Waziri mkuu awachambua CHADEMA; Lema amtuhumu kudanganya

nickname

JF-Expert Member
Dec 20, 2009
544
147
Katika kipindi cha maswali kwa Waziri mkuu leo asubuhi Mh. Waziri mkuu amesimulia kilichojiri katika mauaji ya Arusha na kwa mujibu wa maelezo yake yameonesha kuituhumu CHADEMA kuwa ni chanzo cha mauaji ya raia kwenye maandamano, amesema kuwa Mh. Godbless Lema ni mtu wa fujo fujo hivi na alianzisha fujo kwenye kikao cha pili cha baraza la madiwani halmashauri ya Arusha.

Mwisho Mh. Pinda kawashauri CHADEMA kuunda chama kitakachoaminiwa na wananchi kuongoza taifa hili chama chenye kuleta amani.

Wakati huo huo Mh. Godbless Lema alitumia mwongozo wa Spika kumtuhumu Mh. Waziri mkuu kuwa kalidanganya bunge.
 
Pinda mwongo mkubwa wewe, chadema waliandamana polis wakawapiga mabomu ya machozi na risasi sasa Pinda huwezi kutudanganya na CCm yenu. CCM = Lucifer/ devil i hate youuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu CCM
 
Uliona wapi kesi ya mbuzi anapelekewa chui? CDM wacpoteze muda kukomaa na PM huyu mzee naye kashapoteza channel mpk anasema Dowans walipwe,haitatokea hata cku moja Pinda akakiri makosa yanayofanywa na chama chake,CDM tuendelee kutafuta influnce kwa wotu always PEOPLES POEWR ndo itatulea mabadiliko ya kweli
 
Katika kipindi cha maswali kwa Waziri mkuu leo asubuhi mh.Waziri mkuu amesimulia kilichojiri katika mauaji ya Arusha na kwa mujibu wa maelezo yake yameonesha kuituhumu CHADEMA kuwa ni chanzo cha mauaji ya raia kwenye maandamano,amesema kuwa mh.Godbless Lema ni mtu wa fujo fujo hivi na alianzisha fujo kwenye kikao cha pili cha baraza la madiwani halmashauri ya Arusha.
Mwisho mh.Pinda kawashauri CHADEMA kuunda chama kitakachoaminiwa na wananchi kuongoza taifa hili chama chenye kuleta amani.
Wakati huo huo mh.Godbless Lema atumia mwongozo wa Spika kumtuhumu mh.Waziri mkuu kuwa kalidanganya bunge.
 
Huyu Pinda kumbe naye ni walewale tu!! No wonder alishawahi kutamka hadharani kuwa kazi ya kuongoza serikali ni ngumu kuliko tunavyofikiria. Sasa sijui kwanini kama anaiona ni ngumu bado amekubali badalal ya kuwaachia watu wenye uwezo kuliko kuwa pale na kusubili kusema "YES SIR"
 
Ajali ya Maspika Bungeni Dodoma Kuteleza Jukumu la Kutetea
'Sauti za Wachache' (Minority Voices) Na Hatari yake

Kukuza Mbegu ya Siasa za Chuki kwa Taifa letu
Main%2859%29.jpg

Je, tunapozungumza Kidemokrasia na kwa kuzingatia misingi yote ya UTAWALA BORA hapa nchini kwetu, serikali yetu kweli inafahamu maana halisi na tafsiri ya SAUTI YA KIKUNDI CHA WATU WACHACHE (Minority Voices) WANAPOCHUKUA HATUA YA KUTUMIA SILAHA YA KIDEMOKRASIA KUTOKA NJE YA BUNGE pindi wanapopinga jambo wasiloliafiki kimsingi??

