Waziri Mkuu Majaliwa: Mikataba haitawasilishwa Bungeni

...watawezaje kukata mizizi walikoanzia...ama miti waliyokalia?...kama wameweza ku tolerate watu kama chenge kuwa mwenyekiti wa bunge lao...mtu aliyewahi kuwa mwanasheria mkuu wakati mikataba tata ikifikiwa(ukiwepo ule wa IPTL) mnategemea nini...kama ni kuliwa wabongo wameshaliwa....kilichobaki ni kuganga yajayo....maana hata hiyo ya gesi hamna ajuaye tumepigwa kwa kiwango gani...tunadanganyika na kuwepo wa gesi...lakini hatujui tunapigwaje nyuma ya pazia....
 
Afu kuna vilaza humu ndan wanapigapiga kelele kila cku, ohoo Dk kibuku ana nia njema, kama kweli ni mwema atumbue hayo matambaz ya mikataba ya ges ikasomwe bungen
 
Waziri mkuu amejib vizuri tuu kwani huwezi kupeleka mikataba yootee bungen,, ipo ambayo itakuwa ikipelekwa bungen na pia ambayo Serikali itaendelea kuingia mikataba kwa mjibu wa katiba wakimshirikisha mwanasheria mkuu, lilikuwa swali zuri na jibu ni zuri.
 
Chini ya CCM mambo ni yaleyale kwa style nyingine!Hoja ni kuwa vp kama mwanasheria mkuu sio mwaminifu?Huoni nchi itakuwa imewekwa rehani?Hivi hatujajifunza tu toka kwa chenge aliyepiga pesa madeal yote makubwa makubwa!Mikataba mingi aliyoingia chenge akiwa mwanasheria mkuu wa serikali ni ya kinyonyaji na imekuwa mzigo kwa nchii hii!

Mbona hata wabunge wapo wasio waminifu tunawaaminije ? maana tunashudia katika sakata la Escrow na masakata mengine wabunge wetu walihongwa na wafanya biashara.ishu ni kwamba kama wabunge wanataka kubadili utaratibu wa kutomtumia mwanasheria mkuu basi wafanye hivyo tatizo liko wapi? Watanzania siku hizi tumekuwa hodari sana wa kulalamika aise da.
 
Waziri mkuu amejib vizuri tuu kwani huwezi kupeleka mikataba yootee bungen,, ipo ambayo itakuwa ikipelekwa bungen na pia ambayo Serikali itaendelea kuingia mikataba kwa mjibu wa katiba wakimshirikisha mwanasheria mkuu, lilikuwa swali zuri na jibu ni zuri.

Hata vyama vya siasa navyo haviruhusu wanachama wote kujua chama kinaingia mikataba gani sembuse serikali! tuache ushabiki.
 
Yaani kweli kina mtu alijipa matumaini lwamba CCM ya awamu ya tano italeta hiyo miktaba bungeni.

Kama bunge lenyewe tu hawataki tujue kinachoendelea. Sembuse hiyo mikataba ndiyo watataka tujuye yaliyomo ndani yake.

Jamani upumbavu kujipa matumaini ambayo hayapo
 
chini ya ccm hakuna jipya...uko wa panya hauwezi kubadilika kuwa wa sungura...ccm ni kijiji cha wachawi tu hakuna mwema hata mmoja na haitakuja tokea ccm wakatoa kiongozi mtetezi wa wanyonge....
 
Mwaka 1992 hili dubwana lilitakiwa livunjwe wakat upinzani unaanzishwa.
 
chini ya ccm hakuna jipya...uko wa panya hauwezi kubadilika kuwa wa sungura...ccm ni kijiji cha wachawi tu hakuna mwema hata mmoja na haitakuja tokea ccm wakatoa kiongozi mtetezi wa wanyonge....
Huko unakofikiri kuna mwema tutajie ili umma wa watz umjue,,
 
wewe ndo uache ushabiki, unazifahamu kazi za bunge? unafananishaje bunge na chama?

We unayefahamu haki ya bunge ni kuonyeshwa live umeipata wapi?.Haki ya kupata taarifa/habari ndio iliyoainishwa katika katiba.mwananchi gani huyo ambaye sa 3 asubuhi haendi kazini anaangalia bunge?
 
Madini ambayo ni potential source ya foreign currency yanaelekea kuisha yakiiacha shilingi yetu bila msaada wowote, 1USD = 2200 kama tu ilivyo Congo. Gesi ndo hiyo jamaa hawataki mikataba ijulikane ina nin, na mashabiki wao wanaona ni sawa tu. Sis inawezekana tulilaaniwa si bure, nchi zenye madin kama Botswana na Namibia, South Africa hiz rasilimali zimewatoa sana, sis huku ni kilio.
 
Aaah
Ni bora vitu kujionea mwenyewe, waziri mkuu hakujib vibaya kwa kweli na ame offer bunge lijitungie sheria kama linataka mikataba ya koas kadhaa iwe ina pelekwa bungeni, lakini pia sijajua kama serikali ambayo badly iko bungen itaruhusu bunge lisaidie kaz hyo
 
Serikali inayojifungia ndani na kujadili mambo yanayo wahusu Watanzania bado tuamini maneno ya Waziri mkuu!!!?.Ukishaondoa uwazi hakuna uwajibikaji..
 
...watawezaje kukata mizizi walikoanzia...ama miti waliyokalia?...kama wameweza ku tolerate watu kama chenge kuwa mwenyekiti wa bunge lao...mtu aliyewahi kuwa mwanasheria mkuu wakati mikataba tata ikifikiwa(ukiwepo ule wa IPTL) mnategemea nini...kama ni kuliwa wabongo wameshaliwa....kilichobaki ni kuganga yajayo....maana hata hiyo ya gesi hamna ajuaye tumepigwa kwa kiwango gani...tunadanganyika na kuwepo wa gesi...lakini hatujui tunapigwaje nyuma ya pazia....

Halafu ukichanganya na haya MAPAMBIO yanayoimbwa na wana CCM pamoja na wafuata upepo ,ndio tunaibiwa kabisaa.
 
Mbona hata wabunge wapo wasio waminifu tunawaaminije ? maana tunashudia katika sakata la Escrow na masakata mengine wabunge wetu walihongwa na wafanya biashara.ishu ni kwamba kama wabunge wanataka kubadili utaratibu wa kutomtumia mwanasheria mkuu basi wafanye hivyo tatizo liko wapi? Watanzania siku hizi tumekuwa hodari sana wa kulalamika aise da.

Kwa hiyo unashauri nini hapo!?Sababu nnakuona unalinganisha idadi ya Wabunge na Ofisi ya Mwanasheria mkuu wa Serikali ..
 
Back
Top Bottom