Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron atangaza kujiuzulu baada ya Uingereza kujitoa EU

"I love my country, but it's time for someone else" ~ David Cameron

Cc we know who.

#waytogodavidcameron.
 
Kaka sijui sisi WTZ tunashida gani hata sifahamu. Toka tuko shule kiongozi mzuri ni yule aliyepoa hata kama hawezi kazi, mtu akiwa serious tunasema mnoko hafai kuwa kiongozi. WTZ humu wamekuwa wakimsema vibaya sana Kagame ohoo dikteta mara hivi, nikaamua niende Kigali nikatembee na nijifunze nini kinaendelea kule, niabu kwetu jinsi ambavyo jamaa alivyoitengeneza nchi na kuwa na discpline huwezi amani nchi ipo kwenye mstari ulionyooka. Sisi maneno tu, angalia mimi nafanyakazi Peace keeping Operations, huku tuliko Rwanda inafanyabiahsra na UN imeleta military aviation team mbili zikiwa na helicopter zaidi ya nane zinafanya kazi ya operations na kwakuwa ni military helicopter zinacharge twice ya normal market price kwa kila saa inayoruka na hivyo kila trip moja si chini ya dola 10,000 na pesa wanazozipata wanaendelea kununua military aircraft fleet sisi tunabaki na siasa tu za kijinga. Sasa mimi binafsi nipo pamoja na Magufuli kama atakuwa anafanya ile mimi binafsi naita positive dictatorship yaana kuwaumiza waliotuumiza kwaajili ya maslahi mapana ya taifa acha afanye hivyo kwakuwa nchi yetu imeoza inahitaji mtu kama Magufuli la sivyo hatuwezi kutoka hapa tulipo kwakutumia viongozi poa. Huu si wakati wa siasa huu ni wakati wa kupiga mzigo na ingwewezekana tungeweka sheria Rais aruhusiwe kupiga makonzi na makofi wapuuzi kama wale wa airport waliokuwa wakimdanganya waziwazi, upumbavu mtupu tumechoka sana kwa ufisadi wao.
Ukiona Rais anawekeza kwenye military sana kuliko kwenye kuhudumia jamiii..Unue huyo ni dictator mbaya sana hana mpango wa kutoka madarakani...kwa maneno yako haya . Kagame ni dictator wa kuogopwa kama Adolf Hitler
 
Hujaelewa kabisa hoja yangu. Achana na vyama, havikufikishi popote. Hawa jamaa wamejenga demokrasia yao kwa zaidi ya miaka 200(karne mbili).

Demokrasia yako na yangu hazina hata miaka 30. Tupo mbali sana, lakini ukiangalia kwa umakini tuna safari ndefu. Isingekuwa hawa jamaa kutupa exposure ya teknolojia, sisi wala hatupo 21st century, bado tupo karne ya 17 au 18.

Naomba usiangalie, vyama Jecha wala Lubuva. Look at this with a better scope.
Mkuu life is politics and politics is life. Political party are tools we can't Deny the truth.
 
Nimependa sana jinsi viongozi kama Cameroun wanavyoweza kuwajibika kwa jamii baada ya mambo kuwaendea kombo tofauti na mategemeo yao. Je,sisi watanzania tunajifunza nini kutokana na tukio hili?
 
Ukiona Rais anawekeza kwenye military sana kuliko kwenye kuhudumia jamiii..Unue huyo ni dictator mbaya sana hana mpango wa kutoka madarakani...kwa maneno yako haya . Kagame ni dictator wa kuogopwa kama Adolf Hitler
Umefika Kigali na kuona, umeona investment zilizofanyika kwa IT in Kigali, kila basi la kigali lina 4G internet facility, umeona civilian fleet ya RWANDAIR, umeona town planning ya Kigali ilivyonzuri na inavyopendeza kila eneo lina aina moja ya nyumba, unafahamu kuwa Kigali is the first African country to conduct the drone tests, wanatumia drone for the distribution ya humanitaria aids, umeona jinsi mji ulivyomsafi kwa kupandwa miti na maua na yanalindwa kwa nguvu zote such that huwezi onana na mmachinga hata mmoja kila kitu kipo kwenye order na kila biashara inafanyika panapohitajika in a very formal and orderly manner. Nchi zote zilizoendelea zilijitoa muhanga, wewe unategemea Kagame abembeleze watu kwenye nchi aliyoichukua kutoka kwenye mauji ya halaiki. Ulinzi wa nchi ni muhimu sana na hasa nchi kama Rwanda ambayo inazungukwa na nchi ka Burundi, Congo, Uganda hata TZ ambazo huusiano wake uko very volatile. Unafahamu kuwa pesa anayopata toka UN kwakufanyanao biashara hiyo inaendesha his entire defense capability. Tunahitaji dictator Tanzania kuondoa uzembe uliopo. Nakukumbusha tu kwamba wakati tunasoma wengi walikuwa wakitukashifu kuwa tulikuwa tunasomea vijiji vyetu na tumetumwa na vijiji, waliokuwa wakitusema wao walikua watoto wa mjini na kupuuzia shule, uliza leo wako wapi, ndio hao wengi wao wanalalamika na maisha, lakini sisi tuliopiga shule kisawasawa ndio leo hii tuku huku tuliko and believe me katika kundi lile la waliokuwa wakisomea vijiji vyao hakuna anayejutia kwa kufanya vile. Inapokuja mambo muhimu ya Kitaifa na kimaisha inabidi tuwe serious la sivyo tutaendelea kuachwa nyuma.
 
