Waziri mkuu wa Canada anakuja Tanzania

JK alishakokotwa sasa unategemea zaidi? Kilichobaki ni kuja kuvuna dhahabu, gas, na mengineyo na kuacha shanga nyuma ili tupendeze zaidi hasa tutakapoenda masaini kuuza kile kisehemu kidogo kilichobaki kule Loliondo.
 
Wakuu zangu naomba tujadili hii safari ya waziri mkuu wa Canada, Mheshimiwa Harper ambaye atatua nchini muda wowote itakuwa na manufaa gani kwetu na pia tujadili ni jinsi gani ujumbe wetu unaweza kumfikia..

Kama sikosei, Harper safari ya Harper itajumuisha Tanzania na DRC (madini). Canada ina interest kubwa sana kwenye hizi nchi mbili, safari yake DRC imeleta kelele kidogo huko Canada kwa sababu kuna issues nyingi sana za human right DRC. Wenzetu wakiamua kuwekeza mahali wanaamua kimoja.
 
Kama sikosei, Harper safari ya Harper itajumuisha Tanzania na DRC (madini). Canada ina interest kubwa sana kwenye hizi nchi mbili, safari yake DRC imeleta kelele kidogo huko Canada kwa sababu kuna issues nyingi sana za human right DRC. Wenzetu wakiamua kuwekeza mahali wanaamua kimoja.
Kesha pitia Senegal na South Sudan nadhani kesho atakuwa Bongo, huu mkataba ulowekwa Ottawa majuzi unanipa mashaka makubwa kuhusu miradi yao nchini na ndio sababu nimeweka mada hii niwasikie viongozi wetu wa vyama vya Upinzani wamejiandaa vipi?
 
Katika safari yake ya hivi karibuni huko Canada raisi alishuhudiwa akikokotwa na mikokoteni ya kifahari na baadae akaonekana akisaini mkataba akiwa amezungukwa na wacanada.

Bila shaka ujio wa waziri mkuu wa canada nchini ni kuja kutekeleza mkataba waliosainiana, ambao kimsingi hakuna anayejua ulikuwa ni mkataba wa kitu gani na una terms gani.
 
keshaambiwa kuwa kuna gesi unafikiri ataacha kuja? Halafu makampuni ya kanada nadhani yanafanya utafiti wa gesi na mafuta hapa Tz
 
JK. alipokuwa rais wa kwanza kuonana na Obama, kulikuwa na ahadi kuwa naye angekuja TZ kabla muhula wake wa kwanza haujaisha, imegeuka 'white elephant'. Nadhani naye amemwambia "usije tena kwangu nitakuja kwako". Otherwise he's coming for mines & gas
 
Historia inajirudia, jezi kwa dhahabu na urani, kama ilivyokuwa kwa chifu wa msowero miaka ya 1800 shanga na vioo vya kujitazamia kubadilishana na ardhi
 
Wakuu zangu naomba tujadili hii safari ya waziri mkuu wa Canada, Mheshimiwa Harper ambaye atatua nchini muda wowote itakuwa na manufaa gani kwetu na pia tujadili ni jinsi gani ujumbe wetu unaweza kumfikia..
ot1.jpg


ot1.jpg
 
Saigon,

Unajua picha hizi zinaeleza mambo elfu kidogo. wakati sisi tunakimbilia kununua ma BMW na Range Rover wao wametupandisha ktk mkokoteni unaovutwa na Farasi na kwa ufahari mkubwa zaidi..Sasa jiulize nani mabingwa wa kutengeneza mikokoteni? na wanyama wanaoweza kuvuta mkokoteni tunao sisi..Sasa rais mzima magari ya nini?
 
Last edited by a moderator:
ni wakati wa kulipa fadhila, ukitaka kula lazima na wewe uliwe, ni zamu ya tanzania kuliwA
 
naona baada ya USA kuanza kukosa imani, jirani kaamua kuvuta na kuweka ndani
 
JK. alipokuwa rais wa kwanza kuonana na Obama, kulikuwa na ahadi kuwa naye angekuja TZ kabla muhula wake wa kwanza haujaisha, imegeuka 'white elephant'. Nadhani naye amemwambia "usije tena kwangu nitakuja kwako". Otherwise he's coming for mines & gas

Hapo kwenye bold mkuu wazungu wanasema umehit the nail on the head! Hakuna kingine zaidi hivyo, these guys are not tourists!
 
Saigon,

Viongozi wa nchi za wenzetu,huwa kwanza wanamsoma rais ama kiongozi wa nchi wanayetaka kudeal nayo,halafu wana act accordingly.I might be wrong,but sijawahi kuona kiongozi ie Obama akiwa amepandishwa hiyo mikokotoeni ya mafarasi ambayo hutumika na familia ya kifalme.

