Waziri Mkuu Tanzania - Mtu wa sita kwa hadhi nyuma ya wazanzibari wanne

Tundu lissu ni sehemu ya tatizo..anatumiwa na wanajumuia

Wa-TZ bana, tumelala usingizi zaidi ya wa pono!!! Nakumbuka tulivyokuwa tunakua!! Wakati tunaumwa malaria, ilikuwa balaa wakati wa kumeza dawa, maana dawa ilikuwa ni chloroquine; chungu balaa, so we used to play for God to bring down "dawa tamu"

Muungano wa Tg na Znz, ni timed bomb...
 
Pinda hana sifa ya kuwa PM
Pinda alisema Z'bar siyo nchi kwa mujibu wa katiba ya JMT. Kwa kuwa kauli hiyo iliwaudhi waZb sasa wamemwonesha kwamba kauli yake ime-pinda, wala si chochote katika al-maaruf na kumthibitishia kwamba Zenj bar ni nchi.
 
Tanzania ni nchi moja. Jina lake ni Jamhuri ya Muungano Tanzania. Katafute sehemu yeyote utaona hilo ndio official name.
Muungano ni kati ya bara na visiwani. Hapo pagumu ni lipi?

Mkuu Chapakazi, hata majina ya nchi zilizoungana huzijui!!??...kwa utani kama huu ndio sababu tuna muungano ambao ni mkorogo tu. Pitia hiyo The Articles utayaona majina ya nchi zilizoungana.

Serikali ya Muungano inaangalia vitu vya Muungano na vitu visivyo vya Muungano kwa upande wa Bara.
Sasa ugumu ni upi jamani?
Hapa sio kuwa pana ugumu tu bali ni utata mtupu. Mkorogo, kwa kifupi ndio hali iliyopo.

Hayo mengine yote ni upepo tu unavuma na nyakati. For me, the Union is clear cut!
Kwako wewe unayesoma The articles of union ukazielewa, pia unayesoma Katiba ukaielewa sishangai kwa msimamo wako huu. Lakini kuna wengi wanaoona kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar una utata mwingi. Hata huyu mchangiaji hapa yeye ana mawazo haya.
Muungano wa Tanzania haupo sehemu yoyote duniani, si Union, si federation/confederation, huwezi kuupata muungano kama huu sehemu yoyote duniani.

Huwezi kunitajia hata nchi moja dunia hii ambayo inaundwa na muungano kama wa Tanzania.

Kwa hiyo hata protokali zake ziko evasive kama "wave/particle" like duality ya photon.

Ivi mbona UK nayo ni a Union. Kuna Scotland, England, Wales na Northern Ireland. Kwenye michezo kuna timu ya England, Scotland, Wales na Northern Ireland. Lakini nenda UN utakuta hakuna hizo nchi, ipo UK tu!
Kuna bunge la UK, bunge la Scotland, nk. Lakini hakuna bunge la England. Unaelewa hapo?
Mkuu hapa umeniacha hoi..unasema UK ni muungano wa Scotland, England, Wales na Northern Ireland lakini Tanzania ni muungano wa bara na
visiwani. Unaelewa hapo?
Pia ukumbuke kuwa Northern Ireland imekuwa Annexed katika muungano huo wa UK.

We have a similar situation. Overtime, Znz wanaweza kudai bendera, national anthem, timu yao ya mpira, nk, lakini that does not mean kuwa hakuna a UNION GOVERNMENT! Soma historia ya UK mkuu. Unaweza kufumbuka macho kidogo.
We could be having a similar kind of Union.
Inawezekana kuwa wewe unatamani iwe hivyo kama situation ya UK lakini kama umeisoma historia ya UK basi hujaifahamu au unaipindisha kwa makusudi.
Lakini la msingi ni kusoma historia ya Muungano wa Tanzania na kuifananisha na hiyo ya UK, katika Muungano wa UK hakuna mshirika aliyekufa au kupotea, ndio maana umeweza kutaja majina ya washirika wa muungano wa UK..sasa rudi katika muungano wa Tz uone mazingaombwe. Yet wewe unasema the union is clear cut!