Silaha hii ya kutoka nje ya bunge, kwa wale wanaoelewa vema demkrasia katika vitendo halisi, ni silaha hatari sana ambayo hutumika na waunguana badala ya kupigana ngumi kufuatia mijadala fulani. Silaha hii hutumika hasa pale ambapo KIKUNDI FULANI CHA WATU WENGI KINAPOTUMIA WINGI WAO VIBAYA (Majority Force) kulazimisha jambo BILA KUZINGATI MANTIKI INAYOTAWALA JAMBO HUSIKA NA AU SHERIA, TARATIBU NA KANUNI zilizopo.

Endapo itabainika kwamba serikali yetu chini ya CCM hujionea tu jambo hili kama kiji-sinema wabunge wa chama chochote wanapotibuliwa kupita kiasi na kujiamulia tu kutumia hii salaha kama hatua ya mwisho kabisa kuonyesha KUTOKUAFIKI JAMBA FULANI na pengine serikali hata ikaendelea tu kujifariji kwamba kimataifa LUGHA HII YA MWILI KIDEMOKRASIA haina gharama yake kwa taifa letu, basi watakua wanajidanganya sana mchana mchana. Lakini naamini kwamba watu wengi sana tu wenye upeo mkubwa ndani ya taifa hili wanaelewa fika tafsiri ya lugha hii.

Hakika, utawala bora ni pamoja na KULINDA VILIVYO MINORITY VOICES na pale tunaposhindwa kufanya hivyo basi mjue ya kwamba dereva wa gari lililobeba wale watu wengi huenda asifike salama; atawamwaga njiani abiria wake kabla safari haijakamilika kimatarajio. Kipimo halisia wa utawala bora katika nchi hupimika zaidi kutokama na ujumbe usiokua wa maneno tunaoupata usoni mwake mnyonge.

Mfano mzuri nchini ni kwamba bila Mwalimu Nyerere kutambua ukweli huu leo hii nchini mwetu tusingekua na huu Mfumo wa vyama vingi kamwe.

Dunia inatuangalia sana tunavyoenenda katika kujitawala huku na pengine hata kutucheka jino-pembe kama taifa lililosheheni wanadiplomasia mahiri sana kwa viwango vya kimataifa LAKINI WASIOKUA NA MAANA YOYOTE KWA SEHEMU MUHIMU YA JAMII YAKE YENYE SAUTI DHAIFU!!!

Mhesimiwa Spika, Mama Anna Makinda, kama referee kwenye jumba letu la mijadala Dodoma, wala hatuhija mtu kutukumbusha kwamba wajibu wako namba moja bungeni humo ni KUHAKIKISHA WAKATI WOTE KWAMBA SAUTI DHAIFU INAPEWA SANA UZITO, HULINDWA NA HUPEWA MOYO WA USHIRIKI SALAMA. Mimi naamini sana kwamba hali hii inaweza kabisa ikazuiliwa kwa kupendelea zaidi kutenda haki wakati wote uwapo kazini hapo.

Kinyume cha hapo mama yetu utakapoponyokwa miiko ya usimamizi wa mijadala kwa kulinda HAKI na kuanza KUTIA TIMU kwenye kile kikundi cha 'wasakata kabumbu ya nyumbani' basi hapo ndipo utakapofanikiwa sana kupanda mbegu mbaya sana (Political Animorsity) ya chuki ndani ya taifa letu. Hata kule Pemba na Unguja ile sura mbaya ya vipindi vilivyopita haikunyesha tu kama mvua; tuliilea sisi wenyewe kwa kutovutiwa sana kutenda haki!!!

Na uzoefu unaonyesha kwamba kwa hali ya aina hiyo wewe mwenyewe utakua unasaidia kwa kiasi kikubwa sana kukiangamizi hicho kikundi kipenzi au kiwakilishi chake na wananchi nao kusubiri kukirudishia KURA ZA CHUKI hivo hivo kama ishara ya kutaka kumtetea mnyonge aliyeonekana kunyongwa hadi na HAKI YAKE bungeni - Ndugu Ndugai, hebu litafakari kidogo hili ninalolisema hapa kwa faida ya mijadala ijayo!!!

