Waziri mmoja ni Raia wa Marekani: Gazeti la Dira

Tatizo la Watanzania ni ushabiki na uivu na ndiyo maana nchi yetu haiendelei. Je ni kwanini hatuna Dual Citizenship mpaka sasa

Nchi za ulaya, India, China, Nigeria, Mexico, USA etc zina ruhusu Dual je sisi ni kwanini hatuna, je tuna kitu gani special na hizi nchi nyingine hazina??. Kama mtu ni mzawa au ni mtoto wa mzawa sioni sababu ya muhimu ya kumnyima Dual Citizenship. Zaidi ya kejeli, madongo, na wivu kwa Watanzania wanaoishi nje hakuna sababu ya msingi ya kutokuwa na Dual Citizenship.
Nikweli tunahitaji dual citizenship lakini kwa sheria iliyopo, ukiwa raia wa nchi yoyote ile basi automatically unapoteza sifa za kuwa raia wa Tanzania sasa kama kweli kuna waziri anauraia wa USA basi kapoteza sifa za kuwa mtanzan ia
 
Waziri katajwa soma vizuri thread husika utamjua

Kwani mkuu ukimtaja wewe utapungukiwa na nini? ya nini tuanze kuangaika kuitafuta hiyo thread wakati wewe unamjuwa si ututajie tu kuokoa muda? don't you think!
 
Hiyo Kadi yenyewe ni ya kuchonga:Hebu angalia kwenye rangi nyekundu inaonyesha Card Expires 11/01/94 ikimaanisha muda wake kutumika unaishia tarehe hiyo. Sasa angalia Resident since 11/01/97 inamaanisha ameanza kuwa raia mkazi(permanent Resident) tangu tarehe hiyo iliyotajwa. HII NI CARD YA KUCHONGA!!
 
[/SIZE][/FONT]

Nadhani kuna haja ya kuipenda Tanzania kuliko kujipenda wenyewe. Dual citizenship hakiwezi kuwa kipaumbele cha wala mkakati wa maendeleo kwa watanzania kwa sasa. Siamini kuwa Tanzania itapata maendeleo kwa kutegemea watu wasioaminika, walioamua kuukana utaifa wao ili kupata manifaa binafsi. Hawa ni watafuta chakula above all, period. Ni kutokana na kutafuta chakula tu, hawa jamaa waliamua kuukana uraia wa Tanzania, na sasa wangependa kurudi kwa kupitia mlango wa nyuma; kwamba wanakuja kuwekeza! Hapa hakuna suala la wivu ndugu zangu, it is the matter of sticking to the principle; nani ni raia, nani si raia, period!
Kama diaspora wanataka kuwekeza, si waje wawekeze kama mabepari wengine? Kwani Barrick, Anglogold Ashanti, Resolute Mining, na wengineo walipokuja waliomba uraia wa Tanzania? Hapana, waliomba leseni na mikataba ya uwekezaji.
Uwekezaji na uraia wa nchi mbili havihusiania hata kidogo. Litakuwa ni jambo la ajabu iwapo serikali itaanza kuwakirimu watoro ilihali raia wa kawaida wanaendelea kusota. Mtu yeyote aliyewahi kuwa raia wa nchi hii halafu akakana uraia wa nchi yake hawezi kuaminika, ati apewe uraia tena, kwa kisingizio cha kuleta vitegauchumi (vyake!). Lakini iwapo diaspora yuko huko Ulaya au Amerika, bado hajaukana uraia wa Tanzania na sasa anataka kurudi nyumbani, si arudi? Nadhani huyu hazuiwi na si sehemu ya mjadala huu.
Uraia wa nchi unaweza kulinganishwa na kuwa mwanafamilia. Huwezi kukana familia yako na kuhamia familaia ya jirani, halafu utake kutambuliwa kama mwanafamilia zote mbili; kwa familia inayoheshimika au kujiheshimu haiwezi kukupokea tena aslani. Uliidhalilisha!
Hata hivyo, wahemeaji hawawezi kuleta maendeleo nyumbani, hilo tusahau kabisa, na CCM ikitaka kujichimbia kaburi, basi serikali yake ipeleke muswada wa dual citizenship Bungeni ione.
Wakhtanabahu

The only way mkiendelea kuikataa hii hoja ya dual citizenship ni pale Tanzania itakapojitoa kwenye East African Community. Kenya wameruhusu, kwa maana hiyo Kenyans in diaspora watatupiga bao tena la kisigino.
 
