waziri mkuu Mizengo Pinda iga mfano wa waziri mkuu wa japan

ffoas

Member
Feb 23, 2011
34
5
Ni hivi leo tu kumerushwa habari kwenye televisions na radios kuhusu mlipuko kwenye kwenye sehemu ya kuzalisha umeme(JAPAN),pamoja na maafa mengine yaliyo wakumba,lakini kilichonifuraisha ni jinsi waziri mkuu wa nchi(NAOTO KAN) hiyo kuwapa moyo wananchi nakuwaeleza atalitatua tatizo hilo kwa kipindi chote hicho cha hali ngumu na japani itakuwa mpya tena kama hapo awali,lakini ukilinganisha na hali ngumu tuliyonayo wananchi wa tanzania waziri wetu mkuu hatoi moyo au kuonyesha ufuatiliaji kwa yale yanayotukabili hasa kwa kipindi hichi cha hali ngumu,zaidi kutoa shutuma na kuonyesha mabavu kwenye vyama pinzani vinavyotetea maslai ya wananchi,nahitaji mchango wenu wadau juu ya hili.
 
hapo ni kama mbingu na nchi, viongozi wetu hawana utaratibu wa kujali wananchi. Huwezi amini yeye ndiyo kiongozi wa kamati ya dharura ya maafa kushughulikia hili janga lililowakumba.
Sio kwetu mabomu yanauwa raia na kesho yake mkuu wa nchi anapanda ndege kutalii viwanja. Usalama wa maisha ya raia kwake sio issue..
 
Sisi hatuna waziri mkuu,umeona jinsi huyo mzee alivyoropoka mjengoni juu ya issue ya Arusha?Tangia siku ile alipojibu utumbo wa bata nikamtoa ktk thamani yake.Yeye hana shida sisi tuhangaike kivyetuvyetu.
 
Uliona wapi kiongozi msanii akakaa kufariji watu badala ya kutalii na kubembea? Kwani Tanzania tuna Waziri Mkuu mwenye mamlaka na uwezo wa kuiongoza serikali hadi ikafanikiwa kutatua matatizo ya wananchi kama siyo kuigiza tu kisiasa?
 
Yaani hii mistake ya jk ataijutia,watu wanakufa kwa mabomu ambao ni uzembe wa serikali yake anapanda ndege kutalii?,ni hatari
 
pinda ni picha tu pale anasema anayo agilwa na wakubwa na yeye ni njaa zake zinamuweka hapo
na uhuruma kama hao wa japan
 
Back
Top Bottom