Mwalimu Nyerere yeye alisema hivi, "tangu kuanzishwa kwa Muungano wa nchi zilizokuwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar na Jamhuri ya watu wa Tanganyika, ziliungana na kuwa nchi maja na Taifa moja. Narudia tena, ziliungana kuwa nchi maja na Taifa moja. Kwa lugha ya kigeni, 'One Sovereign State'. Hivyo imejenga msingi imara wa umoja kati ya wananchiwa Tanzania. Tanzania Bara na Visiwani, zimekuwa zikifaidika kisiasa, kiuchumi na kiulinzi chini ya mfumo uliopo wa Muungano. Uk 2

Hapa Mwalimu alikuwa atuorodheshee hizi faida lakini ameiweka kauli yake kama mwanasiasa tu.

Muundo wa Muungano, pamoja na kwamba hatutaki uwe ukitibuliwatibuliwa mara kwa mara, ni suala la sera, si amri ya Mungu. Uk 18

“Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar. Wapendao Utanganyika watakuwa wazalendo zaidi, badala ya kuwa wasaliti, wakiazimia Afrika ya Mashariki iliyoungana kuwa Nchi Moja. kuliko Tanzania iliyotengana ikawa nchi mbili.” Uk 11

Serikali ya Tanganyika ilipasa kufufuliwa tokea mwaka 2000 tulipokubali kuifufua EAC, lakini zaidi sasa kwa vile tumekubali ku-fast track EA Federation.
Wakuu wetu ,they race against time kutuletea serikali moja! Na kutugawia umaskini na magao wa umeme!

Tutakapotoka usingizini tutakuta hizo nchi nyengine wanachama wa EAC wananufaika vyema na EAC wakati sisi tunalumbana juu ya Muungano na Muundo wake.
Mwalimu aliandika kitabu chake 1994. leo ni 2011. Serikali ya Tanganyika iko wapi?

Halmashami Kuu ya Taifa iliketi Unguja ikabadili Azimio la Arusha bila kwanza kutafuta maoni ya wananchi. Na walikuwa na haki kufanya hivyo, maana sera ni yao. Ubaya wao ni kwamba jambo lenyewe walilifanya kwa hila na 'janja janja", na mpaka sasa wanaendelea kudanganya wananchi kwamba sera ya CCM bado ni Ujamaa na Kujitegemea. Uk 18

Hizi hila na ujanja wa CCM unaonekana katika kila kitu, kujivua gamba, kupambana na ufisadi, kwenye chaguzi, sera ya muungano wa kutoka serikali mbili kuelekea moja, tatizo la umeme kuwa historia, “maisha bora kwa kila mtanzania”, katika issue ya katiba mpya….orodha ni ndefu!!!

Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)

Huu ujanja ujanja na utani ndio utakaotupeleka pabaya.
 
.

SIKIZA DOGO, nchi hii hakuna katiba wala protocal, Zanzibar iko ndani ya muungano lakini hawatumii katiba ya muungano, huu ni ushenzi, kwenye msiba wa juzi zanzibar, Dr Jakaya alikuwepo lakini hakuwa mgeni rasmi, mgeni rasmi alikuwa Dr Ali, Zanzibar wana protocal yao na muungano yake.
kiprotocal inamaana kuwa rais wa muungano akiwa zanzibar, anakuwa chini ya rais wa zanzibar kimadaraka, viongozi wa ngazi za juu wa muungano wanakuwa chini ya viongozi wa zanzibar.

Ndo maana siutaki muungano wa aina hii kabisa, bora kutokuwa na muungano kuliko kuwa na muungano wa aina hii,
TUNATAKA TANGANYIKA YETU, TUWE NA RAISI WETU, KATIBA YETU, BARAZA LETU LA WAWAKILISHI, WIMBO WETU WA TAIFA

Nimependa sana post yako, hatuhitaji baraza la wawakilishi!
 
Inawezekana kuwa wewe unatamani iwe hivyo kama situation ya UK lakini kama umeisoma historia ya UK basi hujaifahamu au unaipindisha kwa makusudi.
Lakini la msingi ni kusoma historia ya Muungano wa Tanzania na kuifananisha na hiyo ya UK, katika Muungano wa UK hakuna mshirika aliyekufa au kupotea, ndio maana umeweza kutaja majina ya washirika wa muungano wa UK..sasa rudi katika muungano wa Tz uone mazingaombwe. Yet wewe unasema the union is clear cut!

Mwalimu Nyerere yeye alisema hivi, "tangu kuanzishwa kwa Muungano wa nchi zilizokuwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar na Jamhuri ya watu wa Tanganyika, ziliungana na kuwa nchi maja na Taifa moja. Narudia tena, ziliungana kuwa nchi maja na Taifa moja. Kwa lugha ya kigeni, 'One Sovereign State'. Hivyo imejenga msingi imara wa umoja kati ya wananchiwa Tanzania. Tanzania Bara na Visiwani, zimekuwa zikifaidika kisiasa, kiuchumi na kiulinzi chini ya mfumo uliopo wa Muungano. Uk 2

Hapa Mwalimu alikuwa atuorodheshee hizi faida lakini ameiweka kauli yake kama mwanasiasa tu.

Muundo wa Muungano, pamoja na kwamba hatutaki uwe ukitibuliwatibuliwa mara kwa mara, ni suala la sera, si amri ya Mungu. Uk 18

"Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar. Wapendao Utanganyika watakuwa wazalendo zaidi, badala ya kuwa wasaliti, wakiazimia Afrika ya Mashariki iliyoungana kuwa Nchi Moja. kuliko Tanzania iliyotengana ikawa nchi mbili." Uk 11

Serikali ya Tanganyika ilipasa kufufuliwa tokea mwaka 2000 tulipokubali kuifufua EAC, lakini zaidi sasa kwa vile tumekubali ku-fast track EA Federation.
Wakuu wetu ,they race against time kutuletea serikali moja! Na kutugawia umaskini na magao wa umeme!

Tutakapotoka usingizini tutakuta hizo nchi nyengine wanachama wa EAC wananufaika vyema na EAC wakati sisi tunalumbana juu ya Muungano na Muundo wake.
Mwalimu aliandika kitabu chake 1994. leo ni 2011. Serikali ya Tanganyika iko wapi?

Halmashami Kuu ya Taifa iliketi Unguja ikabadili Azimio la Arusha bila kwanza kutafuta maoni ya wananchi. Na walikuwa na haki kufanya hivyo, maana sera ni yao. Ubaya wao ni kwamba jambo lenyewe walilifanya kwa hila na 'janja janja", na mpaka sasa wanaendelea kudanganya wananchi kwamba sera ya CCM bado ni Ujamaa na Kujitegemea. Uk 18

Hizi hila na ujanja wa CCM unaonekana katika kila kitu, kujivua gamba, kupambana na ufisadi, kwenye chaguzi, sera ya muungano wa kutoka serikali mbili kuelekea moja, tatizo la umeme kuwa historia, "maisha bora kwa kila mtanzania", katika issue ya katiba mpya….orodha ni ndefu!!!

Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)

Huu ujanja ujanja na utani ndio utakaotupeleka pabaya.