Kuna habari kuwa CHADEMA wana mbunge ambaye si raia wa Tanzania...tena kwa kuukana uraia wake. Na kuna taarifa ambazo zinadai kuwa ana passport ya nje (kama Plan B just in case)

Lakini sasa hivi huyu mheshimiwa yuko bungeni kama mmoja ya wanaotunga na kupitisha sheria katika nchi hii

Je hii inaukweli wowote au ndio smear campaigns? Inawezekana CHADEMA wenyewe kwa wenyewe washalizungumza internally.

Mindhali CHADEMA wako humu wanaweza kutuweka sawa kwenye hili.

Thread za kiitaarabu kama hizi hazina mashiko. kama hakuna jina la mtuhumiwa sasa hapa unapost hiyo habari ili tujadili nini? huku ni kupungukiwa maarifa.
 
Umeileta ili kuua nguvu tread ya waziri Mmarekani? Hata aina ya kuileta bado hujui unadhihirisha ulivyotumwa!! Kama ni tetesi kwenye heading sema tetesi! Hili ndio tatizo la kuvamia kizazi cha .com wakati we ni kizazi cha Ngumbalo!! Hapo bado we ni wamakamo je ukizeeka siutakuwa mchawi?
 
attachment.php

Yupo wizara moja ya Viwanda na Biashara !
 
Kati ya hawa hapa unahisi nani anaweza kuwa na uraia wa Marekani? Maana inasemekana ni kutoka wizara ya Viwanda na biashara.

Huyo jamaa aliyeko mkono wa kulia sidhani kama ana uraia wa Marekani kwa sababu ana kesi ya kujibu Virginia. Yeye na January Makamba wanaelewa wazi kuwa hawawezi kukanyaga ardhi au kisiwa kilicho chini ya utawala au uangalizi wa serikali ya Marekani kutokana na uozo waliofanya. Majina yao yako State Dept na TSA. Kama jamaa angekuwa na uraia jamaa wangekuwa wameshamshukia hapa Bongo. Kwa Chami, mmh sina uhakika.
 
Wamefanya nini?
 
Mimi napenda watu wanaozungumza with facts na siyo lazima useme hata kama hujui la kusema. Dual citizenship siyo kitu kigeni duniani Afrika ikiwamo. Tuelezwe ni madhara gani zinapata nchi zilizoruhu dual citizenship. Kama hakuna kitu cha kutisha basi tusemeje kwa anayepinga. Tuseme wivu sioni sabau au tuseme ni kufuata mkumbo au hofu tu isiyo ya msingi. Pilipili usizokula za kuwasha nini. Uganda ina dual citizenship je inajutia nini na kwa nini wasiifute kama haina manufaa kwao?

Katika nchi yoyote kuna makundi na tabaka ambazo zote zinatarajia nchi yao iwatambue kuwa wapo na matakwa yao yanazingatiwa. Mfano passport in haki ya kila raia, kunywa pombe au kuvuta sigara, nk. pamoja na madhara yake ni kwa wachache tu ingawa wote wanaruhusiwa. Hili suala la dual citizenship nijuavyo halina madhara na kama yapo basi ni vipi tunaruhusu uraia wa watu baki kuomba na kupewa uraia. Kama ni usalama ni yupi wa kuogopa zaidi. Hoja ya kipaumbele kuhusu dual citizenship haina mantiki sana hapa maana ruksa yake haizuii mengine unayoona ni ya kipaumbele kufanyika. Dual citizen inapotolewa haibagui ni fursa kwa wote walio na green card na wasio nayo, mtoto wa tajiri na mtoto wa masikini, n.k. Jamani acheni kupotosha umma. kama waziri alivyosema, zipo faina tukifungua malango wa dual citizenship.
 
