,nishati,gesi na mafuta yake zaidi ya upuuzi wao wa kuindana ndani ya bunge,ile report imesukwa kumaliza uhasama na kuyafanya hayo yawe historia.Ndio maana umeona Prof ametulia ama la angewaachia upuuzi woa wa kubebana na kulindana,siasa za maji taka!
 
Naamini kwamba waziri wetu wa nishati na Madini ni aina ya Mtu ambaye Tanzania inakaribia kuwapoteza. Ana tumia akili alizonazo,hashawishiwi kwa pesa na anafuata maadili yake. Tusiwe wajinga hongo iliyopo nishati na madini ni zaidi ya ndoto za wachangiaji kwenye Uzi huu. Tumpe support ndugu yetu HUYU na tuache kulaumu kwa sababu za udhaifu binafsi
 
Ndugu wana jamvi kama mlivyoona kauli ya spika kuwa waziri ni mwongo na asirudie tena kuwatuhumu watu wakat hana ukweli.
je Ana faa kuendelea kuwa waziri wakati ni mwongo?
kwa wasio na kumbu kumbu ya nyuma waziri alisema wabunge wamehongwa na makampun ya uuzaji mafuta ili kuyapendelea! Kamat imesema si kweli!!
Au kwa vile Tanzania kujiuzuru ni neno geni! Na haritumiki kwa serikali hii?
...kwetu sisi wa mtaani ambao tukitazama "necha" ya kinachojadiliwa huamini pia ushahidi wa kimazingira (tofauti kabisa na kina "joni kisomo" wa bungeni, na wa "humu jf" halikadhalika) hatuajaamini kama profesa kaongopa...ushirikiano wa kutafuna "za umma"...huwafanya hata mahasimu wa itikadi za kisiasa kuwa washirika..usisahau somo kwenye skandali ya bi saada wa kiti4..aliekuwa katibu wa cdm alishiriki na wana "nambari 1" kuhujumu...kimazingira, "purofesa" na maswi..wana ukweli, lkn ukweli umehujumiwa "ki-joni kisomo"...voice frm the street...ALUTA CONTINUA...!
...k
 
Ukweli hautaujua kamwe!jaribu kufikiria nje ya box kidogo tu mtaelewa!Prof alitaka apasue ukweli na ku-resign awaachie upuuzi wao na uongo wao waendelee nao,wakaitwa kwa majadiliano,huyo bi kiroboto akaambiwa wasimsumbue Prof maana ana akzi kubwa sana kwa manufaa ya taifa hasa kwenye madini,nishati,gesi na mafuta yake zaidi ya upuuzi wao wa kuindana ndani ya bunge,ile report imesukwa kumaliza uhasama na kuyafanya hayo yawe historia.Ndio maana umeona Prof ametulia ama la angewaachia upuuzi woa wa kubebana na kulindana,siasa za maji taka!

Ingelipendeza kama ungeweka reference mkuu; zaidi ya hapo itakuwa ni porojo mkuu!

Back
Top Bottom