Mkuu, with all due respect, this will be my last commenting on this until i am proven wrong.
1. Unataka kujua majina ya nchi, haya basi haya hapa: Republic of Tanganyika and of the Peoples' Republic of Zanzibar. I dont see how the official names of just a reference to Bara na Visiwani has any significance. Kila mtu anajua Bara na Visiwani.
2. To be a sovereign state does not mean ceasing to exist as individual countries. The UK is a sovereign state, but it is also 'countries within the country' (a phrase used by the British PM). Hizo nyingine ni nchi. Kwa sehemu kubwa kwanza Bara ndio ime-lost its identity kwa sababu ya serikali mbili. A more clear cut separation might be needed to ensure Bara has its own flag, national teams, etc.
3. Unamtaja Nyerere, ambaye ni huyo huyo aliongelea kuhusu umuhimu wa kuwa na serikali mbili. Kwa sababu ya size ya Zanzibar and contribution yake katika Muungano, hakuna haja ya kuwa na serikali tatu. Ni wazi kuwa Tanganyika itaingia hasara kuchangia serikali ya Tanganyika na pia serikali ya Muungano. Kumbuka kuwa Tanganyika ndio contributor mkubwa katika serikali ya Muungano. Kwa hiyo ni 'more effecient' kuwa na serikali ya Muungano, inayoangalia mambo ya Muungano na Bara kwa pamoja, na kuwa na serikali ya Znz. UK wanafanya kitu hicho hicho. England haina Bunge la England, bali Bunge la UK. Ni nchi pekee katika hizo za UK isiyo na bunge lake binafsi. In a sense, haina serikali yake pia. Na ukiangalia sababu ni hizo hizo. Kwa nini wananchi wa England wasidai kuwa na bunge lao kama hao wengine?
4. Hakuna shida yeyote kwa Znz kujiita nchi, kuwa na bendera, timu ya taifa, nk. Scotland, Wales, Northern Ireland nao walidai hivi vitu na wakapewa. Mwisho wa siku lazima WaZnz wajiangalie na kuona faida walionayo katika huu Muungano. Kwa maoni yangu, kama wanataka kuwa na identity, hilo sio shida. Wanaweza kuwa na bendera, nk. Lakini mwisho wa siku wanapata benefits nyingi sana kutoka kwenye huu Muungano. Ni sawa na Scotland ijitoe UK.
5. Kusema kweli, kwangu mimi huu muungano upo wazi. Kama tatizo ni Znz kuwa na mamlaka zaidi, hayo wanaweza kupewa chini ya hizo articles of the union. Sioni shida ya kuwa EAC member hata kidogo.
Mwisho ukisoma nilichoandika earlier on nilisema kuwa 'we could be having a similar kind of union' (as the UK). Hapa sijasema kuwa ni similar, but 'could be more similar than we think'.

Ohh...by the way: Ivi Rais wa kwanza Znz baada ya Muungano ni nani? Na makamu wa kwanza wa Rais Tanzania ni nani? The answer might give you some food for thought....
 
Siku ya jana kulifanyika ibada kubwa pale Zanzibar, na viongozi wakuu wa kitaifa walikuwepo. Nilishangazwa kwa jinsi protokali ya nchi hii ilivyomuweka Pinda nyuma ya JK, Bilal, Shein, Hamad na Idd. Kama ni waziri mkuu wa serikali ya muungano, basi hata rais wa Zanzibar anapaswa kuwa chini yake kwa maana Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.

Hii imenifanya nimwone PM kama kiranja wa 'Bara'. Mtu wa sita kwa hadhi Tanzania atasema nini Zanzibar ilhali juu yake kuna wazanzibari wanne? Najua katiba za Zanzibar ilifanyiwa marekebisho kwa kupeana vyeo lukuki, lakini ni lini katiba yetu imerekebishwa na kumshusha hadhi PM kwa kiasi hiki. Kwangu mimi jaji mkuu chande hata mama Makinda wana hadhi kubwa zaidi ya rais wa Zanzibar kwa sababu wanaweza kurithi urais wa Tanzania.

kuna baadhi ya wachangiaji wanahoji ati thread hii inasaidia nini kupunguza umaskini Tz........

Watu wenye hadhi ya juu ndio wenye ushawishi wa maamuzi yote. Ndio maana mataifa makubwa huya yanahangaika kutafuta "who are the most influencial" na hao ndio waamuzi wa mambo ya dunia likiwemo hilo la umaskini. Kuwa na "top layer" ya wazanzibari wanne ni kuweka mustakabali wa nchi yetu kwenye mikono yao, sawa na kuweka rehani 'utajiri' wetu kwa minajili ya kukubaliana kisiasa. "Our progress depends much on who rules and what shall happen if we are ruled by zanzibaris?

Nafasi ya Waziri Kiongozi ambayo inashikiliwa na Hamad na Idd haina uzito wowote kwani ingekuwa na uzito Shamsi Vuai Nahodha ambaye ni Waziri Kiongozi mstaafu asingekubali ama kuomba Ubunge wa Kuteuliwa Bara ili apate nafasi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ambayo amepigiwa pande na JK. Ingekuwa na uzito angebakia huko huko Zanzibar aendelee kujilia kwa ulaini.
 
Zanzibar! Protokali yao sidhani kama ina maana yoyote ina porojo, Je rais wa Zanzibar ni Amiri Jeshi wa Jeshi lolote? labda jeshi la so and so uchumi KMKM, tell me hiyo nguvu ya protocal inakuwa reinforced na jeshi lipi? Raisi ni yule ambaye Jeshi lina mpa utii what about Zanzibar!
 
Unamwona Dr Shein ana Mwanajeshi nyuma yake mwenye cheo kikubwa tu nadhani Major au Leftnant Canal. Umewahi kuhudhuria au kushuhudia sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar? Umeishuhudia itifaki ilivyo siku hiyo?
 
Unaweza kujibu swali mkuu? Rais wa nchi ni Amir-Jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama ya nchi yake, hebu nambie wapi imeandikwa hivyo kwa Zanzibar? Kwanza jeshi klenyewe lililopo si ni KMKM tu? fikiria basi!
 
Sasa hivi Zanzibar wana JKU ina nguvu pia. Rais wa Zanzibar anawa-commission maofisa wa KMKM, JKU na secret service yao ya ndani pia. Usisahau mabadiliko ya Katiba yao yamewapa NCHI na MIPAKA yake kabisa.
 
Mkuu I want to prove you wrong

Mkuu, with all due respect, this will be my last commenting on this until i am proven wrong.
........Tanganyika ndio contributor mkubwa katika serikali ya Muungano..................England haina Bunge la England, bali Bunge la UK. Ni nchi pekee katika hizo za UK isiyo na bunge lake binafsi................Hakuna shida yeyote kwa Znz kujiita nchi, kuwa na bendera, timu ya taifa, nk. Scotland, Wales, Northern Ireland nao walidai hivi vitu na wakapewa. the answer might give you some food for thought....

1. Tanganyika ni contributor pekee katika serikali ya muungano
2. Hakuna kiongozi yoyote kutoka Scotland, Wales wala N. Ireland aliye na hadhi juu ya PM wa UK au hata mawaziri wake tofauti ya hapa kwetu PM ni mtu wa 6 kwa hadhi na President sio mkuu katika shughuli zinazofanyika visiwani......

tena Shein bila aibu wala adabu anasema "kumbe mwenzangu alikuwa na taarifa za ajali kabla sijampigia simu" mwenzake ni mkewe, JK ni bosi wake bana!
 
Sasa hivi Zanzibar wana JKU ina nguvu pia. Rais wa Zanzibar anawa-commission maofisa wa KMKM, JKU na secret service yao ya ndani pia. Usisahau mabadiliko ya Katiba yao yamewapa NCHI na MIPAKA yake kabisa.
You might be right dear hommie, but i am sorry to say, 'Si amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama! Otherwise it is uncertanly phrased kwenye katiba yao, well but the urgument is right kuhusu sisi wa-Tanganyika!
 
Mimi kinachonitesa, siyo nani yuko juu ya nanai.

Ila nchi kma yetu kuwa na viongozi wa juu sita!!!

Sijui lakini namjua rais na makamu wake kule US, Namjua Waziri Mkuu wa UK, namjua Chancelor wa Ujerumani peke yake!! Sasa sisi....

Marais wawili, Makamu wa rais watatu, Waziri Mkuu .....

It is too much.

matokeo yake hata hao watu wa protokali wanashindwa kupanga who is on top of who!!

