Waziri Mkuu: Serikali kugharamia athari za tetemeko la ardhi Kagera

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali haitawatupa wahanga wa Tetemeko la Ardhi la Kagera. Hayo ameyasema wakati alipowasili Bukoba kujionea mwenyewe athari ya tukio hilo. Amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imetuma Timu ya wataalam kutoka kitengo cha Maafa ambao watashirikiana na Timu ya Mkoa wa Kagera kufanya tathmini ya kina ambayo ndiyo itakayotumika kwa Serikali kufanya maamuzi sahihi kwa wahanga.

Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali imeguswa sana na tukio hilo na ni wajibu wake kuwasaidia wahanga. Amesema kuwa Serikali inataka kufanya jambo kubwa kwa wahusika na kwamba ili mpango huo uweze kutekelezwa, itategemea matokeo ya tathmini hiyo ambayo itaonesha kiwango cha athari na mahitaji kwa kila mhanga. Waziri Mkuu amewashukuru wadau waliojitokeza kusaidia mahitaji ya awali ya wahanga na kwamba Serikali inathamini michango yao na itaendeleza pale walipoishia.

Nao majeruhi na ndugu wa familia zilizoathirika na tetemeko hilo, wameishukuru Serikali kwa huduma wanazotoa kwa wahanga. Wamesema kuwa kwa wale waliofariki, Serikali imegharamia mazishi ikiwa ni pamoja na kununua majeneza, usafiri, chakula kwa waombolezaji na mahitaji mengine. Aidha, kwa wale wagonjwa, wanapewa huduma nzuri kwenye hospitali ya Mkoa wa Kagera na huduma hizo ni za bure. Kwa ujumla, wananchi wameridhika na hatua ya awali iliyochukuliwa na Serikali pamoja na wadau wengine na kwamba wanaendelea kuvuta subira ili kusubiri hatua zaidi za Serikali.

Source: TBC1 Kipindi Maalum cha Tukio la Tetemeko la Ardhi Kagera
 
"Itaendeleza pale walipo ishia" kwann serikali yako isianze kisha wafanyabiashara waendeleze!
 
Sawa ila wamechelewa !!
Kwani wewe ulitakaje? Serikali ya CCM haikurupuki. Lazima mahitaji yajulikane ndipo Serikali ijue cha kufanya. Serikali haifanyi mambo yake kwa mihemko kama ndugu zangu wa CHADEMA
 
Hayo ma trilioni mnayokusanya na kuvuka lengo kila mwezi mnayapeleka wapi?
Serikali ina mambo mengi ya kufanya. Kugharamia maafa ni sehemu mojawapo. Hata hivyo, kote duniani, maafa yanagharamiwa na watu wote. Hata wewe unawajibika kugharamia
 
Back
Top Bottom