Waziri Mkuu Canada atonesha kidonda cha madini Tanzania

Augustine Moshi,
Mjomba, Hata Yesu alipokuwa ktk swaumu ya siku arobaini alipatwa na majaribio mengi tu mojawapo likiwa toka kwa shetani. Na kama angekubali kumsikiliza shetani angefanikiwa ktk mambo fulani na pengine Utajiri. Hizi ndizo siwa za Mkapa unazotupa -Utajiri wa shetani.
Na sina hakika kama kweli unaamini kasi ya mfumko wa bei ulishuka toka asilimia 30 hadi 4.9 kwa mtazamo upi hasa. Kuimbuka kuwa fedha yetu alipopokea nchi ilikuwa ni shilingi 500 kwa dola moja (1 USd) na katuchukua hadi sh. 1000 kwa 1 Usd....Hapa ndipo unaposhindwa kuiona tofauti ya kimahesabu na lugha inayotumiwa na hawa wachumi wa Mkapa. Nitarudia tena kukufahamisha ama kukukumbusha mazungumzo yetu ya miaka ileeee toka Bsctimes.
Sasa unapotazama mathlan thamani ya kitu tuseme Nyama ya ng'ombe. Wakati wa Mwinyi bei ya kilo moja ya nyama ilikuwa shilingi 1000...na wakati wa Mkapa nyama hiyo hiyo ilikuwa ikiuzwa 1500 kwa kilo...
Hapa hawa washenzi wataalamu wa nje ktk mahesabu hawataangalia bei ya nyama toka 1000 kwenda 1500 kwa kilo moja! ila wataitazama thamani ya shilingi yetu ktk dollar na kutoa takwimu zao kulingana na hali iliyopo hata kama sio hali halisi ya Mdanganyika.
Wakati wa Mkapa Sh 1500 unliyonunua kilo ya nyama ni sawa na Usd 1.50 lakini wakati wa Mwinyi ile Shilingi 1000 ilikuwa ni sawa na Usd 2 kwa hiyo wakati wa Mkapa kulikuwepo na upungufu wa bei bila kuzingatia kwamba wananchi wa Tanzania hupokea fedha za madafu na pia mishahara yao haikupanda wala kuongekeza kulingana na kushuka kwa thamani ya fedha yetu.
Mzee wangu, hawa jamaa wa nchi za nje hutupa mahesabu kutokana na figure tulizopewa, hiyo hali halisi tunaifahamu sisi wananchi walalahoi - Mimi na wewe.
 
Augustine Moshi ,

Unaposema kwamba waandishi wanachafua jina la mkapa una maana gani ? Je haukubalini na ukweli kuwa mkapa ame-loot kiwira coal mine , na kama kweli hii issue haina ukweli kwa nini Mkapa mwenyewe aipingi ?

Kitendo cha Mkapa kuweka maslahi binafsi mbele ya taifa , kinaondoa kila jambo zuri alilolifanya in his tenure.
 
Mkapa ata "loot" vipi Kiwira Coal Mine? Hakuna cha kuiba pale! Kama ilikuwa inauzwa na akanunua Mkapa kuna ubaya gani? Kwani ni lazima mali zetu zote zinunuliwe na Wachina au Wakanada tu? Akinunua Mtanzania kuna ubaya gani?

Labda mnataka kusema alinunua kwa bei chee. Mbona Karamagi na JK wanauza machimbo ya dhahabu kwa bei che hata zaidi ya hapo?
Inanikumbusha wakati yalipotolewa malalamko hapa kwamba kuna Mtanzania kanunua shamba kubwa. Sasa haya ni mawazo ya kukanyagwa. Yaani tunavumilia tukiona Giriki kanunua shamba, lakini akinunua Mmatumbi tunalalamika!

Mimi nadhani kama Buzwagi ingekuwa imenunuliwa na Mtanzania nisingeona udhia kiasi hiki. Laiti angekuwa Mkapa ndiye katiliana mkataba na Karamagi kwenye hoteli Kariakoo!

Zimwi likujualo halikuli likakuisha. Ni heri kunyonyana sisi kwa sisi kuliko kunyonywa kishenzi na Wakanada, Wachina na Waingereza.
Ni sawa tulalamike kwamba inabidi Bunge liidhinishe uuzaji wa mali asili ya nchi. Si kulalamika kwa nini kanunua Mkapa. Why not Mkapa
 
Waziri Mkuu wa Canada anachoangalia ni interests za nchi yake na mapato yanayoingia kutokana na makampuni ya nchi yake kufanya kazi TZ. Umaskini wa watanzania sio priority kwake.

Upo sahihi mkuu.. Sasa JPM Anaipitia upya.
 
Wazee wa kufukunyua.
Ni jambo jema kutumia historia kurekebisha sheria zinazotukandamiza dhidi ya matajiri wa ulaya.
Jpm amethubutu, tumuunge mkono.
Mawaziri na wanasheria waliotuingiza mkenge akiwemo kenge mwenyewe, joka la makengeza wazuiwe kusafiri nje ya nchi Wakati wako endelea kufukunyuliwa.
Nyambafu zao
 
Yuko wapi fisadi Mkapa aliyewahi kuitetea mikataba ambayo hadi hii leo bado ni siri kwamba inainufaisha Tanzania!?

