Waziri mkuu kuwajibishwa na bunge inawezekana ila sio kwa bunge hili

Baba Hinda

New Member
Apr 20, 2012
1
1
Napenda kusema kuwa kwa mujibu wa sheria na taratibu inawezekana Waziri Mkuu kuwajibishwa na bunge kama alivyoainisha Mh. Zito jana. Lakini naomba mniamini kuwa Bunge hili haliwezi kufanya hivyo.

Wabunge wengi hawana misimamo thabiti. Ni wabunge wachache wanaoweza kusimamia wanachoamua kwa dhamira ya dhati. Wengi hawana ujasiri huo, hivyo kupata idadi inayostahili kumuondoa Waziri Mkuu kwa sasa si jambo rahisi japo linawezekana.

Sisi sote ni mashahidi juu ya mambo mbalimbali muhimu kwa Taifa letu na yaliyoamuliwa na wabunge wenyewe, lakini baadaye wakayatelekeza ama kuyapuuza kinyume na walivyoamua awali. Uzoefu unatuthibitishia kwamba wengi wa wabunge, hususan wa kutoka CCM, sio watu wa kuaminiwa.

Hawana ustaarabu wa kuheshimu makubaliano lakini pia hawana muda au uwezo wa kufikiri kwa usahihi. Na hii ni kwasababu hawakuwa wabunge kwa maana halisi ya ubunge ila kupata njia ya kufanya au kupata yaliyo ya binafsi. Kwahiyo ninaona kuwa haiwezekani kumuondoa Waziri Mkuu japo ANASTAHILI KUONDOKA.
 
Bunge hili la leo linaweza kufanya miujiza kwani waajiri wa wabunge hao wako hoi,wabunge watapataje mishahara yao?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom