makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,218
Baada ya sakata la TANESCO kutinga Bungeni kufuatia Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nishati na Madini Prof.Muhongo sasa imebainika wazi kuwa kulikuwa na Wabunge kadhaa wa CCM na wachache toka upinzani ndani na nje ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini walikuwa wakipokea Rushwa kutoka kwa Mafisadi ili kundelea kuwanyonya Watanzania kupitia TANESCO!
Kutokana kashfa hii nzito ya Rushwa sasa ni wakti mwafaka kwa Viongozi wakuu wa Bunge letu kujiuzulu mara moja ili kulinda heshima ya Bunge la Tanzania. Viongozi hawa wakuu wanaohusika na Bunge ni Spika Anna Semamba Makinda na Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda ambaye ni Kiongozi Mkuu wa shughuli za Serikali Bungeni.
Hili siyo tukio la kwanza kwa Bunge la Tanzania kukumbwa na kashfa tuhuma za rushwa. Kuna matukio ya Rushwa ambayo yametokea mfululizo kwa kufuatana ndani ya bunge lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na viongozi hawa. Yafuatayo ni matukio hayo:
1. Mbunge David Kafulila kupitia NCCR-Mageuzi aliwahi kuibua kashfa ya Rushwa kwenye Kamati ya Fedha Serikali za Mitaa (LAAC)inayoongozwa na Mhe.Mrema kuwa wajumbe wa Kamati hiyo walikuwa wakijihusisha na Rushwa kwa kuidai ili wawaandikie ripoti safi viongozi wa Halmashauri za Wilaya. Taarifa hii ilipelekwa kwa Spika makinda lakini mpaka leo hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
2. Mbunge wa Jimbo la Bahi (CCM), Omary Badwel kwa tiketi ya CCM alikamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) kwa tuhuma ya kupokea rushwa ya Sh1 milioni kutoka kwa kiongozi wa Serikali toka mojawapo ya Halmashauri za nchi hii.
3. Mbunge Andrew Chenge kupitia CCM alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Fedha na Uchumi ilhali inajulikana kuwa Chenge ni kinara wa Rushwa ya Rada ya waingereza toka BAE system. Kwa Spika makini na Waziri Mkuu makini Chenge hakupashwa kupewa Umwenyekiti wa Kamati ya Bunge tena ya Fedha na Uchumi kwa uchafu alionao. Lakini kwa vile tuna Spika dhaifu,Waziri Mkuu dhaifu na Serikali goigoi ndiyo maana haya yaliruhusiwa.
4. Wakati wa Uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALC)kulikuwa na Rushwa kubwa sana iliyofanyika pale Dodoma. Wagombea wa nafasi hizo hasa kutoka CCM walitembeza rushwa fedha na hata ngono kwa Wabunge ili waweze kupigiwa kura ya kuingia kwenye EALC. Matokeo tuliyaona na ndivyo ilivyokuwa. Habari hizo zilikuwa zinajulikana kwa kila mtu lakini Spika mwanamke dhaifu na PM mwanamme dhaifu walikaa kimya na wakaruhusu uchafu huo ufanyike.
Kwa matukio haya yasiyo na shaka yoyote ya kuwa ni Rushwa tunaomba kwa heshima na taaadhima Spika Anne Makinda na Waziri Mkuu Mizengo Pinda sasa wajiuzulu ili kulinda Heshima na Hadhi ya Bunge letu ili lisiendelee kuchafuliwa na kashfa za rushwa.
Nawasilisha