waziri mkuu ni nani kwa sasa?

ng'wanishi

Member
Jan 23, 2012
34
1
baada ya rais kuteua baraza jipya la mawaziri je waziri mkuu naye atabadilishwa? Maana yeye ndo shina hasa kwa kushindwa kusimamia mawaziri wengine. Naombeni ufafanuzi jamani?
 
Subiri Ijumaa ukampe Jk ushauri msikitini, hapo atakusikia na kukuelewa.
 
Tanzania haijawa na Waziri Mkuu tangu 2010. Kwa hiyo labda Kikwete amteue sasa Waziri Mkuu.
 
Mawaziri wakibadilishwa waziri mkuu habadiliki, waziri mkuu anaondoka pale baraza la mawaziri linapovunjwa.
Kwa issue hii ya juzi baraza la mawaziri halijavunjwa.
 
Nchi hii haina waziri mkuu wala makamu wa rais kama wote hawa wawili walishindwa kumfukuza kazi katibu wa wizara tu wakasubiri rais arudi kuna nini hapo,porojo tupu
 
Nchi hii haina waziri mkuu wala makamu wa rais kama wote hawa wawili walishindwa kumfukuza kazi katibu wa wizara tu wakasubiri rais arudi kuna nini hapo,porojo tupu[/QUOT


Pinda nidhamu imezidi. Alishindwa kumfukuza kazi mtu aliyetaka kubadilisha makao makuu ya wilaya mpya kule nyumbani kwa Hayati mwenye heri baba wa taifa, alishindwa kumtimua Jairo, alishindwa kumtimua profesa mmoja wa UDOM hata alipoambiwa hawamtaki mbele yake, alishindwa kumfanya chochote Luhanjo alipomsafisha Jairo.

Nashindwa kumlaumu huenda anabanwa na muhusika mkuu yaani rais. Haiwezekani waziri mkuu ashindwe kumfukuza kazi Kimakamu Kisaidizi cha Chuo Kikuu cha Umma ambaeye kwa rank ni chini ya mkurugenzi. Maana kumbukeni vyuo vikuu nchini viko chini ya wakurugenzi wa wizara tu, sasa waziri mkuu anashindwa kumtimua kazi hata mtu ambaye yuko chni ya mkurugenzi wa wizara? Aibuu sana nchi hii ina ombwe la uongozi na utawala bora.

 
Pinda ni kama kivuli tu, yupo ili nchi ionekane ina wazr mkuu lakin kiutendaji jk yeye ndiye rais, makamo wa rais na waziri mkuu!
 
Back
Top Bottom