Cyril Chami naona hata USA possibly hajakanyaga. Phd. kasomea Canada

542.png

Name Cyril Chami
Surname Chami
First Names Cyril August
Alternate Name
Title Dr
Country of Birth Tanzania
Positions From To Organisation Position 2008
Ministry of Industry, Trade & Marketing Deputy Minister of Industry, Trade & Marketing 2006 2008
Ministry of Foreign Affairs & International Cooperation Deputy Minister of Foreign Affairs & International Cooperation 2005 Moshi Vijijini Constituency MP for Moshi Vijijini
Date of Birth 9 Feb 1954
Political Affiliation CCM

EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
Albelta - Canada Doctor of Philosophy 1995 2001 PHD
University of Dar es Salaam MBA 1992 1994 MASTERS DEGREE
University of Dar es Salaam BA 1988 1992 GRADUATE
Uru Seminary A-Level Education 1985 1987 HIGH SCHOOL
Uru Seminary O-Level Education 1981 1984 SECONDARY
Manushi Ndoo Primary School Primary Education 1974 1980 PRIMARY
--------------------------------------------------------------------------------
CERTIFICATIONS
Certification Name or Type Certification No. Issued Expires
No items on list
--------------------------------------------------------------------------------
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From Date To Date
Ministry of Foreign Affairs & International Relations Deputy Minister 2006
State House -President's Economic Policy Advisory Unit (PEPAU) Economist 2003 2005
Research on Poverty Alleviation (REPOA) Research Coordinator 2002 2003
University of Dar es Salaam Tutorial Assistant 1992 1995
--------------------------------------------------------------------------------
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of Economic Planning Committee-Kipawa 2004 -
Chama Cha Mapinduzi - CCM Chairman - UVCCM(Uru Seminary) 1983 1987
[ Retrieved on 6/7/2006 - www.parliament.go.tz ]
 
... Dual citizenship siyo kitu kigeni duniani Afrika
Mada sio manufaa ya dual citizenship. Topic ni kwamba kuna allegations za Waziri asiye raia wa Tanzania maana ana uraia wa nchi nyingine. Kama ni kweli, Katiba imevunjwa, kwa sheria zilizopo sasa.
 
hao wanaopiga kelele turuhusu dual citizen walisahau nini tanzania?
kwa nini wanataka kuwa huku na huku kama sio wizi unawasumbua?
wenge wenu hapa ulaya/usa hamna nyumba wala mbele maisha yamewapiga,
natena mtu hasije nivamia na maneno kwamba nina wivu, wengine wenu mnalia kubabuliwa kila siku na vibibi vyenu vya kizungu.
hacheni upuuzi hela ya box unaweza kuwekeza kwenye nini? biashara ya mishuma
kwanza mlikujaje huku kama sio kimtindo mtindo sasa mmeng'ang'ania kutoka,
wakiwa wapi hiyo dual mtakwenda kuiba bongo na kurudi huku ulaya,
mwezi wa pili world bank ilitoa Ksh 60mil kwa ajili ya serikali ya kenya kuhamasisha wakenya warudi kwao wakajenge nchi
hizo hela sio mkopo ni free ina maana hawataki kikalagosi huko kwao ulaya/usa.
wengi wetu hapa mkiambia mseme ukweli wa maisha mnayoishi huko ni ya kubahatisha tu,
rudini nyumbani hacheni kelele za kuiga mambo mara kenya,nigeria upuuzi mtu
turudi kwenye mada
waziri gani ni mmarekani?