Posted Date::11/26/2007
Mwananchi

Waziri Mkuu Canada umechelewa kuja Tanzania (Mhariri)
LEO katika ukurasa wa kwanza wa gazeti hili tumechapisha habari inayomkariri Waziri Mkuu wa Canada, Stephen Harper akisema matatizo yaliyopo katika sekta ya madini hayasababishwi na makampuni ya nchi yake yaliyopo nchini, bali ni udhaifu uliopo kwenye sheria za Tanzania katika mikataba ya madini.

Waziri mkuu huyo ambaye yupo katika ziara nchini, alisema uwekezaji katika sekta ya madini unafanywa kwa kutumia sheria za ndani za nchi hivyo kasoro zote zinazojitokeza kwenye sekta za madini ni matokeo ya ubovu wa sheria hiyo.

Alisema tangu kuanza kwa uhusiano baina ya Tanzania na Canada, nchi yake imekuwa mstari wa mbele kuisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwamo elimu, afya na miundombinu na kwamba anaunga mkono hatua ya iliyochukuliwa na serikali kutaka kuipitia upya sheria ya madini nchini.

Moja ya kampuni ya Canada ambayo imewekaza katika sekta ya madini nchini ni Kampuni ya Barrick Tanzania ambayo inamiliki migodi ya madini ya dhahabu ya Kahama Mining na Buzwagi iliyopo Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Tulawaka uliopo mkoani Kagera, North Mara uliopo mkoani Mara.

Kauli ya Waziri Mkuu Harper imekuja wakati kuna malalamiko makubwa kutoka kwa wananchi ambao wanaona Tanzania ambayo imejaliwa kuwa na hazina kubwa ya madini mbalimbali lakini imeshindwa kunufaika nayo.

Ni kutokanana na ukweli huo ndiyo iliomsukuma Rais Jakaya Kikwete kuchukua uamuzi wa kuunda kamati kupitia upya sheria za madini hivi karibuni ili iweze kutoa mapendekezo yake yatakayosaidia kuboreshwa kwa mikataba ya madini.

Kwa hakika, kauli ya waziri mkuu, huyo wa Canada, imetufumbua macho kuwa tatizo la udhaifu wa shetia ya madini linajulikana na watu wote wakiwamo wafadhili na wawekezaji wenyewe katika sekta hiyo.

Tunachukua nafasi hii kumpongeza waziri mkuu, Herper kukubali kutueleza ukweli Watanzania kwamba haitunufaishi na madini yetu na kwamba tunaopaswa kujilaumu kwanza ni sisi Watanzania wenyewe wala sio mtu mwingine.

Kauli ya waziri mkuu wa Canada pia imetuonyesha kwamba ile hofu ya baadhi ya viongozi wetu serikali kwamba itakuwa ni vigumu kuibadili mikataba tuliyoingia na wawekezaji wa nje, haipo.

Kwa muda mrefu suala la mikataba mibovu katika sekta ya madini limekuwa likizungumzwa sana lakini halijapatiwa ufumbuzi mpaka sasa mbali ya kwamba limeundiwa tume nyingi mno za kufuatilia lakini ripoti ya tume zote zimekuwa zikiishia kuwekwa kabatini bila ya kufanyiwa kazi.

Kama kingozi huyo ametambua kwamba mikataba yetu mibovu ndiyo inayotufanya tushindwe kufaidi matunda ya madini tuliyonayo, ni wazi makampuni yanayotoka katika nchi yake yaliyowekeza katika sekta ya madini yapo tayari kukubali kubadilisha mikataba yao ili pande zote ziweze kunufaika.

Ingawa tunashukuru kauli ya Waziri mkuu huyo, imeamsha hamasa ya wananchi kutaka sheria mpya zitakazowanufaisha, tunadhani hatua hii imechelewa kutolewa na serikali ya Canada.

Tunasema imechelewa kwa sababu tulidhani kwamba, Canada ambayo nchi rafiki na mfadhili mkubwa wa Tanzania katika sekta nyingi, basi ingeweza kutushtua mapema badala ya sasa.

Ni wazi sasa serikali inatakiwa kuichukulia kauli ya waziri mkuu, Heper kama changamoto ya kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya madini ili wananchi waweze kunuifaka nayo kama zinazofaidi nchi nyingine za kiafrika.

Tuna matumaini kwamba kamati ya kupitia upya sheria za madini iliyoundwa na Rais Kikwete itakuja na mapendekezo ambayo yatasaidia kuiboresha mikataba iliyopo na mingine ambayo tutaingia ili madini yaweze kutoa mchango mkubwa katika uchumi wa nchi.
 
Dah halafu Kuna viumbe wanataka Jf ifungwe.. Kweli hamna hata jema kidogo cha kuipongeza Jf?
 
Mungu awabariki sana watu wote mlioipigania nchi hii kwa jasho na nguvu kubwa sana , japo mnakumbana na matusi ya kila namna .
 
mabadiliko makubwa katika sekta ya madini ili wananchi waweze kunuifaka nayo kama zinazofaidi nchi nyingine za kiafrika.

Tuna matumaini kwamba kamati ya kupitia upya sheria za madini iliyoundwa na Rais Kikwete itakuja na mapendekezo ambayo yatasaidia kuiboresha mikataba iliyopo na mingine ambayo tutaingia ili madini yaweze kutoa mchango mkubwa katika uchumi wa nchi
kaka mpo humu kitambo kumbe
 
Back
Top Bottom