Jecha na Lubuva waende huko UK wakajifunze democrasia na kuheshimu mawazo ya watu! Tz tunahitaji tume huru ya uchaguziii na katiba mpya 2020
 
Naona wazee wakudandia tren kwa mbele mmeitumia kura ya Kujitoa UK kwenye EU kama kete yakuanzisha zogo la muungano wetu. Navilaza wengine mnisamehe kwa kuwaita ****** japo ni ****** tu wamekuja na thread eti David Cameron ndio mwana democrasia pasipo kujuwa kile kinaendelea ktk siasa za Ulaya na UK kwa ujumla.
Kama mlikuwa hamjuwa UK ilikuwa bado haijaingia kwa asilimia zote kwenye EU.
Pili UK ilikuwa inatumia bado pound wakati wenzake walikuwa wakitumia Sarafu ya EU.
Tatu mtu alitaka UK kuingia umoja wa Ulaya ni David Cameron ila wenzake ndani ya chama chake wakamtega wakijuwa anaweza ku sign jambo wa UK Hawalitaki na ndani yake wakiwa wana chame wa chama chake. Kwahyo wataalamu wakuwatega watu wakamwambia aitishe kura ya maoni wakijuwa jamaa lazima ata angukia puwa maana sera za UK tangu mwanzo hazina habari ya EU. Na kusema eti jamaa anajiuzulu kwa kupenda sio kweli ana jiuzulu kwa dhambi ali itenda mwenyewe tena akijuwa ni mwiko kufanya hvyo.
Je UK kujiunga na umoja ulaya ulikuwa kwa manufaa ya nani mimi sina muda ila kaziulize nchi za magharibi. Pia je nani anafaidika na Eu? Kawaulize wana Uk why wamejitoa.
Je yalio toke UK NISAWA na Zanzibar na Tanganyika? Jibu hapana sisi tupo ndani ya muungano ulio na histor ilio tukuka ila ikiwa kuna siku vizazi hivi watajitenga basi watajuwa maneno ya wazee ni dhahabu.
Je ipo dalili kuwepo kura ya maoni kuhusu zanziba?
Jibu ni rahsi kawafufuwe waasisi wa taifa hili kuja simamia upigaji kura nje ya hapo iyo kura ipigwe na wazee wamapinduzi waliopo makaburini haki itendeke. Ukishindwa hayo piga kelele choma migomba ya wana ccm ila muungano hakuna anayeweza vunja kwa sasa.
Je vijana wafanyeje?
Tuache uvilaza taifa hili limetoka mbali sana kuliko yale tunayafanya au kuyawaza. Mtu anayetaka watu kujitenga hana tofauti na mchawi. Pia mkumbuke democrasia haipo kwa 100% wala hakuna nchi ina aina ya hyo democrasia. Kama ipo muulize mmarekani United state ilitoka wapi. Pia nivyema kujuwa nyuma ya taifa na rais wapo watu imara kulinda taifa na viongoz type ya David Cameron.
Nonsense
 
Eti kujitoa kwa uingereza ktk jumuia ya ulaya, kuna funzo gani especially kwa Tanzania?
My take: si swali lenye lengo jema kwa mustakbali wa nchi yetu.
 
Eti kujitoa kwa uingereza ktk jumuia ya ulaya, kuna funzo gani especially kwa Tanzania?
My take: si swali lenye lengo jema kwa mustakbali wa nchi yetu.
Mbona swali lipo so clear.

Kwa kuwa Uingereza walikuwa kwenye Muungano wa Nchi za Ulaya, na sisi Tanzania tuna Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar.

Kwa hiyo ni muhimu kutafakari na kujua sababu za waingereza kuona Umoja wao wa Ulaya hauna maana kwao, nasi kama Taifa lenye Muungano wa nchi 2 tuzibaini kero zinazokabili nchi hizi 2 na kujitahidi kuzitatua.

Kitendo cha kufumbia macho kero za Muungano, zinaweza kusababisha iwapo na huku kwetu tutapiga kura za maoni, upo uwezekano kwa majority wakapiga kura ya kutoutaka Muungano wa mfumo tulionao sasa.
 
Mbona swali lipo so clear.

Kwa kuwa Uingereza walikuwa kwenye Muungano wa Nchi za Ulaya, na sisi Tanzania tuna Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar.

Kwa hiyo ni muhimu kutafakari na kujua sababu za waingereza kuona Umoja wao wa Ulaya hauna maana kwao, nasi kama Taifa lenye Muungano wa nchi 2 tuzibaini kero zinazokabili nchi hizi 2 na kujitahidi kuzitatua.

Kitendo cha kufumbia macho kero za Muungano, zinaweza kusababisha iwapo na huku kwetu tutapiga kura za maoni, upo uwezekano kwa majority wakapiga kura ya kutoutaka Muungano wa mfumo tulionao sasa.
Duh kaka upo serious kweli!??

Mbona uelewa wako mdogo sana kuhusu hili suala la UK kujitoa EU....

Kwanza UK ni muungano wa nchi nyingi SCOTLAND,NORTHEN IRELAND,WALES NA ENGLAND YENYEWE!

SASA EU KIREF CHAKE NI EUROPEAN UNION KAMA ILIVO AU AFRICAN UNION....

SO SUALA LA UK KUJITOA EU NI KUBWA KULIKO HUO MFANO WAKO WALA HALIKARIBIANI KWA UZITO WAKE.
 
Back
Top Bottom