Taifa lisiloweza kulinda vilivyo sauti dhaifu katika ngazi yoyote ya jamii haina tofauti sana na wanaukoo wanaogombania mali ya marehemu na kuwaacha solemba wajane na yatima huku wakijipongeza kama zuzu tonge linalobana kwenye koo!!!!
 
Katika kipindi cha maswali kwa Waziri mkuu leo asubuhi mh.Waziri mkuu amesimulia kilichojiri katika mauaji ya Arusha na kwa mujibu wa maelezo yake yameonesha kuituhumu CHADEMA kuwa ni chanzo cha mauaji ya raia kwenye maandamano,amesema kuwa mh.Godbless Lema ni mtu wa fujo fujo hivi na alianzisha fujo kwenye kikao cha pili cha baraza la madiwani halmashauri ya Arusha.
Mwisho mh.Pinda kawashauri CHADEMA kuunda chama kitakachoaminiwa na wananchi kuongoza taifa hili chama chenye kuleta amani.
Wakati huo huo mh.Godbless Lema atumia mwongozo wa Spika kumtuhumu mh.Waziri mkuu kuwa kalidanganya bunge.

Kauli, usemi, lafudhi, uongeaji wa haraka haraka wa Pinda, huhitaji kuambiwa na mtu mwingine kuwa Pinda ni sampuli ya watu wanaopendelea umbea umbea hivi. hiyo tuhuma aliyoitoa ni kama kaiokota bar hivi.

Ni aibu kwa waziri mkuu kutumia mimbari ya Bunge na kutoa habari za kimbea namna hiyo zisizo na facts zozote. He should come up with hard facts!!

RED BOLD ITALIC: Hivi chama cha siasa kinaweza kuunda chama? au tuseme CCM kama chama wameweza kuunda chama cha mafisadi ndani ya ccm?.

Blue: kati ya uamuzi wa Lema na umbea wa Pinda, nani kaonyesha ukomavu?
 
Acha kudanganya watu wewe unasema amesema Lema ni mtu wafujo fujo yeye ndiye aliye leta fujo kwenye baraza la pili la madiwani cyo kweli ktk maelezo ya pinda hakutaja jina la Lema UCFANYE WATU WAJINGA KAMA MAKAMBA ANAVYO POTOSHA WATU UMETUMWA NA CCM NINI NINGEKUWA CJASIKILIZA BUNGE MASWALI YA PAPO KWA PAPO KWANZA PINDA KALIDANGANYA BUNGE NA TAIFA KWA UJUMLA MAELEZO YAKE NITOFAUTI SANA NA YALIYO TOKEA NAKAEGEMEA KUWASEMA CHADEMA BILA KUTAFUTA SULUISHO HUYU NDIYE KIONGOZI WA SEREKALI INASIKITISHA SAAANAAAA
 
toka mtoto wa mkulima mpaka fisadi anayetumiwa na mafisadi papa, shame on u Pinda, umeanza uongo wewe mzee, mbona hujawatuhumu polisi kwa kutumia risasi za moto. unaniudhi sana
 
Katika kipindi cha maswali kwa Waziri mkuu leo asubuhi mh.Waziri mkuu amesimulia kilichojiri katika mauaji ya Arusha na kwa mujibu wa maelezo yake yameonesha kuituhumu CHADEMA kuwa ni chanzo cha mauaji ya raia kwenye maandamano,amesema kuwa mh.Godbless Lema ni mtu wa fujo fujo hivi na alianzisha fujo kwenye kikao cha pili cha baraza la madiwani halmashauri ya Arusha.
Mwisho mh.Pinda kawashauri CHADEMA kuunda chama kitakachoaminiwa na wananchi kuongoza taifa hili chama chenye kuleta amani.
Wakati huo huo mh.Godbless Lema atumia mwongozo wa Spika kumtuhumu mh.Waziri mkuu kuwa kalidanganya bunge.