Dual citizenship kwa Tanzania bado kabisa kufikia huko, na kama tukifanya hivyo sasa ni hatari kubwa sana kwa uchumi na usalama wa nchi yetu. Tusiwe watu wa kukurupuka tu eti kwa kuwa nchi fulani na nchi fulani wana -dual citizenship basi na sisi TZ tuwe hivyo ,no, mazingira yetu bado hayaruhusu. Tukifanya hivyo, watu wabaya hasa viongozi na wafanyabiashara wakubwa watatumia mwanya huo kuhamisha mali zetu kupeleka huko kwenye makazi yao mapya kwa urahisi kabisa na kwa halali kwa kuwa ni mwananchi, na pia hawatajali usalama wa nchi yetu kwa kuwa wao na familia zao wana pa kukimbilia endapo itabidi. Dual citizenship sio mahitaji ya Watanzania hawa ambao hata mlo mmoja tu wa siku unawasumbua sembuse hiyo mitatu, dual citizenship ni mahitaji ya watu wachache sana 0.0001 ya watz milioni 45, ambao wameishaikana nchi yetu au wapo mbioni kuikana ila wanatamani maliasili za tz ambazo bado kwa kiasi kikubwa ni mali ya watz, sasa anaona atazikosa. Hoja zinazotolewa na watetezi wa dual citizenship, hasa waziri wa mambo ya nje wa TZ ni dhaifu mno kuweza kukubalika na watu wanaofanya uchanganuzi wa kina, eti ili hao watz waliopo nje ambao wameshaukana utz na kupata uraia wa huko waweze kuwekeza nchini,hivi kweli hii ndiyo sababu? kwani wote hao wawekezaji tunaowavutia kila siku waje wawekeze nchini ni watz au kwamba tumeweka sharti kwamba ili kuwekeza nchini lazima uwe raia wa tz? Hao Diaspora wanaweza tu kuwekeza nchini kama wageni wowote wa nje wanavyowekeza. Kwa kweli mimi napinga sana wazo hili kwa kuwa tz bado haijajiandaa wala kufikia maendeleo ya kuweza kuwa na dual citizenship, nchi itafirisika haitapata faida yoyote na wala hilo sio hitaji la watz ambao wengi wao hata hiyo passport hawajawahi kuiona, sasa vipi wafikirie kuwa na uraia wa nchi mbili?. Kwa maana hiyo kama kweli yupo waziri kwenye baraza letu la mawaziri mwenye uraia wa marekani, kwa maana kama ana passport ya marekani inatakiwa aachishwe kazi mara moja na kushtakiwa kwa kuvunja sheria ya uhamiaji na kujipatia ajira tz kinyume na sheria.

Dual citizenship ya nini?kuna faida gani kwa sisi wakazi wa uswahilini?

[/SIZE][/FONT]

Nadhani kuna haja ya kuipenda Tanzania kuliko kujipenda wenyewe. Dual citizenship hakiwezi kuwa kipaumbele cha wala mkakati wa maendeleo kwa watanzania kwa sasa. Siamini kuwa Tanzania itapata maendeleo kwa kutegemea watu wasioaminika, walioamua kuukana utaifa wao ili kupata manifaa binafsi. Hawa ni watafuta chakula above all, period. Ni kutokana na kutafuta chakula tu, hawa jamaa waliamua kuukana uraia wa Tanzania, na sasa wangependa kurudi kwa kupitia mlango wa nyuma; kwamba wanakuja kuwekeza! Hapa hakuna suala la wivu ndugu zangu, it is the matter of sticking to the principle; nani ni raia, nani si raia, period!
Kama diaspora wanataka kuwekeza, si waje wawekeze kama mabepari wengine? Kwani Barrick, Anglogold Ashanti, Resolute Mining, na wengineo walipokuja waliomba uraia wa Tanzania? Hapana, waliomba leseni na mikataba ya uwekezaji.
Uwekezaji na uraia wa nchi mbili havihusiania hata kidogo. Litakuwa ni jambo la ajabu iwapo serikali itaanza kuwakirimu watoro ilihali raia wa kawaida wanaendelea kusota. Mtu yeyote aliyewahi kuwa raia wa nchi hii halafu akakana uraia wa nchi yake hawezi kuaminika, ati apewe uraia tena, kwa kisingizio cha kuleta vitegauchumi (vyake!). Lakini iwapo diaspora yuko huko Ulaya au Amerika, bado hajaukana uraia wa Tanzania na sasa anataka kurudi nyumbani, si arudi? Nadhani huyu hazuiwi na si sehemu ya mjadala huu.
Uraia wa nchi unaweza kulinganishwa na kuwa mwanafamilia. Huwezi kukana familia yako na kuhamia familaia ya jirani, halafu utake kutambuliwa kama mwanafamilia zote mbili; kwa familia inayoheshimika au kujiheshimu haiwezi kukupokea tena aslani. Uliidhalilisha!
Hata hivyo, wahemeaji hawawezi kuleta maendeleo nyumbani, hilo tusahau kabisa, na CCM ikitaka kujichimbia kaburi, basi serikali yake ipeleke muswada wa dual citizenship Bungeni ione.
Wakhtanabahu

Unapochukua uraia wa USA huna haja ya kuukana utanzania. You can keep your passport.