Na wanapoanza kutoa hotuba zao inachukua dk 10 nzima kuanza kuzingatia itifaki. Tumekalia misifa huku kazi haifanyiki
 
Nadhani kuna umuhimu mkubwa wa 'kuweka sawa' jambo hili. Naona kama kuna kufanyia "favour" baadhi ya mambo na kuyachukulia kirahisi rahisi tu. Na wengine 'favour' hizo wanachukulia kuwa ni haki na halali yao. Wanasiasa bwana sijui watapona lini ujinga wao, kwa sababu jambo hili ni kama wanaahirisha utatuzi wa tatizo, mwisho wa siku halitavumilika na matokeo yake ni kufumuka kama bovu na watashindwa kuhimili mshindo wake. Ni kwa vile hawaipendi nchi yetu, laiti wangeipenda wangeangalia kwanza mustakabali wa nchi na si vyama, marafiki wala pande za muungano n.k.
 
Mimi nipo hoi na protokali za nchi hii, acha waendelee tu mpaka tutakapo wang'oa madarakani ndio tutajipanga upya. Na hawa ma-alhaji, tunao wengi, watatufungulia milango ya pepo.
 
Mkuu I want to prove you wrong

1. Tanganyika ni contributor pekee katika serikali ya muungano
2. Hakuna kiongozi yoyote kutoka Scotland, Wales wala N. Ireland aliye na hadhi juu ya PM wa UK au hata mawaziri wake tofauti ya hapa kwetu PM ni mtu wa 6 kwa hadhi na President sio mkuu katika shughuli zinazofanyika visiwani.....
Crucifix
Hapa sina nia ya kumtetea Chapakazi lakini hii point (1. Tanganyika ni contributor pekee katika serikali ya muungano) ni misinformation au niseme misstatement.
Ili uwe sahihi katika hii kauli ni lazima ujue kuwa Muungano una mapato na matumizi. Kuna shughuli katika mambo ya muungano zinaingiza fedha katika hazina. Kama washirika wa muungano ni Tanganyika na Zanzibar ni wazi kuwa kama ambavyo wanatakiwa wachangie matumizi na mapato pia yanatakiwa yagawanywe.
Kwa hiyo, usemi wa Chapakazi una uzito zaidi kuliko hii point yako.

Tuache ushabiki, tutafute haki na usawa.
 
Haya nijuze Zanzibar inachangia % ngapi kwa serikali ya muungano ukiacha 20% ya mapato na misaada tunayokusanya na kuwapa watumie?
 
Mkuu I want to prove you wrong

1. Tanganyika ni contributor pekee katika serikali ya muungano
2. Hakuna kiongozi yoyote kutoka Scotland, Wales wala N. Ireland aliye na hadhi juu ya PM wa UK au hata mawaziri wake tofauti ya hapa kwetu PM ni mtu wa 6 kwa hadhi na President sio mkuu katika shughuli zinazofanyika visiwani......

tena Shein bila aibu wala adabu anasema "kumbe mwenzangu alikuwa na taarifa za ajali kabla sijampigia simu" mwenzake ni mkewe, JK ni bosi wake bana!

1. PM sio mtu wa 6! Its that simple. Isome katiba uelewe.
2. PM wa UK ndio head of govt. Hii title Tz ni ya Rais ambaye pia ni head of state!
Pinda anasimamia day-to-day business za govt (tena ya Muungano). which automatically puts him above Rais wa Znz
3. Unaposema tanganyika ndio contributor pekee wa govt...una maanisha Znz hawalipi kodi?
Ni kitu kinatumika kuendesha serikali? mafuta, umeme au kodi?
Pia, ivi Znz wanalipa kodi ya kuweza kuendesha serikali yao wenyewe?au hadi hiyo inachangiwa na bara?

Ninachotaka kujua ni kwa nini Makamu wa Rais ameacha kuwa Rais wa Znz...aside the fact kuwa Mwinyi alipoingia kulikuwa na possibility ya rais na Makamu kutoka znz.
 
Back
Top Bottom