Hivi Pinda anafikiri kuwa wananchi wa Tanzania kweli wanaiamini CCM tena?? Hajui kuwa watu washa kata tamaa na ndiyo maana hata kupiga kura hawaendi na CCM ipo pale tu kwa ajili ya udictator wao na wananchi hawajajua namna ya kuitoa. Since kile kizazi chao kianaisha taratibu wakati vijana wapiga kura wanaongezeka kwa kasi, nafikiri come 2015 hatakuwa anasema haya maneno ya kejeri kwa wananchi wakionyimwa haki yao ya kuchagua viongozi kwa CCM kuchakachua matokeo ya uchaguzi.
 
Pinda anaingia katika mtego wa kujiaribia mwenyewe.Ina maana haoni ukiukwaji wa

kutisha katika mchakato kumchgua meya wa manispaa ya arusha?

hajui kwamba kwa kauli zake wananchi anaweza akawa anajiaribia taswira yake mbele ya wananchi hadi wamwone sio mtoto wa mkulima tena bali ni walewale?
 
Pinda nae anashusha image yake taratibu ktk macho na masikio ya wenye akili. Ukweli acha usimame wenyewe Pinda, why can't he speak from his heart and stand by the truth? He knows what happened, he knows that his co-pilot members - Andengenye, Mwema etc cooked the entire info.... kwanini anaamua kukubali hao mapumba? Why can't he be commonsensical and a critical thinker for issues brought at his table and that needs a public elucidation? Poor Pinda?????
 
Katika kipindi cha maswali kwa Waziri mkuu leo asubuhi mh.Waziri mkuu amesimulia kilichojiri katika mauaji ya Arusha na kwa mujibu wa maelezo yake yameonesha kuituhumu CHADEMA kuwa ni chanzo cha mauaji ya raia kwenye maandamano,amesema kuwa mh.Godbless Lema ni mtu wa fujo fujo hivi na alianzisha fujo kwenye kikao cha pili cha baraza la madiwani halmashauri ya Arusha.
Mwisho mh.Pinda kawashauri CHADEMA kuunda chama kitakachoaminiwa na wananchi kuongoza taifa hili chama chenye kuleta amani.
Wakati huo huo mh.Godbless Lema atumia mwongozo wa Spika kumtuhumu mh.Waziri mkuu kuwa kalidanganya bunge.
 
kuna vita ya CCM + NCCR MAGEUZI + TLP + UDP + CUF zidi ya CDM..kwa hiyo kama kuna mbunge wa CDM alipopata ubunge alitegemea mtelemko alikosea kazi ndiyo kwanza imeanza....
na sisi wananchi wapenda maendeleo tunapaswa kuwaunga mkono CDM kwa dhati...

Mh. Lema ameuliza hivi kiongozi kama waziri mkuu akiongopa bungeni anachukuliwa hatua gani? matokeo yake spika kaanza kujikanyaga ooh hawezi kudanganya...
 
Pinda mwongo mkubwa wewe, chadema waliandamana polis wakawapiga mabomu ya machozi na risasi sasa Pinda huwezi kutudanganya na CCm yenu. CCM = Lucifer/ devil i hate youuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu CCM

CHADEMAZ = A group of insane people in Juda, kweli nimeamini
 
kuna vita ya CCM + NCCR MAGEUZI + TLP + UDP + CUF zidi ya CDM..kwa hiyo kama kuna mbunge wa CDM alipopata ubunge alitegemea mtelemko alikosea kazi ndiyo kwanza imeanza....
na sisi wananchi wapenda maendeleo tunapaswa kuwaunga mkono CDM kwa dhati...

Mh. Lema ameuliza hivi kiongozi kama waziri mkuu akiongopa bungeni anachukuliwa hatua gani? matokeo yake spika kaanza kujikanyaga ooh hawezi kudanganya...

Amemuambia aandike, ili asulubiwe vizuri, umesahau kilicho mpata zitto ?
 
Back
Top Bottom