Na huwezi kuwa na passport ya TZ bila ya kuonyesha uthibitisho wa uraia

USA wanakubali dual nationality Tanzania haina

Sheria za Tanzania ziko wazi ukitaka uraia wa nchi nyingine inabidi uukane uraia wako wa TZ

Nimechukua uraia wa US na nina passport 2, hii ya blue na ya kijani yangu ya kibongo. Sioni tatizo lolote kwangu ama kwa huyo waziri. Shida iko wapi jamani? Yeye bado ni mbongo mwenzetu. Tuko wengi sana wenye pasi mbili wengine wanazo hadi 4

Mada sio manufaa ya dual citizenship. Topic ni kwamba kuna allegations za Waziri asiye raia wa Tanzania maana ana uraia wa nchi nyingine. Kama ni kweli, Katiba imevunjwa, kwa sheria zilizopo sasa.
 
Titan, Masanja, Mwakatare na Sophist mimi naona mawazo yenu yamepitwa na wakati sana!!!

Kuna wanaosema eti Dual citizenship wafanyabiashara watakimbiza pesa nje je ni mfanya biashara gani ambae hawezi kukimbiza pesa nje kwasababu ya uraia. Hapa Marekani mtu yeyote anaweza kufungua account ya bank hata kama si raia, mtu yeyote anaruhusiwa kununua nyumba hata kama si raia!!! sasa mkisema kwasasa wafanyabishara hawapeleki pesa nje kwasababu ya uraia si ukweli kabisa, hata kuna Mawaziri na maraisi wana account nje. Hivyo hii hoja si ya kweli na niya ushabiki maana haina mfano zaidi ya maneno tu.

Hoja nyingine ni kwamba watu watafaidika! je watafaidika na nini? ambacho kwa sasa hawawezi kufaidika je Tanzania itawapa nini hawa watu walioko nje wafaidike?. Hakuna faidi yeyote nchi yetu ni masikini sababu kubwa ni ndugu na jamii. Kama Ndugu zako na mababu wawezikwa Tanzania ni vigumu kuomba visa ya kwenda kuangalia geneza la ndugu zako na ndiyo maana nimesema hii ni kwa watu waliozaliwa Tanzania na wenye wazazi Tanzania. Sasa nyie mnasema kama nina mtoto kazaliwa hapa na atakuwa raia wa marekani kuanzia siku ya kwanza na mimi nikitaka kumpa nyumba yangu kwa uzee haitawezekana na nyumba iende kwa serikali!!! je huyu mtoto au mimi nimefanya kosa gani bali kuwa nje.

Je Watanzania pesa zinazotoka Tanzania kuja kwa watu wanaoishi nje na pesa zinazoingia Tanzania kwa watu wanaoishi nje zipi ni nyingi?? na mnavyosema faida ni zipi hasa? mimi naona faidi ni kwa Tanzania na siyo kwa mtu anayeishi nje. Mimi nikija Tanzania serikali inanisaidia nini kuliko hapa Marekani?? Hakuna msaada wowote watu wa nje tunaoupata kutoka serikalini na sababu kubwa ya kuja na kutuma pesa Tanzania ni kwasababu ya uzawa na ndugu kama wazazi, wajomba, n.k

Kama hamna sababu ya msingi basi tukubaliane ni uivu tu na kutowapenda watanzania wanaoishi nje. Kitendo cha kusema kunawafanyabishara watakimbiza pesa si kweli kwani kunawafanyabishara wangapi wana account nje je mnafikiri Baresa, Mengi, n.k hawanapesa nje au wakitaka kwenda nchi yeyote wanaenda hata kama kuishi na kwa pesa yao wanapewa mpaka uraia.

Fikirieni nchi na si ubinafsi. Mnavyosema itamfaidisha vipi Mtanzania wa kawaida je nyie mnamsaidia vipi Mtanzania wa kawaida! kuna kidu gani ambacho wewe unafanya cha kuisaidia Tanzania kuliko mimi?
 