Halafu cha ajabu ni kwamba hata mwenyeji wake hakuwepo naye kwenye mkokoteni huo.Wanajuwa ni mpenda masifa na ukuu,issue kama zile za wiki leak ndizo haswa wako nazo kwenye makabrasha and therefore wana act accordingly,wanachotaka wao ni rasilimali zetu.Naona yeye kaanguka masaini tu,ila sidhani kama ameisoma vyema mikataba hiyo.Na sidhani hata kama alipata nafasi hiyo.
 
Last edited by a moderator:
JK. alipokuwa rais wa kwanza kuonana na Obama, kulikuwa na ahadi kuwa naye angekuja TZ kabla muhula wake wa kwanza haujaisha, imegeuka 'white elephant'. Nadhani naye amemwambia "usije tena kwangu nitakuja kwako". Otherwise he's coming for mines & gas

PM announces agreement to protect Canadian investors in Tanzania

4 October 2012
Ottawa, Ontario

Prime Minister Stephen Harper today announced the conclusion of negotiations toward a Foreign Investment Promotion and Protection Agreement (FIPA) between Canada and Tanzania. The announcement was made during an official visit to Canada by Jakaya Kikwete, President of Tanzania.

"Our Government is focused on creating jobs, growth and long-term prosperity, and to creating the right conditions for Canadian businesses to compete internationally," said the Prime Minister. "This new agreement with Tanzania will encourage investment between our two countries and better-protect Canadians that do business in Tanzania."

Now that negotiations have concluded, both countries will conduct a legal review of the agreement and proceed with its signing and ratification. The potential for increased Canadian investment in Tanzania is important, especially in the mining, oil and gas, power infrastructure, mining equipment and services, and transport sectors.

Total cumulative mining assets in Tanzania were valued at $2.3 billion in 2011.
Since 2006, Canada has concluded or brought into force FIPAs with 13 countries, and is in active negotiations with 13 others.


Read more at http://www.stockhouse.com/bullboards/messagedetail.a
 
Anakuja kuchukua malipo ya kumpandsha kwenye vitoroli vya farasi kada mwezangu Ritz unaionaje hii ziara?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mkandara heshima mbele.

Tanzania ni moja ya nchi zilizo karibu na Canada kwa kushirikiana kwenye mambo aina mbili.

Kwanza ni ushirikiano ambao unawekwa wazi kwa kila mtu kufahamu kinachoendelea, mambo kama uzazi wa mpango, udhibiti wa vifo vya watoto na wanatoa mahela kwelikweli kwenye hizi programs na hasa ile ya elimu ya AIDS.

Lakini kwa upande wa pili wa shilingi ni hili neno "Partners" au mshirika. Tanzania ni moja ya nchi mshirika wa Canada katika kuisaidia nchi hiyo kufikia malengo yake hasa kwenye suala la uwekezaji na other strategic interests kama madini.

Hili la pili huwa halisemwi sana kuondoa makelele kwani linahusu interests za watu na hata likisemwa huwa ni nusunusu tu basi hakuna mjadala.

Nimetumia neno kuisaidia Canada kwasababu ni nchi hiyo ndio itakayonufaika na hiyo FIPA - yaani Foreign Investment and Protection Agreement ambapo moja ya mambo mhimu ni kampuini zote za uwekezaji kutoka Canada zitayarishiwe mazingira mazuri ya kuweza kufanya biashara bila kusumbuliwa na ukiritimba wa kodi mbalimbali kutoka TRA.

Inasemekana Tanzania ni moja ya nchi zenye "complex tax systems" (wanavyodai wao) kiasi cha kwamba wale wanaojiita wawekezaji wanatumia visingizio kwamba hawazielewi kodi hizo na kudai ziwe more simplified huku wakijua wanatunyonya na kutupunja fedha yetu ambayo ingetusaidia kuleta maendeleo ya haraka.

Kwahio kwa kuwa wenzetu wanao uwezo wa kuzungumza kiingereza na kikaeleweka basi inabidi wakutane wao kwa wao kuonyeshana hiyo mikataba na kuhakikishiwa kwamba ni raisi mwenyewe ametoa go ahead, na pia iwe ni formalities ya wao kwa wao tu huku sisi wenye nchi tukiambulia kutoa matabasamu tu.

Kwahio sisi pia tutamkaribisha kiongozi huyo na atafanyiwa hospitality ya nguvu na kumpikia pilau (kama anapenda) lakini ndio tunazidi kudidimia.

Ni hayo tu mkuu.
 
Back
Top Bottom