Huyo jamaa aliyeko mkono wa kulia sidhani kama ana uraia wa Marekani kwa sababu ana kesi ya kujibu Virginia. Yeye na January Makamba wanaelewa wazi kuwa hawawezi kukanyaga ardhi au kisiwa kilicho chini ya utawala au uangalizi wa serikali ya Marekani kutokana na uozo waliofanya. Majina yao yako State Dept na TSA. Kama jamaa angekuwa na uraia jamaa wangekuwa wameshamshukia hapa Bongo. Kwa Chami, mmh sina uhakika.
Mimi kwa kuangalia haraka haraka anaweza kuwa jamaa wa kulia. kwa sababu jamaa wa kushoto alishawahi kuwa ktk serikali ya awamu ya Kwanza ya JK. kama angekuwayeye wangelisha muumbua.
 
Dual citizenship kwa Tanzania bado kabisa kufikia huko, na kama tukifanya hivyo sasa ni hatari kubwa sana kwa uchumi na usalama wa nchi yetu. Tusiwe watu wa kukurupuka tu eti kwa kuwa nchi fulani na nchi fulani wana -dual citizenship basi na sisi TZ tuwe hivyo ,no, mazingira yetu bado hayaruhusu. Tukifanya hivyo, watu wabaya hasa viongozi na wafanyabiashara wakubwa watatumia mwanya huo kuhamisha mali zetu kupeleka huko kwenye makazi yao mapya kwa urahisi kabisa na kwa halali kwa kuwa ni mwananchi, na pia hawatajali usalama wa nchi yetu kwa kuwa wao na familia zao wana pa kukimbilia endapo itabidi. Dual citizenship sio mahitaji ya Watanzania hawa ambao hata mlo mmoja tu wa siku unawasumbua sembuse hiyo mitatu, dual citizenship ni mahitaji ya watu wachache sana 0.0001 ya watz milioni 45, ambao wameishaikana nchi yetu au wapo mbioni kuikana ila wanatamani maliasili za tz ambazo bado kwa kiasi kikubwa ni mali ya watz, sasa anaona atazikosa. Hoja zinazotolewa na watetezi wa dual citizenship, hasa waziri wa mambo ya nje wa TZ ni dhaifu mno kuweza kukubalika na watu wanaofanya uchanganuzi wa kina, eti ili hao watz waliopo nje ambao wameshaukana utz na kupata uraia wa huko waweze kuwekeza nchini,hivi kweli hii ndiyo sababu? kwani wote hao wawekezaji tunaowavutia kila siku waje wawekeze nchini ni watz au kwamba tumeweka sharti kwamba ili kuwekeza nchini lazima uwe raia wa tz? Hao Diaspora wanaweza tu kuwekeza nchini kama wageni wowote wa nje wanavyowekeza. Kwa kweli mimi napinga sana wazo hili kwa kuwa tz bado haijajiandaa wala kufikia maendeleo ya kuweza kuwa na dual citizenship, nchi itafirisika haitapata faida yoyote na wala hilo sio hitaji la watz ambao wengi wao hata hiyo passport hawajawahi kuiona, sasa vipi wafikirie kuwa na uraia wa nchi mbili?. Kwa maana hiyo kama kweli yupo waziri kwenye baraza letu la mawaziri mwenye uraia wa marekani, kwa maana kama ana passport ya marekani inatakiwa aachishwe kazi mara moja na kushtakiwa kwa kuvunja sheria ya uhamiaji na kujipatia ajira tz kinyume na sheria.

Crack down
 
Well said hata mm na resident permit ya nchi fulani huku nikiwa na passport ya Tanzania. Ni watu wachache wenye kuelewa BUT labda wana strong argument dhidi ya huyo waziri let us give them space and time to see..

Mbona kwanza kama ni hii imesha expire 1994?

Hiyo permanent resident permit not meaningful expired ndio maana ni permanent resident permit, not temporal resident permit. Card hutolewa mpya kila baada ya miaka 10 kwa sababu ya security issues, mtu anabadilika sura, sheria za nchi zinabadilika, status ya mtu inaweza kuwa na migogoro, mtu anaweza asiwe anafuata sheria, ndio maana baada ya miaka hiyo unapoomba for renewal, ni nafasi ya authority to review regal behaviour.

Kwa kawaida mtu akiwa na permanent resident status is for good, isipokuwa criminal cases can change her/his status or be deported.
 
Back
Top Bottom